SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Simu ya Infinix Zero X Pro na Sifa Zake (2022)

Sifa za simu

Sihaba Mikole

May 4, 2022

Simu ya infinix zero x pro ni simu ya android 11 ya mwaka 2021

Ni moja ya simu ya daraja la kati yenye bei kubwa, kwani bei ya infinix zero x pro inazidi shilingi laki nane kwa maduka mengi Tanzania

Hii ni infinix ambayo ina ubora mkubwa unaoizidi simu za hot 10 play 

infinix zero x pro muonekano

Ukisoma makala yote utajua bei halisi na sifa zake zinazoifanya simu kuwa na gharama kubwa

Bila kusahau simu mbadala (washindani)

Bei ya Infinix Zero X Pro Tanzania

Maduka ya simu ya kariakoo wanaizua infinix zero x pro kwa bei ya shilingi 820,000/=

Ni bei ya zero x pro yenye ukubwa wa GB 128 na RAM ya GB 8

Swali la kujiuliza,

Bei ya simu inaakisi ubora na je hakuna simu ya bei nafuu yenye ubora unaoizidi zero x pro?

Swali la kwanza jibu utalipata kwa kutazama sifa za simu za infinix.

Pia zipo simu zenye ubora zaidi ya hii zinazopatikana chini kwa laki nane au chini ya hapo

Utafahamu hiyo simu baadae inayoizidi hii simu sifa nyingi

Sifa za simu ya infinix x pro

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – Mediatek Helio G95
  • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.05 GHz Cortex-A76
  • Core Za kawaida(6) – 6×2.0 GHz Cortex-A55
  • GPU-Mali-G76 MC4
Display(Kioo) AMOLED, Refresh rate:120Hz
Softawre
  • Android 11
  • XOS 7.6
Memori UFS 2.2, 256GB,128GB, na RAM 8GB
Kamera Kamera tatu (infinix macho matatu)

  1. 108MP,PDAF(wide)
  2. 8MP. AF(ultrawide)
  3. 8MP, PDAF(Periscope Telephoto)
Muundo Urefu-6.67inchi
Chaji na Betri
  • 4500mAh-Li-Po
  • Chaji-45W
Bei ya simu(TSH) 820,000/=

Upi ubora wa infinix zero x pro

Infinix zero x pro ni infinix ya macho matatu yenye kamera zinazotoa picha nzuri

Kama unatafuta infinix yenye kamera nzuri basi zero x pro inastahili sifa hiyo

Ina mfumo wa chaji unaojaza betri kwa haraka

nfinix zero x pro summary

Betri lake ni kubwa na linatunza moto muda mrefu

Ina kioo kizuri na chepesi kutachi sababu ya kuwa na refresh rate kubwa

Simu ina kuja na memori kubwa inayotoshereza kujaza app nyingi

Kiujumla zero x pro ni simu bora ukifananisha na infinix zero x

Uwezo wa Network

Infinix hii ya septemba 2021 ni simu ya 4G

4g ni aina ya LTE Cat 12 inayokubali masafa 12 yakiwemo yanayotumika na mitandao ya simu nchini Tanzania

Spidi ya juu kabisa ya kudownload ya LTE Cat 12 ni 600Mbps

infinix zero x pro network

Kwa bahati mbaya hakuna laini ya simu inayotoa spidi kubwa ya kiasi hapa nchini

Mtandao wa 4G wenye kasi zaidi kwa sasa Tanzania ni Halotel

Na spidi ya 4G ya Halotel kwa maeneo ya Mwanza ni 42Mbps

Ubora wa kioo cha infinix zero x pro

Infinix ina kioo kizuri kinachoonyesha vitu kwa ustadi na kwa uhalisia kwa kiwango kikubwa

Hii inasababishwa na simu kutumia kioo cha amoled

Ubora wa vioo vya amoled unasababishwa na uwezo wake wa kuonyesha rangi nyingi

Lakini pia kioo chake kimeboreshwa kwa kuwekewa refresh rate kubwa ya 120Hz na resolution ya 1080 x 2400 pixels

Na kama utaitumia simu ukiwa juani kioo kitaonyesha vizuri tu

Kwa sababu uangavu wa kioo cha infinix zero x pro unafikia 700 nits

Nguvu ya processor MediaTek Helio G95

Simu ya infinix zero x pro inatumia processor ya MediTek Helio G95

Helio G95 ni processor ya simu ya daraja la kati yenye utendaji mkubwa na wa kuridhisha

Ina jumla ya core zipatazo nane zinayoifanya simu kuweza kucheza gemu lolote kwa urahisi

Kwenye app ya antutu Helio G95 ina alama 336,000

infinix zero x pro processor helio g95

Na kwenye app ya geekbench chip ina alama 511 kwenye core moja

Hizi ni alama zinazoonyesha processor ina uwezo mkubwa kiutendaji

Hii inachangiwa na aina ya muundo wa core kubwa na core ndogo

Uwezo wa core kubwa

Chip ina jumla ya core zenye nguvu zipatazo mbili

Spidi ya juu kabisa ya kila core ni 2.05 GHz

Kwa maana processor inaweza kufanya kazi kwa mizunguko bilioni 2.05 kwa sekunde

Na zimeundwa kwa muundo wa Cortex A76

Cortex A76 ni muundo unaoifanya chip kuweza kufanya kazi nne kwa mzunguko mmoja

Hii inaipa simu uwezo wa kuweza kufungua app nyingi zinazotumia nguvu kubwa kiurahisi

Pitia hapa kuelewa, kazi ya processor kwenye simu

Uwezo wa core ndogo

Kuna core zenye nguvu ndogo zipatazo sita.

Kikawaida hizi core zinakuwa na mizunguko  michache ya kufanya kazi

Hivyo hutumia nguvu ndogo

Helio G95 core zake ndogo zina spidi isiyozidi 2.0 GHz

Hizi hufanya kazi pale simu inapofanya kazi kama kutuma meseji au kupiga simu (kazi ndogo ndogo)

Uwezo wa betri na chaji

Betri ya infinix zero x pro inaweza kukaa na chaji masaa 119 simu ikiwa inatumika mara chache.

Kama ikiwa inatumia intaneti muda wote chaji yake inaisha baada ya masaa 14

Kiwango cha ukaaji wa chaji kinaendana na samsung galaxy s21 ultra

Infinx ina muda mrefu wa ukaaji wa chaji kwa sababu ya betri lake kubwa la 5000 mAh

Na pia chip yake ina matumizi madogo ya umeme

Chaji ya zero x pro inaweza kujaza betri kwa 40% ndani ya dakika 15

Ukubwa na aina ya memori

Simu ina usafirishaji wa kasi kubwa data kitu kinachofanya simu kuwaka kwa haraka na app kufunguka kwa upesi

Hii inasababishwa na aina ya memori simu inayotumia.

Memori zake ni aina UFS 2.2 ambazo husafirisha data kwa kasi ya 1200MBps

Aina ya memori ina mchango mkubwa katika kuongeza utendaji wa simu

Kuna matoleo mawili ya infinix zero x pro upande wa memori

Kuna infinix ya 128GB na infinix ya 256GB zenye RAM ya 8GB

Uimara wa bodi ya infinix zero x pro

Hii ni infinix ambayo imewekewa glasi upande wa nyuma

Hivyo hautokuwa na mashaka kuhusu kuchunika kwa rangi

infinix zero x pro bodi

Haifahamiki aina ya kioo japokuwa si gorilla lakini uimara wa vioo ni mkubwa kuliko plastiki

Plastiki zimewekwa upande wa pembeni (fremu)

Simu ni ndevu na inavutia kuishika kwani ina urefu na upana wa inchi 6.67

Ubora wa kamera

Infinix zero x pro ni moja ya infinix yenye muundo bora wa kamera

Simu ina kamera ya telephoto inayoweza kupiga picha kitu cha mbali kwa kuzoom mara tano bila kupungua kwa ubora wa picha

Lakini pia kamera zake zinaweza kupiga eneo pana kwa nyuzi 120

infinix zero x pro camera

Kamera yake inarekodi mpaka video ya 4k kwa spidi ya 30fps

Kamera ya infinix zero x pro ina texture inayoonyesha vitu kwa uzuri nyakati za mchana na usiku

Simu inaweza wa kukusanya mwanga wa kutosha na kufanya picha kutokea vizuri mchana na pia kwenye mwanga hafifu.

Ziangalie, picha zilizopigwa na kamera ya infinix zero x pro kutoka gsmarena

Ubora wa Software

Infinix zero x pro inatumia mfumo endeshi wa Android 11 na XOS 7.6

XOS 7.6 ina ulinzi wa kuficha app na data zingine kwa kutumia applikesheni ya XHIDE

Pia ina kitu kinafahamika kama Theft Alert

Hii inafanya simu kupiga alarm ikiwa chaji imechomolewa

XOS inakuwezesha kuchagua vitu ambavyo mtoto anapswa kuviona kwenye simu

Hivyo inapunguza wasiwasi wa mtoto kufungua website zenye picha chafu

Yapi Madhaifu ya infinix zero x pro

Udhaifu mkubwa wa infinix zero x pro ni kukosekana uwezo wa kuzuia maji kupenya

simu nyingi za infinix huwa hazina viwango vyovyote IP hata vile vidogo vya IP53

Display yake haijawekewa HDR10+

Japo ni infinix yenye kamera nzuri, ila kwa kulinganisha na simu za sony, infinix kamera zake ni za chini

Simu haina mtandao wa 5G

Simu nyingi za daraja la kati 2021 zilikuwa zinakuja na 5G

Pia utendaji wa processor yake si wa kiwango kikubwa kinachoendana na bei simu

Neno la Mwisho

Simu ni nzuri kiujumla ila bei yake inaleta utata

Kwa sababu bei ya infinix zero x pro inaweza kununua simu ya Samsung Galaxy S9 used na Redmi Note 11 Pro Plus 5G

Wakati huo redmi inaiacha infinix mbali sana

Pitia hii linki uweze kujua ubora wa simu ya Redmi Note 11 Pro Plus 5G

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

infinix note 30 vip thumbnail

Bei ya Infinix Note 30 VIP na Sifa Zake

Infinix kwa mwaka 2023 wameachia matoleo mengi yakiwemo ya note series Moja ya toleo hilo ni Infinix Note 30 VIP ambayo imetoka mwezi Juni Haina tofauti sana na infinix note […]

infinix zero 30 5g thumbnail

Ubora na Bei ya Infinix Zero 30 5G (Infinix Kali)

Ni infinix kwa mara nyingine inajaribu kutengeneza hisia chanya juu ya ubora wa simu zao Unaweza kuliona hili kwa toleo jipya la Infinix Zero 30 5G Hii ni simu kali […]

iphone 15 pro thumbnail

Bei ya iPhone 15 Pro na Sifa Zake Muhimu

Kama ilivyotarajiwa hapo awali kuhusu ujio wa simu mpya za iphone kwa mwaka huu 2023 Moja ya simu hiyo ni iPhone 15 Pro ambayo imeongezewa utendaji Kiumuonekano hauwezi kutofautisha sana […]

iphone feki 2

Simu Origino ni Zipi na Unazitambuaje? (Hatua za kufuata)

Matoleo ya simu yamekuwa yakitoka mara kwa mara yakiwemo yenye bei kubwa na zinazotamaniwa na watu wengi Aina hizi ya simu huvutia watu wasio waaminifu kutengeneza simu feki zenye ufanano […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram