SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Ubora na bei ya simu ya Samsung Galaxy A53 5G[Simu Mpya]

Simu Mpya

Sihaba Mikole

April 10, 2022

Simu ya Samsung Galaxy A53 5g ni simu mpya ya samsung iliyotangazwa machi 2022 na kuingia sokoni mwezi aprili.

Ubora mkubwa wa simu ya galaxy A53 5G ni kuwa na sifa nyingi zinapatikana kwenye simu za daraja la juu.

Ni simu chache za Samsung matoleo ya A-series zilizo na uwezo wa kuzuia maji pale simu inapotumbukia kwenye maji ya kina cha mita moja.

Tutaziangazia kiundani sifa zote za simu mpya ya samsung galaxy a53.

Sifa zinazoifanya simu ya A53 kuwa simu bora ya daraja la kati kwa sasa.

Bei ya simu mpya ya Samsung Galaxy A53 5G

Bei ya samsung galaxy a53 5g inatofautiana kulingana na ukubwa wa ROM na RAM

Samsung galaxy a53 ya 128GB inauzwa shilingi 928,800/= za Tanzania

Bei ya Galaxy A53 5G ya 256GB na Ram ya 8GB inauzwa shilingi 1,274,778.00/=

Kwa kuzingatia simu nyingi ambazo zimejaduliwa hapa, hii simu ya samsung ina gharama

Ukisoma kila kitu cha hii simu ilichonacho, utakili kuwa ni simu ya bei nafuu

Zifuatilie sifa za galaxy a53 upande wa software, network, betri na ugumu wa bodi ya simu

Pitia, vitu vya kuzingatia unapotaka kununua simu mpya

Sifa za samsung galaxy a53 5g kwa ufupi.

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
  • CPU -Exynos 1280 (5 nm)
  • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.4 GHz Cortex-A78
  • Core Za kawaida(6) – 6×2.0 GHz Cortex-A55
  • GPU-Mali-G68
Display(Kioo) Super AMOLED, Refresh rate:120Hz
Softawre
  • Android 12
  • One UI 4.1
Memori  UFS 3.1,128GB, 256GB na RAM 8GB,6GB,4GB
Kamera Kamera nne

  1. 64MP,PDAF(wide)
  2. 12MP(ultrawide)
  3. 5MP(macro)
  4. 5MP(depth)
Muundo Urefu-6.5inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-25W
Bei ya simu(TSH) 928,800/=

Upi ubora wa simu ya samsung galaxy a53 5g?

Ubora wa galaxy a53 5g unapatikana kwenye kioo

Kioo cha samsung galaxy a53 kina rangi nyingi na chepesi kucheza gemu kama za magari

Ni simu ambayo ina bodi ngumu

Na betri lake ni kubwa linaloweza kukaa na chaji muda mrefu

Network yake inasapoti network bands za mitandao ya aina mbalimbali

Kamera yake moja ina teknolojia zinazoimarisha uchukuaji wa video mzuri.

Utendaji wa processor upoje?

Samsung galaxy a53 5g imepewa nguvu na processor ya Exynos 1280

Utendaji wa processor ya Exynoss 1280 ni mkubwa kwa kutazama uwezo wa core kubwa na core ndogo.

Ni processor yenye core nane zilizogawanyika sehemu mbili.

Taarifa za samsung galaxy a33

Kwenye app ya antutu Exynos 1280 ina alama 381,594

Na app ya geekbench inaipa processor alama 725 kwenye core moja

Kiuhalisia exynos 1280 inazipita chip nyingi za daraja la kati

Nguvu kubwa hiyo inatokana na aina ya miundo ya core kubwa na ndogo.

Uwezo wa core kubwa za Exynos 1280

Exynos 1280 ina core mbili zenye nguvu kubwa

Kila core ina spidi inayofikia 2.4GHz

Core zote zinatumia muundo unaochakata data kwa nguvu kubwa aina ya Cortex A78

Processor za simu zenye nguvu zimetumia Cortex A78 kwa miaka ya karibuni

Muundo wa Cortex A78 unatumia umeme mdogo lakini inafanya shughuli kubwa za simu kwa wepesi

ARM wanaisifia kuwa ni muundo wenye nguvu inayokaribia laptop

Uwezo wa core ndogo za Exynos 1280

Core ambazo ni maalumu kwa kufanya kazi ndogo zipo sita.

Kila core ina spidi inayofikia 2.0GHz

Ubora wa core ndogo unapimwa kwa kuzingatia uwezo wake wa matumizi madogo ya betri.

Kama core inatumia umeme mwingi wakati wa kupiga simu basi hiyo core ina uwezo mdogo.

Lakini sio kwa core aina ya Cortex A55 iliyopo kwenye Exynoss 1280

Chakufurahisha utendaji wake umeongezeka hivyo vitu kama kuangalia video au kupiga simu vitafanyika kwa urahizi zaidi

Network

Simu ya Samsung Galaxy A53 5G inakubali mtandao wa 2g, 3g, 4g na 5g

Simu ina network bands za 4G 18 ikiwemo bands za mitandao ya Tanzania

Aina ya 4G ya hii simu ni LTE Cat 24

LTE Cat 24 inaweza kudownload faili kwa spidi inayofikia 2 Gbps

Kama mtandao wa simu una kasi hii basi simu itamaliza kudownload faili kwa sekunde chache sana

Na inasapoti 5g aina ya mmWave ambayo huwa na kasi kubwa zaidi ya kupakua mafaili.

Display(kioo) cha galaxy a53 5g?

Kioo cha samsung galaxy a53 5g ni aina ya super amoled.

Super amoled ni kioo cha amoled kinachotengenezwa na samsung wenyewe.

Vioo vya super amoled huwa na contrast kubwa inayosaidia kioo kuwa na utajiri wa rangi.

Wingi wa rangi unafanya simu kuonesha vitu kwa rangi sahihi kwa asilimia kubwa

Na refresh rate ya kioo inafikia 120Hz.

Unapoperuzi namba za simu, simu inakuwa fasta na jina unalolitafuta unalifikia kwa haraka

Resolution yake pia ni kubwa kwani ina pixels 1080 x 2400, yaani kioo cha full hd

Bei ya kioo cha amoled huwa ni kubwa lakini hii simu ina ulinzi madhubuti kuepusha simu kupasuka kirahisi

Ubora wa kamera

Samsung galaxy a53 5g inakuja na kamera nne

Katika kamera nne hakuna kamera ya Telephoto kwa ajili ya kupiga picha vitu ambavyo vipo mbali.

Hivyo simu inatumia app ya kamera(digital zoom) kupiga kitu ambacho kipo mbali.

Ubaya wa digital zoom ni kupoteza pixels.

kamera ya samsung galaxy a53

Kukwepa kupoteza ubora pale unapozoom itakulazimu kuseti kamera iwe na resolution ya 64MP

Kikawaida ukipiga piccha hujisevu kwa resolution ya 12MP

Ubora wa video

Kamera zake zinaweza kurekodi video zenye ubora wa 4k(ultra hd) na full hd.

Video za 4k zinarekodiwa kwa spidi ya 30fps.

Wakati za full hd spidi yake hufika 60fps

Japo ingekuwa safi zaidi kama video za 4k zingekuwa zinarekodiwa kwa spidi inayofika 60fps

Upande wa Software upoje?

Simu ya galaxy a53 5g ni simu mpya ya android 12 yenye software ya One UI 4.1.

Android 12 ni toleo jipya kabisa lenye vitu vya ziada ambavyo havikuwepo kwenye toleo lililopita

Moja ya vitu hivyo ni simu kukuonyesha app zinazotumia kamera na mic bila wewe kujua.

Hilo linakulahishia kufahamu app zinazorekodi mazungumzo yako

One UI 4.1 na yenyewe ina vitu vingi

Kimojawapo ni kukupa uwezo wa kuongeza RAM kutoka kwenye memori ya simu

RAM inapokuwa kubwa inaongeza utendaji wa simu kiasi fulani

Uimara wa bodi ya simu?

Simu ina viwango vya IP67.

IP67 inakuonyesha uwezo wa simu kuzuia maji pindi inapodumbukia kwenye kina cha mita moja.

Hivyo Samsung Galaxy A53 5G ni moja ya simu isiyopitisha maji

Hii simu ni ngumu.

Upande wa kioo unalindwa na vioo vya Corning Gorilla Glass 5

Corning Gorilla Glass 5 ni glassi ambazo ni ngumu kupasuka hasa simu ikianguka kwa urefu wa mita 1.2

Pitia majaribio ya maabara yaliyofanywa na kampuni ya Corning utaona

Uwezo wa Betri na Chaji?

Betri ya samsung galaxy a53 5g ni aina ya Li-Po yenye ukubwa wa 5000mAh

Na chaji yake inapitisha umeme kwa spidi inayofikia 25W

Hii ni spidi inayoweza jaza betri chini ya masaa mawili

Betr zenye ukubwa wa 5000mAh zinaweza kutumika kwa zaidi ya masaa 13 simu ikiwa inatumia intaneti masaa mengi mfululizo

Ushindani na simu mbadala?

Zipo simu za makampuni mengine ambazo zinakaribiana ubora na simu ya samsung galaxy a53 5g.

Moja ya mshindani mkubwa ni Redmi Note 11 Pro+ 5g

Redmi Note 11 Pro+ 5g ina mfumo mzuri wa kamera kuliko galaxy a53

Processor iliyomo kwenye Redmi Note 11 Pro+ 5g ina nguvu inayoizidi processor ya Exynos 1280

Kioo cha Redmi Note 11 Pro+ 5g kina HDR10 wakati samsung hii haina.

Ila tu software ya Redmi sio nzuri ukilinganisha na One UI

Maoni 4 kuhusu “Ubora na bei ya simu ya Samsung Galaxy A53 5G[Simu Mpya]

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

thumbnail

Bei ya Samsung Galaxy A35 na Sifa zake

Samsung Galaxy A35 ni toleo jipya la samsung lilotoka mwezi machi 2024 Ni simu ya daraja la kati iliyochota baadhi ya sifa muhimu kutoka kwenye galaxy yenye bei kubwa Ndio […]

simu mpya

Simu mpya kali 20 na bei zake kwa mwaka 2024

Hii ni orodha ya simu mpya ambazo zimetoka mwaka 2024 ama mwishoni mwa mwaka 2023 kutoka kwa kampuni zipatazo 11 Ni orodha inayohusisha simu za daraja la kati na la […]

samsung s24 plus thumbnail

Bei ya Samsung Galaxy S24+ na Sifa Zake

Kisifa Samsung Galaxy S24 Plus ina sifa nyingi zinazoendana kwa kiasi kikubwa na Samsung Galaxy S24 Ultra Kwa maana Galaxy S24+ ubora wake unazipita simu nyingi na mkubwa, hivyo bei […]

samsung s24 ultra thumbnail

Bei ya Samsung Galaxy S24 Ultra na Sifa zake

Hivi karibuni simu mpya ya Samsung Galaxy S23 Ultra imeingia sokoni huku bei yake ikiwa haitofautiani sana na Apple iPhone 15 Pro Max Kwenye soko la dunia bei ya samsung […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram