Simu ya infinix zero ultra ni simu nyingine ya 5G kutoka brand ya Infinix ya 2022
Utaweza kutumia mtandao wa 5G wa Vodacom kwa hapa Tanzania
Kwa kuwa ni moja ya simu bora ya 5G, bei ya infinix zero ultra inazidi shilingi milioni moja
Uwepo wa teknolojia yenye kasi kubwa ya mawasiliano haitoshi kukujulisha ubora na kasoro zake hasa ukifananisha na simu zingine za 5G kutoka Samsund, Oppo, Xiaomi, Realme nk
Hivyo hii posti inafafanua kinaga ubaga sifa,bei na ubora wa infinix zero ultra
Bei ya Infinix Zero Ultra ya GB 256
Hii simu ya infinix ina toleo moja tu ambayo ina ukubwa wa GB 256
Bei yake inaanzia shilingi 1,500,000/= (milioni moja na nusu) kwa hapa Tanzania
Simu inauzwa kiwango hiko kutokana na ubora wake kwenye kamera, display (kioo), chaji na utendaji
Changamoto kubwa kwa infinix zero ultra inakuja kwa washindani wake hasa Redmi Note 11 5G Pro Plus
Hizi simu mbili zinaendana kwenye nyanja nyingi ila redmi ina bei nafuu zaidi (shilingi 920,000)
Sifa za Infinix Zero Ultra
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | AMOLED, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.1,256GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera TATU (macho matatu)
|
Muundo | Urefu-6.8inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 1,500,000/= |
Upi ubora wa Infinix Zero Ultra
Ubora wa infinix umejikita zaidi kwenye spidi ya chaji na uwezo mkubwa wa processor
Ni moja ya simu inayochukua muda mfupi kujaza betri ya simu
Ina kioo kinachoonyesha vitu kwa ustadi
Ni simu mpya ambayo inakuja na mtandao wenye kasi zaidi
Ni simu ndefu na pana na yenye kamera iliyo na lenzi kubwa
Kiuhalisia infinix zero ultra ina kasoro ndogo sana
Hii inaweza ikawa ni SIMU BORA YA INFINIX katika simu zote walizowahi tengeneza mpaka sasa
Fuatilia kila kipengele ujue kwa nini
Uwezo wa Network
Baada ya kuzinduliwa kwa Infinix Note 12 VIP yenye 5G basi infinix wameweka tena 5G kwenye toleo jipya
Kununua simu ya 5G sio upotezaji wa pesa kwa sababu Tanzania ina huu mtandao
Inakubali aina zote za 5G ambazo ni SA, NSA na Sub-6
Vodacom Tanzania inatumia 5G aina ya NSA inayomaanisha Non Stand Alone
Kuelewa teknolojia hii ya mawasiliano inakubidi upitie, maana ya 5G
Kwa sasa kupata spidi inayofika 200Mbps ni kawaida hapa nchini ila si maeneo yote yenye 5G
Pia inakubali mtandao wa 4G na 3G vilevile
Ubora wa kioo cha Infinix Zero Ultra
Kioo cha infinix ultra zero ni aina ya AMOLED lakini sio Super Amoled
Vioo vya amoled huwa vinaonyesha rangi nyingi kitu kinachofanya vitu kuonekana kwa rangi zake sahihi kwa aslimi kubwa
Uzuri pia kioo chake kinakuja a refresh rate inayofikia 120Hz
Umuhimu wa refresh rate kubwa ni simu kuwa nyepesi ukitachi kwa kuperuzi na pia gemu huchezeka vizuri
Pia resolution yake ni kubwa yenye pixels 1080 x 2400
Kadri kioo kinavyokuwa na pixels nyingi ndivyo simu inavyoonyesha vitu kwa ustadi
Nguvu ya processor MediaTek Dimensity 920
Processor ya Mediatek dimensity 920 inaifanaya simu ya infinix zero ultra kuwa na uwezo wa kufanya vitu vingi bila simu kukwama kwama
Japokuwa kiuwezo haifikii simu ya iphone 14 pro max kwa sababu dimensity 920 ni chip ya kundi la kati
Kwenye app ya geekbench, dimensity ina alama 811
Uwezo mkubwa wa processor yake unaweza kuonekana zaidi kwenye kucheza gemu
Kwani gemu nyingi zinaweza kucheza kwa fremu zaidi ya fremu 60 kwa muonekano wa Ultra HD
Nguvu kubwa inasababishwa na processor kutumia muundo wa Cortex A78 kwenye core mbili zenye nguvu zaidi
Na pia spidi ya mizunguko ya core kubwa kuwa ni 2.5GHz
Uwezo wa betri na chaji
Chaji ya Infinix Zero Ultra inapeleka umeme unaofikia wati 180
Ni umeme mkubwa hivyo betri inachukuwa muda mchache kujaa
Kwa mujibu wa Infinix, chaji yake inajaa kwa DAKIKA 12
Hii ni zaidi ya fast chaji ukizangitia ukubwa wa betri ni 4500mAh aina ya Li-Po
Utunzaji wa chaji unaweza kuzidi zaidi ya masaa 14 ikiwa simu inatumia intaneti muda wote
Lakini swala la utunzaji wa chaji inategemea sana na aina ya matumizi
Kwa mcheza magemu betri huwai kuisha
Ukubwa na aina ya memori
Simu ya Infinix Zero Ultra ina toleo moja tu upande wa memori
Ukubwa wa memori ni 256GB na RAM ya GB 8
Aina ya memori haijainishwa ila chip ya dimensity 920 inasapoti memori aina ya UFS pekee
Hivyo usafirishaji wa data ni wa haraka na hivyo utendaji unaongezeka
Uimara wa bodi ya Infinix Zero Ultra
Hii simu inakuja na bodi ya kioo upande wa nyuma na mbele
Wenyewe infinix wanaita “Glass and Star Trail Design”
Vyovyote vile, bodi za vioo huepusha rangi ya simu kuchunika kwa haraka
Ila haikuanishwa kama vioo ni vya aina ya Gorilla
Bahati mbaya simu haina ulinzi wa kuzuia maji kupenya ndani ya simu
Kikawaida simu za bei zaidi ya milioni huwa zinakuwa na IP ratings ambazo huonyesha uwezo simu kuzuia maji kupenya
Ubora wa kamera
Infinix Zero Ultra ina kamera tatu kwa jina lingine infinix macho matatu
Kamera kubwa zaidi ina megapixel 200
Kwenye mwanga hafifu picha zinaonekana kwa vizuri
Na kamera ya 200MP inakoleza zaidi rangi ukilinganisha na kamera ya kawaida ya kawaida ya 12MP
Ila zoom yake haitoi picha nzuri hasa ukiikuza picha mara 10
Inazidiwa mbali sana na simu ya samsung galaxy s22 ultra 5G
Sio kesi sana, kamera zake zina ulengaji unaoweza kukipiga kitu kilicho kwenye mwendo kwa usahihi mkubwa
Inatokana na kamera yake kuwa na ulengaji wa dual pixel pdaf
Upande wa video pia ni wa kuvutia
Kamera yake inaweza kurekodi mpaka video za 4K kwa fremu 30fps
Ukirekodi video ukiwa unatembea bado itatokea vizuri bila kutingishika
Hii inatokana na kamera kuwekewa OIS (Optical Image Stabilization)
Ubora wa Software
Simu inakuja na android toleo la 12 ikiwa na mfumo XOS 12
Muonekano wa XOS 12 unakurahisishia kuingia apps za Instagram na youtube kwa haraka
Kwa maana zimeekwa kwenye folda moja kwenye home screen
Hivyo ukiwasha simu mara ya kwanza utazikuta hizo apps kwenye screen
Kitu kingine ni kuwa XOS 12 inakupa uwezo wa kuongeza ukubwa wa RAM
Japokuwa RAM ya GB 8 inatosha sana kwa sasa ila kuna nyakati kiasi kikubwa cha RAM kinahitajika
Ukizingatia XOS 12 inakuja na applikesheni nyingi sana ambazo hutoweza kuzitoa
Yapi Madhaifu ya Infinix Zero Ultra
Kamera za Infinix Zero Ultra hazina optical zoom
Optical zoom hii ni aina ya zoom inayotumia lenzi kukikuza kitu cha mbali
Hivyo ubora haupotei ukilinganisha na zoom ya app ya simu
Kukosekana kwa IP67 ni kasoro nyingine
Simu kama Samsung Galaxy A53 ina IP67 hivyo haipitishi maji
Wakati huo galaxy a53 inapatikana kwa bei ya 800,000/=
Utatambua kasoro zingine za Infinix zero ultra kwa kuitazama simu ya Redmi Note 11 Pro+ 5G
Matumaini ni kuwa haya mapungufu yatarekebishwa kwenye matoleo mapya ya infinix
Neno la Mwisho
Infinix inazidi kupiga hatua katika kuzikabili simu za makampuni mengine
Na kwa sasa infinix inajaribu kulipata soko la 5G ambapo litashika kasi siku za mbeleni
Kasoro kubwa ya infinix ni kuwa simu zao nzuri zinakuwa na bei kubwa iliyopitiliza
Kitu kinachoweza kumshawishi mtumiaji wa simu kutafuta simu mbadala yenye sifa sawa au zaidi na kwa bei ya chini zaidi
Wazo moja kuhusu “Bei ya Simu ya Infinix Zero Ultra na Ubora Wake”
Wanasimu nzuri Lakini kwanini nisinunue simu mbadala yenye sifa sawa nahiyo Lakini inabei nafuu? Ukilinganisha kwamba simu Bora zipo nyingi na infinix wanajitafuta