Simu ya iPhone 11 Pro Max ni simu ya iphone ya daraja la juu ambayo imetoka 2019
Ubora uliotumika kuiunda hii simu inafanya bei ya iphone 11 pro max kuzidi milioni 1.3 mpaka sasa 2022
Japokuwa ni moja ya simu bora ya mwaka 2019 ila kuna simu chache zinazoweza kuizidi iphone 11
Ila inaweza kuzidiwa na simu nyingi za sony mpya
Kwa kulinganisha bei yake na sifa zake itakupa sababu kwa nini bado gharama yake ni kubwa hata yenye memori ndogo
Bei ya iPhone 11 Pro Max ya GB 64
Bei ya iPhone 11 Pro Max ambayo ukubwa wake ni GB 64 na RAM yake ni GB 4 ni shilingi 1,500,000/= hapa Tanzania
Ila hii bei ni kubwa sana
Kwa sababu mtandao wa amazon wanauza iphone 11 pro max kwa shilingi 1,300,000/=
Kwa kutazama matoleo ya Pro Max ya 2020 na 2021, hii ya 2019 ina bei ndogo
Unafuu huo wa bei unaendana kwa kiasi kikubwa na sifa zake ambazo zimeambatanishwa kwenye jedwari chini
Sifa za simu ya iPhone 11 Pro Max
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super Retina XDR OLED, |
Softawre |
|
Memori | NVMe, 256GB,128GB,64GB,512GB na RAM 4GB |
Kamera | Kamera tatu (iphone macho matatu)
|
Muundo | Urefu-6.5inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 1,500,000/= |
Ni Upi ubora wa iPhone 11 Pro Max?
iPhone 11 Pro Max ina utendaji wenye nguvu kutokana na kutumia chip yenye uwezo wa kuchakata vitu vingi kwa urahisi
Ina screen inayoonyesha vitu kwa rangi zinazoendana kwa uhalisia kwa kiwango kikubwa
Kamera zake zinatoa picha nzuri nyakati zote (iwe usiku au mchana)
Ina mfumo wa memori ambao una kasi kubwa ya kusafirisha data
Simu inaweza kupokea matoleo mapya ya mfumo endeshi wa iOS
Ukifuatilia uwezo wa simu kuanzia network mpaka software utaona kuwa ni simu yenye mapungufu machache kwa kulinganisha na simu mpya zilizotoka 2020 hadi 2022
Uwezo wa Network
Mtandao wenye kasi kubwa zaidi kwenye hii simu ni 4G kwa sababu haina 5G
Aina ya 4G simu inayotumia ni LTE Cat 18
Kama mtandao wa simu una kasi inayoendana na LTE Cat 18 basi simu inaweza kudownload faili la ukubwa wa 1500MB kwa sekunde kumi
Lakini kwa Tanzania hakuna laini ya simu ambayo inatoa kasi ya 1200Mbps
Mitandao yote ya simu nchini inakubali intaneti ya LTE
Kwani simu ina masafa karibu ya kila nchi upande 3G na 4G
Ubora wa kioo cha iPhone 11 Pro Max
Kioo cha iPhone 11 Pro Max ni cha aina ya Super Retina XDR OLED
Super Retina XDR ni neno la kimasoko la apple lakini kiujumla ni kioo cha OLED kama tu vioo vilivyotumika kwenye baadhi ya simu za huawei
Kama ilivyo ada, oled huonyesha rangi nyeusi kama inavyoonekana na jicho la binadamu
Vioo vya oled huwa vina contrast kubwa kitu kinachoipa screen uwezo wa kuonyesha rangi nyingi za aina tofauti tofauti
Ustadi wa kioo chake unachangiwa na simu kuwa na HDR10
HDR10 hufanya screen ionyeshe vitu kwa namna jicho la binadamu linavyoona kwenye mazingira halisi
Kuelewa kiundani ufanyaji kazi wa hdr pitia: maana ya hdr kiundani
Nguvu ya processor Apple A13 Bionic
Kwa miaka mingi kampuni ya apple imekuwa ikitengeneza processor za simu zenye nguvu kubwa kiutendaji kuliko kampuni yoyote
Hii imekuwa ikiifanya kuwa moja ya kampuni bora duniani za simu
Tazama: orodha ya kampuni bora zinazotengeneza simu
Kwa kuzingatia data za app ya geekbench inayopima ubora wa processor Apple A13 Bionic ina alama 1319 kwenye core moja
Ndio maana hii chip inaweza kucheza gemu linalohitaji nguvu la PUBG Mobile kwa resolution kubwa na kwa kasi 57fps
Kikawaida processor ikiwa na nguvu huwa inatumia umeme mwingi
Kitu kinachopelekea betri kuwahi kuisha
Lakini matumizi ya umeme kwenye apple a13 bionic ni madogo ukilinganisha na chip iliyotumika kwenye iPhone XR
Kwa mujibu wa apple, kuna ongezeko la utendaji kwa 20% kwenye core mbili zenye nguvu
Na pia core zinazotumia umeme mdogo zimepunguza matumizi ya umeme kwa 40% ikilinganishwa na Apple A12 Bionic
Uwezo wa betri na chaji
Kwa kutazama kwa macho betri ya iphone 11 pro max ni dogo
Kwani lina ukubwa wa 3969mAh
Lakini namba zisikudanganye kwani hii ni moja ya iphone inayokaa na chaji masaa mengi hata kwenye intaneti
Kwa mujibu wa GSMArena, iPhone 11 Pro Max inaweza kukaa na chaji masaa 102 simu ikiwa inatumika mara chache.
Ikiwa inaperuzi intaneti masaa mengi mfululizo, inaweza chukua masaa 15 mpaka chaji kuisha
Ni masaa ambayo simu kama ya Redmi Note 10 hayafikii ikiwa inaperuzi intaneti
Wakati simu ya Redmi ina betri kubwa la 5000mAh
Upande wa chaji kasi yake ni ya wastani
Kwani chaji yake inapeleka umeme wa wati 20
Ukubwa na aina ya memori
Memori za simu ya apple ni tofauti na zile kwenye simu za android
Apple hutumia memori aina ya NVMe wakati android hutumia eMMC, au UFS
NVMe huwa unausafirishaji mkubwa wa data zaidi ukilinganisha na aina zingine
Usafirishaji mkubwa wa data huifanya simu kuwa nyepesi na app kufunguka kwa haraka
Kiujumla kuna iphone 11 pro max za matoleo matatu upande wa memori
Ukiwa na bajeti ndogo utapata yenye GB 64
Ila kama bajeti ni kubwa unaweza ukapata ya GB 256 au GB 512
Uimara wa bodi ya iPhone 11 Pro Max
Mara nyingi bodi ya simu za apple huwa ni ngumu kuvunjika ama kuchunika
Hii inatokana na simu kutengenezwa na kioo cha gorilla upande wa mbele na nyuma
Na pia kuwekewa chuma upande wa pembeni
iPhone huwa zinakuja na viwango vya IP68
IP68 inaonyesha uwezo wa simu kuzuia maji na vumbi
Kama simu ikidumbukia kwenye maji ya kina cha mita 4 kwa muda wa nusu saa maji hayatopenya
Tazama hii video inayoonyesha maji yakishindwa kuingia ndani ya hii simu
Kiujumla hii ni simu ambayo haihitaji kava wala screen protector ya ziada
Ni simu chache sana za android ambazo za daraja la kati zinazoweza zuia maji ya kiwango cha mita 4
Hata simu mpya ya bei kubwa ya Xiaomi 12 Pro haina IP68
Ubora wa kamera
Hii ni iphone ya macho matatu yenye kamera aina ya telephoto, ultrawide na wide
Hivyo simu inaweza kupiga eneo pana sana la nyuzi 120
Uwepo wa kamera ultrawide unaiwezesha simu kuzoom kitu cha mbali kwa kutumia lenzi ambazo ubora wa picha haupotei
Ubora wa kamera ya hii simu unaongezwa na kutumika kwa ulengaji aina ya dual pixel autofocus
dual pixel pdaf hulenga na kutambua eneo linalopaswa kupigwa picha kwa haraka
Kamera ya iPhone 11 pro max inarekodi mpaka video za 4K kwa kasi inayofika 60fps
Uzuri ni kuwa kamera ya telephoto na wide zina OIS
OIS hutuliza mitikisiko kwenye video wakati wa kurekodi
Ubora wa Software
Simu inatumia mfumo endeshi wa iOS 13
iOS ufanyaji kazi wake hauendani na Android
japokuwa iOS uko “optimized” kitu kinaachofanya simu kuwa nyepesi
Lakini ule uhuru unaopatikana kwenye android haupo kwenye mfumo endeshi wa apple
Hivi karibuni apple imezindua toleo jipya la iOS 16
iPhone 11 Pro Max ni moja ya simu itakayopata mfumo endeshi mpya kabisa
Yapi Madhaifu ya iPhone 11 Pro Max
Kasoro kubwa ni simu kutokuwa na mtandao wa 5G
Lakini pia simu haina sehemu ya kuweka memori kadi
Kama utanunua simu ya GB 64 ikiwahi kujaa unakuwa hauna mbadala zaidi ya kupunguza mafaili kama unataka kuweka faili jipya
Pia simu haina redio wala sehemu ya kuweka earphone
Neno la Mwisho
Kiujumla bei ya iphone 11 pro max sio kubwa kwa kutazama ubora wa simu kwa nyanja nyingi
Ila ukinunua hii simu Tanzania tarajia bei kuwa kubwa kuliko uhalisia
Kama utaipata chini ya shilingi milioni na laki mbili ni jambo zuri
Vinginevyo ni bora kutazama simu mbadala kama iphone se 2022
Maoni 6 kuhusu “Bei ya Simu ya iPhone 11 Pro Max na Sifa Zake (2022)”
Utofauti Kati ya iphone 11 pro na pro max ni upi ukiachilia size ?
Kuna tofauti ndogo kwenye betri na kioo.
Kioo cha pro max resolution yake kubwa kidogo na betri yake ni kubwa inakaribia 4000mah wakati betri ya iPhone 11 pro ni 3046mah, vitu vingine karibu vyote vipo sawa.
Ninahitaji simu hiyo nipo tabora ninazipenda sana Iphone kwa nguzu kwenye internent
+255789077741
Ombi lako limefika kiongozi
Ninahitaji i phone 11 pro max mpya
Naomba na bei ya i phone 12 pro max