SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Simu Nzuri za Kuwa Nazo 2022

Miongozo

Sihaba Mikole

February 6, 2022

Kiasi cha pesa iwe kidogo ama kikubwa kinaweza kununua simu nzuri ambayo ina kamera bora, screen ya simu bora, uwezo wa kukaa na chaji muda mrefu, intaneti yenye kasi, SoC(processor ya simu) yenye nguvu, na uwezo wa kujaza betri ya simu kwa haraka.

Simu bora mara nyingi huundwa kwa vifaa imara na vyenye uwezo mkubwa.

Vifaa hivyo huchangia simu kufanya kazi kwa haraka na pia simu kudumu muda mrefu. 

Chukulia mfano wa simu wa samsung galaxy S21+ na iphone 13 pro max.

Simu hizi zina uwezo kuzuia maji na vumbi kuingia ndani ya simu.

Hata ukiizamisha ndani ya maji kwa muda wa nusu saa maji hayaingii.

Zipo simu kali nyingi za bei nafuu zenye ubora kwenye nyanja nyingi mbali na simu za Samsung na iphone.

Hizi ni baadhi ya smartphone zenye sifa nzuri.

Kwa nini Infinix hot 11 play ni ya mwisho na Sony Xperia ni ya kwanza?

Fuatilia sifa za kila simu ujue tofauti ya ubora wa kila simu janja hapo juu.

Sony Experia PRO-I

Sony experia ni smartphone iliyotengenezwa na Kampuni ya Sony ya japan.

Inatumia SoC(System on Chip) ya Snapdragon 888.

Kwenye simu processor hufahamika kama SoC.

Kila kinachofanywa kwenye simu, SoC huchakata na kisha kutoa matokeo unayotarajia simu kufanya.

Kuna processor za simu zenye uwezo mkubwa na mdogo.

Simu nzuri hutumia SoC zenye nguvu.

Snapdragon 888 ni moja ya chipset bora kwenye ulimwengu wa simu kwa sasa.

Chipset ya Sony eperia ina nguvu kwa sababu inaundwa na CPU yenye core(mgawanyo wa processor) 8 yaani octacore.

Core 4 ni processors yenye spidi ya 1×2.84 GHz(inasomeka jigahazi) Kryo 680 na 3×2.42 GHz Kryo 680 maalum kwa ajili ya kufungua vitu vinavyoitaji nguvu kubwa mfano kucheza magemu.

Na Core 4 zilizobaki ni processors zenye spidi ya 4×1.80 GHz Kryo 680

Hizi ni core kwa ajili ya kufanya kazi za kawaida.

Muundo huu husaidia simu kukaa na chaji muda mrefu wakati huo ikifanya kazi kubwa.

Kucheza gemu na kuwasha data inasababisha SoC ya simu kufanya kazi kubwa.

Bila kutenganisha Cores simu mfano wa Sony xperia pro betri yake ingekuwa inaisha chaji haraka sana.

Sony xperia pro-i ni simu nzito kidogo kuibeba kwa sababu ina uzito wa gramu 211.

Simu hii iliyozinduliwa oktoba 26, 2021 ina network(mtandao) ya 5G na 4G.

Na inakubali 4G na 5G ya kila mtandao.

Uwezo wa network wa hii simu ya wajapani ni wa kasi sana.

Inatumia modem ya Snapdragon x60 5g yenye uwezo wa kudownload vitu kwa spidi zaid ya 500Mbps.

Ukiwa unaangalia youtube video haitokwama na kucheza gemu mtandaoni inafaa sana.

Xperia pro-i ina IP68 ambayo ni code inayoomaanisha simu ina waterproof.

Simu yenye IP68 haipitishi maji hata ikizamishwa kwenye kina cha mita 1.5 kwa muda wa dakika thelathini.

Sony xperia pro ni moja ya simu yenye kamera bora katika upande sensors na lens.

Ina kamera nne(4) yaani quad camera ambazo zinapitisha mwanga wa kutosha unaosaidia kamera kwenye picha vizuri kwenye mwanga hafifu.

Japokuwa kamera yake ina resolution ya megapixel 12 bado ni kamera yenye sensa kubwa ya 24mm.

Ikumbukwe megapixel si kigezo pekee cha kamera bora bali huelezea ukubwa wa picha.

Kamera ya sony xperia hutumia OIS(Optical Image Stabilization) kutuliza kamera wakati ukichukua video au selfie huku ukitembea hivyo video kuonekana vizuri bila kutingishika.

Pia ina kamera ya ultrawide ambayo inaweza kupiga picha eneo kubwa kwa upana wa nyuzi 124.

Ina kamera yenye zoom kubwa yaani telephoto yenye uwezo wa kuonyesha kitu vizuri hata kikipigwa umbali wa mita mia.

Kamera yake inaweza kurekodi video yenye resolution kubwa yaani 4k kwa spidi ya 30fps na pia video za 1080 kwa spidi ya 30fps, 60fps, 120fps na 240fps.

Kamera ya nne ni kwa ajili ya kuscan kitu kinachopigwa kiundani ili kila pande ionekane.

Kuna mengi mazuri ya hii simu.

Kiufupi, ina kioo cha OLED kinachoonyeza picha kwa uharisia.

Inajaa chaji kwa haraka kwa sababu inapitisha umeme wa wati 30 unaojaza betri ya simu ya 4500mAh kwa asilimia 50 ndani ya nusu saa.

Vitu vizuri siku zote vina bei.

Bei ya Sony Xperia Pro-i ni shilingi 3,222,450/= za kitanzania.

iPhone 13 Pro Max

Iphone 13 pro max ni simu toka apple ya Marekani iliyozinduliwa mwaka 2021.

Inatumia SoC ya Apple A15 Bionic ambayo inaizidi uwezo kidogo processor ya Snapdragon 888.

Kama ilivyo ada simu nzuri siku zote hutumia processor yenye uwezo mkubwa.

iPhone 13 pro max inatumia ram yenye ukubwa wa 6GB.

Na memory yake(ROM) ni 128gb, 516gb na 1TB. Zipo matoleo hayo matatu.

Aina ya memory iliyomo ndani iphone zinafahamika kama NVMe kirefu chake ni Non Volatile Memory Express.

Ina kasi kubwa kuliko memory zinazotumika kwenye smartphone nyingi (UFS na EMMC).

Ukikopi faili kubwa kwenda kwenye simu ya iphone, faili humalizika kukopi ndani ya muda mfupi sana.

Ina tachi screen aina ya super Retina XDR Oled ambacho kina refresh rate 120Hz.

Hii inasaidia screen kucheza gemu kwa upesi na haraka, pia ku-scroll(kushusha juu au chini) kwa kasi hasa ukiwa unasoma kitabu au ukiwa unatafuta file kwenye folder lenye mafaili mengi.

Iphone pro max huambatana na kamera nne.

  • Main(Wide) yenye 12 megapixel
  • Ultrawide angle inayochukuwa picha kwa upana wa nyuzi 120
  • Telephoto kwa ajili ya kupiga picha vitu vya mbali.
  • Lidar kwa ajili ya kuscan kiundani kitu kinachopigwa picha

Ina 5g na 4g na inakubali frequency za mitandao yote duniani.

Ina IP68 inayozuia maji kuingia ndani ya simu.

Inatumia gollila glass imara kulinda screen ya simu. Hivyo huitaji screen protector.

Betri ya iphone 13 pro max ni aina ya Li-ion na ni kubwa na saizi yake ni 4352mAh.

Betri ya 4352mAh hujaa chaji kwa asilimia 50 ndani ya nusu saa kwa sababu chaji ya iphone hupeleka umeme wa wati 27.

Ni moja ya simu ambayo inakaa na chaji kwa muda mrefu, ikiwa imetulia chaji hukaa kwa masaa 121 ambazo ni sawa na siku tano.

Iphone ina mifumo zaidi ya mitatu ya gps.

Bei ya iphone 13 pro max kwa tanzania ni shilingi 2,310,000/= mpaka 3,500,000/=

Samsung s21 ultra fe 5g

Samsung s21 ultra fe 5g imezinduliwa mwaka 2022.

Inatumia SoC ya Snapdragon 888 5g kwa samsung zinazotumika Marekani na China.

Na SoC ya Exynos 2100 kwa samsung zinazotumika sehemu zingine duniani ikiwemo Tanzania.

 Kwa samsung ya snapdragon ina vitu vingi vinavyofanana na experia pro-I.

Exynos pia SoC nzuri ila ina changamoto zake(Tuweke kipolo)

S21 ultra fe ina ram ya 6gb na 8gb inayowezesha kufungua vitu vingi sana kwenye simu.

Inatumia memory aina ya UFS 3.1 yenye kasi kubwa ya kukopi na kuhifadhi vitu.

Ukubwa wa memory umegawanyika katika makundi matatu.

  • Samsung ya 128gb ram 6gb
  • Samsung ya 128gb ram 8g
  • Samsung ya 256gb

S21 ina uwezo wa kuhifadhi mafaili mengi ya ukubwa tofauti.

Kioo cha Fe 21 5g ni super amoled chenye uwezo wa kuonyesha rangi zaidi bilioni moja.

Tegemea kuona vitu kwa uhalisia.

Pia kuna kamera nne kama zilivyo simu zilizotangulia ambazo zinapiga picha vizuri kwa umbali na upana tofauti tofauti.

Samsung s21 ultra fe 5g kama jina linvyojieleza inaweza kutumia mtandao wa 5g na 4g kwa spidi kubwa.

Betri ya ni aina ya Li-Ion yenye ukubwa wa 4500mAh(Milli A mpere Hour).

Hujaa chaji kwa asilimia 50 ndani ya dakika thelathini(30).

Simu hii ina uwezo wa kutumika kama power bank kwa sababu inaweza kuchaji vifaa vingine.

Ina mfumo wa Reverse charging unaotoa umeme wa wati 15 kuchaji kifaa kingine cha kiilectroniki.

Na pia chaji hupeleka umeme wa wati 27 hivyo husaidia betri kujaa kwa haraka bila kujali ukubwa wa betri.

Bei ya samsung s21 ultra fe 5g ni shilingi 1,337,490/=

Vivo x70 pro+

Simu ya vivo x70 pro+ ni flagship ambayo ilizinduliwa mwezi septemba mwaka 2021.

Screen yake inatumia LTPO Amoled yenye refresha rate ya 120h.

Pia kioo kina HDR10+ ambayo hufanya picha ionekane vizuri ikiwa imechukuliwa kwenye mwanga mdogo.

Simu kali za android za mwaka 2021 nyingi zimepewa nguvu na procsessor(SoC) ya Snapdragon 888.

Vivo x70 pro+ inatumia hiyo chipset vilevile.

Kwa maana hiyo inatet ya hii simu inaweza kutumia network ya 5g yenye kasi.

Na pia inakubali 4g ya mitandao yote duniani

Kwenye upande wa memory, x70 pro+ zipo za matoleo mawili.

Toleo lenye RAM ya 6GB na toleo lenye 12GB.

Simu ya RAM 12GB inafaa sana kwa mtu anaefungua vitu kwenye simu kwa wakati mmoja.

Kwenye upande wa ROM(memory ya kuhifadhi) mafaili zipo za saizi tatu.

  • Vivo x70 pro+ ya  256GB inatumia RAM ya 6gb
  • Vivo x70 pro+ ya  256GB inatumia RAM ya 12gb
  • Vivo x70 pro+ ya  512GB inatumia RAM ya 12gb

Kiuhalisia kutokana na aina ya kamera ya hii simu, memorykubwa ni muhimu.

Kwa sababu kamera ya x70 pro+ ina megapixel 50.

Hii inamaanisha picha ama video zitakazokuwa zinapigwa na kamera zitakuwa ni kubwa.

Hivyo kuchukua nafasi kubwa ya simu.

Umeshawahi kusikia neno gimbal?

Gimbal ni aina ya IOS iliyoboreshwa na kampuni ya vivo.

Gimbal hufanya picha au video kuonekana vizuri hata ukiwa unakimbia ama kutembea.

Vivo ina kamera nne na zote zimetengenezewa OIS.

Wide, ultrawide na telephoto mbili.

Selfie Kamera ina megapixel 32 ni kubwa kiuhalisia.

Baadhi ya wachambuzi wanaitunuku Vivo x70 pro+ kuwa simu yenye kamera kali zaidi mpaka sasa.

Ila simu hii ina changamoto ya ukaaji wa chaji betri yake ni ndogo yenye ukubwa wa 4500mAh.

Kwenye matumizi ya kawaida inakaa na chaji masaa 84.

Bei ya simu ya vivo x70 pro+ ni shilingi 2,122,566.60/=

Xiaomi 11t pro

Ni simu ya bei nafuu yenye vitu vikali na bora.

Inatumia processor ya snapdragon 888 hivyo inafanana vitu vingi na simu zenye SoC hii.

Kitu kikubwa cha tofauti na simu zingine nyingi ni uwezo wake wa fast charge(chaji ya haraka).

Chaja yake hupeleka umeme wa wati 120.

Ndio ni wati 120.

Betri yake ina ukubwa wa 5000mAh ni Li-Ion.

Kwa umeme wa wati 120 betri yake hujaa asilimia 70 kwa haraka ndani ya 10 tu.

Kwa nyakati hizi za umeme kukatika mara kwa mara hii ni simu nzuri ya kuwa nayo.

Na inaweza kukaa na chaja kwa matumizi ya kawaida kwa muda wa masaa 92.

Simu ya Xiaomi 11t pro ina ram ya ukubwa wa 8gb na 12bg.

Zipo 11t pro zenye memori za ukubwa wa  128gb na 256gb.

Simu haina sehemu ya kuweka memory card yaani memory ya ziada kama 128gb au 256gb ikijaa.

Na zote ni memory zenye kasi kubwa aina ya UFS 3.1

Upande wa kamera ni wa kawaida sana.

Xiaomi 11t pro ina kamera tatu ambazo hazina OIS.

Ukipiga picha au video huku unatembea picha inaweza isitokee vizuri.

Au kinachopigwa picha hakitulii picha inaweza isitokee vizuri vilevile.

Kioo chake ni Super Amoled  chenye kuonyesha vitu kwa ubora na uharisia.

Huku ikiwa na refresh rate ya 120hz na hdr10+

Simu ya xiaomi 11t pro inagharimu kiasi cha shilingi 1,420,650/=

Simu nyinginezo

Simu yenye ubora wa juu zilizobaki ni oppo reno 6 5g ina vitu vingi sana vinavofanana na simu zingine na ina 5g vile vile.

Na inatumia SoC yenye nguvu Snapdragon 870.

Simu zilizobaki ni za kawaida ambazo nimeona niziweke.

Simu hizo ni Huawei reno 9, Tecno phantom x, nokia g20 na Infinix hot 11 play hazina 5g.

Zina vitu vichache sana vinavyoipa smartphone ubora.

Tutazitathmini kiundani nyakati zingine.

Maoni 6 kuhusu “Simu Nzuri za Kuwa Nazo 2022

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

google pixel 8 appearance

Google Pixel 8, Simu ya Teknolojia ya Akili Bandia (AI)

Google Pixel 8 na Pro zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi wa kumi tarehe nne Matoleo mapya ya pixel yatatumia toleo la android 14 Android 14 ilitangazwa tangu mwezi wa pili lakini […]

iphone 15 muonekano

Ujio wa Simu mpya za iPhone 15 Septemba 2023

Kwenye tarehe 12 mwezi wa tisa 2023 kwenye ukumbi wa Steve Jobs makao makuu ya apple kutakuwa kuna uzinduzi wa bidhaa kutoka kwa kampuni ya apple Tukio hili litarushwa moja […]

oppo find x6 pro thumbnail

Oppo Yenye Kamera Nzuri na Ubora wa Picha

Kuna matoleo mengi ya simu za oppo zenye ubora tofauti tofauti Zipo ambazo zina ubora wa kati, wa juu na wa chini Katika hizo, nyingi zinajitahidi kuwa na kamera zinazotoa […]

No Featured Image

Simu Mpya za Samsung na Bei Zake 2023

Kama unatafuta samsung mpya kwa mwaka 2023 basi upo sahihi Kwenye hii kuna simu zipatazo saba na maelezo mafupi kuhusu sifa zake Kwenye hii orodha ya simu mpya za samsung […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram