SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Simu za samsung galaxy S22, S22+ na S22 Ultra 5G

Simu Mpya

Sihaba Mikole

February 15, 2022

Samsung electronic imezindua simu mpya za samsung galaxy S22.

Simu zilizozinduliwa ni tatu

 • Samsung galaxy S22
 • Samsung galaxy S22+
 • Samsung galaxy S22 ultra.

Kimuonekano simu zote zinafanana kiasi kikubwa na Samsung note Series ambazo zilisitishwa kutengenezwa mwaka 2020.

Matoleo mapya ya galaxy yameboreshwa kiufanisi na kiuwezo.

Vitu vilivyoimarishwa ni GPU, processor na Software bila kusahau upande wa chaji.

Simu ya Samsung galaxy s22 ultra ina betri kubwa kuliko samsung galaxy S22 na S22+

Wataalamu wa simu wameshaanza kuzichambua na kuzijaribu.

Kwa ufupi, tuangazie sifa za samsung galaxy katika nyanja nane.

 1. Processor
 2. Memory
 3. Bodi ya simu
 4. Display(Kioo)
 5. Betri na mfumo wa chaji
 6. Bei
 7. Kamera
 8. Washindani

Kwa kuzifahamu simu hizi katika pande nane inasaidia kuutambua ubora wa matoleo ya samsungĀ  ya 2022.

Processor (SoC)

Samsung galaxy S22 series zimeboresha processor kwa kuweka chip mpya ya Snapdragon 8 gen 1 na Exynos 2200.

Simu za samsung za snapdragon 8 gen 1 huuzwa Marekani na Exynoss 2200 huuzwa kwenye soko la kimataifa nje ya USA.

Processor zote za Snapdragon 8 gen 1 na Exynos 2200 zinatumia muundo wa Cortex X2 kwa core zenye nguvu.

Na cortex A710 zenye nguvu kiasi na Cortex A510 kwa core zenye nguvu ndogo.

Kuhusu cortex x2, qualcomm wanadai ufanisi wa matumizi ya chaji ni mkubwa kwa 30% kulinganisha Cortex x1 iliyotumika kwenye samsung galaxy s21.

Kwa maana hiyo Galaxy S22 inaweza kukaa na chaji mpaka masaa 17 ikiwa inatumia intaneti kwa sababu majaribio ya betri ya Galaxy S21 yalionyesha betri inakaa na chaji kwa muda masaa 15.

Chipset ya exynos 2200 ina GPU ya Xclipse 920 ambayo imebuniwa na AMD, imeonyesha kuwa na ubora kuliko GPU ya snapdrago 8 ambayo ni Adreno 730

Test za OpenCL zimeipa point nyingi Xclipse ukilinganisha na test za kwenye Adreno 730 zilizofanywa kwenye simu za oneplus.

Fuatilia ripoti za gpu hapa: Xclipse 920 vs Adreno 730

Jambo la mwisho kuhusu socs ni kuwa na modem za 5G.

Kweye upande wa network Snapdragon ni “beast” siku zote huwa yupo mbele.

Chip snapdragon 8 gen 1 ina modem ya Snapdragon X65 5G Modem-RF System.

Ni modem yenye spidi kubwa ya mtandao wa 5G kwa sasa.

Na inasapoti aina za 5G karibu zote.

Bodi ya simu

Simu ndevu zaidi kati ya hizi tatu ni Samsung galaxy S22 Ultra 5g.

Galaxy S22 Ultra ina kimo cha inchi 6.4 na upana wa inchi 3.07 na wembamba wa inchi 0.35.

Vipimo hivyo vikubwa vinachangia simu kuwa nzito(gramu 228) kuliko galaxy 22+ na galaxy 22.

Kwa wapenzi wa screen kubwa hilo ndio chaguo zuri.

Simu inafuatia ni S22+ na simu ndogo zaidi ambayo ni “portable” ni S22.

Moja ya kitu kizuri kwa smartphone hizi ni kuwa na viwango vya IP(Ingression Protection)

IP huonyesha ulinzi wa simu dhidi ya maji na vumbi kupenya ndani ya simu.

Simu zote zina IP68, kwa maana maji hayawezi penya pale simu inapodumbukia kwenye kina cha mita 1.5 kwa muda wa nusu saa.

Ni vizuri ukawa makini kwa sababu IP68 inaweza isiwe msaada simu ikizama kwenye pool au bahari.

Upande wa display unalindwa na protector ya glass aina ya gorilla Glass Victus+.

Gorilla glass victus+ pia ipo nyuma ya simu zote za samsung s22, upande wa pembeni simu ina alumunium.

Gorilla glass victus ni kioo kigumu kupasuka iwapo simu imeanguka kwa urefu wa mita 2

Tazama majaribio ya kugandamiza na kuangisha simu yenye kioo cha Gorilla glass victus.

Display(Kioo)

Kwa sifa ambazo zimeshaainishwa zinaonyesha tu kuwa matoleo ya Samsung S22 yana ubora mkubwa.

Kama ilivyoada simu bora mara nyingi hutumia vioo vya amoled.

Samsung s22, s22+ na ultra zina display ya dynamic amoled 2x.

Dynamic Amoled ni display ambayo imeboreshwa rangi kwa uwiano mzuri rangi.

Amoled hii haitoi miale ya bluu kama samsung wanavyodai.

Miale ya bluu huuminza macho ukiwa unatumia muda mrefu.

Kwa wapenzi wa gemu watafurahia uwepo wa refres kubwa ya 120Hz, gemu inakuwa fasta.

Ukifungua folder lenye mafaili basi faili lako utalipata kwa haraka kwa sababu ukiwa una-scroll screen kwenda chini mafaili yanaenda juu kwa haraka sana.

Kioo cha samsung s22 ni angavu na kinaonyesha vizuri hata ukiwa kwenye jua kali.

Hili linachaguzwa na kuwa na nits nyingi zinazokaribia 1700.

Betri na Chaji

Hii ni sekta ambayo Samsung galaxy s22 ultra imetofautiana na galaxy 22 na galaxy 22+

Kitu ambacho kipo sawa upande wa betri ni aina ya betri ambayo ni Li-Ion

Hii ni tofauti na simu nyingi za oppo au xiaomi ambazo hutumia betri za Li-Po

Samsung s22 ina betri kubwa la 5000mAh.

Samsung S22+ ina betri la wastani la 4500mAh wakati S22 betri lake lina ukubwa wa 3700mAh.

Sijui kwa nini wamepunguza ukubwa wa betri kwenye galaxy zingine.

Izingatiwe hizi simu zinatumia processors zenye nguvu.

Japokuwa Qualcomm wanasema ufanisi kwenye chaji umeongezeka, bado hizi processor zitatumia umeme mkubwa.

kuna uwezekano wa Samsung galaxy s22 kutokukaa na chaji muda mrefu ukilinganisha na wenzake.

Ukiitazama simu za infinix kwa mfano huwa wanaweka betri kubwa japo kiuwezo simu zake si mkubwa.

Kitu kimoja wapo kizuri ni uwezo wake kuchaji simu kwa haraka.

Simu zote zina fast chaji ila kiasi cha kupeleka umeme kinatofautiana.

Galazy s22 inapeleka umeme wa 25W wakati Samsung galaxy ultra 22 na 22+ chaji zake zinapeleka umeme wa 45W.

S22 inaweza kuchelewa kujaa ijapokuwa betri lake ni dogo.

Simu zote zina teknolojia ya “Reverse Charge” kwa maana zinaweza kuchaji vifaa vingine mfano wa simu.

Kama vile unavyoona laptop inavyoweza kuchaji kwa kutumia USB basi galaxy hizi pia zinaweza kuchaji simu nyingine tena kwa umeme wa 15W

Kamera

Kamera za samsung zina vitu vingi ambavyo vipo sawa na simu nyingine za samsung.

Galaxy S22 na Galaxy 22+ zina kamera tatu na Galaxy Ultra S22 ina kamera nne.

Kamera mbili za Galaxy S22 na Galaxy 22+ zina OIS na kamera kubwa pia zina dual pixel PDAF.

OIS hutuliza kamera kamera wakati ukichukua video huku unatembea.

Wakati dual pixel PDAF hufanya kamera kulenga kitu kinachotembe kupigwa kwa usahihi.

Kwa mfano ukiwa unapiga picha mwewe akiwa angani, kamera inakuwa inatrak mwendo wa mwewe hivyo ukipiga picha inatokea vizuri.

Kamera kuu ya S22 Ultra ina megapixel 105 wakati zingine zina megapixel 50.

Kamera za Telephoto zote zina megapixel 10, Hizi ni kamera kwa ajili ya kupiga vitu vya mbali kwa kuzoom.

Zoom yake ni aina ya optical zoom ambayo husogeza lens mbali na sensor ya kamera.

Pia kamera zinazotumuka kupiga eneo pana(ultrawide) zina megapixel 12, galaxy Ultra 22 ina telephoto mbili.

Telephoto moja inafahamika periscope telephoto ambayo inaweza kuki-zoom kitu cha mbali mara 10 na picha ama video ikaonekana vizuri.

Memori

Ukiwa na simu ambayo inasapoti mtandao wa 5G na processor yenye nguvu, basi ufanisi unakuja simu ikiwa na mfumo wa memori wenye kasi.

Simu za samsungĀ  galaxy s22 zinatumia storage(memori) aina ya UFS 3.1

UFS 3.1 huwa ina kasi kubwa sana kuhifadhi vitu.

Pitia hapa uifahamu aina za memori.simu bora za kuwa nazo

Upande wa samsung galaxy 22 na samsung galaxy 22+ zipo zenye ukubwa wa 256GB na 128GB na RAM 8G.

Wakati memori za Samsung galaxy S22 Ultra zipo zenye ukubwa wa 128GB, 256GB, 512GB na 1TB.

RAM zi za 8GB na 12GB

Software

Simu zote zimewezeshwa Android 12 na One UI 14.1

Bei za Samsung galaxy s22

Samsung galaxy S22 – 1,849,600

Samsung galaxy S22+ – 2,312,000

Samsung galaxy S22 Ultra-2,768,491

Maoni 2 kuhusu “Simu za samsung galaxy S22, S22+ na S22 Ultra 5G

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

No Featured Image

Simu Mpya za Samsung 2024 (za bei rahisi na ghari)

Kuna simu zaidi ya tisa zilizotengenezwa na kampuni ya Samsung kutoka Hapa kuna orodha ya simu kumi mpya za samsung ambazo zimetoka mwishoni mwa mwaka 2023 hadi mwaka 2024 Ni […]

Bei ya Samsung Galaxy A25 na Sifa zake

Simu ya Samsung Galaxy A25 ilitoka rasmi mnamo mwezi desemba 2023 Ni simu ya daraja ambayo bei yake kwa Tanzania ni shilingi laki saba (700,000/=), hii ikiwa ni bei ya […]

samsung galaxy a15 thumbnail

Bei ya Samsung Galaxy A15 na Sifa Muhimu

Mwezi wa desemba 2023 ni mwezi ambao Simu ya Samsung Galaxy A15 ilizinduliwa Ni simu ya daraja la kati ambayo ina vitu vichache vinavyopatikana kwenye samsung za bei kubwa Ndio […]

samsung a55 showcase

Bei ya Samsung Galaxy A55 na Ubora wake

Samsung Galaxy A55 imetoka mwezi machi mwaka 2024 na ni simu ya daraja la kati Bei ya Samsung Galaxy A55 kwa Tanzania ni shilingi milioni moja na laki moja na […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram