Simu ya OPPO A77 ni simu janja ya android 12 iliyoingia sokoni mwezi juni 2022
Simu hii inaingia katika kundi la kati kutokana na sifa na ubora wake
Bei ya OPPO A77 inazidi shilingi laki tano kwa hapa Tanzania
Japokuwa ina bei kubwa, ila ubora wake ni wa wastani hasa upande wa utendaji na kamera
Bei ya OPPO A77 ya GB 128 Tanzania
Oppo yenye GB 128 inauzwa shilingi 540,000 kwa hapa nchini
Kuna utofauti wa 2% wa bei ya hii simu kati ya Kenya na TZ
Kwani hii simu nchini Kenya inapatikana kwa shilingi 524,000
Bei yake si ya kiushindani kutokana na sifa zake na pia uwezo wake wa processor kiutendaji
Ukizifuatilia sifa za oppo A77 zinaweza zikakufanya kutafuta simu mbadala kutokana na aina ya bei
Sifa za Oppo A77
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD |
Softawre |
|
Memori | eMMC 5.1, 128GB na RAM 4GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.56inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 540,000/= |
Ni upi Ubora wa Simu ya Oppo A77?
Oppo A77 ina memori kubwa inayoweza kuhifadhi na kuweka applikesheni nyingi
Mtumiaji hatopata wasi wasi wa simu kujaa
Ni simu inayokaa na chaji masaa mengi ikizingatiwa chip yake inatumia umeme mdogo
Ujaaji wa chaji ni wa haraka sana
Kwani chaji yake inapeleka umeme mwingi wa kutosha
Pia ina kamera kuu yenye megapixel nyingi japokuwa wingi wa megapixel si kigezo cha simu kuwa na kamera nzuri
Simu inakuja na toleo jipya la android ambapo kuna baadhi ya simu mpya bado zinakuja na Android 11
Ila si vitu vyote vya oppo a77 vipo kwenye viwango vya simu nyingi zinauzwa zaidi ya laki tano
Fuatilia makala yote ufahamu nyanja ambazo simu ipo vizuri na zile ambazo hazipo vizuri
Uwezo wa Network
Oppo A77 ni simu ya 4G
4G inayotumia ni aina ya LTE Cat 7 yenye kasi ya juu kabisa ya kupakuwa faili ya 300Mbps
Kwa Tanzania, hakuna mtandao wa simu kwa sasa unaotoa spidi hiyo
Kama ungekuwepo basi simu ingekuwa inamaliza kudownload faili la ukubwa wa 3600MB kwa sekunde 100
Ambazo ni sawa na dakika moja na sekunde 40
Uzuri ni kuwa ina masafa yote yanayotumiwa na mitandao ya simu nchini
Hivyo basi, intaneti za 4G za laini zote zitafanya kazi
Pia pitia: Maana ya 5G kiundani
Ubora wa kioo cha OPPO A77
Moja ya kitu kinachoifanya bei ya OPPO A77 kuonekana kuwa kubwa ni aina ya kioo inachotumia
Kioo cha Oppo A77 ni cha IPS LCD chenye resolution 1612 x 720 pixels
Hiyo ni resolution yenye pixel chache kitu kinachofanya muonekano wa vitu kutokuwa na ubora mkubwa sana kama vioo vya pixels nyingi
Baadhi ya simu kama Redmi Note 10 Pro zinatumia vioo vya AMOLED
AMOLED ina rangi nyingi zinazochangia vitu kuwa na muonekano halisi kwa kiasi kikubwa
IPS LCD huwa hazionyeshi rangi nyeusi halisi.
Tazama, jinsi kioo cha amoled cha samsung a52 kinavyoonyesha rangi nyeusi
Pia refresh rate yake ni ya kawaida inayoendana na uwezo wa processor
Nguvu ya processor Meditek Helio G35
Processor ya Mediatek helio G35 ndio inayoipa nguvu simu ya OPPO A77
Ni chip ya daraja la chini kwani inaundwa na core zenye nguvu ndogo pekee
Ina jumla ya core zipatazo nane.
Hivyo ni simu inayomfaa mtumiaji asiyetumia applikesheni zinazotumia nguvu kubwa
Ukiwa na simu yenye chip dhaifu kuna vitu vingi hutovifanya kwa ufanisi
Ni vizuri ukajua namna ya kujua simu yenye processor yenye nguvu
Pitia hapa: Jinsi ya kujua simu nzuri kwa kuangalia uwezo wa processor
Kwenye app ya Geekbench helio g35 ina alama 171 ambayo inaendana kwa kiasi fulani na chip ya Exynos 850
Exynos 850 imetumika kwenye simu ya Samsung Galaxy A13
Uwezo wa GPU ya PowerVR GE8320
Kirefu cha GPU ni Graphics Processing Unit
Ni aina ya processor ambayo ina kazi ya kuonyesha picha na kuchora picha za michoro ya 2D na 3D na kuonyesha video kwenye screen
Bila GPU simu haiwezi kucheza magemu.
Picha ambazo GPU inaziandaa huitwa frame, na huandaa kwa kuzingatia resolution
GPU ikiwa inaweza kuonyesha fremu nyingi kwa sekunde basi uwezo wake ni mkubwa
PowerVr GE8320 ina uwezo mdogo wa kucheza gemu kwenye ubora wa juu
Gemu ya simu ya PUBG inacheza kwa fremu 24 kwa sekunde (24fps), kikawaida chip nzuri huzalisha zaidi ya 60fps
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya Oppo A77 ina ukubwa wa 5000mAh
Huu ni ukubwa unaoifanya simu kuweza kukaa na chaji masaa mengi (zaidi ya 14)
Ikizingatiwa, simu haitumii processor inayokula moto mwingi, na kioo chake hakina ulaji mkubwa wa chaji
Chaji yake inapeleka umeme mwingi
Ambao unaweza ukajaza betri ndani ya dakika 80 kama ilivyo kwa Redmi Note 10
Kwani chaji ya oppo a77 inapeleka umeme wa wati 33
Ukubwa na aina ya memori
Hii simu inatumia memori aina ya eMMC 5.1
Uwezo wa memori kusafirisha data nyingi huongeza utendaji wa simu
Lakini eMMC 5.1 inaweza kusafirisha data kwa spidi ya 600MBps
Ni kasi kubwa ila sio kubwa kama simu zinazotumia UFS 2.1 au NVMe ya iPhone 12 Pro Max
Kuna toeo moja tu la oppo a77 upande wa memori
Toleo hilo lina GB 128 na GB 4
Ukubwa wa memori kwa kiasi kikubwa unachangia simu kuuzwa kwa bei kubwa
Hata simu za makampuni nyingine bei huongezeka kutokana na ukubwa wa memori na RAM
Ubora wa kamera
Simu ina kamera mbili ambapo kamera moja ina kiwango kidogo cha megapixel (2MP)
Kamera nzuri za simu huwa zinakuwa na simu zenye resolution ya kuanzia 10MP
Mfumo mzima wa kamera za hii simu ni wa kawaida sana
Kwani inatumia ulengaji AF, utambuzi wake wa kitu kinachopigwa si mkubwa kama PDAF.
Kwenye mwanga hafifu kamera kuu haitoi picha nzuri
Ila kwenye mwanga mwingi (hasa mchana) picha zinatokea vizuri japo huwezi linganisha na Tecno yenye kamera nzuri
Japokuwa kamera kubwa ina 50MP ila simu haiwezi kurekodi video za 4K
Hii inatokana na nguvu ndogo ya processor
Ubora wa Software ya ColorOS 12.1
Ukiondoa mfumo wa Samsung wa One UI 4.1, ColorOS ni mfumo mzuri unaorahisha matumizi ya simu
Oppo A77 inatumia ColorOS 12.1 na Android 12
Aina za emoji ambazo ColorOS 12.1 ni wa kipekee zenye muundo wa 3D
Kitu kizuri ni kuwa mfumo unaruhusu kuhariri (editing) emoji na kuweka kwenye muundo unaoutaka wewe
Jambo jingine la kupendeza ni uwezo wa simu kutumia applikesheni mpaka tatu kwa wakati mmoja
ColorOS 12.1 inaweza kuzigawanyisha app katika sehemu tofauti
App ya kwanza unaweza kuiweka upande wa kushoto mwa screen ya pili kulia, na zote zikawa zinatumika wakati mmoja
Yapi Madhaifu ya Oppo A77
Oppo A77 inatumia processor yenye nguvu ndogo huku bei yake ikiwa kubwa
Kamera zake hazitoi picha zenye ubora mkubwa hasa nyakati za usiku
Simu inatumia kioo cha LCD chenye resolution ndogo
Haina 5G, Vodacom wamezindua uanzishwaji wa mtandao wa 5G
Hivyo Tanzania itaanza kunufaika na teknolojia hii mpya ya mawasiliano
Haina viwango IP(Ingression Protection) kwa ajili ya ulinzi wa maji na vumbi
Neno la Mwisho
Kama unahitaji simu nzuri kwa ajili shughuli za kawaida basi bei ya oppo a77 haiwezi kukuzuia kuwa nayo
Lakini kama unahitaji zaidi ya simu, kuna machaguo mengi ya simu mazuri yanauzwa kwa chini ya laki tano