SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Samsung Galaxy A14 5G na Sifa zake kuu

Sifa za simu

Sihaba Mikole

April 10, 2023

Samsung za 5G mfano wa Samsung Galaxy 23+ bei yake ni kubwa

Kiasi cha kudhani kuwa simu za 5g zina bei sana ila yapo matoleo ya samsung yenye bei nafuu kidogo

Moja ya toleo hilo ni Samsung Galaxy  A14 5G ambayo imetoka mwezi januari 2023

samsung a14 showcase

Bei ya samsung galaxy A14 5G kwa Tanzania inazidi laki tano

Simu ina maboresho kadhaa ukilinginisha na toleo lilopita ila inakutana na ushindani wa kampuni za china zilizotoa simu zinazoendana kiubora na galaxy A14 5G kama utakavyoona

Bei ya Samsung Galaxy A14 5G ya GB 128

Galaxy A14 5G ya GB 128 inauzwa shilingi 620,000 kwa Tanzania

Ila ya GB 64 inapatikana kwa laki nne na nusu

Ukifananisha na simu kama Redmi 10C utaona kuwa redmi ni nafuu sana kwani bei yake ni chini ya hapo

samsung galaxy summary

Ila Galaxy A14 5G ni simu yenye ubora mwingi kwenye nyanja tofauti

Ukizisoma sifa zake kwenye jedwari chini utagundua kuwa ni simu yenye nguvu, fasta, kioo kizuri na hata kamera

Lakini hii haimaanishi kuwa hakuna washindani waliotoa simu bora kama hii mwaka 2023, wapo na utawajua

Sifa za Samsung Galaxy A14 5G

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
 • CPU – Exynos 1330 (5nm)
 • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.4 GHz Cortex-A78
 • Core Za kawaida(6) – 6×2.0 GHz Cortex-A55
 • GPU-Mali-G68 MP2 – SM-A146B
Display(Kioo) IPS LCD, Refresh rate:90Hz
Softawre
 • Android 13
 • One UI Core 5
Memori 128GB,64GB na RAM 8GB,6GB,4GB
Kamera Kamera tatu

 1. 50MP,PDAF(wide)
 2. 2MP(macro)
 3. 2MP(depth)
Muundo Urefu-6.5inchi
Chaji na Betri
 • 5000mAh-Li-Po
 • Chaji-15W
Bei ya simu(TSH) 620,000/=

Upi ubora wa Samsung Galaxy A14 5g

Simu iko fasta kutokana na kuwa na processor yenye nguvu

Inakaa na chaji masaa mengi ambayo yanakaribia ishirini

Ina kioo chenye resolution kubwa hivyo muonekano wa vitu ni mzuri

Uangavu wake wa kioo ni mkubwa unaosaidia kioo kuonyesha vitu vizuri hata ukiwa juani

Inakuja na uwezo wa kutumia mtandao wa 5G ambao kasi yake ya kupakua na kupandisha ni ya haraka

Ni moja ya simu chache za siku hizi zinazokuja na redio, sehemu ya memori card na ya earphone

Uwezo wa Network

Galaxy A14 5G ina mtandao wa 5G kama jina lake linavyojionyesha

Tanzania kuna mitandao miwili inayotumia 5G ambayo ni vodacom na Tigo

Japo haijasambaa maeneo mengi ila matarajio yakutanuka mbeleni yapo

Upande wa 4G ina masafa yote yanayotumika hapa nchini

Na inatumia aina zote tatu za 5G, kwa hapa Tanzania mitandao inatumia NSA (Non Stand Alone)

samsung galaxy a14 network

NSA huwa inatumia miundombinu ya 4G ndio maana laini ya 4G inaweza kutumika kwa ajili ya 5G

Aina ya 4G inayotumiwa na hii simu ni LTE Cat 18 yenye kasi ya 2550Mbps sawa na 318.75MB/s

Kasi hii inaweza kupakua gemu Call of duty la 2GB kwa sekunde tisa tu

Kwa Tanzania unaweza pata nusu ya kasi hii kama utakuwa unatumia 5G ya Tigo kama wenyewe wanavyojitangaza

Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy A14 5G

Upande wa kioo simu inatumia kioo cha IPS LCD chenye refresh rate 90Hz

Hiki ni kioo kama cha Tecno Spark 10 Pro isipokuwa kioo cha samsung kina resolution kubwa

Hivyo muonekano wa picha na video ni mzuri kiasi kwani resolution yake ni 1080 x 2408 pixels

Ila kumbuka vioo vya IPS sio vizuri ukilinganisha na vioo vya AMOLED

samsung galaxy a14 display

Ndio maana simu za amoled huwa zina bei kubwa kidogo na hata kioo kikiharibika utahitajika kujichanga

Refresh rate kubwa hufanya simu kuwa “smooth”(laini, nyepesi) wakati wa kutachi

Refresh rate Inapukuwa kubwa kama 90Hz mwitikio wa kioo ndio unakuwa mzuri zaidi

Bahati mbaya refresh rate kubwa hutumia umeme mwingi na pia unaweza kuizima kama hupendelei

Nguvu ya processor Exynos 1330

Kuna matoleo mawili ya Samsung Galaxy A14 5G upande wa processor

Kwa simu zinazouzwa India zinatumia Exynos, na kwa Marekani ni Dimensity 700

Kwa hiyo kutakuwa kuna mchnaganyiko wa simu kwa hapa kunaangaziwa inayotumia Exynoss 1330

samsung galaxy a14 5g processor

Exynoss 1330 imegawanyika sehemu mbili

 • Core ya Cortex A78 (ina nguvu sana) zipo mbili
 • Core ya Cortex A55 ya kazi ndogondogo zipo sita

Uwepo wa core aina ya Cortex A78 inaifanya simu kufungua app yoyote kwa haraka na kwa matumizi madogo ya umeme

Chip hii inacheza gemu nyingi kwa resolution kubwa bila kupata tatizo lolote kama kuganda ganda

Exynoss 1330 ina ufanisi wa 89% katika matumizi ya betri ndio maana unaweza ukaitumia simu kwa mambo mengi ila betri ikachelewa kuisha

Uwezo wa betri na chaji

Galaxy A14 5G ina mfumo unaopitisha chaji kwa kasi ya wati 15

Kama unaichaji simu kwa kutmia chaji ya wati 25 inachukua masaa mawili kujaza betri kwa asilimia 100

Kwa chaji ya 15 itachukuwa muda zaidi ya huo

Betri yake ina ukubwa wa 5000mAh na ni aina ya Li-Po

samsung galaxy a14 5g

Kwenye matumizi ya intaneti simu inakaa na chaji mpaka masaa 19 ukiwa unaperuzi

Ukiwa unatazama video inachukua masaa 13 kwa chaji kumalizika

Haya ni masaa yanayozidi simu ya iPhone 14 Pro Max

Hii ni moja ya Samsung ambayo hutowaza kuhusu ukaaji wa chaji kabisa

Ukubwa na aina ya memori

Kuna matoleo mawili ya samsung galaxy a14 5g linapokuja ukubwa wa memori na matoleo hayo yanatofautiana ukubwa wa RAM

Kuna ya RAM 4, 6 na 8 na upande wa memori kuna GB 64 na 128

Kwa mtumiaji sana wa simu ni vizuri ukachukua ya GB 128 na RAM gb 8

Kwa maaana utaweza hifadhi vitu vingi na kufungua apps nyingi bila RAM kujaa kwa haraka

Mfumo wa Android huwa una matumizi makubwa ya RAM, lakini machaguo mengine yote yapo sawa

Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy A14 5G

Hii simu ina plastiki ya kawaida upande wa nyuma na haijawekewa vioo vya gorilla upande wa screen

Kwa mantiki hiyo simu inaweza pasuka kirahisi kama ikianguka sehemu mbaya

samsung galaxy a14 body

Na pia itakulazimu kuwa makini kwani haina uwezo wa kuzuia maji kama ilivyo kwa samsung galaxy s23

Ila hata hivyo hii ni samsung ya bei nafuu hutarajii kuwa na vitu vya hali ya juu sana

Upande wa pembeni wa hii simu kuna fingerprint na ni simu ya laini mbili kwa india na laini moja kwa Marekani pia haina esim

Ubora wa kamera

Galaxy A14 5G ni samsung ya macho matau ila kamera kubwa ndio ina megapixel 50 pekee

Kamera zilizobaki zina megapixel 2

Na kiuhalisia simu ina kamera mbili kwa sababu kamera ya depth kazi yake ni kupima umbali kati ya kinachopigwa picha na kamera

