Infinix wamemua kutia mkazo kwa kuja na simu yenye uwezo mkubwa kiutendaji ya infinix zero 5G.
Imezoeleka kuwa simu nzuri za infinix au Tecno hutumia processor za MediaTek zenye ubora wa kati.
Infinix zero 5G ni tofauti.
Imeundwa kwa processor yenye nguvu na memori yenye kasi kubwa ambazo hutumika sana na simu kubwa kama Samsung na Sony.
Kwa mtumiaji wa simu anayepependa performance Zero 5G ni simu pia ya kuweka kwenye orodha.
Kuna maboresho baadhi ya sehemu lakini pia zipo vitu ambavyo havijaboreshwa.
Itazame Infinix Zero katika nyanja zifuatazo.
Processor
Simu ya infinix zero 5G inapewa nguvu ni processor za MediaTek aina ya Dimensity 900 5G
Processor ya Dimesity inasapoti mtandao wa 5G ambao una kasi kubwa kudownload na kuupload.
Kwa eneo lenye 5G nzuri modem ya dimensity 900 inaweza kudownload file mpaka kwa spidi ya 2.77Gbps.
Kwa mfano kama unadownload file la ukubwa 3GB, basi kudownload kutamalizika ndani ya sekunde 9
Dimensity 900 5G imegawanyika katika sehemu(Core) nane, yaani Octacore.
Core zinafanya kazi mkubwa mfano kucheza gemu zipo mbili ambazo zinatumia muundo wa Cortex A78.
Kiuwezo, Cortex 78 inaenda sambamba na Cortex x1 iliyotumika kwenye Snapdragon 888.
Cortex 78 pia inafanya kazi kubwa kwa kutumia umeme mdogo hivyo betri yake inadumu kwa 50% ukilinganisha na Samsung Galaxy S20 5G.
Samsung Galaxy S20 5G ina chip ya Snapdragon 865+ ambayo ina Cortex A77
Application zote zitafunguka vizuri na kwa wepesi.
Core ambazo zimeundwa kutumia betri kidogo zipo sita.
Mara nyingi simu huwa inafanya kazi ndogo za kawaida zisizotumia nguvu kubwa.
Ili kuokoa matumizi makubwa betri, simu hutumia core zenye nguvu ndogo ambazo kenye zero 5g ni Cortex A55.
Upande wa GPU, SoC inatumia Mali-G68 MP4 yenye core 6.
Picha za mnato(animation) za mabarafu yanayoporoka huwa zinaifanya GPU kutumia nguvu kubwa kuonyesha video zake.
Ni njia moja wapo ya kujua ubora na spidi ya GPU.
Mali-G68 MP4 haina spidi kubwa sana yani ni kati kati.
Iwapo simu inacheza gemu la Asphalt 9: Legends, ubora wa picha inabidi upunguzwe kuepuka gemu kukwama.
Bodi ya simu
Bodi ya simu ya simu ya infinix zero 5G imeundwa kwa plastiki upande wa nyuma na kwenye fremu za pembeni.
Glassi ipo mbele lakini sio cha gorilla victus ambacho huwa kinazua simu kupasuka ikianguka kwa kimo cha mita 2.
Pamoja na kuwa na processor Zero 5G haina viwango vya IP.
Umakini unahitajika kwa maana simu ikizama kwenye maji haiwezi kuzuia yasiingie ndani ya simu.
Kampuni inayound simu za tecno na infinix haiwekagi mkazo kwenye usalama wa maji.
Materio ya plastiki huwa yanachunika kwa haraka kadri muda unavyoenda na simu inavyoendelea kutumika.
Upande wa muundo wa simu Infinix Zero 5G haijatendewa haki.
Display
Kioo cha infinix zero 5g ni cha IPS LCD.
IPS LCD ni display ya bei nafuu ambayo ubora wake si mkubwa sana ukilinganisha na AMOLED.
AMOLED huonyesha vitu kwa uhalisia na kwa rangi iliyokolea.
Angalia kwenye hii link ya samsung s22 series
IPS LCD ya zero 5g inakosa HDR10 na kuendelea.
Hivyo video za HDR10 hazitoenesha vitu kwa ubora wake wa awali.
Refresh yake ni kubwa ya 120Hz.
Refresh 120Hz inafanya simu ku-scroll kwa haraka na simu kuwa nyepesi unapotachi.
Hivyo simu inakuwa inacheza gemu vizuri.
Kioo si angavu sana ukiwa unatumia simu juani.
Hii inasababishwa na nits chache za 500.
Hata hivyo nits 500 bado huonyesha vitu vya screen vizuri ukiwa nje nyumba kwenye jua.
Betri na Chaji
Ukubwa wa betri ya infinix zero 5g ni 5000mAh.
Betri ni aina ya Li-Po
Kutokana na kutumia display ya kawaida na processor yenye kutumia umeme mdogo, na betri kubwa Zero infinix inakaa na chaji muda mrefu sana.
GsmArena wameijarabu upande wa betri.
Uvumulivu wa ukaaji wa chaji ni masaa 140.
Simu ikiwa inatumia intaneti betri hudumu kwa masaa 18 mpaka iishe.
Chaji yake inapeleka umeme mwingi wa 33W unaofanya simu kujaaa ndani ya lisaa kimakadirio.
Uchambuzi wa gsmarena umeonyesha chaji ya infinix zero 5g inajaza simu kwa masaa mawili
Kwa bahati simu haina teknolojia ya reverse charging ambayo hutumika kuchaji vifaa vingine.
Lakini pia haina uwezo wa kuchaji kwa wireless.
Memori
Hii ni simu ya infinix ambayo inatumia mfumo wa memori wenye kasi kubwa aina ya UFS 3.1
Simu yenye kasi kubwa ya kudownload vitu inahitaji kuhifadhi vitu kwa haraka ili spidi ya intaneti.
Hivyo mfumo wa memori wenye kasi unatumika sana kwenye simu zenye 5G ili mafaili yaifadhiwe kwa haraka.
Infinix zero 5g ipo ya aina moja tu ambayo memori ina ukubwa wa 128GB.
RAM yake ina ukubwa wa 8GB
Aina ya ram iliyopo kwenye processor Dimensity 900 hutumia chaneli tano zenye bandwidth kubwa.
Kwa hiyo processor inaweza kupokea data nyingi za kuchakata.
Na hivyo simu inaweza kufungua apps nyingi kwa wakati mmoja bila kukwama.
Aina ya RAM iliyopo humu haijainishwa ni ipi kati ya LPDDR4x na LPDDR5
Lakini zote hizi zinapitisha data kwa spidi kubwa na zinatumia umeme kidogo.
Haishangazi infinix zero 5g kuwa simu inayokaa na chaji muda mrefu.
Kamera
Kwa wapenzi wa kamera wanaweza wasivutiwe sana na mfumo wa kamera wa Infinix Zero 5g.
Kamera za infinix zinapiga picha nzuri wakati wa mchana na hata usiku kwwenye mwanga.
Japokuwa kamera ina changamoto hasa upande wa softawre lakini inajitahidi sana.
Kamera ya Infinix Zero inatumia sensor ya Samsung ISOCELL Plus S5KGM1.
Sensa ya Samsung ISOCELL Plus S5KGM1 imetengenezwa na Samsung.
Kwa bahati mbaya kamera kubwa yenye resolution ya 48mp haina OIS wala teknolojia dual pixel AF.
Unapopiga kitu kinachotembea unahitaji kukilenga kwa umakini sana.
Optical zoom yake inazoom kwa kiwango kidogo ukilinganisha na simu ya samsung s22 ultra.
Zero 5g inazoom kitu cha mbali mara mbili wakati s22 ultra ni mara 10.
Lakini ina digital zoom ambayo inaweza kuzoom mara 30.
Optical zoom ni nzuri kuliko digital.
Optical zoom haipotezi ubora wa picha yaani resolution wakati digital zoom inapunguza resolution na kuongeza ukubwa pixel.
Kamera zingine ni hiyo telephoto ambayo resolution yake 13Mp yenye digital zoom na kamera ya tatu ina megapixel 2.
Kamera zinaweza kurekodi video za 4K kwa spidi ya kawaida.
Selfie kamera yake ina megapixel 16 na ina flash light.
Software
Hii ni simu mpya ya infinix ambayo imetoka mwaka huu 2022 lakini inatumia Android 11.
Inawezekana labda simu ikapokea Android 12 huko mbeleni kama infinix watabadilika.
Android 11 ya zero 5g inaambatana na software ya XOS 11.
Ukiwa na XOS uwe tayari kuona apps nyingi ambazo zimewekwa na infinix.
Nyingi ya hizi apps wala hutozihitaji na nyingine zinaleta matangazo mara kwa mara
Ukiachilia na kasoro hiyo XOS inasapoti kutumia apps mbili kwa wakati mmoja(dual apps)
Pia software ya XOS inazima Wi-Fi yenyewe inapoona network haipo inasaidia kupunguza matumizi ya betri
Ina apps ambayo inapunguza ukubwa wa picha bila kupoteza ubora.
Moja jingine zuri la XOS 10 ni app ya youtube kufunguka background.
Kwa maana video inaendelea kufunguka ukiwa unatumia app nyingine.
Bei ya Infinix zero 5g
Bei ya infinix zero 5g kwa maduka ya Nigeria na India ni Tsh 658,100.54
Simu ni nzuri lakini inakosa baadhi ya vitu vya msingi ambavyo vinaweza mfanya mteja kughairi kununua simu nyingine na kuchagua zero 5g.
Zipo simu ambazo zimekamilika kwenye nyanja na zinapatikana kwa bei ya chini ya hiyo.
Kwa mfano Xiaomi Redmi Note 11 (China) inatumia chip ya MediaTek Dimensity 810 na bei yake ni 520,425.00