Simu ya vivo v23 5g ni android ya 5G ambayo imetoka mnamo januari ya 2022.
Kiuwezo vivo v23 5g inazidiwa na vivo v23 pro
Ila bei ya vivo v23 5g ni nafuu zaidi kwani inauzwa chini ya milioni moja
Ukizisoma sifa zake utajua kwa nini simu inastahili kuuzwa bei hiyo
Hivyo kwenye hii post utafahamu bei ya simu kulingana na ukubwa wake na sifa zinazoifanya vivo kuwa na bei kubwa
Bei ya Vivo V23 5G Tanzania
Bei ya vivo v23 5G yenye ukubwa wa memori ya 128GB ni shilingi 914,184.29/= amazon
Hivyo kwa maduka ya Tanzania bei inaweza kuwa kubwa
Hii simu ya daraja la kati ina bei kubwa kiasi.
Bei inaendana na sifa zake ila kuna simu utazifahamu amabazo ubora wake ni mkubwa kuliko V23 lakini bei ni ndogo
Fuatilia sifa zake halafu zilinganishe na simu zitakazotajwa humu.
Sifa za simu ya Vivo V23 5G
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | AMOLED, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.1, 256GB,128GB na RAM 8GB,12GB |
Kamera | Kamera tatu (vivo macho matatu)
|
Muundo | Urefu-6.44inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 915,000/= |
Upi ubora wa vivo v23 5g
Ubora wa vivo v23 5g upo kwenye uwezo wake wa utendaji
Simu ina nguvu na inakubali mtandao wa 5G
Ina kioo chenye rangi za vitu kwa ustadi
Na ni kioo kwa kizuri kucheza gemu
Ina chaji inayopitisha umeme unaojaza betri kwa dakika chache
Na hata ukaaji wake wa chaji ni wa uda mrefu
Uwezo wa Network
Vivo v23 5g ni simu ya 5G inayosapoti mtandao wa 4G aina ya LTE Cat 18
Aina ya 5G ni ile ya masafa ya chini na ya kati kwani haina uwezo wa kutumia 5G yenye kasi sana ya mmWave
Pitia hii linki uitazame, simu ya samsung galaxy s22 ultra 5g yenye kasi kubwa ya 5G
LTE Cat 18 ina spidi ya juu ya kudownload inayofikia 1200Mbps
Kwa hiyo mafaili makubwa yanaweza kumalizika ndani ya sekunde chache
Lakini si kwa Tanzania hakuna mtandao wa simu wenye spidi hii
Simu ina masafa yote ya 4G yanayotumiwa na mitandao ya simu ya Tanzania
Ubora wa kioo cha vivo v23 5g
Kioo cha vivo v23 ni cha aina ya amoled
Vioo amoled huwa na uwezo wa kuonyesha rangi nyingi
Hivyo ubora wa vitu vinavyoonekana kwenye screen ya vivo haupungui
Refresh rate ya 90Hz inaiongezea ubora kioo chake
Huku HDR10+ inaifanya kioo cha vivo kuonesha vitu kwa jinsi vinavyoonekana kwenye mazingira halisi
Lakini pia itakusaidia kuangalia video zenye ubora wa HDR za youtube
Nguvu ya processor Dimensity 920
Vivo v23 5g inatumia processor ya Mediatek dimensity 920 katika kufanya kazi zake
Dimensity 920 ni chip ya simu ya toleo la kati yenye idadi ya core nane
Ni processor yenye nguvu ya kusukuma gemu ya graphic kubwa ya PUBG Mobile kwa ubora wa Ultra HD na kwa spidi ya 64fps
Hii chip inaifanya simu isipate moto sana inapofanya kazi kubwa kwa sababu ina nguvu kubwa
App ya kupima nguvu ya processor inaipa dimensity 920 alama 783
Nguvu kubwa ya chip inasababishwa na muundo wa Cortex A78 kwenye core mbili kubwa
Kwani inaweza kufanya mizunguko bilioni mbili na laki tano kwa sekunde
Na kila mzunguko mmoja unafanya idadi ya kazi zipatazo nne
Wakati core ndogo aina ya Cortex A55 inahakakikisha matumizi madogo ya umeme
Uwezo wa betri na chaji
Chaji ya vivo v23 5g inapeleka umeme wa wati 44
Huu ni umeme unaojaza betri lake la 4200mAh kwa lisaa tu
Betri lake linakaa na chaji muda mrefu
Kwenye data za gsmarena, vivo v23 5g inakaa na chaji masaa 103
Sio masaa mengi sana ukilinganisha na simu ya tecno camon 18 premierĀ
Ukubwa na aina ya memori
Kuna matoleo mawili tu ya vivo hii
Toleo la kwanza lina ukubwa wa 128GB na RAM ya 8GB
Na toleo la pili linaukubwa wa 256GB na RAM ya 12GB
Aina za memori za vivo ni za UFS
Hivyo ufungukaji wa app ni wa haraka na kukwama ni nadra
Uimara wa bodi ya vivo v23 5g
Bodi ya hii simu ni ngumu kutokana na kuwekewa glasi upande wa mbele na nyuma
Lakini kwa bahati mbaya simu haiwezi kuzuia maji kupenya
Hivyo mtumiaji anapaswa kuwa makini
Lakini pia, uwepo wa kioo upande wa nyuma unaiepusha bodi ya simu kuchunika rangi
Hivyo umuhimu wa kava sio mkubwa
Ubora wa kamera
Vivo v23 5g ni vivo macho matatu
Kamera zake zinapiga vizuri hasa nyakati za mchana
Ila usiku kuna kiwango kidogo sana cha noise kinachoweza kuonekana
Lakini kiujumla kamera inatoa picha nzuri kwa viwango vya kawaida
Jifunze, jinsi ya kujua kamera nzuri ya simu
Simu inaweza kurekodi video za 4k na full hd kwa spidi ya 30fps
Kamera yake ya ultrawide inaweza kurekodi eneo pana sana kwa nyuzi 120
Ubora wa Software
Simu inakuja na mfumo endeshi wa Android 12 na Funtouch 12
Funtouch 12 ina mpangilio mzuri wa app pale unapotumia app nyingi (Mult Task)
Kwa maana inazipanga app kwa muundo wa grid
Muundo wa grid unatengeneza urahisi wa mtumiaji kuhama kutoka app moja na nyingine
Kwa upande wa android 12 inakupa uwezo wa mfumo wote kukopi rangi ya wallpaper
Tazama, vitu vipya vya android 12 ambavyo havikuwahi kuwepo
Yapi Madhaifu ya vivo v23 5g
Simu haina uwezo wa kuzuia maji kwani haina viwango vya ip67
Wakati simu kama ya samsung galaxy a53 5g inayoendana bei inayo
Lakini pia v23 haijatumia kioo cha gorilla
Na pia mfumo wake wa kamera si mzuri sana
Kwani hakuna kamera yoyote inayotumia mfumo wa ulengaji wa dual pixel pdaf
Neno la Mwisho
Bei ya vivo v23 5g inaweza kununua simu ya redmi note 11 pro plus 5g
Redmi imetumia chip moja na vivo v23
Lakini ina vitu vya ziada vingi ambavyo havipo kwenye hii vivo
Kwa mfano note 11 ina chaji inayopeleka umeme wa wati 120
Na hapo bei ya redmi ni chini ya laki nane kwa masoko ya aliexpress
Hapa kuna ufafanuzi wa kiundani, ubora wa simu ya redmi note 11 pro plus 5g