SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Simu ya infinix yenye camera nzuri [Infinix Zero X Pro]

Miongozo

Sihaba Mikole

May 8, 2022

Katika orodha ya simu nyingi za infinix ambazo umewahi kuziona ni simu ya infinix zero x pro ndio yenye camera nzuri zaidi

infinix zero x pro muonekano

Japokuwa camera ya infinix haitoi picha nzuri kama samsung galaxy s22 ila inazizidi infinix karibu zote

Ubora wa kamera unatokana na uwezo wa kamera zake kutumia sensa ya Samsung S5KHM2

Kiujumla hii post itakujuisha ubora wake wa picha, aina zake za kamera na usahihi wa rangi wa vitu vinavyopigwa picha

Pia utaoziona picha zilizopigwa na infinix zero x pro

Idadi na aina ya kamera za infinix zero x pro

Infinix zero x ina kamera tatu ambazo ni

  1. Wide yenye resolution ya 108MP
  2. Ultrawide yenye resolution ya 8MP
  3. Periscope telephoto yenye resolution ya 8MP

Kamera kubwa (wide) ina OIS  na inatumia ulengaji (autofocus) aina ya PDAF

infinix zero x pro

Kamera ikiwa na ois inakuwa inarekodi video bila kutikisika

Na kamera kwa ajili ya kupiga vitu vilivyo mbali sana na kamera (periscope telephoto) pia ina OIS na PDAF

Wakati kamera ya ultrawide inayopiga eneo pana kwa nyuzi 120 haina pdaf na ois bali ina AF ya kawaida

Kwa upande wa hardware zero x pro iko vizuri

Huu ndio msingi wa simu kuwa na kamera nzuri kabla ya vitu vingine

Uwezo wa kamera kukusanya mwanga

Kamera aina ya wide inaweza kupitisha mwanga mwingi na kuupeleka kwenye lens ya kamera

Kwa sababu aperture yake ina vipimo vya f/1.8

Ili kamera itoe picha nzuri mwanga wa kutosha unahitajika

Kamera inayopitisha mwanga mdogo hutoa picha mbaya hasa nyakati za usiku

Kamera ya ultrawide na periscope telephoto zinapitisha mwanga wastani kwa sababu vipimo vya aperture ni vikubwa vya f/2.2

Kuelewa kuhusu aperture, pitia hapa sifa za simu zenye kamera nzuri

Ubora wa picha wakati wa mchana

Ubora wa picha unaangaliwa kwa kutumia usahihi wa rangi halisi

Baadhi ya kamera zinatoa rangi ambazo ukizitazama haziendani na jinsi ya kitu kinavyoonekana kwenye uhalisia wake

Infinix zero x pro inatoa picha nzuri kwa kiasi kikubwa nyakati za mchana

Lakini ina tatizo la contrast kiasi fulani

Kwa maana kamera zake zinashindwa kutofautisha rangi kwa usahihi

Hapa tutachukua baadhi ya picha zilizopigwa na infinix zero x pro kutoka gsmarena

Kisha tutathmini ubora wake

Kamera kuu

Kamera kubwa ina sensa inayoweza kupiga picha kwa megapixel 108

Lakini simu inapiga picha za 12MP

Simu kuwa na megapixel kubwa haimaanishi kuwa hiyo kamera ni nzuri

Kiuhalisia 108MP kwenye infinix zero x na simu nyingine hazina ubora wowote unaozizidi kamera za 12MP

Ndio maana simu za iphone huwa na kamera za 12MP

Hii ni picha ya zero x pro kutoka gsmarena

Kwa jicho la haraka simu inajitahidi kuonyesha vitu kwa rangi zake

Lakini kuna sehemu rangi ya vivuri inakuwa kubwa kiasi cha majani kupoteza rangi

Tazama upande wa kulia wa picha kwenye mkusanyiko wa majani

infinix zero x pro main kamera main tone

Kamera inapoteza ubora kwenye mwanga mogo zaidi

Kiasi cha rangi za majani kutoonekana kwa uhalisia wake

Tazama na linganisha picha za eneo hilo hilo ambazo zimepigwa na kamera ya iphone 13 pro max

infinix zero x pro main kamera vs iphone 13 pro max

Kamera ya iphone ina uwezo mzuri wa kutofautisha rangi hata mwanga ukiwa mdogo

Ukitatazama upande wa kulia kwenye kifusi cha majani kamera ya iphone haijapoteza rangi za majani sababu ya kivuli

iphone 13 pro max tone

Kama unavyoona kipande hiki rangi za majani zipo kama zilivyo tofauti na kamera ya infinix zero x pro ambayo haionyeshi kwa usahihi

Hili tatizo linafahmika kama overxeposure na uwezo wa kamera kuwa mdogo kutofautisha rangi za vitu

Kamera ya Ultrawide

Kamera ya ultrawide ya infinix zero x pro inaweza kupiga picha kwa upana wa nyuzi 120

Wakati wa mchana kamera inatoa picha nzuri

Lakini pia ina changamoto ambayo ipo kwenye kamera kuu

Changamoto yake kubwa ni usahihi wa rangi

Na inakumbana na tatizo la over-exposure na contrast inayoshindwa kutofautisha rangi kwa usahihi

Tazama picha ya kamera ya ultrawide ya zero x pro

infinix zero x pro ultrawide daylight

Kisha tazama upande ule ule wa kulia wa kifusi cha majani

Majani yametopoteza ubora wa rangi zake halisi kiasi cha rangi nyeusi ndio kuonekana zaidi

infinix zero x pro ultrawide daylight tone

Kisha linganisha upande huo huo ambao ambao umepigwa na kamera ya ultrawide ya iphone 13 pro max

phone 13 pro max ultrawide tone

Kiujumla zero x pro ina noises ambazo zinaweza onekana wazi

Ila infinix hii inapiga picha nzuri kuliko infinix ambazo unazifahamu

Ubora wa picha nyakati za usiku

Kamera za zero x pro za ultrawide na wide zinatoa picha zinazoweza kuonyesha kila kinachotakiwa wakati wa usiku

Rangi za vitu vinavyopigwa picha zinatokea kwa usahihi wa wastani

Ila contrast yake haziwezi kutofautisha rangi nyeusi ya anga na sehemu zenye mwanga mwingi wa taa

infinix zero x pro main kamera night

Kama unvyoona kwenye logo ya bluu rangi ya bluu imetawala sehemu kubwa

Hii rangi imetapakaa sehemu kubwa kwenda kushoto

Pia inaweza kuonekana upande wa kulia

Kuna sehemu rangi za anga hazikupaswa ziwe na hio rangi ya bluu

Hii inasababishwa na overexposure iliyopitiliza

Ubora wa Video

Kmaera za infinix zero x pro zinaweza kurekodi mpaka video za 4K kwa 30 fps

Baadhi ya video za ubora wa 4k zinaonyesha video kwa ustadi

Ila kuna kiwango cha noise (ukungu ukungu) kwa mbali ambao unaonekana

Hizi hasa ni zile video ambazo zimechukuliwa nyakati za usiku kwenye mwanga mdogo

Itazame hii video ambayo imerekodiwa na zero x pro

Hata video za full hd simu inajitahidi kwa kiasi kikubwa

Ila kamera zake zina ubora wa chini upande wa selfie camera

Utulivu wakati wa kurekodi video

Kama unarekodi video ukiwa unatembea mara nyingi video inatokea kwa kutotulia

Ili tatizo halipo kwenye zero x pro kwa sababu simu ina OIS na EIS

Kirefu cha OIS ni optical image stabilization

Hivyo hautokuwa na wasi mkono ukiwa hautilii wakati wa kuchukua video

Tazama utulivu uliopo kwenye infinix zero x pro wakati wa kurekodi video

Aina ya HDR za kamera

Infinix zero x pro ina kamera ambazo zimewezeshwa HDR ya kawaida

HDR huwa inarekebisha muonekano wa kinachopigwa picha hasa ukiwa kwenye mwanga mdogo

Hivyo inafanya picha na video zionyeshe vitu kama jicho la binadamu linavyoona

Lakini dynamic range ya infinix (HDR) ni ya kawaida

Uboreshaji wa picha sio mkubwa sana ukilinganisha na kamera zenye HDR10 au HDR10+

Na ushahidi upo kwenye picha ya kwanza kabisa.

HDR yake haijasaidia kuonesha rangi za majani kwa usahihi kwenye kifusi cha majani

Hitimisho

Kwa mtumiaji wa simu anayetafuta infinix yenye camera nzuri basi infinix zero x pro itampa picha ambazo ni nzuri na tofauti na simu nyingi za infinix

Ila mtumiaji atalazimika kuongeza bajeti yake ili kuipata simu hii

Tembelea, simu ya infinix zero x pro na bei yake kupata taarifa za kiundani kuhusu infinix hii

Wazo moja kuhusu “Simu ya infinix yenye camera nzuri [Infinix Zero X Pro]

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

infinix note 30 vip thumbnail

Bei ya Infinix Note 30 VIP na Sifa Zake

Infinix kwa mwaka 2023 wameachia matoleo mengi yakiwemo ya note series Moja ya toleo hilo ni Infinix Note 30 VIP ambayo imetoka mwezi Juni Haina tofauti sana na infinix note […]

infinix zero 30 5g thumbnail

Ubora na Bei ya Infinix Zero 30 5G (Infinix Kali)

Ni infinix kwa mara nyingine inajaribu kutengeneza hisia chanya juu ya ubora wa simu zao Unaweza kuliona hili kwa toleo jipya la Infinix Zero 30 5G Hii ni simu kali […]

iphone 15 pro thumbnail

Bei ya iPhone 15 Pro na Sifa Zake Muhimu

Kama ilivyotarajiwa hapo awali kuhusu ujio wa simu mpya za iphone kwa mwaka huu 2023 Moja ya simu hiyo ni iPhone 15 Pro ambayo imeongezewa utendaji Kiumuonekano hauwezi kutofautisha sana […]

iphone feki 2

Simu Origino ni Zipi na Unazitambuaje? (Hatua za kufuata)

Matoleo ya simu yamekuwa yakitoka mara kwa mara yakiwemo yenye bei kubwa na zinazotamaniwa na watu wengi Aina hizi ya simu huvutia watu wasio waaminifu kutengeneza simu feki zenye ufanano […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram