Kuna simu ya 5G ya Samsung Galaxy A14 5G utendaji wake unaweza usikushawishi.
Hapa ndipo Samsung Galaxy A34 5G inapokuja kuokoa jahazi
Kutokana na utendaji mkubwa bei ya Samsung Galaxy kwa Tanzania inaenda zaidi ya laki Tisa.
Toleo hili linatofatiana pakubwa na toleo kama la simu nyingine ya 5g ya Oppo A78 5G
Ukizisoma sifa za Galaxy A34 haitokustaajabisha kuona bei yake kuwa inakaribia milioni.
Bei ya Samsung Galaxy 34 5G ya Gb 128
Kwa Tanzania simu inauzwa kwa shilingi 930,000/-
Kwa nchi zingine kiwango hiki Cha pesa ni kidogo ila kwa hapa Tanzania ni Hela nyingi
Utendaji wa simu kwenye kamera, chaji na kioo bila uimara wa bodi ya simu ni moja ya sababu za simu kuuzwa kwa bei hiyo
Hivyo kama unazingtia simu yenye ubora mwingi huna budi kutafuta bajeti kubwa vinginevyo matoleo ya Spark 10 yanaweza kusadia kusukuma siku.
Sifa za Samsung Galaxy 34 5G
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super Amoled, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | 256GB,128GB na RAM 8GB,6GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.6inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 930,000/= |
Upi ubora wa Samsung Galaxy A34 5G
Hiini simu ya daraja la kati la juu hivyo ubora upon kwenye nyanja
Mfano ni ukaaji wa chaji
Ni simu inayoweza kukaa na chaji karibu siku ukiwa kwenye intaneti
Ina utendaji mkubwa wa kufungua Kila aina ya app bila shida yoyote
Inakuja na mtandao wa 5G ambao ndipo wenye Kasi zaidi kwa Sasa
Kamera zake zinatoa picha zenye ubora hasta kwenye mwanga mwingi
Ina teknolojia ya utulizaji wa kamera wakati wa kurekodi video Hulu ukiwa unatembea
Kiufupi simu ina mapungufu machache Sana kama utakavyoona huko baadae
Uwezo wa Network
Simu inakuja na mtandao ya aina yote ikiwemo 4G na 5G kama ilivyonsimu zingine za 5g
Inasapoti aina zote tatu za 5G ikiwemo Ile ambavyo imetumia na mtandao wa Vodacom na Tigo
Aina ya 4G imu inayoumia ni LTE Cat 18 ambavyo Kasi yake inafika 2770Mbps saw na 346MB/s.
Yaani kama ukiwa unpakuwa gemu la Dream Soccer lenye MB 700 Kyle play store, simu italipkuwa kwa sekunde mbili
Ila Kasi ya intaneti itategemea na mtandao unaotumia Tena kwa hapa nchini so rahisi kuipata spidi kwenye 4G labda 5G
Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy A34 5G
Kioo inachotumia Galaxy A34 5G ni super Amoled
Ni kioo kinachoonyesha rangi nyeusi iliyokorea na halisi tofauti na vioo vya LCD
Kwenye rangi za vitu vinaonekana kwa kiwango sahihi na kwa rangi zilizokorea
Kwa mpenzi wa magemu ataridhika kuwa na simu hii kwani Ina refresh rate ya 120Hz
Refresh rate ya 120Hz itakufanya ufurahie kutumia kutokana na ulaini na uharaka pale unapokuwa unaperuzi
Muonekano wa vitu kwenye kioo cha hii simu unachangiwa na kiwango kikubwa cha resolution’
Resolution ya kioo cha galaxy a34 5g ni 1080×2340 pixels
Kama utakuwa unaangalia picha ya aina moja kwenye simu ya Tecno Spark 10 Pro, Oppo A78 na Samsung Galaxy A14 5G na A34 utaona utofauti kwenye muonekano wa hio picha
Nguvu ya processor MediaTek Dimensity 1080
Galaxy A34 5G inatumia chip ya MediaTek Dimensity 1080
Ina sehemu mbili, sehemu ya kwanza ina core kubwa aina ya Cortex A78
Ukiona processor ina Cortex A78 jua kuwa simu itakuwa ina nguvu na pia utumiaji wake wa chaji
Kwenye samsung galaxy a34 5g hii chip inaweza kucheza gemu nyingi kwneye resolution na kwa idadi ya wastani upande wa fremu
Kwa mfano gemu ya PUBG inacheza kwa fremu 40 kwa wastani
Kwa jinsi chip ilivyo na utendaji, inafanya simu kuwahi kuwaka na kufungua apps kwa haraka
Na sehemu ya pili ya dimensity 1080 inaundwa na core maalumu kwa kazi zisizohitaji nguvu kubwa
Core hizi zipo sita na aina ya Cortex A55
Uwezo wa betri na chaji
Ukinunua hii simu utakutana na waya wa USB bila kichwa cha chaji
Hivyo basi itakulazimu utumie chaji ama ununue chaji za samsung
Hata hivyo mfumo wake chaji unaweza kupokea umeme mpaka wa wati 25
Betri ya hii simu ina ukubwa wa 5000mAh
Ukaaji wa chaji ni wa kiwango kikubwa kabisa na unaweza usichaji simu mara kwa mara
Kwa wastani ukiwa unaperuzi intaneti galaxy a34 5g inachukuwa masaa 19 kuisha
Ukiwa unatazama video muda wote mfululizo simu inachukua masaa 13 betri kusiha
Na kwa matumizi ya kawaida yasiyohusisha intaneti, magemu na video betri inaweza chukua zaidi ya siku nne kwa betri kuisha
Ni simu yenye utendaji mkubwa na wakati huo matumizi ya betri ni madogo
Ukubwa na aina ya memori
Samsung wanakupa machaguo matatu kwenye upande wa memori
Machaguo yenye memori ndogo ni GB 128, hapa unaweza ukapata RAM ya GB 6 au ya GB 8
Na chaguo la tatu lina GB 256 na RAM ya GB 8
RAM kubwa ni nzuri, na inakusaidia kufungua vitu vingi kwa ufanisi
Hii simu ina sehemu ya kuweka memori kadi
Aina ya memori haijainishwa ila chip ya hii simu inaweza kutumia memori mpaka za UFS 3.1
Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy A34 5G
Upande wa mbele simu imewekewa kioo kigumu cha Gorilla 5
Simu ikianguka kwa kimo cha mita 1.5 itavumilia kupasuka na kuchunika, ila inategemea na uso wa eneo hiyo simu ilipoanguka
Upande wa nyuma umewekewa plastiki
Simu haiwezi kupitisha maji kama ikizama kwenye kina cha mita moja kwa muda wa nusu
Yaani unaweza ukaja maji kwenye ndoo ya lita 10 na ukaizamisha simu kamwe maji hayatoingia na ukiitoa, simu itaendelea kufanya kazi
Kiufupi, ukiona simu ina viwango vya IP67 basi jua hii inamaanisha si vumbi wala maji yataweza kupenya ndani ya simu
Ubora wa kamera
Simu ina kamera tatu na haina kamera ya depth sensor ambayo hainaga umuhimu kwa sasa
Kamera kubwa ina megapixel 48 na kamera nyingine ni maalumu kupiga eneo pana sana na ina megapixel 8 na nyingine 2MP
Kamera kuu inatumia ulengaji aina ya PDAF japo haiko vizuri kama dual pixel pdaf ila sio mbaya
Ubora wa picha ni mkubwa hata bila kutumia Auto HDR
Kamera yake inaweza kutofautisha rangi kwa usahihi mkubwa, hivyo muonekano wa vinavyopigwa picha unaendana na muonekano halisi
Kitu kimoja ambacho kinakosekana ni kamera ya telephoto pamoja na kutokuwepo kwa optical zoom
Video pia inafanya vizuri unaweza kurekodi mpaka video za 4K kwa fremu 30 kwa sekunde
Pia ina OIS hivyo kutakuwa kuna utulivu wakati ukirekodi video huku ukitembea
Ubora wa kamera Ubora wa Software
Samsung Galaxy 34 5G inakuja na mfumo wa Android 13 na One UI 5.1
Kuhusu android 13, unaweza pitia: vitu vilivyomo kwenye android 13
Samsung watakuwa wanatoa matoleo mapya ya android kwenye hii simu kwa muda wa miaka minne
Na maboresho ya mifumo ya kiusalama kwa muda wa miaka mitano
Hii inamaanisha utapokea Android 14, 15, 16 na 17
One UI 5.1 ina mfumo mmoja wa akili bandia (AI) kwenye app yake kamera
Inakuruhusu kukitoa kitu chochote kwenye picha na kisha ukifadhi ama kuinga na picha nyingi
Kwa mfano, umepiga picha kwenye eneo la watu wengi na wewe ukawa huitaji wale watu watokee
Kamera iliyomo kwenye One UI 5.1 inakusaidia kutoa picha yako na ukaweka kwingine kwenye simu
Yapi Madhaifu ya Samsung Galaxy A34 5G
Kasoro chache zilizopo kwenye hii simu kwanza ni kutokuwepo tundu la earphone
Pia simu haina radio kwa hiyo ukitaka kusikiliza redio basi intaneti inakuhusu
Kingine ni simu kutokuja na chaji kunaongeza gharama kama hukuwahi miliki chaji ya samsung
Neno la Mwisho
Kwa mtu mwenye bajeti ya laki saba mpaka laki tisa lazima afikirie kuimiliki hii simu
Ni simu inayokuja na uwezo kuridhisha kwenye maeneo mengi na imara
Ukizingatia simu itakuwa inapokea matoleo mapya ya Android
Kitu kitakachokuwa kinatunza thamani ya simu kwa muda mrefu
Maoni 10 kuhusu “Bei ya Samsung Galaxy A34 5G na Ubora wake”
Kwanini sim za samsung za A mfano A34 au A24 na A nyingne ram yake imeandikwa ram plus alafu ukiangalia kama ni 6 lakin haifik y inakua 5.3
Ram plus ni ule uwezo WA simu kutumia storage(memori) ya simu kama RAM, unapata uwezo WA kuongeza ram kutoka kwenye storage. Uwezekano ni kuwa ni namna mfumo WA simu unavyokokotoa ukubwa WA memori ndio maana haionyeshi ukubwa wrote WA ram
Nataka kujua huo ukubwa wa GB 128 ni saw na ukubwa wa GB 256 Au tofaut maan maelezo kidg yamenichanganya
Ni tofauti kiongozi
Hivi simu hiyo inatumia Type c au usb ya kawaida
Ndio inatumia usb type c
Pia kuna utofauti gani kati ya hii simu na sumsung S 10 au zote ziko sawa
Hapana hazipo sawa A34 Kwa sasa ni nzuri kuliko s10
Tundu la earphones lipo, unatumia earphones ya type c
Mbona ya kwangu ilizima glafla alafu haiwaki tena shida nini na piah kioo chak cha simu shilingi ngapi