Hii ni orodha ya simu mpya ambazo zimetoka mwaka 2024 ama mwishoni mwa mwaka 2023 kutoka kwa kampuni zipatazo 11
Ni orodha inayohusisha simu za daraja la kati na la juu
Hivyo basi bei zake sio ndogo kwa maana inahusisha simujanja zinazouzwa kwa zaidi ya laki sita
Ipo pia orodha ya mwaka 2023 ya simu za bei rahisi zenye kamera nzuri
TWENDE KAZI
1. Sony Xperia 5 V
Bei inayouzwa: 2,100,000/=, ukubwa ni : GB 256, RAM GB 8
Sony Xperia 5 V kwa mara ya kwanza iliwekwa wazi mwezi septemba 2023
Bado ni simu mpya upande wa Sony japo inatumia processor ya Snapdragon 8 Gen 2
Ina kamera mbili za ultrawide na wide ambazo zote zinapuga picha kwa ufanisi mzuri
Betri yake ujazo wake ni 5000mAh na chaji ina kasi ya 30W
2. Samsung Galaxy S24 Ultra
Bei inayouzwa: 3,500,000/=, ukubwa ni : GB 256, RAM GB 12
Utendaji wa Samsung Galaxy S24 Ultra ni mkubwa sana kwani inatumia processor yenye nguvu ya Snapdragon 8 Gen 3
Hii simu imetoka mnamo mwezi januari 2024
Inatarajiwa kuwa ndio simu bora kwa mwaka huu kutokana na uwepo wa mambo mengi ya akili bandia(Artificial Intelligence)
Tembele hapa, uwezo na ubora wa Samsung Galaxy S24 Ultra
3. Samsung Galaxy S24+
Bei inayouzwa: 2,500,000/=, ukubwa ni : GB 256, RAM GB 12
Ina jumla ya kamera zipatazo tatu na zote zinapiga picha nzuri
Utendaji wake na wenyewe ni mkubwa kwani inatumia chip yenye nguvu kwa kila kazi
Betri inakaa na chaji muda mrefu tu kwani ina ukubwa wa 4900mAh
Chaji inapeleka kasi ya wati 45
4. Redmi Note 13 Pro+
Bei inayouzwa: 930,000/=, ukubwa ni : GB 256, RAM GB 12
Redmi Note 13 Pro+ ina utendaji wa kuridhisha kwa sababu chip iliyotumika ya MediaTek Dimensity 7200 zina core zenye muundo wenye kusukuma kazi tano kwa mzunguko mmoja kati ya mizunguko bilioni mbili kwa sekunde
Japokuwa utendaji wake unaachwa kwa mbali na Snapdragon 8 gen 3 ila ni chip nzuri pia kwenye utendaji
Hii simu pia imetoka septemba mwaka 2023, lakini bado ni toleo jipya upande wa simu za note
5. Xiaomi 14 Pro
Bei inayouzwa: 1,800,000/=, ukubwa ni : GB 256, RAM GB 12
Xiaomi 14 Pro inaweza ikawa ni mbadara mzuri wa Samsung Galaxy 24 Ultra
Maana sifa kwenye utendaji, kioo, na betri zinafanana
Moja ya kitu utakachofulia kwenye Xiaomi 14 Pro ni kasi yake ya kuchaji inayofika wati 120
Hii inaweza jaza betri ndani ya dakika thelathini kwa 100% toka zero
6. iQOO 12
Bei inayouzwa: 1,600,000/-, ukubwa ni : GB 256, RAM GB 12
Jina la hii simu linaweza kuwa gani masikioni mwa wa Tanzania wengi
Ila simu za iQOO huwa ni nzuri na kampuni ambayo ni tawi la vivo
Utendaji wa iQOO hautofautiani na Xiaomi 14 Pro kwani na yenyewe inafanya kazi kwa kutumia processor ya Snapdragon 8 Gen 3
Kioo chake na chenyewe ni cha LTPO AMOLED kama ilivyo kwa simu zingine za matoleo ghari
7. iQOO 12 Pro
Bei inayouzwa: 1,800,000/=, ukubwa ni : GB 256, RAM GB 12
iQOO 12 Pro ni kaka mkubwa wa iQOO 12
Hii simu inapeleka chaji kwa umeme mkubwa wa wati 120
Hivyo ndani ya nusu saa betri linaweza kujaa kikamilifu
Pia Snapdragon 8 Gen 3 ndio imetumika kama processor kwenye simu ya iQOO 12 Pro
8. Asus Rog Phone 8 Pro
Bei inayouzwa: 3,400,000/=, ukubwa ni : GB 512, RAM GB 16
Katika hii ordha hii ndio simu yenye bei kubwa zaidi
Kisifa, inafanana na simu zingine zilizotangulia kwani inatumia processor ya Snapdragon 8 Gen 3
Utofauti ambao Asus Rog Phone 8 Pro imejiwekea ni ukubwa wa RAM ambayo ni GB 16.
Ina betri yenye ukubwa wa 5500mAh na Chaji yenye kasi ya wati 65
Kamera zake zipo tatu na nzuri kiasi chake
9. Asus Rog Phone 8
Bei inayouzwa: 2,500,000/=, ukubwa ni : GB 256, RAM GB 16
Hii simu na yenyewe utendaji wake ni mkubwa kwani inatumia Snapdragon 8 Gen 3
Kioo chake ni cha LTPO Amoled kama ilivyo kwa simu nyingi za bei kubwa
Kamera zake zinaweza kurekodi mpaka video za 8K ambayo ni resolution kubwa inayohitaji simu yenye uwezo mzuri kurekodi
Betri yake ukubwa ni 5500mAh na kiwango cha kasi ya kuchaji ni wati 65
10. Tecno Spark 20 Pro+
Bei inayouzwa: -, ukubwa ni : GB 256, RAM GB 8
Hii ni simu nyingine ya daraja la kati ambayo imetoka desemba 2023
Hivyo ni simu ambayo ipo kwenye trendi kwa mwaka 2024
Kioo chake ni cha aina ya amoled chenye refresh rate ya 120Hz
Utendaji wake ni wa wastani unaoweza kidhi vitu kwa ustadi
11. Tecno Phantom V Flip
Bei inayouzwa: 1,500,000/=, ukubwa ni : GB 256, RAM GB 8
Simu ya Tecno Phantom V Flip ni simujanja kukunja na kukunjua
Ubora wake umejikita kwenye kwenye utendaji , kioo cha amoled na kasi kubwa ya kuchaji simu
Ina jumla ya kamera mbili tu zenye lenzi za ultrawide na wide
Betri yake si kubwa kutokana na udogo wa simu kwani ina 4000mAh
12. Infinix Hot 40 Pro
Bei inayouzwa: 450,000/=, ukubwa ni : GB 256, RAM GB 8
Infinix Hot 40 Pro ndio simu ya bei nafuu zaidi kwenye hii orodha
Ni simu ya daraja la kati na utendaji wake ni wastani kwani inatumia chip ya Mediatek Helio G99
Kamera zake ni za kawaida japo zinaendana na bei ya simu kiujumla
Unaweza ifuatilia kiundani hapa: Ubora na bei ya infinix hot 40 pro
13. Oppo Find X7 Ultra
Bei inayouzwa: 2,300,000/=, ukubwa ni : GB 256, RAM GB 12
Oppo Find X7 Ultra ni moja ya simu bora kwa mwaka 2024 inachuana na simu za iPhone na matoleo ya Samsung S24
Idara yake ya kamera iko kamili sana kwenye kamera zake zote nne
Kioo chake ni cha LTPO AMOLED ambacho kimetumiwa na matoleo mengi ya daraja la juu
Betri ni kubwa kwa ujazo wa 5000mAh
14. Oppo Find X7
Bei inayouzwa: 2,300,000/=, ukubwa ni : GB 256, RAM GB 12
Oppo Find X7 ni moja ya simu yenye kamera kali na nzuri kwa mwaka 2024
Inatumia processor yenye nguvu kubwa ya kiutendaji ambayo ni Mediatek Dimensity 9300
Kioo chake kina vikorombwezo vyote vinavyoboresha muonekano wa vitu, ikizingatiwa ni cha aina ya LTPO AMOLED
Kama ilivyo kwa simu nyingi kuwa na betri ya 5000mAh, na hii pia ina ukubwa huo
15. Vivo V30 Lite
Bei inayouzwa: 1,300,000/=, ukubwa ni : GB 256, RAM GB 8
Vivo V30 Lite ni simu aina ya daraja la kati iliyotoka desemba 2023 yaani ina miezi miwili tangu iingie sokoni
Utendaji wake sio mkubwa ni wa wastani kwani inatumia chip ya Snapdragon 695 5G
Kamera zake zipo tatu ikiwemo ya Ultrawide
Kioo chake ni kizuri pia ambacho ni amoled chenye refresh rate kubwa
Betri yake ni kubwa ila haifiki 5000mAh bali ni 4800mAh
16. Vivo Y100
Bei inayouzwa: 800,000/=, ukubwa ni : GB 128, RAM GB 8
Vivo Y100 ilingia rasmi sokoni februari ya mwaka 2024
Hii simu inatumia processor ya Snapdragon 4 Gen 2 ambayo ina core zenye kubwa za wastani zipatazo mbili
Simu ina idadi ya kamera mbili aina za wide na ultrawide
Betri yake na yenyewe ni kubwa kama ilivyo kwa simu zingine, ukubwa wake ni 5000mAh
17. Huawei Nova 12 Ultra
Bei inayouzwa: 1,800,000/=, ukubwa ni : GB 512, RAM GB 12
Huawei Nova 12 Ultra imetoka mwezi wa kwanza 2024
Utendaji wake unategemea processor iliyoundwa na Huawei wenyewe ya Kirin 9000S ambayo imewafanya USA kubaki midomo wazi
Pitia hapa kujua kwa nini: Hatua kubwa imepigwa na Huawei
Betri yake ni 4600mAh na idadi ya kamera ni mbili
18. Huawei Nova Y72
Bei inayouzwa: 1,600,000/=, ukubwa ni : GB 128, RAM GB 8
Hii ni simu inayotumia mfumo wa HarmonyOS 4.0
Soko kubwa la hii simu ni china kwa maana kuna baadhi ya apps za google hazifanyi kazi kwenye hii simu
Utendaji wake wa wastani kwani inatumia chip ya Kirin 710A yenye Cortex ya kitambo kutokana na vikwazo
Betri yake ina ukubwa wa 6000mAh na kamera zake zipo mbili tu
19. Google Pixel 8 Pro
Bei inayouzwa: 1,600,000/=, ukubwa ni : GB 128, RAM GB 12
Google Pixel 8 Pro ni simu ya kwanza kuja na Android 14 Oktoba 2023
Bado ni simu nzuri sana na shindani kwa mwaka 2024
Utendaji wake wa kuridhisha unachagizwa na kutumia chip ya Google Tensor G3
Betri ina ujazo wa mAh 5050 ambayo ni kubwa tu
Pia kioo aina ya LTPO OLED chenye refresh rate ya 120, kioo kizuri kiujumla
20. OnePlus 12
Bei inayouzwa: 2,400,000/=, ukubwa ni : GB 512, RAM GB 16
OnePlus 12 iliingia rasmi mwishoni mwa mwaka 2023
Utendaji wa hii simu ni mkubwa na unaendana na kwa kiasi fulani na Samsung Galaxy S24
Ukubwa wa betri ni 5400mAh ambayo inaweza kukaa na chaji masaa zaidi ya kumi hata ukiwa unacheza gemu
Kioo chake ni cha ltpo amoled na kamera zake zipo tatu
Maoni 23 kuhusu “Simu mpya kali 20 na bei zake kwa mwaka 2024”
Simu ya laki mbili
Zipo ila sio nzuri kama hizi
Xm ya laki 3
Za Redmi ama Oppo tazama hapa https://simunzuri.com/simu-mpya-za-redmi-2024/
Samsung
samsung a05
Me nahitaji Infinix hot 40po ya mkopo ila Nina laki2 ya kianzio.
Asanteni kwa kututangazia bithaa
Napo nina swali kidogo
Ninaweza pata simu mpya iliyo toka mwezi huu yaani isizidi mwezi mmoja kutoka kiwandani?
Inawezekana
Hongereni kwa kutujuza
mmmmmmmh ni balaa me nataka sony xperia ila ntalipa milion mbili af nyingine ntalipa kidogo dogo sijui kama itawezekana?
Unapatikana wapi
NATAKA SIMU 2 KWA MKOPO SAMSUNG S24 UTLRA NA SAMSUNG FLIP 6 AU 5
NAOMBA NIJIBIWE NA NAISHI MOROGORO MJINI NAMBA YA YA SIMU 0655546474
Nakubali
Mko vizuri
Nahitaji pixel 6
Simu nzuri ya original ya kununua ni ipi mkuu
Inategemea na bajeti
Trevour plz nitafte 0753058280
A14 128 5g zipo bei gani?
How much for infinix note 11 pro ?
You can reply through whatsApp sms via 0755220741