Android ni mfumo endeshi(yaani operating system) wa simu ambao uko chini ya usimamizi wa kampuni ya Google
Mfumo endeshi (Operating System) ni software(mfano applikesheni) unaosimamia vifaa vifaa vya simu au kompyuta kiingereza hutambulika kama hardware na appliksheni.
Appliksheni inapotaka kufanya kazi inapita kwenye mfumo endeshi kisha mfumo endeshi unaipa appliksheni huduma inayohitaji
Kwa mfano ukifungua app ya kamera ni mfumo endeshi (OS) ndio utakaounganisha applikesheni na kamera
Mfumo endeshi wa android una matoleo mengi yanayofahamika kama Android Versions ambayo yamefika 13
Na toleo jipya kabisa ni Android 14 inayotazimiwa kuachiwa rasmi muda wowote mwaka huu 2023
Kwa hapa tunaenda kuitazama vitu vilivyopo kwenye android 13
Ijue Android 13
Android 13 ni operating system iliyotoka mwezi wa nane mwaka 2022
Simu za mwanzo kupokea android 13 zilikuwa ni simu za pixel ambazo hutengenezwa na google
Mfumo huu una vitu vya ziada na mabadiliko yanayofika 15
Mabadiliko haya yamegawanyika kwenye usalama, maboresho ya kimuonekano na matumizi rahisi ya simu
Hakuna mabadiliko makubwa sana ila mabadiliko machache yana upekee na kuongeza uhuru wa matumizi ya simu
Baadhi ya simu ambazo zina Android 13 ni samsung galaxy s23 Ultra na Google Pixel 7 Pro
Baadi ya vitu vilivyoongezwa ni kama ifuatavyo.
Notification lazima ziombe ruhusa ya mtumiaji
Kwenye matoleo ya zamani appliksheni za simu zilikuwa zinatoa notification bila ruhusa yako
Iwapo appliksheni nyingi zinafanya hivi inakuwa kero kwa kiasi kikubwa
Na kwa baadhi ya simu unakuwa unashangaa notification ni nyingi na hujui zimekujajew
Google kwenye Android 13 kila app inayotaka kutuma ujumbe kwa njia ya notification lazima ipate ridhaa ya mtumiaji
Maana yake utaweza kuzuia app ambazo hutaki zitume notification na zile unazotaka
Hii inapunguza usumbufu
Ruhusa ya kuruhusu app kutuma nofication inakuja pindi unapoipakuwa app kutoka play store
Ukiifungua tu ujumbe wenye machaguo mawili utakuja na kukutaka kuchagua “Allow” au “Don’t Allow”
Kuchagua Lugha Yoyote kwenye app Husika
Matoleo ya Android kabla ya Android 13 yalikuwa yanatumia lugha uliyoichagua kabla kwenye kila app
Yaani kwenye settings kuna sehemu ya kuchagua lugha kama ukichagua English basi english inatumika kwenye kila app
Mabadiliko yamefanywa kwenye toleo la 13 ambapo utaweza lugha mbalimbali kwa kila app
Kwa mfano kama unataka app ya Chrome iwe na settings za kiswahili pekee basi hivi sasa unaweza kufanya hivyo bila kuathiri mpabngilio wa lugha kwenye app zingine
Ili kubadirisha lugha ya app husika unachatakiwa kufanya ni kwenda kwenye settings na kisha chagua apps
Itakuja orodha ya app zote zinazopatikana kwenye simu
Utabonyeza app unaoitaka kisha unaenda sehemu ya “Language” na kuchagua lugha unayopendelea itumiwe na app hiyo
Kukufahamisha app zinazofanya kazi bila mtumiaji kuziona (Background apps)
Kuna apps huwa zinafunguka pasipo wewe kujua kuwa app imefunguka
App ikifunguka kwa mtindo huu inaitwa background app mfano mzuri ni app za mijandao ya kijamii instagram
Hizi huwa zinafunguka mara nyingi hata kama huitumii na ndio maana huwa zinatuma notification mara kwa mara
Background huchangia matumizi makubwa ya betri
Pitia: Simu kupata moto sana na jinis ya kuzuia
Android 13 itakujulisha apps ambazo zipo “active”
Na hivyo utaweza kuifunga, hii ni njia moja wapo ya kudhibiti appiksheni zinazotrack mawasiliano na data zako pasipo wewe kujua
Ulinzi wa data zinazokopiwa umeongezwa
Unapokopi maandishi kwenye simu za android taarifa huwa zinaifadhiwa kwanza kwenye kitu kinaitwa Clipboard
Clipboard inasaidia kuhamisha taarifa kutoka app moja kwenda nyingine
Kitendo hiki kinaipa nafasi app mbalimbali kupata hizo data
Hivyo kuna changamoto ya kiusalama inaibuka
Inakuwaje app zenye ambazo zinazamilia kuiba password yako zikifanya hivyo?
Android 13 imeboresha Clipboard kwa kuipa uwezo wa kuondoa taarifa “automatically” baada ya muda fulani baada ya kuwa umeshatumia
Hii inaepusha app zinazotumia mwanya huo kuchukua taarifa pasipo ridhaa yako
Muonekano mpya wa app ya audio
App ya kusikiliza mziki na vitu vingine una muonekano unaokujulisha kwa haraka urefu wa windo ambao tayari ushasikiliza
Kwenye mstari unaonyesha muda (urefu wa audio) husika kuna muonekano wa mawimbi kwenye kipande ambacho umeshasikiliza
Itakusaidia kujua kwa haraka kujua urefu uliobaki
Lakini ni muonekano unaovutia na kukufanya kutazama simu muda wote
Kitufe cha settings kimeamishwa upande wa chini
Kikawaida ukitaka kwenda settings njia ya haraka ni kubonyeza kitufe cha settings ambacho huwa kipo juu
Kwa sehemu ndefu kama Tecno Phantom X2 Pro inaweza ikawa kero kiasi fulani
Android 13 imerahisisha kufikia kitufe cha settings
Uki-swipe simu kutoka juu kitufe hiki kinaenda chini kabisa
Unakuwa unakifikia kwa haraka na urahisi
Kwa simu zenye inchi nyingi huu ni msaada mkubwa
Simu yako inaweza pata Android 13?
Sio simu zote zinazopata matoleo mapya ya Android
Simu za madaraja ya juu huwa yanapokea maboresho ya Android kila yanapotoka
Kwa simu za bei ndogo huwa zinakumbana na changamoto ya kupata mfumo endeshi mpya
Kikawaida watengeneza simu hawazitilii maanani sana simu za daraja la chini
Zipo njia mbadala ambazo zinaweza saidia mtumiaji kupata toleo lolote la android
Njia hizo zinahusisha kuweka ROM (hapa panahitajika utaalamu) vinginevyo utalazimika kununua simu mpya
Hitimisho
Pamoja na android 13 kuja baada ya Android 12 ila hakuna tofauti kubwa sana kati ya mifumo miwili
Tofauti ambazo zimekuwa zinakuja ni zile zinazohusisha maboresho ya kiusalama zaidi
Kadri muda unavyokwenda android inazidi kuwa na ulinzi madhubuti dhidi ya app ambazo si salama
Maoni 2 kuhusu “Android ni nini na Ifahamu Android 13”
Samsung a90 inaweza kupata toleo la 13?
Inapokea mwisho android 11