Hii inasaidia kuweka “brul”(ukungu nyuma ya anayepigwa kamera). Sio muhimu kwa sababu app za kamera zinawezwa fanya hiyo kazi kutumia depth camera

Kmaera ya 50MP inapiga picha nzuri hasa kwenye mwanga mwingi

samsung galaxy a14 photo quality

Inatoa rangi halisi kwa kiwango kikubwa kama zinavyoonekana kwenye mazingira yake

Ila kamera aina ya macro haipigi picha nzuri kabisa hata nyakati za mchana

Simu inarekodi video za full hd na haina mfumo kutuliza kamera yaani OIS

Ubora wa Software

Simu inakuja na Android 13 na One UI Core 5

One UI Core 5 ina vitu vingi vinavyopatikana kwenye One UI iliyopo kwenye samsung s-series

samsung galaxy a14 5g software

Isipokuwa utakosa smasung pay kwa kulipia vitu mbalimbali ila kwa hapa kwetu watu wachache wanatumia huu mfumo wa malipo

Kitu kimojawapo kizuri cha One Ui Core ni uwepo wa mfumo unaitwa Bixby Text Call

Bixby Text Call inaweza kubadirisha sauti kuwa maandishi na maandishi kuwa sauti

samsung galaxy a14 5g software 2

Hivyo unaweza ukawa unajibu kwa maandishi bixby ikawa inatengeneza sauti na kuwasiliana kwa mtindo huo

Lakini kiswahili si moja ya lugha inayofanya vizuri kwenye mfumo huu

Yapi Madhaifu ya Samsung Galaxy A14 5G

Kamera moja ya Galaxy A14 5G ndio inayotoa picha za kuvutia

Simu haijawakewa aina yoyote ya IP kuonesha uwezo wa simu kuzuia maji

Haiwezi kurekodi video za 4K kwa sababu kuna simu kama Redmi Note 10 inafanya hiyo kazi na bei zinaendana

Inatumia kioo cha IPS ambavyo ubora wake sio mkubwa kama amoled

Izingitiwe kuwa samsung huunda aina hii ya vioo

Kasoro kubwa ziadi ni uwepo wa matoelo mawili ya simu moja yanayotofautiana nguvu ya utendaji

Kuna toleo la galaxy a14 5g yenye chip ya dimensity 700 ambayo nguvu yake inazidiwa na galaxy a14 5g yenye exynoss 1330

Ni mkanganyiko kwa mteja

Neno la Mwisho

Sifa za samsung galaxy a14 5g nyingi zinavutia na uwepo wake unazipa changamoto simu za Tecno Spark 10 Pro

Ila hii simu inakumbana na ushindani mkali zaidi na simu za Oppo A78, Vivo Y72 5G, Xiaomi Poco M45G na Oppo A53s

Hizo simu tano zina bei nafuu kidogo huku ubora ukiwa unaendana kwa kiwango cha juu

Kiujumla, hii ni samsung nzuri ya 5G yenye bei nafuu ambayo unaweza kuimiliki kama utajichanga

Maoni 18 kuhusu “Bei ya Samsung Galaxy A14 5G na Sifa zake kuu

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

samsung galaxy a15 thumbnail

Bei ya Samsung Galaxy A15 na Sifa Muhimu

Mwezi wa desemba 2023 ni mwezi ambao Simu ya Samsung Galaxy A15 ilizinduliwa Ni simu ya daraja la kati ambayo ina vitu vichache vinavyopatikana kwenye samsung za bei kubwa Ndio […]

samsung a55 showcase

Bei ya Samsung Galaxy A55 na Ubora wake

Samsung Galaxy A55 imetoka mwezi machi mwaka 2024 na ni simu ya daraja la kati Bei ya Samsung Galaxy A55 kwa Tanzania ni shilingi milioni moja na laki moja na […]

thumbnail

Bei ya Samsung Galaxy A35 na Sifa zake

Samsung Galaxy A35 ni toleo jipya la samsung lilotoka mwezi machi 2024 Ni simu ya daraja la kati iliyochota baadhi ya sifa muhimu kutoka kwenye galaxy yenye bei kubwa Ndio […]

simu mpya

Simu mpya kali 20 na bei zake kwa mwaka 2024

Hii ni orodha ya simu mpya ambazo zimetoka mwaka 2024 ama mwishoni mwa mwaka 2023 kutoka kwa kampuni zipatazo 11 Ni orodha inayohusisha simu za daraja la kati na la […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram