SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Huawei Mate 60 Pro Pigo kwa Marekani?

Brand

Sihaba Mikole

September 7, 2023

Kama ni mfuatiliaji wa habari za teknolojia utakuwa unafahamu vikwazo vya Marekani dhidi ya huawei

Huawei kutoka china imekuwa na wakati mgumu wa kutumia teknolojia mbalimbali zenye mafungamano na marekani

Kwani USA inaishutumu huawei kuwa na mafungamano na serikali ya China

uawei mate 60 pro showcase

Kitu ambacho kimeinyima kampuni hiyo kubwa ya simu teknolojia muhimu kwa ajili ya kutengeneza simu za kisasa zinazokidhi mahitaji ya wateja wengi

Kwa muda mrefu huawei imeshindwa kutengeneza simu zenye 5G

Chip zilizoruhusiwa kuuziwa huawei ni zile za 4G, na China chip za 5G zinatoka nje

Ila simu mpya ya Huawei Mate 60 Pro inakuja na uwezo wa 5G

Processor ya huawei mate 60 pro

Kampuni nyingine ya China ambayo ipo kwenye kaa la moto la USA ni SMIC

SMIC ni kampuni inayotengeneza chip(processor)

Yenyewe imeuzuliwa kununua mashine zinatumika kutengeneza chip zenye uwezo mkubwa zaidi

Ni kampuni moja tu duniani tena kutoka Uholanzi inayoitwa ASML

Machine za asml zinahusisha vifaa vingi vinavyoundwa kutoka nchi mbalimbali ikiwemo marekani

Kwa maana hiyo hata ASML inabidi afuate masharti ya taifa lenye uchumi mkubwa zaidi duniani

Hata hivyo safari hii SMIC wamefanakiwa kutengeneza chip ya 5g na processor ya muundo wa 7nm bila kutumia vifaa vya ASML

Wameunda processor ya Kirin 9000S kwa kutumia teknolojia ya zamani ya DUP

Wachambuzi wanasema chip kuundwa kwa mtindo huo kutafanya gharama kuwa mara 100 ya chip zinazoundwa kwa vifaa vya kisasa.

Kupiga Simu kwa setilaiti

Simu ya iPhone 14 Pro Max ina uwezo wa kutuma meseji kwa njia ya setilaiti

Ila Huawei Mate60 Pro inapiga na kutuma sms kwa njia ya setilati

Setilaiti inasaidia ukiwa upo eneo ambalo mitandao ya simu haipatikani

Ni njia ya dharura kwa sababu mawasiliano kwa njia ya setilaiti hayana kasi ya kuridhisha japo setilaiti inaweza kukava eneo kubwa

Hivyo kama upo eneo lenye ukosefu wa network huawei mate inaweza kukusaidia bila shida

Wireless chaji yenye kasi

Kuchaji bila kutumia waya kwenye simu nyingi kasi yake huwa sio kubwa

Kwenye huawei mpya kasi inafika mpaka 20W

Hii ni kasi kubwa kwani kuna baadhi ya simu nyingi zinapeleka chaji ya waya kwa kasi ndogo

Wati 20 inaweza kuchaji simu kwa muda mfupi.

Hitimisho

Tutaingazia hii simu kiundani kwenye post yake nyingine kwa maana ndio imetoka hivi karibuni

Uwepo wa huawei yenye chip ya 5G kunatengeneza maswali mengi juu ya vikwazo mbali mbali ambavyo marekani imekuwa ikiviweka kwa china.

Je vikwazo vya marekani vinaipa nchi na nafasi ya kuwa wabunifu zaidi?

 

Maoni 2 kuhusu “Huawei Mate 60 Pro Pigo kwa Marekani?

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

[VIDEO]: Simu bora duniani na bei zake 2024

Huu ni muendelezo mwingine wa simu tano ambazo hazitumikii sana na watanzania. Lakini kiulimwengu ni kati ya simu bora duniani kwa mwaka 2024. Hizi ni simu zenye utendaji mkubwa kwenye […]

Simu bora duniani na bei zake 2024

Leo tuzungumzie kuhusu simu bora duniani na bei zake kwa mwaka 2024 Kuna matoleo mapya ya simu kali yenye ubora wa kiutendaji na wenye nguvu madhubuti katika maeneo mengi Ubora […]

google pixel fold thumbnail

Ubora na bei ya simu mpya ya Google Pixel Fold

Fold ni aina ya simu za kujikunja. Kwa muda mrefu makampuni ya Samsung, Huawei na Oppo wamekuwa wakitengneza simu za aina hii Hivi karibuni tecno na pixel pia zimeingia katika […]

No Featured Image

Bei ya Simu mpya ya Sony Xperia 1 V na Sifa Zake

Sony, kampuni ya japan imeachia toleo lingine jipya la xperia mwezi julai 2023 Toleo hilo ni Sony Xperia 1 IV ambalo ni la daraja la juu kwenye makundi ya simu […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company