SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Orodha ya Simu Mpya Za Tecno na Bei Zake 2023

Brand

Sihaba Mikole

June 3, 2023

Kama ni mfuatiliaji utakuwa unajua aina nyingi za tecno ambazo zimetoka hivi karibu

Matoleo ya tecno huwa ni ya kundi la kati na daraja la chini

Katika orodha hii utafahamu baadhi ya simu mpya za tecno katika matoleo ya Camon, Spark, Phantom na Pop

Na bei zake bila kusahahu sifa za kila simu kwa ufupi utakutana nazo

Tecno Camon 20

Simu ya tecno camon 20 ni tecno ya 2023 ambayo iliingia sokoni mwezi mei

Ina kioo cha amoled chenye resolution kubwa

Ni simu ambayo ina memori kubwa ya GB 256 inayotesheleza kuhifadhi mafaili mengi

tecno camon 20

Chaji yake inajaza betri kwa haraka kwani chaji yake ina wati 33 na betri ya 5000mAh

Hii ni moja ya simu ya tecno yenye IP53 ikimaanisha uwezo wa kuzuia maji yenye kasi ndogo na vumbi pia

Unaweza kuisoma kiundani kuhusu hii simu kwenye huu kurasa

Sifa na ubora wa Tecno Camon 20

Tecno Camon 20 bei yake ni shilingi 600,000 kwa hapa Tanzania

Tecno Camon 20 Pro 5G

Moja ya simu za Tecno mpya yenye utendaji mkubwa ni Tecno Camon 20 Pro

Inatokana  na simu kutumia processor yenye nguvu kiutendaji

Kwa mcheza magemu hii simu inafaa sana

Kwenye kioo na yenyewe inatumia kioo cha amoled ambacho resolution yake ni 1080 x 2400 pixels

tecno camon pro 5g showcase

Na refresh rate ya kioo ni kubwa na inafika kiwango cha juu 120Hz

Pia betri yake ni kubwa inakaa na chaji masaa mengi na kasi yake ya kuchaji ni wati 33

Upande wa kamera zipo tatu ila moja ndio inapiga picha vizuri

Pitia: Ubora wa simu ya Tecno Camon 20 Pro 5G kujua zaidi

Tecno Camon 20 Premier 5G

Kwenye orodha ya matoleo ya Camon 2023, Tecno Camon 20 Premier 5G ndio simu bora zaidi kwa sasa upande wa tecno

Na ndio tecno yenye kamera nzuri zaidi ukilinganisha na tecno zingine

Kamera yake ina uwezo wa kurekodi video za 4K

Kwenye mfumo wa kamera simu inatumia teknolojia mbili za ulengaji ambazo ni Laser AF na PDAF

camon 20 premier

Na haitoshi kuwa kamera kuu ina OIS ambayo hutuliza video wakati wa kurekodi

Kiutendaji simu inatumia chip yenye nguvu

Kiufupi ni kuwa tecno camon 20 premier 5g inaweza kuwekwa kwenye kundi la daraja la kwanza

Ni simu inayobadirisha mtazamo juu ya ubora wa simu za tecno

Bei ya tecno camon 20 premier 5g inazidi milioni moja

Tecno Camon 20 Pro

Tecno Camon 20 Pro ina ufanano na camon 20

Hata utendaji hautofautiani sana unaendana kwa sababu zote zina processor za helio japo za matoleo tofauti

Kiuhalisia sifa zote unazoziaona za camon 20 ndio zipo kwenye hii simu

Na bei hazitofautiani kwa kiwango kikubwa

Tecno Spark 10C

Matoleo ya Spark huwa ni matoleo ya daraja na bei zake huwa ni ndogo pia

Ni tofauti na na matoleo ya camon

Tecno Spark 10C iliingia sokoni mwezi machi 2023 ikichukua nafasi ya spark 9c

Bei ya tecno spark 10c ni shilingi 410,000

tecno spark 10c showcase

Ukitazama bei utaona ni bei ya wastani hii ni kutokana na sifa za kiujumla za simu kuwa za kawaida

Ambazo hazina vitu vingi

Kwa mfano upande wa kamera kuna camera mbili huku kubwa ikiwa megapixel 16

Zile teknolojia za kwenye camon premier hazipo hapa hivyo ubora wa picha sio mkubwa kiivyo

Tecno Spark 10

Simu ya Tecno Spark 10 inartumia kioo cha IPS LCD chenye resolution ndogo ya 720 x 1612 pixels

Pia ina utendaji mdogo unaofaa kwa kazi zisizohitaji nguvu kubwa kutokana na kutumia chip ya Helio G35

Kiubora tecno spark 10c inaweza ikawa nzuri zaidi ukilinganisha na hili toleo

tecno spark 10 thumbnail

Ndio maana bei yake sio kubwa na inavumilika

Kwa hapa Tanzania unaweza kuipata kwa kima cha shilingi 315,000

Kuijua hii simu kiundani pitia

Bei ya tecno spark 10 na sifa zake muhimu

Tecno Spark 10 Pro

Kwenye matoleo ya Spark za mwaka 2023 Tecno Spark 10 Pro ndio toleo bora zaidi

Japo si zaidi ya toleo lolote la camon kwa mwaka huu

Kioo chake ni cha ips lcd na resolution yake sio kubwa ila utendaji wa simu ni wa wastani

Yenyewe inasapoti mtandao wa 4G pekee kwani haina uwezo wa 5G

tecno spark 10 pro showcase

Ina jumla ya kamera tatu na kamera kubwa ina megapixel 50

Ubora wa picha wa kamera ni wa wastani

Ukaaji wa chaji ni wa kuridhisha kwani betri yake ni kubwa inayofika 5000mAh

Bei ya Tecno Spark 10 Pro ni shilingi 415,000

Kuijua kiundani tembelea, ubora na bei ya tecno spark 10 pro

Tecno Phantom x2 Pro

Katika orodha ya simu za tecno 2023 tecno phantom x2 pro ndio simu bora zaidi

Kiutendaji inaizidi simu ya tecno camon 20 premier

Isipokuwa camon premier ina kamera nzuri zaidi ukifananisha na phantom

Ila unapozungumzia nguvu ya utendaji na ukaaji wa chaji phantom x2 pro iko mbele

Chaji yake inapeleka umeme wa wati 45 unaoweza kujaza simu kwa 100% ndani ya dakika 60 tu

Inatumia kioo cha amoled na resolution yake na kubwa

Kwenye kamera, zipo kamera zipatazo tatu ikiwemo kamera ya telephoto

Pia inatumia processor yenye nguvu kubwa aina ya dimensity 9000

Bei ya Tecno Phantom X2 Pro ni shilingi 1,500,000/=

Tecno Pop 7 Pro

Tecno Pop 7 Pro ni simu ambayo imetoka januari mwaka 2023

Katika orodha ya simu zilizopo hii ndio yenye nguvu ndogo sana

Yaani kama wewe unapenda kufanya vitu vingi kutumia simu ikiwemo kucheza magemu hii inaweza kuwa isikufae

Simu inakuja na memori ndogo upande wa ram

Kwani memori yake ni ya GB 64 na RAM ni gb 3(sio mbaya sana)

tecno pop 7 pro

Moja ya kitu utakachofurahi ni ukaaji wa chaji kwa sababu inatumia chip yenye core chache

Processor za simu siku hizi huja na core nane ila pop 7 pro ina idadi ya core nne pekee

Kwenye kamera pia kuna kamera mbili huku kamera kubwa ikiwa na megapixel 13

Ila kumbuka usiangalie wingi wa megapixel unapofuatilia kamera nzuri

Kwa mfano iphone 13 pro max kamera yake ina megapixel 12 lakini ni moja ya simu zenye kamera nzuri zaidi duniani

Bei ya Tecno Pop 7 Pro ni chini ya laki tatu kwa sasa

Hitimisho

Tecno imetoa matoleo yanayolenga aina nyingi ya watumiaji na kiwango cha kipato

Kwa mtumiaji anayezingatia ubora wa kamera basi matoleo ya phantom x2 na camon 20 yatamsaidia kutimiza haja yake

Kwa ambaye ana pesa ndogo sana chini ya laki tatu au mbili toleo la tecno pop ndio mbadala sahihi

Tofauti na hapo matoleo ya spark yanaweza kukidhi baadhi ya vitu vinavyopatikana kwenye matoleo ya daraja la kati

 

Maoni 18 kuhusu “Orodha ya Simu Mpya Za Tecno na Bei Zake 2023

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

Bei ya Tecno Spark 20 Pro+ na Sifa zake

Simu ya Tecno Spark 20 Pro+ ilitoka rasmi desemba ya mwaka 2023 ila kwa Tanzania imeanza kupatikana miezi ya karibuni Kwa Tanzania bei ya juu kabisa ya Tecno Spark 20 […]

simu mpya

Simu mpya kali 20 na bei zake kwa mwaka 2024

Hii ni orodha ya simu mpya ambazo zimetoka mwaka 2024 ama mwishoni mwa mwaka 2023 kutoka kwa kampuni zipatazo 11 Ni orodha inayohusisha simu za daraja la kati na la […]

Bei ya Tecno Spark 20 na Sifa Zake Muhimu

Tecno Spark 20 ni toleo la Tecno lilotoka mwishoni mwa mwaka 2023 hivyo ni simu inayofaa hata kwa mwaka 2024 Bei ya Tecno Spark 20 yenye ukubwa wa memori ya […]

No Featured Image

Bei ya Tecno Spark 4 na Spark 3 Pro na sifa muhimu 2023

Simu za Tecno Spark 4 na Spark ni simu za daraja la chini za mwaka 2019 Spark 3 ilitangulia kabla ya spark 4 Kiteknolojia, hazina vitu vizuri na hivyo basi […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram