SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Simu mpya 12 nzuri za Oppo na bei zake 2024

Simu Mpya

Sihaba Mikole

February 27, 2024

Tangu mwishoni mwa mwaka 2023 mpaka sasa 2024 tayari kampuni ya OPPO toka china wametoa simu zaidi ya 15 za madaraja mbalimbali

Hapa utakutana na orodha ya simu mpya za oppo na bei zake kwa mwaka 2024

Hii orodha inahusisha OPPO za bei rahisi na Oppo za bei kubwa

Kwa maana kuna oppo za madaraja ya chini na za madaraja ya juu kabisa

Kwa maana hiyo utafanya uchaguzi kulingana na bajeti yako pamoja na vigezo unavyopendelea simu kuwa navyo

1. OPPO Reno11 F

Bei ya OPPO Reno11F: 870,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM:  8GB

Simu ya OPPO Reno11 iilianza kupatikana sokoni mnamo february 8

Ni OPPO ya kamera tatu na inayotumia kioo cha AMOLED chenye kuonyesha rangi zaidi ya bilioni

Hii oppo ni ya daraja la kati japo nkiharaka bei yake

oppo reno11 f

Utendaji wake una nguvu kwa sababu chip yake imeundwa kwa muundo wa Cortex A78 kwenye core zenye nguvu

Inatumia processor ya mediatek Dimnensity 7050

Betri yake ina ukubwa wa 5000mAh na chaji yake inapeleka umeme wa wati 67 hivyo hujaa ndani ya muda mfupi

2. OPPO Pad Neo

Bei ya OPPO Pad Neo: 680,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM:  6GB

Oppo Pad Neo ni kishikwambi(tablet) chenye ukubwa wa inchi 11.4

Ukubwa wake unavizidi vishikwambi vya walimu

Kioo cha Oppo pad neo kina resolution kubwa inayofanya vitu kuonekana vizuri

oppo pad neo

Betri yake ina ujazo wa kukaa na chaji masaa mengi kwani ukubwa wake ni 8000mAh

Kamera yake sio nzuri ila chaji yake inachaji simu kwa haraka kutokana na kupeleka umeme wa wati 33

3. OPPO Reno 11 Pro

Bei ya OPPO Reno11F: 1,300,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM:  12GB

Moja ya kitu cha kuvutia kwenye OPPO Reno 11 Pro ni kio chake kuwa na HDR10+

Hii inafanya kioo kuwa na utajiri wa rangi unafanya vitu kuonekana kwa uzuri

oppo reno11 pro

Kamera zake tatu na zote ni nzuri zenye uwezo wa kurekodi video za 4K

Chaji yake inapeleka umeme wa wati 80, hii inaweza kuijaza betri yake ndani ya dakika 45 kwa 100% kutoka zero

Ila betri yake sio kubwa kama zilivyo simu nyingi za siku hizi kwani ukubwa wake ni 4600mAh

Nguvu ya utendaji ni ya kuridhisha kwani inatumia chip ya Mediatek Dimensity 8200

4. OPPO Reno 11

Bei ya OPPO Reno11: 1,000,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM:  8GB

Kisifa ni ngumu kuitofautisha OPPO Reno11 na OPPO Reno11F

Zote zinatumia processor ya aina moja ambayo ni Mediatek Dimensity 7050

oppo reno11

Hivyo hakuna utofauti katika utendaji

Kiuhalisia ukiiona Reno11F ni kama umeiona Reno 11

Inawezekana ikawa ni simu moja yanayotofautiana bei kutokana na soko lengwa

5. OPPO Find X7 Ultra

Bei ya OPPO Find X7 Ultra: 2,500,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM:  12GB

Oppo Find X7 Ultra ni simu kali kabisa ya OPPO ambayo ipo kwenye kundi la daraja la juu

Simu inatumia chip yenye nguvu kubwa na iliyotumika kwenye simu nyingi za madaraja ya juu

Chip hiyo ni Snapdragon 8 Gen 3 ambayo hata Samsung Galaxy S24 Ultra wameitumia kwa samsung za Marekani

oppo find x7 ultra

Hii simu inakupa na mfumo wa chaji unaosapoti umeme wa kasi ya wati 100, hii inajaza simu kwa wastani wa dakika 30

Ni simu yenye kamera nne na zote zinapiga picha vizuri kwa nyakati zote(mchana na kwenye mwanga mdogo)

Hii ni oppo yenye waterproof

6. OPPO Find X7

Bei ya OPPO Find X7: 2,400,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM:  12GB

Oppo Find X7 zinafanana na mkubwa kitu kinachotofautiana na aina za processor

Oppo Find X7 inatumia processor ya Dimesnity 9300

oppo find x7

Hata Chip ya mediatek dimensity 9300 na Snapdragon 8 gen hazina tofauti kihivyo kiutendaji

Na kwa mtumiaji yeyote anaweza asione tofauti

Sifa zingine zote kuanzia betri, kioo na chaji zipo sawa na Find X7 Ultra

7. OPPO A59

Bei ya OPPO A59: 450,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM:  6GB

Oppo A59 ni simu ya daraja la kati ambayo haina vitu vingi vizuri kama simu zilizotangulia

Hii simu iliingia sokoni mnamo mwezi desemba mwaka 2023

Kwa mpenzi wa oppo za bei nafuu huu ndio mbadala

oppo a59

Kikubwa ambacho ni kizuri ni chaji ya wati 33 na uwepo wa kioo chenye refresh rate

Ni simu nzuri kama hujari sana ubora wa kamera

Utendaji wake ni wa wastani kwani chip yake ni Dimensity 6020 ambayo haina nguvu kama dimensity 9300

8. OPPO Pad Air2

Bei ya OPPO Pad Air2: 500,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM:  6GB

Hii ni tablet(kishkwambi) chenye ukubwa wa inchi 11.4

Haina sehemu ya kuweka laini ya simu hivyo ukitaka kuunga intaneti itakulazimu kuunga wifi

opo pad air2

Kwa maana sio kishikwambi kwa ajili ya kupiga simu

Utendaji wake sio mkubwa ni wa wastani na inatumia processor ya Mediatek helio G99 kufanya kazi zake

Betri yake na yenyewe ni kubwa ina mAh 8000 inayoifanya simu kukaa na chaji masaa mengi

9. OPPO A2

Bei ya OPPO A2: 500,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM:  6GB

Simu ya OPPO A2 ni simu nyingine iliyotoka mwishoni mwa mwaka 2023

Hii simu ina kamera mbili, ila moja tu ndio inatoa picha nzuri

oppo a2

Inatumia processor yenye nguvu ya wastani hivyo utendaji wake sio mkubwa

Chaji yake inasapoti umeme wa wati 33 kama ilivyo kwa OPPO nyingi za siku hizi

Ukubwa wa betri ni 5000mAh

10. OPPO A79

Bei ya OPPO A79: 550,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM:  8GB

Oppo A79 na yenyewe iliingia sokoni mwishoni mwa mwaka 2023

Ni simu ya daraja la kati inayospaoti mtandao wa 5G

oppo a79

Inatumia chip ya Dimensity 6020 katika kufanya kazi zake

Pia chaji yake inapeleka umeme wa wati 33 unaoweza kujaza simu kwa asilimia mia moja kwa DAKAIKA 80

Ubora wa kamera yake ni wa kuridhisha pia

11. OPPO Find N3

Bei ya OPPO Find N3: 5,000,000/= ,Ukubwa wa Memori: 512GB, RAM:  12GB

Kwa kuangalia bei ya simu tayari unapata picha ubora wake ukoje

Hii ni simu ya kukunja na kukunjua na kioo chake cha LTPO Amoled

Kamera zake zote ni nzuri katika upigaji wa picha

oppo find n3

Betri yake ina ukubwa wa wasatani wa 4800

Chaji ina kasi yakujaza simu kwa muda mfupi kutokana na kupeleka umeme wa wati 67

Inahitaji uwe na bajeti nzuri kununua simu ya milioni tano

12. OPPO A2X

Bei ya OPPO A2X: 400,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM:  6GB

Oppo A2X ndio oppo ya bei nafuu na ndogo kwenye orodha iliyopo

Inatumia chip ya dimensity 6020 kama ilivyo kwa matoleo mengine ya adaraja ya kati ya oppo kwa mwaka 2023 na mwaka 2024

Kwa bahati mbaya kamera yake sio ya kuvutia sana kama ilivyo oppo zingine za hapa tofauti na vishikwambi

-oppo a2x

Pia chaji inapeleka umeme kidogo ukilinganisha na oppo zote zilizopo kwenye orodha

Ni simu inamfaa mtu asiehitaji mambo mengi sana

Kumbuka: bei za simu zinabadilika kutokana na mambo mbalimbali, si lazima bei unayoiona hapa ikawa kama ilivyo kwa nyakati zote

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

simu mpya

Simu mpya kali 20 na bei zake kwa mwaka 2024

Hii ni orodha ya simu mpya ambazo zimetoka mwaka 2024 ama mwishoni mwa mwaka 2023 kutoka kwa kampuni zipatazo 11 Ni orodha inayohusisha simu za daraja la kati na la […]

No Featured Image

Bei ya sasa ya Oppo A17K na Sifa Zake

Oppo  A17K ni simu iliyotoka mwishoni mwa mwaka 2022 mnamo mwezi oktoba Ni simu ya daraja nafuu ambayo haihitaji bajeti kubwa kuimiliki Kwani bei ya oppo A17K haizidi laki tatu […]

iphone feki 2

Simu Origino ni Zipi na Unazitambuaje? (Hatua za kufuata)

Matoleo ya simu yamekuwa yakitoka mara kwa mara yakiwemo yenye bei kubwa na zinazotamaniwa na watu wengi Aina hizi ya simu huvutia watu wasio waaminifu kutengeneza simu feki zenye ufanano […]

oppo find x6 pro thumbnail

Oppo Yenye Kamera Nzuri na Ubora wa Picha

Kuna matoleo mengi ya simu za oppo zenye ubora tofauti tofauti Zipo ambazo zina ubora wa kati, wa juu na wa chini Katika hizo, nyingi zinajitahidi kuwa na kamera zinazotoa […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram