SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Simu Infinix Hot 10t na Sifa Zake (2022)

Sifa za simu

Sihaba Mikole

August 6, 2022

Simu ya infinix hot 10t ni simu ya daraja la kati ambayo imetoka mwaka 2021 mei

Utendaji wake ni wa kiwango cha wastani kulingana na aina ya processor iliyotumika

Bei ya Infinix Hot 10t inatofautiana kulingana na ukubwa wa memori lakini ni simu ya zaidi ya laki mbili na nusu

infinix hot 10t muonekano

Sifa zake zinaendana na bei kwa kiasi kikubwa

Lakini weka akilini baadhi ya vina ubora mzuri vingine vina ubora wa chini kama utakavyoona kwenye ufafanuzi uliopo

Bei ya Infinix Hot 10t ya GB 64

Bei halisi ya infinix hot 10t kwa maduka mengi ya Dar Es Salaam ni shilingi laki tatu (300,000)

Kwa kuangazia sifa zake bei ni shindani kwa kiasi kikubwa

infinix hot 10t summary

Kwa sababu hot 10t inaendana kiubora na Redmi 9A na Realme C3

Na bei za simu hizo mbili kwa Tanzania hazitofautiani sana

Na zina mapungufu katika sifa za upande wa kamera na memori

Sifa za Infinix Hot 10t

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – Mediatek Helio G70
  • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.0 GHz Cortex-A75
  • Core Za kawaida(6) – 6×1.7 GHz Cortex-A55
  • GPU-Mali-G52 2EEMC2
Display(Kioo) IPS LCD
Softawre
  • Android 11
  • XOS 7.6
Memori eMMC 5.1, 128GB,64GB na RAM 4GB
Kamera Kamera mbili

  1. 48MP,PDAF(wide)
  2. 2MP
Muundo Urefu-6.82inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
Bei ya simu(TSH) 300,000/=

Ni upi ubora wa simu ya Infinix Hot 10t

Ni simu inayokuja na betri kubwa inayokaa na chaji masaa mengi

Kioo chake kinatumia umeme mdogo kutokana na muundo wake

Memori yake inaruhusu kuhifadhi vitu vingi

Na hata RAM inatosheleza kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja

Simu ina utendaji unaoweza kufungua applikesheni nyingi kiurahisi

Ni simu ndefu inayompa mtumiaji uhuru wa kuona vitu kwa ukubwa

Pamoja na  uborahuo kuna baadhi ya vitu Infinix wamepunguzia ubora hii simu

Katika maelezo yaliyopo utaweza kufahamu mapungufu yake na nguvu yake kwenye nyanja kama nane hivi

Uwezo wa Network

Infinix Hot 10t ni infinix ya 4G

Na inatumia LTE aina ya LTE Cat 7

LTE Cat 7 ina spidi ya kudownload vitu inayofika 300Mbps

Kwa maana kama simu inapakua faili la ukubwa wa 1200MB, itachukuwa  sekunde 32 kumaliza

infinix hot 10t network

Kwa bahati mbaya mitandao mingi Tanzania haivuki kasi ya 100Mbps

Hivyo kwa mazingira ya nchini itakuwa ngumu kupata kasi hiyo

Japokuwa ni kasi ndogo ukilinganisha na Tecno yenye kamera nzuri

Ubora wa kioo cha Infinix Hot 10t

Kioo cha Infinix Hot 10t ni cha IPS LCD ambacho kina resolution ndogo ya 720 x 1640 pixels

Kitu kinachofanya simu kuwa na ubora wa wastani katika kuonyesha vitu

Simu ikiwa na resolution kubwa huwa inaonyesha vitu vizuri zaidi

infinix hot 10t display

Katika uonyeshaji wa rangi kwa usahihi IPS LCD huwa inaachwa nyuma na vioo vya AMOLED

Kama unaangalia sana picha za instagram utaona raha ukiwa na simu yenye amoled

Mfano mmoja wapo ni katika kuonyesha rangi nyeusi

IPS LCD huwa haionyeshi rangi nyeusi halisi

Nguvu ya processor Mediatek Helio G70

Infinix Hot 10t inatumia processor ya Mediatek Helio G70 katika kufanya kazi zake zote

Helio G70 ni processor yenye uwezao wa wastani inayoweza kucheza gemu nyingi bila tatizo

Nguvu yake inatokana na kutumika kwa muundo wa Cortex A75 kwenye core kubwa

Cortex A75 inafanya kazi kwa mizunguko ya 2.0GHz

infinix hot 10t processor

Hii inasababisha chip kupata alama nzuri kwenye app ya Geekbench

Geekbench 5 inaipa Helio G70 alama 391

Mediatek helio g70 haina ufanisi mkubwa kwenye kucheza gemu kwa resolution za juu

Inakulazimu kupunguza resolution ili simu icheze gemu kwa kuongeza idadi ya fremu kiasi

Gemu ya PUGB Mobile 2018 inacheza kwa resolution za chini na kwa fps chache ambazo ni 30fps

Uwezo wa betri na chaji

Simu ina betri yenye ujazo wa 5000mAh

Hii inamaanisha ina uwezo wa kukaa na chaji masaa mengi

Kiwastani, itachukua zaidi ya masaa 14 mpaka chaji kuisha kama utatumia intaneti pekee

Na betri inaweza kuisha baada ya masaa 11 kama utakuwa unacheza gemu muda wote

Hii simu haina chaji inayopeleka umeme mwingi kama Tecno Camon 19 Pro 5G

Hivyo chaji yake itachukua muda kujaza betri kubwa ya 5000mAh

Ukubwa na aina ya memori

Kwenye upande wa memori kuna Infinix Hot 10t za aina mbili

Ipo yenye ukubwa wa GB 64 na GB 128

Na zote zinatumia RAM ya ukubwa wa GB  4

Kwa bahati mbaya aina ya memori simu inayotumia ni eMMC 5.1

Aina za memori huwa zinachangia katika kuongeza utendaji wa simu

Hii inatokana na kasi ya kusafirisha data

eMMC 5.1 usafirishaji wake wa data hauzidi 600MBps

Wakati memori za UFS 2.1 inasafirisha data kwa kasi inayofika 1200MBps

Kasi hii huwa inafanya simu kufungua app kwa haraka

Uimara wa bodi ya Infinix Hot 10t

Bodi ya Hot 10t ni ya plastiki

Bodi za plastiki huwa si imara katika kuzuia kuchunika rangi

infinix hot 10t bodi

Ni muhimu kununua kava kwa ajili ya kuilinda rangi yake isipoteze ubora kwa kipindi kirefu

Kwenye screen kuna kioo cha kawaida na sio cha gorilla

Pia simu haina viwango vya IP vinavyotamburisha uwezo wa simu kuzuia maji na vumbi

Ubora wa kamera

Hii simu ina kamera mbili pekee ambapo kamera kubwa ina 48MP

Inatumia ulengaji wa PDAF ambao unaboresha ubora wa picha

Ila PDAF inapata shida kutoa picha nzuri nyakati za usiku tofauti na kamera yenye dual pixel pdaf

infinix hot 10t kamera

Ifuatilie: Ubora wa kamera ya Tecno Phantom X inayotumia dual pixel pdaf

Hot 1ot inaweza kurekodi video za full hd pekee kwa kasi 30fps

Haishangazi sana kutokana kiasi ambacho simu inauzwa

Ubora wa Software

Simu ya infinix hot 10t inakuja na android 11 na mfumo wa XOS 7.6

Kwenye XOS 7.6 kuna machaguo ya kuzuia baadhi ya vitu wakati wa kucheza gemu

Maana kuna mfumo unaoenda kwa jina la Game Zone

Game Zone inaruhusu kuzuia meseji na simu zinazopigwa

Hii inakusaudia kuwa bize na kucheza gemu kama hutaki usumbufu wakati huo

Kwenye multitask(kufungua app nyingi kwa wakati mmoja) xos 7.6 inakurahishia kazi hiyo

infinix hot 10t multitask

Kwani inaruhusu muundo unaofanya app iwe inaelea kwenye screen ndogo

Na hivyo inakupa nafasi ya kufungua app nyingine na kuweza kuzitumia zote mbili kwa wakati mmoja

Yapi Madhaifu ya Infinix Hot 10t

Simu ina kioo chenye resolution ndogo

Kamera yake ina kiwango cha kawaida

Haiwezo kurekodi video za 4K, na hata video za full hd inarekodi kwa fremu ndogo

Chaji yake inachukua muda mwingi kujaza betri

Ina memori yenye usafirishaji wa data mdogo kitu kinachoshusha utendaji wa simu

Simu haina viwango vya IP angalau IP53 inayoonyesha simu kuzuia  maji yanayotiririka

Utendaji wake si wa kiwango kikubwa sana ukilinganisha na Redmi 10C

Neno la Mwisho

Bei ya Infinix Hot 10t inaiweka simu katika kundi la simu nzuri za bei nafuu

Ukikutana na samsung yenye sifa sawa na hot 1ot basi tarajia bei inayoenda karibu laki nne

Ila sasa infinix inakuja na app nyingi ambazo nyingine hutotumia

Hizo app ndizo zinafanya simu kuwa na bei nafuu

Ila kiujumla simu ya infinix hot 10t ni ya kuwa kama una bajeti ndogo

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

infinix note 30 vip thumbnail

Bei ya Infinix Note 30 VIP na Sifa Zake

Infinix kwa mwaka 2023 wameachia matoleo mengi yakiwemo ya note series Moja ya toleo hilo ni Infinix Note 30 VIP ambayo imetoka mwezi Juni Haina tofauti sana na infinix note […]

infinix zero 30 5g thumbnail

Ubora na Bei ya Infinix Zero 30 5G (Infinix Kali)

Ni infinix kwa mara nyingine inajaribu kutengeneza hisia chanya juu ya ubora wa simu zao Unaweza kuliona hili kwa toleo jipya la Infinix Zero 30 5G Hii ni simu kali […]

iphone 15 pro thumbnail

Bei ya iPhone 15 Pro na Sifa Zake Muhimu

Kama ilivyotarajiwa hapo awali kuhusu ujio wa simu mpya za iphone kwa mwaka huu 2023 Moja ya simu hiyo ni iPhone 15 Pro ambayo imeongezewa utendaji Kiumuonekano hauwezi kutofautisha sana […]

iphone feki 2

Simu Origino ni Zipi na Unazitambuaje? (Hatua za kufuata)

Matoleo ya simu yamekuwa yakitoka mara kwa mara yakiwemo yenye bei kubwa na zinazotamaniwa na watu wengi Aina hizi ya simu huvutia watu wasio waaminifu kutengeneza simu feki zenye ufanano […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram