SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Simu za infinix za bei rahisi 2022

Bei Nafuu

Sihaba Mikole

April 29, 2022

Hii ni orodha ya simu kumi za infinix za bei rahisi ambazo bado zinapatakana sokoni kwa mwaka 2022

Katika orodha utazifahamu infinix za bei nafuu za mwaka 2020, 2021 na infinix mpya za mwaka 2022

Utafahamu ubora wa infinix zilizopo ambazo bei zake ni chini ya laki tano kwa sasa.

Japokuwa orodha inahusisha simu zisizo na bei kubwa, ila inafaa kujua sifa za kila infinix iliyopo.

Sifa za simu zitakuongoza kuelewa kama simu inakufaa ama haikufai

Infinix hot 10

Simu ya infinix hot 10 ni simu ya android 10 ambayo imetoka mwaka 2020

Infinix hot 10 inakuja na betri yenye ujazo mkubwa wa 5200mAh

Hivyo ni simu inayokaa na moto masaa mengi.

Uwezo wake wa kutendaji ni wa wastani kwa sababu inatumia processor ya daraja la kati ya Helio G70

Display yake haina resolution kwani ni IPS LCD yenye resolution ya 720×1640 pixels

Hivyo ubora wa picha hautokena kwa uzuri

Infinix hot 10 ni simu ya 4G na yenye kamera nne zenye ubora wa chini kwani zinarekodi video za full hd pekee yake

Bei ya infinix hot 10

Bei ya infinix hot 10 yenye ukubwa wa RAM ya  GB 4 na memori ya GB 64 ni shilingi 210,000/=

Ni bei kwa maduka ya simu ya dar es salaam Tanzania.

Ni bei inayoendana na sifa za simu kwa sasa kwani ubora wake ni wa chini

Infinix zero 8

Infinix zero 8 ni moja ya simu bora ya infinix ya mwaka 2020 yenye mfumo endeshi wa android 10

Infinix zeo 8 ni simu ya macho(kamera) manne yenye kamera mojawapo ya resolution 64MP

Betri yake si kubwa sana kwani ujazo wake ni 4500mAh

infinix zero 8

Lakini ni simu inayokaa na chaji kwa masaa takribani 116 simu ikiwa haitumiki mara kwa mara

Inatumia processor yenye uwezo wa kufungua app ya aina yoyote kwa urahisi

Processor yake ni Helio G90T

Upande wa kamera za mbele ina kamera mbili

Kioo cha infinix zero 8 ni cha aina ya IPS LCD.

Kioo chake ni chepesi sababu ya refresh rate inayofika 90Hz na resolution kubwa ya 1080 x 2460 pixels

Bei ya Infinix Zero 8

Wakati simu inatoka bei yake ilikuwa ni shilingi 530,000/=

Lakini kwa sasa kwenye maduka ya kisutu bei ya infinix zero 8 ya 128GB ni shilingi 400,000/=

Bei yake ni kubwa kutokana na uwepo simu zingine za bei rahisi zinazoizidi ubora infinix zero 8

Zitazame, simu za iphone za bei rahisi ambazo zina nguvu na kamera kali

Infinix smart 5

Simu ya infinix smart 5 ni simu ya daraja la mwisho ambayo imetoka mwaka 2021

Kioo cha infinix smart 5 ni cha aina ya IPS LCD chenye resolution ndogo ya 720×1600 pixels

Betri lake lina ukubwa upatao wa 5000mAh hivyo ukaaji wa chaji ni mkubwa

infinix smart 5

Kamera za infinix smart hazitoi picha nzuri na zinarekodi video za ubora wa chini

Utendaji wa simu ni wa kiwango cha chini kinachochangiwa na kutumika kwa chip ya mediatek helio A20

Simu ina vitu vizuri vichache vizuri

Bei ya infinix smart 5

Kwa Tanzania, bei ya infinix smart 5 ya ukubwa wa GB 32 na RAM ya 2GB ni shilingi 180,000/=

Bei yake ni kubwa kwa sababu kuna simu za itel zinazodi smart 5 ubora

Pitia,na uone kwenye hii linki simu za itel zenye ubora kuliko infinix smart 5

Infinix hot 11s

Simu ya infinix hot 11s ni simu ya adroid 11 ambayo imetoka mwaka 2021

Ni infinix yenye betri linaloweza kukaa na chaji masaa mengi sababu ukubwa wake ni 5000mAh

Simu imeundwa kwa plastiki upande wa nyuma na frem hivyo uimara si mkubwa

infinix hot 11s

Kamera zake tatu zina ubora wa kiwango chini kwani ni moja tu yenye resolution kubwa ya 50MP

Utendaji wake una nguvu ya wastani inayoweza kufungua app nyingi ikiwemo magemu

Kioo cha infinix hot 11s ni cha aina ya IPS LCD chenye resolution kubwa 1080 x 2480 pixels

Na ubora wa kioo unachagizwa na refresh rate inayofikia 90Hz ambayo inaifanya kioo chake kuwa kilaini wakati wa kutachi

Bei ya Infinix Hot 11s

Ukiinunua infinix hot 11s ya GB 64 kariakoo bei yake utaipata kwa shilingi 280,000/=

Bei inaendana na sifa za simu kiujumla

Infinix hot 11 play

Infinix hot 11 play ni simu ya 4G ambayo iliingia sokoni mnamo mwishoni mwa mwaka 2021

Kioo cha infinix hot 11 play kinatumia teknolojia ya IPS LCD na simu ni ndefu kwa kimo cha inchi 6.82

Infinix hot 11 play ina kamera mbili tu ambazo ubora wake upo chini

simu ya infinix hot 11 play

Kwani kamera moja tu ina teknolojia ya ulengaji yenye ubora wa chini na nyingine ina resolution ndogo sana (qvga)

Betri yake inastahamili kukaa na chaji muda mrefu sababu betri yake ina ujazo wa 6000mAh

Utendaji wa simu sio mkubwa kutokana na uwepo wa chip ya MediaTek Helio G35

Pia kamera zake mbili zinatoa picha kwa ubora mdogo

Bei ya Infinix Hot 11 Play

Bei halisi ya infinix hot 11 play mpya ya GB 64 ni shilingi 265,000/= kwa maduka ya ilala na kariakoo

Bei itaongezeka kama utanunua ya GB 128

Infinix hot 12i

Kwa mwaka 2022 infinix wametoa simu mpya ya infinix hot 12i

Ni simu ya 4G inayotumia mfumo endeshi wa android 11

Kuielewa ubora na mapungufu yake pitia hii linki, ubora wa kiundani wa infinix hot 12i

infinix hot 12i upande wa nyuma

Lakini kiujumla mfumo wake wa kamera hauna kamera nzuri.

Kioo cha infinix hot 12i ni cha ips lcd ambacho kina resolution ndogo ya 720 x 1612 pixels

Simu hii itapata shida kucheza gemu zanye graphics kubwa kwa sababu ya uwezo mdogo wa processor aina ya MediaTek Helio A22

Bei ya infinix hot 12i

Bei ya infinix hot 12i kwa maduka ya simu ya kariako  ni shilingi 280,000/=

Hii ni bei itakayokupa infinix hot 12i ya 64GB na 2GB ya ram

Bei yake ni ya juu kwa sababu kuna simu ya redmi 9a inapatikana chini ya hapo kama ukiagiza mtandaoni japo huchelewa kufika

Infinix hot 12 play

Simu ya infinix 12 play ni simu mpya ya infinix ambayo imetoka mwaka 2022

Ni simu ya bei rahisi ya infinix ambayo inakuja na toleo jipya la android 12

Kioo cha infinix hot 12 play kina resolution ndogo ya 720×1620 ambayo haionyeshi picha kwa uzuri mkubwa.

simu ya infinix hot 12 play

Betri y INFINIX HOT 12 PLAY inatunza moto muda mrefu kwani ina ukubwa wa 6000mAh

Kwa mujibu wa infiix, betri inakaa na chaji masaa 58 kwa kupiga simu masaaa mengi mfululizo

Utendaji wa hot 12 play ni wa chini kutokana na simu kutumia processor ya Mediatek Helio G35

Kamera zake na zenyewe si za kuvutia kwani hazina teknolojia ya dual pixel pdaf

Bei ya infinix hot 12 play

Bei ya infinix hot 12 play inakadiriwa kuwa ni shilingi 313,740.00/=

Bei yake rasmi bado haijafahamika kwa sababu ni simu mpya kabisa

Infinix smart 6 hd

Simu ya infinix smart 6 hd ni simu ya android 11 ambayo imetoka 2021

Simu ina utendaji wa chini kwa sababu ina chip yenye uwezo mdogo

Chip yake ni Unisoc SC9863A

infinix smart 6 hd

Kioo cha infinix smart 6 aina ya IPS LCD kina resolution ndogo ya 720 x 1600

Uwezo wa simu kukaa chaji ni mkubwa kutokana na utendaji wa chini na betri kubwa la 5000mAh

Simu imeundwa kwa plastiki upande wa nyuma hivyo si imara sana

Na inahitaji kava na screen protector.

Bei ya infinix smart 6

Maduka mengi ya kariakoo nchini Tanzania yanauza infinix smart 6 kwa bei ya shilingi 280,000/=

Hii ni smart 6 ya GB 32.

Japo maduka mengine bei ya simu ni shilingi laki mbili na nusu.

Lakini kiuhalisia bei ya simu ni kubwa

Infinix hot 10 play

Infinix hot 10 play ni moja ya infinix za bei rahisi ambazo zina betri kubwa sana la 6000mAh

Kiasi ambacho kinaipa simu uwezo wa kukaa na chaji masaa mengi.

Ukicheza gemu kubwa la fortnite tegemea utendaji wa chini.

infinix hot 10 play

Kwa sababu processor yake aina ya MediaTek Helio g25 ina nguvu ndogo

Kioo cha infinix hot 10 play ni cha aina ya IPS LCD chenye resolution ndogo ya 720×1640 pixels

Infinix hot 10 play haina kamera nzuri japo ni simu ya macho mawili(kamera mbili)

Bei ya infinix hot 10 play

Ukitembelea baadhi ya maduka ya simu kariakoo utakuta bei ya infinix hot 10 play ni shiling 300,000/=

Hii ni bei ya hot 10 play ya 32GB kwani infinix yenye 64GB.

Infinix hot 9 play

Simu ya infinix hot 9 play ni simu ya android 10 ya mwaka 2020

Pia resolution ya kioo cha infinix hot 9 play haitoonyesha vitu kwa ustadi sababu ina udogo wa 720 x 1640 pixels

Processor yake ya MediaTek Helio A22 inaweza ikawa inapata shida kucheza gemu kubwa za simu kama Call of Duty Mobile

Processor za simu aina ya Helio A22 zina nguvu ndogo

Kamera zake mbili hazitoi picha zenye ubora stahiki kwani hazina dual pixel pdaf na kamera ya pili ina resolution ndogo sana

Betri ya infinix hot 9 play inaweza kukaa na chaji masaa mengi

Betri yake ina ukubwa wa 6000mAh

Bei ya hot 9 play

Bei ya zamani ya infinix hot 9 play ilikuwa ni shilingi 300,000/=

Lakini kwa sasa simu inaweza kupatikana kwa bei ya chini ya laki mbili

Maoni 6 kuhusu “Simu za infinix za bei rahisi 2022

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

nokia thumbnail

Simu mpya za Nokia zilizotoka 2023-2024 na bei zake

Kwa mwaka 2024, kampuni ya HMD Global inayotengeneza simu za Nokia hawajatoa toleo jipya mpaka sasa machi 2024 Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali zinasema HMD inatarajia kutoa matoleo 17 mwaka 2024 […]

Bei ya Tecno Spark 20 na Sifa Zake Muhimu

Tecno Spark 20 ni toleo la Tecno lilotoka mwishoni mwa mwaka 2023 hivyo ni simu inayofaa hata kwa mwaka 2024 Bei ya Tecno Spark 20 yenye ukubwa wa memori ya […]

redmi 10a thumbnail

Bei ya Sasa ya Redmi 10A na Sifa Muhimu

Simu ya Redmi 10A iliiingia sokoni mwaka 2022 Ni aina ya simu inayolenga watu wenye matumizi ya kawaida kama sio machache Hivyo bei ya Redmi 10A ni chini ya laki […]

No Featured Image

Simu Mbalimbali za Vodacom Tanzania na Bei Yake

Hii ni orodha inayohusisha simu ambazo zinauzwa na kampuni ya vodacom na bei zake Kwenye orodha kuna simu zipatazo nane (8) za bei nafuu, kati na bei kubwa Ni simu […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram