Simu ya samsung galaxy a32 ni simu ya daraja la kati ambayo imetoka 2021
Pamoja na simu kutimiza mwaka ila galaxy a32 ina vitu vingi ambavyo vinakosekana kwenye baadhi ya simu mpya za 2022
Changamoto ni kuwa bei ya samsung galaxy a32 ni kubwa kuliko uhalisia
Kwani kwa Tanzania bei yake inazidi laki sita
Hii post itakaonyesha bei yake kutokana na ukubwa wa memori na sifa zake
Na utajua simu zingine zenye sifa zinazoizidi a32 kwenye nyanja na zenye bei nafuu zaidi
Bei ya Samsung Galaxy A32 Tanzania
Bei halisi ya samsung galaxy kwenye masoko ya mtandaoni hasa amazon ni shilingi 533,341.00/=
Ila kwa Tanzania bei ni kubwa mara dufu kwa maduka mengi ya simu
Kwa mfano maduka mengi ya kariakoo wanaiuza simu kwa shilingi 700,000/=
Hii inasababishwa na aina ya kioo na uimara wa bodi
Lakini sifa za kiujumla za kiutendaj zinaifanya simu kutoendana na bei inayopatikana kwa sasa
Sifa za simu ya samsung galaxy a32
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super Amoled, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | 128GB,64GB na RAM 8GB,6GB,4GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.4 inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 700,000/= |
Upi ubora wa samsung galaxy a32
Ubora wa samsung galaxy a32 upo hasa kwa kiasi kikubwa kwenye ubora wa kioo
Kioo chake kina ufanisi mzuri wa uonyeshaji vitu kwa rangi stahiki
Ina utendaji unaoweza kufungua app za kila aina bila simu kupata joto jingi
Inakaa na chaji masaa mengi kutokana na kuwa na betri kubwa
Simu ina na memori kubwa inayoqweza kuhifadhi app na mafaili mengi
Ni moja ya samsung yenye kamera inazokupa machaguo mengi ya kupiga picha ama kurekodi video
Uwezo wa Network
Samsung galaxy a32 ni simu ya 4G aina ya LTE Cat 7
LTE Cat 7 spidi yake ya juu ya kupakua ni 300Mbps
Iwapo mtandao wa simu unakupa spidi basi simu inaweza kudownload faili la ukubwa wa 1200MB kwa sekunde 40
Uzuri ni kuwa galaxy hii ina nmasafa ya 4G yapatayo 10
Hivyo 4G ya mitandao ya smile, ttcl, tigo, halotel, airtel na vodacom itakubali kwenye simu hii
Ubora wa kioo cha samsung galaxy a32
Kioo cha samsung galaxy a32 ni cha super amoled
Super amoled hutongezwa na kampuni ya samsung yenyewe
Vioo vya amoled huwa na ufanisi mkubwa wa kuonyesha rangi hasa rangi nyeusi
Hiyo inatokana na vioo kuwa na uwezo wa kuonyesha rangi nyingi
Pia ubora wake umeongezwa na kuwa na resolution kubwa ya 1080 x 2400 pixels
Na pia refresh rate ya 90Hz
Refresh rate kubwa inafaya simu kuwa nyepesi wakati wa kutachi
Tazama hii video uone utofauti kati ya simu yenye refresh rate ya 90Hz na 60Hz
Nguvu ya processor MediaTek Helio G80
Galaxy A32 inatumia chip ya MediaTek Helio G80 kufanya kazi zake
Helio G80 ni processor ya simu ya daraja la kati
Utendaji wake ni wastani kwani si mkubwa sana kama simu ya samsung s21 ultra
Kwani app ya antutu inaipa alama 231,000 na geeekbench 5 inaipa alama 353
Ila ina uwezo wa kucheza gemu nyingi kwa ubora wa Full HD na kwa spidi inayozidi 30fps
Uwezo wa wasatani unachangiwa hasa na aina ya muundo wa core kubwa na core ndogo
Uwezo wa core kubwa
Helio G80 ina core zinazofanya kazi kubwa sana zipatazo mbili
Hizi core spidi yake ya juu ni 2.0 GHz ambayo ni ndogo kwa core kubwa nyingi
Spidi hiyo inamaanisha chip inaweza kufanya kazi kwa mizunguko bilioni mbili kwa sekunde
Na kila mzunguko mmoja unafanya kazi zipatazo 3
Kwa sabau zimetengenezwa kwa muundo wa Cortex A75
Wakati cortex A76 inafanya kazi nne kwa mzunguko mmoja
Uwezo wa core ndogo
Simu ya samsung galaxy 132 ina jumla ya core ndogo zipatazo sita
Simu inazitumia hizi core ikiwa inafanya kazi inayotumia nguvu ndogo
Kwa mfano kupiga simu, kutuma sms, kuchati whatsapp nk
Spidi ya juu kabisa ya kila core ndogo ni 1.8 GHz na zina muundo wa Cortex A55
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya galaxy a32 ina ukubwa wa 5000mAh
Kutokana na simu kuwa na utendaji wa wastani unafanya ukaaji wa chaji kuwa mkubwa
Simu nyingi zenye betri za 5000mAh hukaa na chaji masaa yanayoweza kuzidi 15
Kwa bahati mbaya simu ina spidi ndogo ya kuchaji
Kutokana na chaji yake kupeleka umeme usiozidi 15W kama kiwango cha juu
Hivyo betri inaweza kuchukua muda mrefu kujaa
Ukubwa na aina ya memori
Kuna matoleo manne ya samsung a32 upande wa memori
Kuna galaxy a32 ya 64GB na ram ya 4GB
Kuna ya 128GB na ram ya 4GB
Glaxy a32 ya 128GB na ram ya 6GB
Na kubwa kabisa ya 128GB na ram ya 8GB
Uimara wa bodi ya samsung galaxy a32
Bodi ya samsung galaxy a32 upande wa mbele imewekewa ki00 cha gorilla 5
Kuna majaribio mengi ambayo yameonyesha ugumu wa gorilla 5 kupasuka
Kwani inaweza simu inaweza isivunjike endapo ikianguka kwa kimo cha mita mbili kutoka juu
Lakini upande wa nyuma simu inatumia bodi ya plastiki
Hivyo kava ni muhimu kuepusha kuchunika kwa rangi
Ubora wa kamera
Simu ina jumla ya kamera nne
Kamera kubwa ina resolution ya 64MP
Ila kamera yake haiwezi kurekodi video za 4K
Na ulengaji sio mkubwa kutokana na simu kutumia autofocus ya PDAF badala ya dual pixel pdaf
Ina kamera aina ya ultrawide inayoweza kupiga na kurekodi eneo pana kwa nyuzi 123
Ubora wa Software
Simu ya samsung galaxy a32 ni simu ya android 11 inayokuja na software ya One UI 3.1
Katika software za android one ui huzishinda softaware nyingi
Ni nyepesi na ina vitu vingi bila kuwa na matangazo mengi
Yapi Madhaifu ya samsung galaxy a32
Simu haina uwezo wa kuzuia maji kwa sababu haina viwango vya ip67
Simu nzuri za matoleo ya kati huwa na angalau IP53
Kamera zake si za kuvutia
Kwani zina rekodi ubora wa full hd kwa kasi ndogo
Lakini pia, zinatumia teknolojia ya ulengaji ambayo kwa sasa inapitwa na wakati ya PDAF
Chaji yake inapeleka umeme mdogo unaojaza betri kwa masaa mengi
Neno la Mwisho
Bei ya samsung galaxy a32 kwa Tanzania inaweza kununua simu ya redmi note 10 5G na chenji ikabaki
Kiubora galaxy a32 inaachwa mbali na redmi kwenye swala la utendaji
Kiukweli simu zenye processor ya Helio G80 hazipaswi kuzidi laki nne
Maoni 5 kuhusu “Bei ya simu ya Samsung Galaxy A32 na Sifa Zake [2022]”
Nimeipenda bei tatizo hela sina mm na 350000
Naomba kuuliza kwasasa hiyo simu itakuwa na bei gan? Hasa yenye 4gb&64gb msaada tafadhali
Haijabadirika Sana Kwa zile mpya
Naomba mnisaidie kuuza sm yangu samsung A32
Fone no 0683840191
Hiyo simu ina line ngap?