Simu ya infinix hot 11 ni simu ya android 11 ambayo imetoka mwaka 2021
Lakini ni simu ambayo inaendana na soko la sasa 2022
Bei ya infinix hot 11 kwa sehemu nyingi Tanzania ni chini ya shilingi laki tatu.
Bei yake ndogo inatokana na sifa zake nyingi ambazo zinaipeleka simu kwenye kundi la daraja la chini
Kiufupi, utafahamu bei yake maeneo ya Dar na sifa zake muhimu kiunaga ubaga.
Bei ya infinix hot 11
Kwa maduka ya simu Tandika bei ya infinix hot 11 ya 64GB ni shilingi 280,000/=
Wakati huo maduka mengi ya simu ya ilala na kariakoo wanauza infinix hot 11 kwa shilingi laki mbili na nusu.
Hivyo ukiona duka linaiuza hii simu kwa zaidi ya laki tatu basi hiyo sio bei stahiki.
Kabla ya kufanya maamuzi ya kuinunua hot 11, ni vizuri ukajilizisha ubora wake.
Utaufahamu ubora wa simu kwa kuzifahamu sifa za sehemu za simu husika.
Sifa za infinix hot 11
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, |
Softawre |
|
Memori | eMMC 5.1, 128GB, 64GB na RAM 4GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.5inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 280,000/= |
Upi ubora wa infinix hot 11
Ubora wa simu ya infinix hot 11 upo katika sehemu kuu mbili
Ukaaji wa chaji na processor yenye nguvu ya wastani
Hot 11 ina utendaji mzuri unaweza kucheza gemu nyingi za simu japo si kwa ubora mkubwa.
Simu ina betri kubwa inayofanya kukaa na chaji masaa mengi
Kwenye nyanja nyingine ubora unatofautiana.
Hasa ukiangalia kioo na kamera kama inavyofafanuliwa.
Uwezo wa Network
Network ya hot 11 inakubali mtandao wa 4G aina ya LTE Cat 7
4G yake ina network bands zipatazo saba
Zote zinakubali mitandao ya simu Tanzania yenye network ya 4G.
Kama ufahamu kuhusu network bands, pitia hapa, Network za mitandao ya simu Tanzania
LTE Cat 7 ina spidi ya kudownload inayofikia 300Mbps.
Ni spidi inayoweza kudownload faili la 1200Mb kwa sekunde 40
Ila Tanzania hakuna mtandao wa simu za mkononi unaotoa spidi ya 300Mbps
Ubora wa kioo cha infinix hot 11
Kioo cha infinix hot 11 ni aina ya ips lcd chenye resolution kubwa ya 1080 x 2408 pixels
Uangavu wake si mkubwa sana kwani nits zake 500
Hivyo ukitumia simu kwenye jua kali sana screen inaweza isionyeshe vitu kwa uwazi
Bei ya kioo aina ips lcd ni ya chini kwa sababu ubora wake huwa ni mdogo ukilinganisha na vioo vya amoled
Nguvu ya processor MediaTek Helio G70
Processor ya infinix hot 11 ni MediaTek Helio G70
Utendaji wa Helio G70 ni wastani na unaweza kufungua app nyingi kiurahisi.
Kwani ni chip inayoweza cheza gemu ya PUBG Mobile kwa resolution ya Full HD na kwa kasi ya 30fps
App zinazopima nguvu ya processor zinaipa alama za kiwango cha kati.
Geekbench inaipa Helio G70 alama 391 kwenye core moja
Na App ya antuntu inaipa chip alama 205,296 wakati chip Snapdragon 450 ya Huawei Y7 ina alama 99,631
Kwa nini Helio G70 ina utendaji wa wastani?
Kujibu swali inabidi utazame uwezo wa core kubwa na core ndogo
Uwezo wa core kubwa
Helio G70 ina core zenye nguvu zipatazo mbili
Core kubwa mbili kila moja ina kasi inayofikia 2.0 GHz
Zimeundwa kwa muundo wa Cortex A75
Muundo wa cortex a75 unaweza kuchakata kazi(instructions) bilioni sita kwa sekunde
Ni muundo wenye uliongozeka kwa matumizi madogo ya umeme yapatayo wati 2
Uwezo wa core ndogo
Kuna jumla ya core sita zenye nguvu ndogo aina ya Cortex A55
Kila core ina spidi inayofikia 1.7 GHz
Hizi core zimetengenezwa kutumia umeme mdogo na utendaji wake sio mkubwa
Hutumika pale simu inapofanya kazi zinazohitaji nguvu ndogo
Cortex A55 inaweza kufanya shughuli chache kwa wakati mmoja
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya infinix hot 11 inastahimili ukaaji wa chaji masaa mengi
Kikawaida simu zenye betri la ujazo wa 5000mAh hukaa na chaji masaa zaidi ya 14 simu ikitumia intaneti.
Infinix 11 ina betri la ujazo wa 5200mAh
Hivyo basi ukaaji wake wa chaji data ikiwa haijazimwa unaweza kuzidi masaa 15
Kitu kinachosababisha ukaaji wa chaji ni utndaji wa wastani na kioo kinachokula umeme kidogo.
Kwa bahati mbaya simu haina fast chaji hivyo simu inaweza kujaa kwa masaa zaidi ya matatu
Ukubwa na aina ya memori
Kuna matoleo ya aina mbili ya infinix hot 11 upande wa memori
Kuna infinix ya 64 GB na ya 128 GB
Infinix ya 128GB bei yake ipo juu na inaweza kuzidi laki tatu.
Lakini memori zake hazina kasi kubwa ya kusafirisha data.
Kwani ni aina ya eMMC 5.1, kitu kinachopunguza uwezo wa simu kiutendaji
Uimara wa bodi ya infinix hot 11
Bodi ya hii simu imeundwa kwa plastiki upande wa nyuma na kwenye frem za pembeni
Bodi za plastiki zina kawaida ya kuchunika rangi kadri muda unavyoenda
Hivyo kuimarisha muonekano wa simu muda mrefu kava na screen protector zitahitajika
Kwa sababu screen ya simu haijatumia vioo vigumu vya gorilla
Simu si nyembamba sana na ina uzito wa gramu 201
Pia ina urefu na upana upatao inchi 6.6
Ubora wa kamera
Infinix hot 11 ina kamera mbili zenye ubora mdogo.
Ubora wa chini wa kamera unasababishwa na kamera zake kukosa teknolojia dual pixel pdaf
Na kamera ya pili aina QVGA ina resolution ndogo sana isiyoendana na nyakati za sasa
QVGA haitoi picha nzuri
Pia simu inaweza kurekodi video zenye resolution 1440p pekee
Ubora wa Software
Simu ya hot 11 inatumia toleo la android 11 lenye software ya XOS 7.6
XOS 7.6 kupitia app ya XHIDE itakusaidia kuficha taarifa zako za simu na app nyingine
Hivyo yeyote atakaetaka kutumia simu yako atahitaji ruksa yako
Pia xos 7.6 inapiga kelele simu ikiondolewa kwenye chaji.
Ni njia moja ya uzibiti wa simu kupotea
Yapi Madhaifu ya infinix hot 11
Infinix hot 11 ina mapungufu mengi
Japo huwezi kuilalamikia simu kutokana na bei yake
Simu haina uwezo wa kuzuia maji wala vumbi kwa maana haina viwango vya IP53
Kioo chake hakina HDR10 inayoboresha muunokano wa vitu kuendana na namna jicho la binadamu linavyoona kwenye mazingira halisi
4G yake ina masafa machache
Chaji yake inapeleka umeme taratibu
Lakini ulinzi wa kwenye kioo ni wa kiwango cha chini
Kutokana na kutokuwa na kioo cha gorilla angalau Gorilla 3
Neno la Mwisho
Kama utapata infinix hot 11 chini ya laki tatu bila kujali ukubwa wa memori itakuwa ni jambo sahihi
Ni bei inayoendana na ubora wake.
Ila kuna simu zinazofanana vitu na hii infinix ambazo zina sifa za ziada.
Mfano mzuri ni simu ya Realme C3 yenye processor Helio G75 lakini pia Tecno camon 17
Realme C3 ina kioo cha gorilla 3
Maoni 7 kuhusu “Bei ya Simu ya Infinix Hot 11 na Sifa Zake Kiundani (2022)”
Hivi tofauti ya Infinix hot 11 play na Infinix hot 11 note ni ipi na kama kuna simu Bora kabisa ya Infinix ni ipi
Utofauti ni kwenye utendaji na kamera, infinix hot 11 ina utendaji mkubwa na kamera nzuri kidogo kuliko hot 11 play
Mimi nachokiona simu ya Infinix hot 11 play naona kwa upande wa chaji Ipo vizuri sana,na camera Ipo vizuri sana ya mbele ila ya kujipiga mwenyewe ndo sio nzuri,ila kwa mtandao Iko powa sana,Mimi nimeuziwa laki mbili na sitini26,0000/=
Kwahiyo nauliza Kuna tofauti gani kati ya Infinix hot 11play na Infinix hot 12?
Kuna tofauti kwenye upande WA kioo na uwezo WA kiutendaji WA simu, hot 12 ina nguvu zaidi hivyo ni nzuri zaidi ya hot 11 play
Hii simu ni nzuri sijui napataje kwa sasa
Hii simu naipataje maana ni nzuri sana