SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Tecno Camon 20 Pro 5G na Ubora Wake

Simu Mpya

Sihaba Mikole

May 28, 2023

Mwaka huu 2023 tecno wameachia simu ya daraja la kati ya Tecno Camon 20 Pro 5G

Ina vitu vipya ambavyo havipo kwenye Camon 19 Pro 5G

Matoleo ya camon ni matoleo mazuri upande wa kampuni ya tecno

tecno camon pro 5g showcase

Hivyo bei ya Tecno Camon 20 Pro 5G inazidi milioni moja kwa hapa Tanzania

Kuna tofauti kubwa sana kati ya hii simu na matoleo ya Tecno Spark

Fuatilia sifa zake ujue sababu ya bei yake kuwa kubwa

Bei ya Tecno Camon 20 Pro 5G ya GB 256

Tecno Camon 20 Pro 5G yenye ukubwa tajwa inauzwa kwa shiligi 1,521,000/=

Ni simu yenye utendaji mkubwa na kioo kizuri na chaji yenye kasi ya kujaza simu kwa haraka

Sifa za hii zinajotofautisha na tecno zingine na ipo kwenye ushindani na simu za madaraja ya kati na ya juu kutoka kampuni zingine

Mfano mmoja wapo ni nguvu kubwa kwenye network na kioo chenye refresh rate

Ila bei yake inaipeleka kwenye ushindani wa simu kutoka Samsung, Xiaomi, Realme na baadhi ya iPhone hasa za zamani

Sifa za Tecno Camon 20 Pro 5G

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
  • CPU – Mediatek Dimensity 8050
  • Core Zenye nguvu Zaidi(1) – 1×3.0 GHz Cortex-A78
  • Core Zenye Nguvu(3)-3×2.6 GHz Cortex-A78
  • Core Za kawaida(4) – 4×2.0 GHz Cortex-A55
  • GPU-Mali-G77 MC9
Display(Kioo) AMOLED, Refresh rate:120Hz
Softawre
  • Android 13
  • HIOS 13
Memori UFS 3.1, 256GB, na RAM 8GB
Kamera Kamera tatu

  1. 64MP,PDAF(wide)
  2. 2MP(macro)
  3. 2MP(depth)
Muundo Urefu-6.67inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-33W
Bei ya simu(TSH) 1,521,000/=

Upi Ubora wa Tecno Camon 20 Pro 5G

Ni simu inayokuja na mtandao wa 5g, utafurahia kasi kubwa kama eneo ulilopo lina 5G

Ina kioo kizuri chenye kuonyesha vitu kwa ufanisi

Ukaaji wa chaji ni mkubwa kutokana na kuwa na betri kubwa

Inakuja na chaji inayojaza simu kwa muda mfupi hivyo hutoisubiria muda mwingi kujaa

Ina mfumo wa memori wenye kasi kubwa ya kusafirisha data

Inakuja na toleo jipya kabisa la android na pi mfumo wa HiOS

Kiujumla ina mazuri mengi ukilinganisha na kasoro

Uwezo wa Network

Simu inasapoti mpaka mtandao wa 5G

Japo kwenye kurasa za tecno haijaelezwa masafa simu iliyonayo ila ina masafa yanayopatika hapa Tanzania na maeneo mengi ya afrika

Kasi ya mtandao  kwenye kupakua vitu inafika 4.5Gbps

Ambayo ni sawa na 562MBps kwa maana kama kama unapakuwa kitu cha MB 1000 kitamalizika kwa sekunde mbili

Ila hii ni kasi ya 5G aina ya mmWave ambayo hapa Tanzania haipo

Kwa sababu kwa Tanzania kuna ya masafa ya kati hivyo kupata kasi kubwa ya namna ni ngumu kwa sasa

Ila sio mbaya kwani makampuni yanaweza kuongeza uwekezaji kwenye sekta ya mawasiliano huko mbeleni

Ubora wa kioo cha Tecno Camon 20 Pro 5G

Kioo cha Tecno Camon 20 Pro 5G ni aina ya amoled chenye resolution ya 1080 x 2400 pixels

Na kiwango cha refresh rate kinafika 120Hz kitu kinachofanya simu kuwa nyepesi unapokuwa unatachi

Uwepo wa kioo cha amoled chenye resolution kubwa inasaidia simu kuonyesha vitu kwa rangi sahihi

Usahihi wa rangi kwenye aina hii ya vioo ni mkubwa ukifananisha na simu za IPS LCD

Hii inatokana na amoled kutokutimia taa za LED kuzalisha mwanga

tecno camon 20 pro 5g display

Pia simu inaruhusu kubadili kiwango cha refresh rate kuwa 90Hz au 60Hz

Kikawaida refresh rate kubwa inaambatana na matumizi makubwa ya betri

Kama betri inakaribia kuisha na haupo maeneo yenye umeme sio mbaya kupunguza kiwango cha refresh rate

Nguvu ya processor MediaTek Dimensity 8050

Simu inatumia processor ya MediaTek Dimensity 8050 kufanya kazi zake zote

Imegawanyika katika sehemu tatu huku sehemu yenye nguvu sana ikiwa na kasi inayofika 3.0GHz

Hizi core zeye nguvu zote zinatumia muundo wenye nguvu aina Cortex A78

Cortex A78 unasifika kuwa na utendaji mkubwa na matumizi madogo ya betri

tecno camon 20 pro 5g processor

Hivyo gemu kubwa zinacheza vizuri bila kukwama kwama na hata kama ikitokea ni kidogo

Ndio maana hata ukaaji wa chaji unachukua muda mrefu kwenye hii simu hata ukiwa unacheza gemu mara kwa mara

Core zenye nguvu ndogo zipo nne na zinatumia muundo wa Cortex A55

Hizi hutumika pale simu inapfanya kazi zinatumia nguvu kwa kiasi kidogo

Uwezo wa betri na chaji

Chaji ya Tecno Camon 20 Pro ina kasi ya kupeleka umeme unaofika wati 33

Aina yake ya chaji ni USB Type C ambazo huwa na kichwa kipana

Betri yake ina ukubwa wa 5000mAh

tecno camon 20 pro 5g chaji

Kwa kasi ya chaji inajaza betri kwa 49% ndani ya nusu saa

Kwa maana hiyo ndani ya dakika 70 simu inachajiwa kwa asilimia 100

Simu inafika zaidi ya masaa 15 ukiwa unaperuzi intaneti muda wote

Ni kiwango kikubwa kwa simu kustahamili muda wote huo na pia simu nyingi zenye betri kubwa zinafika muda huo

Ukubwa na aina ya memori

Kuna toleo la aina moja la camon 20 pro 5g linapokuja swala la memori

Ukubwa wa memori ni GB 256 na RAM ni GB 8

Kiwango cha ram kinaweza kuongezwa kwa GB 5 na hivyo kufanya kuwa na GB 13

Kuwa na ram kubwa ni muhimu kwenye simu za Android

Android huwa zina matumizi makubwa ya RAM  na ndio maana simu zenye ram ndogo sana huwekwa toleo la android Go Edition

Aina ya memori ya hii simu ni UFS  bila shaka kwa sababu processsor iliyopo inasapoti aina hiyo ya memori

UFS husafirihisha data kwa kasi kitu kinachoimarisha utendaji wa simu

Uimara wa bodi ya Tecno Camon 20 Pro 5G

Bodi ya Tecno Camon 20 Pro 5G haipitishi maji yaakiwa kwenye kiwango cha kunyunyuzia

Na pia ina uwezo wa kuzuia vumbi kuingia ndani ya simu

Hii inatokana na simu kuwa na viwango vya IP53

IP53 inamaanisha kuwa kifaa kinazuia maji yenye yanayotiririka kwa kasi ndogo na kiwango kidogo

Ila ukizamisha kwenye maji mengi yataingia ndani ya simu

Pia simu inakuja na kava

Ubora wa kamera

Simu ina jumla ya kamera tatu ambazo ni wide, macro na depth

Ifahamike depth huwa sio kwa ajili ya kupiga picha bali kufanya vipimo na haina umuhimu kama simu ina teknoljia za ulengaji za PDAF

Hivyo kiuhalisia kuna kamera mbili pekee

Kamera kubwa ina megapixel 64 na ulengaji wa PDAF

tecno camon pro 5g camera

Kwenye ubora wa picha simu inajitahidi ila sio sawa kama na simu ya oppo find x6 pro

Inajitahidi kutoa vitu kwa rangi halisi ila kuna hali kuzidi kwa mng’ao kwa mtu mwenye ngozi nyeusi

tecno camon 20 pro 5g photo quality

Kwenye vitu vingine utofautishaji wa rangi ni mkubwa kwa maana dynamic range inafanya kazi vizuri

Ubora wa Software

Tecno Camon 20 Pro 5G inatumia mfumo wa Android 13 na HiOS 13

Kwenye hios 13 kumepunguzwa app zinazokuja na simu, hili ni jambo zuri

Ukiwa unaongea na simu maeneo yenye kelele hios ina mfumo wa akili bandia(AI) unaoondoa hizo kelele

tecno camon 20 pro 5g software

Hivyo unayeongea naye ataweza kusikia sauti yako vizuri

Wenyewe wanaiita AI noise Cancelation

Pia ni mfumo wenye app inayoweza kupangilia picha kwenye makundi yanayoendana

Washindani wa Tecno Camon 20 Pro

Mshindani wa kwanza wa Camon 20 Pro ni Samsung Galaxy A54 5G

Kila unachokiano kwenye tecno samsung anacho na ina bodi ambayo haipitishi maji kabisa

Haitoshi kuwa kioo cha galaxy a54 kina hdr10+ kitu kinchoboresha muonekano wa kitu kwa rangi sahihi zaidi

Na pia samsung imewekewa protekta ya kioo cha gorilla ila bei ya samsung galaxy a54 ni shilingi 950,000/=

Mshindani mwingine ni Redmi Note 12 Pro Plus ambayo inakuja na chaji ya wati 120

Ina kioo cha oled chenye hdr10+ na dolby vision na pia ina kamera ya ultrawide

Wakati huo bei ya Redmi Note 12 Pro Plus ni shilingi 980,000/=

Neno la Mwisho

Kama wewe ni muhitaji wa tecno nzuri weka akilini kuwa Tecno Camon 20 Pro 5G ndio tekno kali kwa sasa

Bei yake ni kubwa ila inaendana na ubora wa simu kwa kiwango kikubwa

Kamera, network na kioo chake kinaifanya camon 20 kuwa moja ya simu bora kwa mwaka 2023

Maoni 12 kuhusu “Bei ya Tecno Camon 20 Pro 5G na Ubora Wake

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

Bei ya Tecno Spark 20 Pro+ na Sifa zake

Simu ya Tecno Spark 20 Pro+ ilitoka rasmi desemba ya mwaka 2023 ila kwa Tanzania imeanza kupatikana miezi ya karibuni Kwa Tanzania bei ya juu kabisa ya Tecno Spark 20 […]

simu mpya

Simu mpya kali 20 na bei zake kwa mwaka 2024

Hii ni orodha ya simu mpya ambazo zimetoka mwaka 2024 ama mwishoni mwa mwaka 2023 kutoka kwa kampuni zipatazo 11 Ni orodha inayohusisha simu za daraja la kati na la […]

Bei ya Tecno Spark 20 na Sifa Zake Muhimu

Tecno Spark 20 ni toleo la Tecno lilotoka mwishoni mwa mwaka 2023 hivyo ni simu inayofaa hata kwa mwaka 2024 Bei ya Tecno Spark 20 yenye ukubwa wa memori ya […]

No Featured Image

Bei ya Tecno Spark 4 na Spark 3 Pro na sifa muhimu 2023

Simu za Tecno Spark 4 na Spark ni simu za daraja la chini za mwaka 2019 Spark 3 ilitangulia kabla ya spark 4 Kiteknolojia, hazina vitu vizuri na hivyo basi […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram