SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Simu za chini ya laki mbili na nusu zenye unafuu kiutendaji

Bei Nafuu

Sihaba Mikole

December 7, 2024

Hii ni orodha ya baadhi ya simu za laki mbili na nusu kwenda chini zilizotoka miaka ya karibuni

Simu nyingi zenye ubora wa wastani mara nyingi huanzia laki tatu kwenda juu

Ila asilimia kubwa ya simu zinazouzwa chini ya laki tatu huwa na ubora mdogo kwa ajili ya matumizi ya kawaida

Kwa maana usitarajie vitu vikubwa sana ikiwemo kamera

Hizi ni baadhi ya simu za bei rahisi ambazo zina unafuu kiutendaji japo sio sana

Tecno Pop 7  – Bei 240,000

Tecno Pop 7 ni simu ya mwaka 2023

Bei hii ni ile yenye ukubwa wa GB 64 na RAM GB 2

Ina kamera moja tu yenye megapixel 8 ikiwa na uwezo wa kurekodi video za full hd pekee

tecno pop 7

Utendaji wake ni mdogo na inatumia mfumo endeshi wa Android 12 Go edition

Ila kwa mtumiaji mwenye matumizi ya kupiga simu, kutokucheza gemu kubwa, sio mpenzi sana wa kamera, Tecno Pop 7 inaweza kidhi mahitaji yake

Na betri yake ni kubwa ina mAh 5000 ila chaji ina kasi ndogo ya wati 10

Tecno Pop 7 Pro – Bei 250,000

Kuna tofauti ndogo kati ya Tecno Pop 7 Pro na Tecno Pop 7

Tofauti hiyo ni kwenye ukubwa wa ram, kamera na mfumo wa software

Ambapo Pop 7 Pro RAM yake ni GB 3

RAM ya GB 3 imeifanya kutumia mfumo wa Android 12 wenyewe unaoambatana na HIOS 12

Kamera yake ni moja na ina 13MP ikiwa na uwezo wa kurekodi video za full hd pekee

Pia inatumia processor ya Helio P22 yenye nguvu ndogo

Infinix Smart 8 – Bei 240,000

Hii ni bei ya Infini Smart 8 ya GB 64

Kiutendaji hii ina unafuu sana kutokana na kutumia chip ya Unisoc T606

Kamera zipo mbili ila kubwa ina megapixel 13 na nyingine ndogo sana (megapixel 0.08)

3-infinix smart 8

Na yenyewe betri yake ina ukubwa wa mAh 5000 na chaji ina wati 10

Na uzuri  ni kwamba hii simu inatumia toleo la android 13 japo kwa sasa kuna android 15

Infinix Smart 8 Plus – Bei 250,000

Simu ya Smart 8 Plus ilitoka mwanzoni mwa mwaka 2024

Kamera yake ina sensa kubwa ila inaweza kurekodi video za full hd

Ukubwa wa kamera ni megapixel 50

infinix smart 8 plus

Na betri ya ni kubwa sana kutokana na kuwa na mAh 6000

Chaji inapeleka umeme mwingi kiasi wa wati 18

Pia simu inaruhusu reverse charging yaani unaitumia simu kama power bank

Itel A80 – Bei 235,000

Hii ni itel ya mwaka huu kabisa 2024 tangu mwezi wa novemba

Ina kamera moja ya ukubwa wa megapixel 50

Inarekodi video za full hd pekee

itel a80

Betri yake ina ukubwa wa mAh 5000 na chaji ya wati 10

Na inakuja na toleo la Android 14 tofauti na simu zingine zilizotangulia

Hii ni bei inayokupa itel a80 ya GB 128

Itel S18 – Bei 240,000

Itel S18 ni simu ya mwaka 2022

Ubora wake sio kama wa itel a80 katika maeneo mengi

itel s18

Simu ina kamera mbili, kubwa ikiwa na megapixel 8 zingine zikiwa ndogo zaidi

Betri yake ina ukubwa wa 5000mAh

Utendaji wake sio mkubwa kutokana na processor inayotumia

Wazo moja kuhusu “Simu za chini ya laki mbili na nusu zenye unafuu kiutendaji

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

iphone 16 pro

Kampuni bora za Simu duniani (2024/2025)

Pamoja na uwepo wa makampuni zaidi ya 100 ya kutengeneza simu bado kampuni zilezile zimeendelea kushika soko kwa sehemu kubwa duniani, kampuni hizo ni apple, samsung na xiaomi na nyinginezo. […]

huawei mate

Simu Bora 15 Duniani 2024 (na zitakazotamba 2025)

Kwa mwaka 2024, soko la simu janja yaani smartphone duniani lilitawaliwa na makampuni ya Apple, Samsung, Xiaomi, Vivo na Oppo Kwa hapa Afrika kampuni ya Samsung inaongoza kwa mauzo ikifuatiwa […]

infinix hot 50i thumb

Simu mpya za Infinix hot 50 na bei zake

Kuelekea mwishoni mwa mwaka Infinix imekuja na matoleo ya simu za Infinix Hot Hii post imeorosheshwa kwa ufupi simu 4 za infinix hot, moja ya infinix smart na ya zero […]

infinix hot 50i

Bei ya Infinix Hot 50i na sifa zake muhimu

Infinix hot 50i ilitangazwa mwezi septemba na kuingia sokoni rasmi mwezi oktoba 2024 Ni simu ya daraja la chini ila ina maboresho mazuri katika maeneo matatu kama utakavyoona Bei ya […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: 0756 077262 au 0683 420543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company