SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Simu za Sony Xperia na Bei Zake Tanzania (2022)

Brand

Sihaba Mikole

April 30, 2022

Kwenye hii posti kuna ufafanuzi na orodha ya simu kumi za sony xperia na bei zake kwa mwaka 2022.

Utazifahamu simu za sony ambazo zimetoka kati ya mwaka 2017 mpaka 2021

Ufafanuzi utakujulisha sababu ya simu za sony kuwa na bei kubwa

Lakini pia utaelewa kiundani ubora wa simu aina ya sony experia unaotofautina na simu nyingi za android

Sony Xperia 1

Simu ya Sony Xperia 1 ni simu ya android ambayo ilitoka mnamo mwaka 2019.

Pamoja na kuwa sokoni muda mrefu, sony xperia 1 ni simu yenye utendaji unaozishinda simu mpya nyingi za android za mwaka 2022

Ubora wa simu aina ya sony xperia unachagizwa na processor yenye nguvu ya Snapdragon 855

Pia kioo chake chake cha OLED ambacho kina uwezo wa kuonyesha rangi zaidi ya bilioni moja.

simu ya sony xperia 1

Sony Xperia 1 ni moja ya simu yenye camera nzuri.

Kwa sababu kamera zake mbili kati ya tatu zina teknolojia nzuri ya ulengaji(autofocus) matata aina ya predictive dual pixel pdaf na predictive pdaf.

Na pia kamera zake zinatumia OIS(Optical Image Stabilization) kutuliza video wakati wa kurekodi.

Changamoto kubwa ya sony xperia ni betri yake kukaa na chaji masaa machache.

Hili linachangiwa na betri yake ndogo ya 3330mAh

Simu ya Sony Xperia haipitishi maji kwa muda wa nusu saa kama ikiingia kwenye maji ya kina  cha mita moja na nusu

Bei ya Sony Xperia 1

Bei halisi ya sony xperia 1 yenye ukubwa wa 64GB na RAM ya 6GB ni shilingi 555,675.00/=

Hii ni bei inayopatikana aliexpress.

Ubora wa simu hii ya sony unaifanya bei yake kuwa ni nafuu sana.

Sony Xperia Pro-I

Simu ya Sony Xperia Pro-I ni simu ya sony ambayo ina kamera nzuri sana

Xperia Pro-I inakuja na android 11 na ni simu inayokubali mtandao wa 5G

Kioo cha sony xperia pro-i kinaonyesha picha kwa ubora wa juu sababu ya ni kioo cha OLED chenye resolution ya 1644 x 3840 pixels

Betri yake ina ukubwa wa 4500mAh japokuwa simu inakaa na chaji kwa masaa machache.

simu ya sony xperia pro-i

Utendaji wa xperia pro-i unaweza kusukuma gemu kubwa za simu kwa resolution ya ultra hd bila shida

Inatokana na simu kuwekewa chip ya Snapdragon 888 5G

Sony Xperia Pro-I ni simu yenye uwezo wa kutopitisha maji kwani ina viwango vya IP67

Kamera zake zinaweza kurekodi video mpaka za 4k kwa spidi ya 120fps na full hd kwa spidi ya 240fps

Bei ya Sony Xperia Pro-I

Bei ya sony xperia Pro-I yenye ukubwa wa 512GB ni shilingi 2,741,175.00/=

Gharama kubwa ya simu inasababishwa na processor yenye nguvu na aina ya kioo ambaccho simu inatumia.

Vitu vingi vya sony xperia pro-I vina uimara na ubora mkubwa

Sony Xperia 1 III

Sony Xperia 1 III ni simu ya android 11 inayokubali toleo jipya la Android 12

Xperia 1 III ni simu ya 5G inayokubali network bands za 4G zipatazo 25

Kwa maana simu inaweza kutumika na mitandao yote ya 4G hapa Tanzania

Kioo cha sony xperia 1 iii ni aina ya OLED kinachoongezewa ubora wa kuwa na resolution na refresh rate kubwa.

Simu ya Sony Xperia 1 III

Refresh rate ya kioo chake ni 120Hz, inafanya simu kuwa nyepesi

Xperia inaweza kucheza gemu zote kubwa kwa ubora wa ultra hd kwa sababu simu ina processor yenye nguvu ya Snapdragon 888 5g

Simu ina kamera nne, tatu zina ulengaji mzuri zaidi sababu zimewezeshwa teknolojia ya dual pixel pdaf

Sony inashika nafasi ya 65 kwa kamera nzuri (Kwa mujibu wa DXOMark)

Ukaaji wa chaji wa xperia 1 iii si mkubwa pamoja na kuwa na betri ya 4500mAh.

Na ina chaji inayopeleka umeme mwingi wa 33W

Bei ya Sony Xperia 1 III

Bei ya sony xperia 1 iii yenye ukubwa wa 256GB na RAM ya 12GB ni shilingi 1,915,769.51/=

Bei yake ni kubwa kwa sababu processor ya simu ina nguvu kubwa

Na kioo cha sony xperia ni vioo vinavyoonyesha picha kwa ubora kitu kinachofanya bei ya kioo kuwa kubwa pia

Sony Xperia XZ3

Simu ya sony xperia xz3 ni toleo la android la mwaka 2018.

Ni simu ya muda mrefu inayoweza kushindana na simu mpya za redmi, oppo, vivo na hata samsung za matoleo mapya ya kati.

Ubora wa sony xperia xz3 unachangiwa na processor ya snapdragon 845 yenye nguvu kubwa.

Simu ya Sony Xperia XZ3

Ubora wake pia unachagizwa na uwezo wa simu kutopitisha maji kwani xperia xz3 ina ip65 na ip68

Kioo cha sony xperia xz3 ni cha p-oled ambacho kimeongezewa uzuri na resolution ya 1440 x 2880 pixels

Kamera ya simu ya xperia xz3 zinaweza kurekodi video za 4K

Uwezo wa sony xperia xz3 kukaa na chaji ni mdogo.

Kwa sababu betri yake ina ukubwa wa 3300mAh

Bei ya Sony Xperia XZ3

Bei ya sony xperia xz3 ya 64GB na RAM ya ukubwa wa 4GB ni shilingi 1,250,199.33/= za Tanzania

Kisifa simu inaendana sana na sony xperia 1

Hivyo unaweza kuchukua xperia 1 iwapo utaona bei ya xz3 kuwa kubwa.

Sony Xperia 5 III

Sony xperia 5 iii ni toleo la sony linalokubali mtandao wa 5G.

Xperia 5 III ni moja ya simu bora ya mwaka 2021.

Ubora wake upo kwenye nyanja za processor, kioo, ugumu wa bodi, network, kamera na uwezo wa kukaa na chaji.

Processor ya simu aina ya sony xperia 5 III ni Snapdragon 888 5G.

simu ya Sony xperia 5 iii

Hii ni chip inayoipa simu nguvu kubwa ya kiutendaji

Simu inatumia kioo cha oled chenye refresh rate kubwa ya 120Hz

Simu ina betri ya 4500mAh inayoweza kukaa na chaji masaa 100 simu ikiwa haitumiki mara kwa mara

Sony xperia 5 III ni simu isiyopitisha maji hata ikidumbukia kwenye kina cha mita moja

Ni sony ya macho matatu yenye mfumo mzuri wa kamera unaweza kuekodi mpaka video za 4K

Bei ya sony xperia 5 iii

Bei ya sony xperia 5 iii ya ukubwa wa 128GB na ram ya 8GB ni shilingi za Tanzania 1,487,976.32/=

Bei ya simu inaendana na sifa zake kwani simu zenye snapdragon 888 5g huuzwa kwa bei inayozidi milioni.

Sony Xperia XZ2

Sony xperia xz2 ni toleo la simu la mwaka 2018

Ni simu yenye uwezo wa kawaida lakini inazizidi simu nyigi mpya za infinix za bei rahisi na bei kubwa

Simu ya sony xperia xz2 ni sony ya kawaida kutokana na aina ya kioo, chip, betri, na chaji

Kioo cha sony xperia xz2 ni cha ips lcd ambacho kiubora kinazidiwa na kioo cha oled

simu ya ony xperia xz2

Betri ya hii simu ni ndogo kwani ukubwa wake ni 3180mAh

Simu ina kamera moja inayoweza kurekodi video za 4K kwa spidi 30fps

Bodi yake haipitishi maji kwani ina ip68

Bei ya Sony Xperia XZ2

Sony Xperia XZ2 ya ukubwa wa 64GB ni shilingi 882,493.65/=

Uwezakano ni kuwa bei yake inaweza kushuka zaidi kwa sababu simu ni ya muda mrefu

Ila inaendana na wakati huu.

Sony Xperia 10 III

Simu ya sony xperia 10 III ni simu ya toleo la mwaka 2021 inaweza kupokea toleo jipya la android 12

Hii ni simu ya daraja la kati inayotumia kioo aina ya oled

Simu inakubali mtandao wa 5G

sony xperia 10 iii

Na ina utendaji mkubwa kwa sababu ya kutumia processor ya Snapdragon 690 5G

Ina betri ya ukubwa wa 4500mAh hivyo ukaaji wa chaji ni wa kuridhisha

Simu inatumia kioo cha oled chenye rangi zaidi ya bilioni

Ni simu ambayo haipitishi maji kwani ina IP68

Sony xperia 10 III ina macho matatu zenye ubora wa wastani

Bei ya xperia 10 iii

Bei ya xperia 10 iii ya ukubwa wa 128GB na 6GB ni shilingi 1,022,983.72/=

Kiushandani simu inaendana na Redmi note 11 pro plus 5G

Ila xperia ina bei kubwa inayosababishwa na ubora wa ziada unaokesakana kwenye redmi

Sony Xperia 5

Sony Xperia 5 ni simu ya mwaka 2019 inayoweza kukubali android toleo la 11

Utendaji wa simu ni mkubwa kwa sababu ina processor yenye nguvu ya Snapdragon 855

Ukaaji wa chaji sio mkubwa kwa sababu simu inatumia betri ndogo ya 3140mAh

simu ya Sony xperia 5

Kioo cha sony xperia ni cha oled kinachoonyesha picha kwa ustadi mkubwa

Simu ni ngumu na haipistishi maji

Simu ina kamera tatu zenye ulengaji wenye usahihi mzuri sababu kamera zinatumia predictive Dual Pixel PDAF

Bei ya sony xperia 5

Sony xperia 5 ni simu ya bei nafuu ya sony

Kwani bei yake ni shilingi 544,041.34/=

Japokuwa ni simu ya 2019 lakini ni mara chache kupata simu ya ubora huu kwa chini ya laki sita kwa sasa

Sony Xperia XZ1

Simu aina ya sony xperia xz1 ni toleo la sony la mwaka 2017.

Ni takribani miaka mitano tangu simu imetoka.

Lakini kiubora inaweza kuzishinda simu mpya nyingi.

Kwa mfano, ni simu chache za daraja la kati na chini zinaweza kuzuia maji kupenya

simu ya Sony xperia xz1

Ila xperia xz1 haipitishi kwani ina viwango vya IP68

Kasoro kubwa ya simu ya xz1 ni betri ndogo ya 2700mAh

Lakini kamera yake inatoa picha bora kutokana na kuwa na Laser AF

Kioo cha sony xperia xz1 ni cha ips lcd ambazo kimeboreshwa na hdr10

Hivyo ubora wa picha kiasi fulani ni mzuri

Bei ya simu ya sony xperia xz1

Bei ya sony xperia xz1 inapaswa iwe chini ya shilingi laki mbili na nusu

Kwa sababu kwa sasa utapata simu hii used na sio mpya

Sony Xperia 10 III Lite

Sony Xperia 10 III Lite ni simu ya mwaka 2021 yenye android 11

Ina utendaji wa wastani kwa sababu simu ina chip ya Snapdragon 695 5G

Kioo cha sony xperia 10 III lite ni aina ya OLED kilicho na ubora zaidi ya kioo cha IPS LCD

simu ya Sony xperia 10 iii lite

Simu ina betri kubwa lenye ujazo wa 4500mAh

Ni simu ya 5G inayokubali network bands za 4G nyingi ikiwemo zote zinazopatikana Tanzania

Bei ya sony xperia 10 iii lite

Bei ya sony xperia xperia 907,007.36/=

Hii ni bei ya sony ya GB 64 na RAM ya GB 6

Maoni 20 kuhusu “Simu za Sony Xperia na Bei Zake Tanzania (2022)

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

[VIDEO]: Simu bora duniani na bei zake 2024

Huu ni muendelezo mwingine wa simu tano ambazo hazitumikii sana na watanzania. Lakini kiulimwengu ni kati ya simu bora duniani kwa mwaka 2024. Hizi ni simu zenye utendaji mkubwa kwenye […]

simu mpya

Simu mpya kali 20 na bei zake kwa mwaka 2024

Hii ni orodha ya simu mpya ambazo zimetoka mwaka 2024 ama mwishoni mwa mwaka 2023 kutoka kwa kampuni zipatazo 11 Ni orodha inayohusisha simu za daraja la kati na la […]

google pixel 8 appearance

Google Pixel 8, Simu ya Teknolojia ya Akili Bandia (AI)

Google Pixel 8 na Pro zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi wa kumi tarehe nne Matoleo mapya ya pixel yatatumia toleo la android 14 Android 14 ilitangazwa tangu mwezi wa pili lakini […]

iphone 15 muonekano

Ujio wa Simu mpya za iPhone 15 Septemba 2023

Kwenye tarehe 12 mwezi wa tisa 2023 kwenye ukumbi wa Steve Jobs makao makuu ya apple kutakuwa kuna uzinduzi wa bidhaa kutoka kwa kampuni ya apple Tukio hili litarushwa moja […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company