Kama ni mfuatiliaji utakuwa unajua aina nyingi za tecno ambazo zimetoka hivi karibu
Matoleo ya tecno huwa ni ya kundi la kati na daraja la chini
Katika orodha hii utafahamu baadhi ya simu mpya za tecno katika matoleo ya Camon, Spark, Phantom na Pop
Na bei zake bila kusahahu sifa za kila simu kwa ufupi utakutana nazo
Tecno Camon 20
Simu ya tecno camon 20 ni tecno ya 2023 ambayo iliingia sokoni mwezi mei
Ina kioo cha amoled chenye resolution kubwa
Ni simu ambayo ina memori kubwa ya GB 256 inayotesheleza kuhifadhi mafaili mengi
Chaji yake inajaza betri kwa haraka kwani chaji yake ina wati 33 na betri ya 5000mAh
Hii ni moja ya simu ya tecno yenye IP53 ikimaanisha uwezo wa kuzuia maji yenye kasi ndogo na vumbi pia
Unaweza kuisoma kiundani kuhusu hii simu kwenye huu kurasa
Sifa na ubora wa Tecno Camon 20
Tecno Camon 20 bei yake ni shilingi 600,000 kwa hapa Tanzania
Tecno Camon 20 Pro 5G
Moja ya simu za Tecno mpya yenye utendaji mkubwa ni Tecno Camon 20 Pro
Inatokana na simu kutumia processor yenye nguvu kiutendaji
Kwa mcheza magemu hii simu inafaa sana
Kwenye kioo na yenyewe inatumia kioo cha amoled ambacho resolution yake ni 1080 x 2400 pixels
Na refresh rate ya kioo ni kubwa na inafika kiwango cha juu 120Hz
Pia betri yake ni kubwa inakaa na chaji masaa mengi na kasi yake ya kuchaji ni wati 33
Upande wa kamera zipo tatu ila moja ndio inapiga picha vizuri
Pitia: Ubora wa simu ya Tecno Camon 20 Pro 5G kujua zaidi
Tecno Camon 20 Premier 5G
Kwenye orodha ya matoleo ya Camon 2023, Tecno Camon 20 Premier 5G ndio simu bora zaidi kwa sasa upande wa tecno
Na ndio tecno yenye kamera nzuri zaidi ukilinganisha na tecno zingine
Kamera yake ina uwezo wa kurekodi video za 4K
Kwenye mfumo wa kamera simu inatumia teknolojia mbili za ulengaji ambazo ni Laser AF na PDAF
Na haitoshi kuwa kamera kuu ina OIS ambayo hutuliza video wakati wa kurekodi
Kiutendaji simu inatumia chip yenye nguvu
Kiufupi ni kuwa tecno camon 20 premier 5g inaweza kuwekwa kwenye kundi la daraja la kwanza
Ni simu inayobadirisha mtazamo juu ya ubora wa simu za tecno
Bei ya tecno camon 20 premier 5g inazidi milioni moja
Tecno Camon 20 Pro
Tecno Camon 20 Pro ina ufanano na camon 20
Hata utendaji hautofautiani sana unaendana kwa sababu zote zina processor za helio japo za matoleo tofauti
Kiuhalisia sifa zote unazoziaona za camon 20 ndio zipo kwenye hii simu
Na bei hazitofautiani kwa kiwango kikubwa
Tecno Spark 10C
Matoleo ya Spark huwa ni matoleo ya daraja na bei zake huwa ni ndogo pia
Ni tofauti na na matoleo ya camon
Tecno Spark 10C iliingia sokoni mwezi machi 2023 ikichukua nafasi ya spark 9c
Bei ya tecno spark 10c ni shilingi 410,000
Ukitazama bei utaona ni bei ya wastani hii ni kutokana na sifa za kiujumla za simu kuwa za kawaida
Ambazo hazina vitu vingi
Kwa mfano upande wa kamera kuna camera mbili huku kubwa ikiwa megapixel 16
Zile teknolojia za kwenye camon premier hazipo hapa hivyo ubora wa picha sio mkubwa kiivyo
Tecno Spark 10
Simu ya Tecno Spark 10 inartumia kioo cha IPS LCD chenye resolution ndogo ya 720 x 1612 pixels
Pia ina utendaji mdogo unaofaa kwa kazi zisizohitaji nguvu kubwa kutokana na kutumia chip ya Helio G35
Kiubora tecno spark 10c inaweza ikawa nzuri zaidi ukilinganisha na hili toleo
Ndio maana bei yake sio kubwa na inavumilika
Kwa hapa Tanzania unaweza kuipata kwa kima cha shilingi 315,000
Kuijua hii simu kiundani pitia
Bei ya tecno spark 10 na sifa zake muhimu
Tecno Spark 10 Pro
Kwenye matoleo ya Spark za mwaka 2023 Tecno Spark 10 Pro ndio toleo bora zaidi
Japo si zaidi ya toleo lolote la camon kwa mwaka huu
Kioo chake ni cha ips lcd na resolution yake sio kubwa ila utendaji wa simu ni wa wastani
Yenyewe inasapoti mtandao wa 4G pekee kwani haina uwezo wa 5G
Ina jumla ya kamera tatu na kamera kubwa ina megapixel 50
Ubora wa picha wa kamera ni wa wastani
Ukaaji wa chaji ni wa kuridhisha kwani betri yake ni kubwa inayofika 5000mAh
Bei ya Tecno Spark 10 Pro ni shilingi 415,000
Kuijua kiundani tembelea, ubora na bei ya tecno spark 10 pro
Tecno Phantom x2 Pro
Katika orodha ya simu za tecno 2023 tecno phantom x2 pro ndio simu bora zaidi
Kiutendaji inaizidi simu ya tecno camon 20 premier
Isipokuwa camon premier ina kamera nzuri zaidi ukifananisha na phantom
Ila unapozungumzia nguvu ya utendaji na ukaaji wa chaji phantom x2 pro iko mbele
Chaji yake inapeleka umeme wa wati 45 unaoweza kujaza simu kwa 100% ndani ya dakika 60 tu
Inatumia kioo cha amoled na resolution yake na kubwa
Kwenye kamera, zipo kamera zipatazo tatu ikiwemo kamera ya telephoto
Pia inatumia processor yenye nguvu kubwa aina ya dimensity 9000
Bei ya Tecno Phantom X2 Pro ni shilingi 1,500,000/=
Tecno Pop 7 Pro
Tecno Pop 7 Pro ni simu ambayo imetoka januari mwaka 2023
Katika orodha ya simu zilizopo hii ndio yenye nguvu ndogo sana
Yaani kama wewe unapenda kufanya vitu vingi kutumia simu ikiwemo kucheza magemu hii inaweza kuwa isikufae
Simu inakuja na memori ndogo upande wa ram
Kwani memori yake ni ya GB 64 na RAM ni gb 3(sio mbaya sana)
Moja ya kitu utakachofurahi ni ukaaji wa chaji kwa sababu inatumia chip yenye core chache
Processor za simu siku hizi huja na core nane ila pop 7 pro ina idadi ya core nne pekee
Kwenye kamera pia kuna kamera mbili huku kamera kubwa ikiwa na megapixel 13
Ila kumbuka usiangalie wingi wa megapixel unapofuatilia kamera nzuri
Kwa mfano iphone 13 pro max kamera yake ina megapixel 12 lakini ni moja ya simu zenye kamera nzuri zaidi duniani
Bei ya Tecno Pop 7 Pro ni chini ya laki tatu kwa sasa
Hitimisho
Tecno imetoa matoleo yanayolenga aina nyingi ya watumiaji na kiwango cha kipato
Kwa mtumiaji anayezingatia ubora wa kamera basi matoleo ya phantom x2 na camon 20 yatamsaidia kutimiza haja yake
Kwa ambaye ana pesa ndogo sana chini ya laki tatu au mbili toleo la tecno pop ndio mbadala sahihi
Tofauti na hapo matoleo ya spark yanaweza kukidhi baadhi ya vitu vinavyopatikana kwenye matoleo ya daraja la kati
Maoni 33 kuhusu “Orodha ya Simu Mpya Za Tecno na Bei Zake 2023”
Nikiitaji cm ntaipataje me nipo mkoan
Upo mkoa gani
Kweli mnatoa elimu vzr hongereni
Eeeh kwame nimeweza kujua ubora wa kutumia toreo jipya la simu hasa kwa Tecno ahsante
Infinix hot 13 zipo
Nashida na simu
Ya Aina gani
Naitaji simu nzuri kabisa aina ya Tecno ni ipi ?
Camon 20
Nimeona tangazo kwenye tv mnatoa sim za mkopo bila riba, tecno camoon 20 naipataje
Hayo ni matangazo ya voda nadhani ndio wanaokopesha
haya ni matangazo tu
Naipenda sana kampuni ya Tecno kwa sababu tangia nianze kutumia simu za smart phone sijawahi kubadilisha kampuni nyingine yote ni kwa sababu ya kuimarishwa kwa mfumu wa betri huwa ni tofauti na makampuni mengine.Kwa sasa natamani nipate Tecno Camon 20 naomba msaada jinsi ya kupata.Mimi napatikana Mkoa wa Morogoro wilaya ya Kilombero
Inamaan Camon20 kwa upande wa Tecno ndio simu bora? Nilikuwa na mpango wa kuchukuwa pop7 kumbe ni mbivu?
Kweli mm enyewe nakubali sana Tecno spark 10
Ahsante Kwa kutupa elimu Ili tuweze kuofahamu ipi simu nzuri.
Je, TECNO POVOUR 3 saizi ni pesa ngap
Nimependa
mko vizuri sana mimi bwana nina shida na simu yenye gb 128 Ila Nina 200,000 zipo?? iwe ni TECNO
Haiwezekani
Nahitaji tecno spark 10 pro inauzwa shilingi ngapi kwa sasa? niko kigoma na naipataje
Bei ndio kama hiyo unayoona
Naitaji simu ya 150
Brand yoyote?
Au ya laki mbili2
Kweli nahitaji sim ya 300000 ipinzulizaid
Kama ni tecno kwa bajeti hii matoleo ya spark 20 yanafaa
2najifunza sana kwenu asante kwa elim nzur
Naitaj spark 20
asanteni sana kwa kuja na simu tofauti tofauti zenye uwezo mkubwa na mzur.
Ninashida na phantoms napataje nipo iringa>mafinga
Vipi kuhusu spark go bei yake na ipoje hamjasema
Nataka kujuwa spark go bei yake na ipoje ki ubora