SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Simu mpya ya Sony Xperia 1 V na Sifa Zake

Simu Mpya

Sihaba Mikole

August 1, 2023

Sony, kampuni ya japan imeachia toleo lingine jipya la xperia mwezi julai 2023

Toleo hilo ni Sony Xperia 1 IV ambalo ni la daraja la juu kwenye makundi ya simu

Hivyo bei ya sony xperia kwa hapa Tanzania inazidi milioni mbili

Vitu vingi vya hii simu ni vya viwango vikubwa ndio maana bei yake ni ya juu

Utalielewa ukifutilia sifa zake na ubora wake ulioelezwa hapa

Bei ya Sony Xperia 1 V ya GB 512

Sony Xperia 1 V yenye ukubwa wa GB 512 inauzwa shilingi 3,300,000

Yaani milioni tatu na laki tatu

Hii bei ni kubwa kuliko hata simu za samsung na iphones

Lakini sony hulenga watu wanaoitumia simu kwa matumizi mengine ya ziada yanayousiana na kazi

Kwa mfano kwenye kamera kuna mambo ya ziada yameongezwa ambayo hayapo kwenye simu nyingine

Kamera zake zina vitu ambavyo mpiga picha vinamfaa kwa mfano ni teknolojia ya kuzoom

Sifa za Sony Xperia 1 V

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
 • CPU – Snapdragon 8 Gen 2
 • Core Kubwa Zaidi(1): 1×3.2 GHz Cortex-X3
 • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.8 GHz Cortex-A715
 • Core Za Wastani(2) – 2×2.8 GHz Cortex-A710
 • Core Ndogo(3)-3×2.0 GHz Cortex-A510
 • GPU-Adreno 740
Display(Kioo) OLED, Refresh rate:120Hz
Softawre
 • Android 13
Memori UFS ,256GB,512GB na RAM 12GB
Kamera Kamera tatu

 1. 48MP,Dual pixel PDAF(wide)
 2. 12MP, dual pixel pdaf(ultrawide)
 3. 12,dual pixel pdaf(Telephoto)
Muundo Urefu-6.5inchi
Chaji na Betri
 • 5000mAh-Li-Po
 • Chaji-30W
Bei ya simu(TSH) 3,300,000/=

Upi ubora wa Sony Xperia 1 V

Sony Xperia 1 V ina mfumo wa kamera unaojtahidi kwa kiwango kikubwa kupiga picha zinazoendana muonekano halisi wa kitu

Simu ina nguvu kubwa ya kiutendaji kutokana na kutumia chip yenye nguvu kutoka snapdragon

Ni simu ya 5G

Ina kioo chenye uwezo wa kuonyesha rangi nyingi kitu kinachochangia kufanya muonekano sahihi bila kupoteza uhalisia wa rangi

Ukaaji wa chaji pia ni wa kuridhisha japo si wa kiwango kikubwa sana kama kwenye iphone 14 pro max

Ni simu yenye uwezo wa kiwango cha kuzuia maji kupenya ndani ya simu

Pia itapokea matoleo mapya kwa siku za mbeleni

Kiujumla hii sony mpya 2023 ina ubora kwenye vipengele vingi vinavyochangia bei ya simu kuwa kubwa

Uwezo wa network

Simu inasapoti mitandao ya aina yote ikiwemo 5G

Ina masafa mengi yakiwemo yanayotumiwa na makampuni ya simu nchini

Kwa waliopo dar es salaam hasa maeneo ya mjini 5G ya voda ipo

Hivyo unaweza ukanufaika na kasi kubwa ya intaneti kutumia hii simu

Aina ya 4G inayotumika na hii simu ni LTE Cat 24 yenye kasi inayofika 10000Mbps sawa na 1250MBps

Hii inamaanisha kama unapakuwa kitu cha GB 1 simu itamaliza kudownload ndani ya sekunde moja

Hata hivyo, hii spidi haipo hapa Tanzania, muhimu ni kuwa uwezo wa intaneti wa sony ni mkubwa

Ubora wa kioo cha Sony Xperia 1 V

Kioo cha sony ni cha OLED chenye resolution ya 1644×3840 pixels

Kwa maana ni kuwa muonekano wa vitu unaonekana vizuri bila kupoteza ubora wake

Labda tu kama picha au video imerekodiwa na kamera yenye ubora mdogo

Mbali na hilo kioo kina refresh rate inayofika 120Hz

Refresh rate kubwa inafanya kioo kuwa kilaini wakati wa kutachi hakuna kuganda ganda

Ni kitu kingine kizuri ni kwamba kioo chake kina hdr2020

Kitu kinachoengeza ukubwa wa rangi

Na hivyo kuongeza ubora wa jinsi skrini inavyoonyesha vitu

Nguvu ya processor ya Snapdragon 8 gen 2

Sony Xperia V 1 inatumia processor ya snapdragon 8 gen 2 iliyotoka mwaka 2022

Hii chip ina ufanisi mkubwa kwenye matumizi ya chaji na uwezo wa kusukuma app zinazotumia nguvu kubwa

Kwa mfano magemu makubwa kama ya PUBG Mobile yanacheza kwa kiwango cha 90fps

Gemu inayocheza kwa fps huwa na muonekano mwororo

Na jinsi gemu inavyocheza ni kama vile unarekodi video

Hii inamaanisha simu haiwezi kukumbwa na tatizo la kuganda ganda ama kuwa nzito

Nguvu yake inatokana na kutumia mgawanyo uliojitawanya katika sehemu nne

Huku sehemu yenye nguvu sana ikitumia muundo wa Cortex X3

Uwezo wa betri na chaji

Ukubwa wa betri ya sony i v ni 5000mAh

Kwenye makaratasi simu inapaswa ikae na chaji masaa mengi

Ila ukiwa unaperuzi intaneti inachukua masaa 13 betri kuisha

Ukilinganisha na betri ya iphone 14 pro max ambayo betri yake ni dogo, sony inakaa na chaji masaa machache

Kasi yake ya chaji inapeleka umeme wa 30W

Ambayo inajaza chaji kwa 50% baada ya dakika 30

Hivyo simu inaweza kuchukua mpaka dakika 70 kujaa kwa asilimia 100 kutoka zero

Maana chaji nyingi zenye kasi ya 30W hujaza simu kwa masaa hayo

Mfano redmi note 10 chaji yake kasi yake ni kama ya sony na simu inajaa kwa 100 baada ya dakika 70

Ukubwa na aina ya memori

Kuna matoleo mawili ya sony kwenye upande wa memori

Kuna ya GB 256 na GB 512

Bei zake hazitofautiani sana na zote zina RAM ya GB 12

RAM kubwa inatoa nafasi kubwa ya kufungua vitu vingi kwa wakati mmoja mfano magemu

Kwa mpenzi wa kucheza magemu mengi ram ni muhimu kuwa kubwa

Baadhi ya magemu hujaza ram kitu kinachoweza sababisha simu kuwa nzito kiutendaji

Jambo zuri ni kuwa mfumo wa memori unaotumika ni UFS

Ambayo kasi yake ni kubwa katika kusafirisha data

Uimara wa bodi ya Sony Xperia 1 V

Bodi ya Sony Xperia 1 V haipitishi maji iwapo simu ikizama kwenye kina cha mita 1.5

Yaani kama unachukua ndoo ya maji iliyojaa na ukazamisha simu, maji hayatoingia hata ukiiacha kwa muda wa nusu saa

Ni ishara kuwa bodi yake ni ngumu

Kwenye kioo imewekwa skrini protekta Gorilla Glass Victus 2

Kampuni ya gorilla inadai kuwa vioo vyake vyake  vya aina hii ni vigumu kupasuka na kuchubuka hata simu ikianguka kwa kimo cha mita 2 toka juu

Hata hivyo, swala la kioo kupasuka inategemea sana na uso wa eneo simu ilipoangukia na aina ya madini

Ubora wa kamera

Sony Xperia 1 V ina jumla ya kamera tatu ambazo zina lenzi za wide, telephoto na ultrawide

Bila kuzama kiundani, uwepo wa dual pixel pdaf kwenye kila kamera inaonyesha wazi kuwa simu kamera zake ni nzuri.

Kwenye ubora wa picha, kamera kubwa ina usahihi wa rangi na muonekano wa vitu unaondana muonekano kwenye mazingira halisi

Hata picha ya megapixel 12 ukiikuza ikawa kubwa bado vitu vinaweza kuonekana kwa uzuri na kwa kutambulika

Nyakati za usiku pia muonekano wa vitu ni mzuri

Kiwango cha noise ni kidogo sana kiasi cha kwamba kiza kikubwa hakiiathiri sehemu zenye mwanga hafifu kutoonekana

Upande wa video simu inaweza kurekodi za 4K kwa kiwango mpaka cha 120fps na kwa hdr

Ila kitu cha kutia akilini aina hii ya video inachukua memori ya simu

Ubora wa Software

Sony Xperia 1 V inatumia mfumo endeshi wa Android 13

Sony huwa haina mifumo mingine ya ziada kama ilivyo kwa makampuni mengine

Hata hivyo android 13 bado ina vitu vyote vya muhimu vinavyohitajika na mtumiaji wa simu

Na pia simu itapokea toleo jipya la android 14 pindi likitoka rasmi

Washindani wa Sony Xperia 1 V

Washindani wakubwa wa sony xperia 1 v ni simu zote zilizopo daraja juu

Baadhi ya washindani hao ni iPhone 14 Pro Max ambayo ina simu mpaka ya 1TB na ukaaji wake chaji ni mkubwa kuliko sony

Wakati huo bei ya iphone ni ndogo ukilinganisha na sony

Mshindani mwingine ni Xiaomi 13 Ultra

Xiaomi 13 Ultra ina kamera zenye kila kitu unachokiona kwenye sony

Kizuri zaidi ni kuwa xiaomi 13 ultra inaweza kurekodi mpaka video za 8K

Na chaji yake inaweza kujaza simu kwa 100% ndani ya dakika 35

Hata bei yake ni nafuu kwani inauzwa kwa kiasi cha shilingi milioni 2.8 ya 1TB

Kiuhalisia simu ipo kwenye kipengele kigumu kinachohusisha kampuni zinazotengeneza simu kali

Neno la Mwisho

Kwa mwaka 2023 sony ni aina nyingine ya simu bora iliyopo sokoni

Inawafaa watu wa aina mbalimbali ikiwemo wanaotumia simu katika majukumu ya kikazi pia

Bei yake ni kubwa na inaipeleka simu kwenye ushindani mkubwa

Maoni 2 kuhusu “Bei ya Simu mpya ya Sony Xperia 1 V na Sifa Zake

 • kwa details hizo simu za sony xperia zina ubosa, ila makapuni mengi huwa wanaanza kuchakachua baada ya kuaminika kwa muda mrefu kwa kutoa vitu original. sasa je naweza kuagiza sony xperia 512GB na kwa utaratibu upi?

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

[VIDEO]: Simu bora duniani na bei zake 2024

Huu ni muendelezo mwingine wa simu tano ambazo hazitumikii sana na watanzania. Lakini kiulimwengu ni kati ya simu bora duniani kwa mwaka 2024. Hizi ni simu zenye utendaji mkubwa kwenye […]

OnePlus 11R

Simu 15 za OnePlus na Bei zake (Aina zote)

OnePlus inaweza ikawa ni jina geni kwa watumiaji wengi smartphone Tanzania Ila OnePlus ni moja ya kampuni kutoka china inayotengeneza simujanja za madaraja ya kati na ya juu Simu nyingi […]

simu mpya

Simu mpya kali 20 na bei zake kwa mwaka 2024

Hii ni orodha ya simu mpya ambazo zimetoka mwaka 2024 ama mwishoni mwa mwaka 2023 kutoka kwa kampuni zipatazo 11 Ni orodha inayohusisha simu za daraja la kati na la […]

huawei mate60 pro

Huawei Mate 60 Pro Pigo kwa Marekani?

Kama ni mfuatiliaji wa habari za teknolojia utakuwa unafahamu vikwazo vya Marekani dhidi ya huawei Huawei kutoka china imekuwa na wakati mgumu wa kutumia teknolojia mbalimbali zenye mafungamano na marekani […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company