Moja ya sifa za kipekee ya simu ya samsung galaxy a22 ni uwezo wa simu kukaa na chaji muda mrefu
Kiukweli ukaaji wa chaji wa Samsung Galaxy A22 unaizidi simu mpya ya samsung galaxy s22 ultra
Simu ina sifa chache nzuri ila zinashawishi kuimiliki
Ni moja ya simu nzruri ya samsung iliyotoka mwishoni mwa mwaka 2021
Sifa zingine hazina upekee mkubwa kiasi cha kwamba inafanya simu kuwa ya kawaida.
Ni simu nzuri ya tabaka la chini kutoka samsung kwa kuangalia ubora wa sifa.
Sifa za Samsung Galaxy A22
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super AMOLED, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | eMMC, 128GB,64GB na RAM 6GB,4GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.4inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 501,753.78/= |
Upi ubora wa Samsung Galaxy A22
Ubora wa kioo cha super amoled ni ubora mkubwa wa samsung galaxy A22
Simu ya samsung galaxy A22 ina utendaji wa kuridhisha kutokana na kuwa na chipset yenye utendaji mkubwa
Betri yake ni kubwa ambayo inakaa na chaji muda mrefu sana.
Ni simu chache za samsung zinaweza kutunza moto muda mrefu kama Galaxy a22
Moja ya kamera yake ina teknolojia ya kutuliza kamera kutikisika
Network
Samsung galaxy a22 inakubali aina zote za mtandao isipokuwa 5G.
4G ya simu ni ya kundi la 7 (lte cat 7)
Spidi ya juu kabisa ya cat7 ya kudownload ni 301.5Mbps ambayo ni sawa na 37.68MBps
Spidi hii inadownload file la ukubwa wa 1300MB kwa sekunde 35, inategemea na aina ya mtandao
Simu hii ya samsung ina network bands za 4G kumi.
Bands hizo ni 1, 3, 5, 7, 8, 20, 28, 38, 40 na 41
Hivyo laini zote za simu zinakubali intaneti ya 4g hapa Tanzania
Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy A22
Kioo cha samsung galaxy a22 ni aina ya super amoled.
Resolution ya kioo ni 720 x 1600 pixels
Na uangavu wake unafikia 600nits
600nits huweza kuonyesha vitu vizuri simu ikiwa inatumika juani
Vioo vya amoled vina rangi zinaofikia bilioni moja.
Idadi kubwa ya rangi hufanya kioo kuonyesha rangi za vitu kwa usahihi wa juu
Ila resolution ya hii simu ni ya kawaida
Bei ya kioo cha samsung aina ya super amoled ni gharama, kuwa makini utumiapo simu
Nguvu ya processor MediaTek Helio G80
Processor ya MediaTek Helio G80 ndio ubongo wa Samsung galaxy a22.
Ni processor yenye core nane(octacore)
Core zenye nguvu zipo mbili na zenye nguvu ndogo zipo sita.
Chip ya helio g80 ina utendaji wa wastani kwenye simu nyingi zinazotumia hii processor
Hilo linatokana na namna core zilivyoundwa
Uwezo wa core zenye nguvu kubwa
Kila core yenye nguvu ina spidi inayofikia 2.0GHz
Core zenye nguvu za Helio g80 zimeundwa kwa kutumia Cortex A75
Cortex A75 inaweza kusukuma gemu nyingi unazozifahamu kiurahisi
Kwa sasa utendaji wa Cortex A75 unazidiwa na Cortex A77 ambao una matumizi mazuri ya umeme
Kiujumla muundo huu unakuwezesha kucheza gemu la Mobile Legends: Bang Bang kwa spidi ya 57fps kwa resolution kubwa
Ni core zenye kasi kubwa
Uwezo wa core zenye nguvu ndogo
Core zenye nguvu ndogo zimeundwa kwa kutumia muundo wa Cortex A55
Cortex A55 inatumia umeme mdogo sana pale simu inpofanya kazi ndogo ndogo.
Kama unapenda kupiga simu tu simu inakaa na chaji muda mrefu
Kila core ina kasi ya 1.8GHz
Cha kufurahisha Cortex A55 ina utendaji mkubwa kidogo ukilinganisha na cortex a53 iliyopo kwenye simu ya Nokia G20 yinayotumia chip ya simu ya Helio g35
Alama za antuntu na geekbanch
antuntu na geekbench hizi ni app zinazopima uwezo wa processor za simu
Processor ya Helio G80 inachuana na snapdragon 680 4g kwenye alama za antuntu n geekbench
Chip ya Helio g80 ina alama 353 kwenye core moja(geekbench)
Wakati Antutu inaonyesha alama 66,889
Kwa kuzingatia hizo point Helio g80 inazidiwa na Snapdragon 680 iliyopo kwenye simu ya Samsung galaxy A23
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya samsung galaxy a22 ina ukubwa wa 5000mAh
Na chaji yake inapeleka umeme wa wati 15
Kiasi hiki cha umeme kinajaza betri si chini ya masaa mawili
Betri yake infanya simu kukaa na chaji masaa 121 simu ikiwa imetulia (gsmarena)
Kwa mujibu wa GSMarena Samsung galaxy a22 inakaa na chaji masaa 17 simu ikiwa inatumia intaneti yaani data ikiwa ON masaa yote
Ukubwa na aina ya memori
Samsung galaxy a22 inatumia memori aina ya eMMC.
Kasi ya eMMC ni ndogo ukilinganisha na memori aina ya UFS
Na aina ya ram iliyotumika ni LPDDR4x zinazotumia umeme mdogo kusafirisha data
Zipo aina tatu za simu ya samsung galaxy a22
- 128GB ROM na 4GB RAM
- 128GB ROM na 6GB RAM
- 64GB ROM na 4GB RAM
Bei ya simu inatofautiana kulingana na ukubwa wa memori
Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy A22
Bodi ya simu imeundwa kwa plastiki upande wa pembeni na nyuma.
Ina ulinzi wa kioo lakini sio aina ya gorilla
Simu ni nzito kidogo kwa maana ina gramu 186
Ina urefu wa inchi 6.4 na inajaa kwa kiasi kikubwa kwenye mkono
Bodi za plastiki zina changamoto ya kuchunika rangi
Hivyo utahitaji kava ya simu kuzuia hilo
Ubora wa kamera
Simu ya samasung galaxy a22 ina kamera nne.
Katika kamera nne inakosekana aina moja ya kamera ya Telephoto
Kama ni kuzoom simu itategemea app ya kamera
Kamera kuu ina OIS ambayo inafanya video kutotikisika kutokana na kutisika kwa mkono
Ubora wa picha
Ubora wa picha zinazopigwa na samsung galaxy a23 si wa kuvuitia.
Ukipitia baadhi ya picha kutoka samsung galaxy a23 za gsmarena utaona kamera haipigi picha nzuri usiku.
Wakati wa usiku kamera inazalisha picha zenye texture mbaya
Noise(vichengachenga) zinaonekana kwa wazi ukiizoom picha kiogo
Ubora wa rangi ni mzuri kwa kiasi kikubwa wakati wa mchana
Ubora wa video
Kamera za hii simu zinaweza kurekodi video za aina moja.
Ukiwa unachukua video kwa kutumia galaxy a22 utapata video za full hd kwa spidi ya 30fps
Haiwezi kurekodi video za 4k na 8k zenye resolution kubwa zaidi.
Spidi ya 30fps si nzuri sana hasa ukiwa unarekodi kitu kinachokimbia kwa kasi
Ubora wa Software
Samsung a22 inakunaja na android 11 na One UI Core 3.1
Software ya One Ui 3.1 ina video call inayoruhusu kuweka ukungu(brul) kwenye background
Kuna onegezeko la video effects kwa simu za video
Mtumiaji wa simu anaweza pia kuondoa data zinazoonyesha eneo wakati wa kupiga picha
One ui inaweza kuchuja mwanga wa blue ambao huumiza macho
Bei ya Samsung Galaxy A22 Tanzania
Kwa baadhi y maduka kariakoo bei ya samsung a22 inafika 520,000 kwa samsung ya 64GB
Na kwa samsung a22 ya 128GB bei inafika shilingi 580,000/=
Kuna simu aina ya redmi zenye kamera na chip bora zaidi za dimensity zinazopatikana chini ya 500,000
Simu ya vivo t1 5g ina nguvu kuliko galaxy a22
Lakini bei ya vivo t1 5g haifiki 500,000/=
Yapi Madhaifu ya Samsung Galaxy A22
Samsung galaxy a22 haina viwango vya IP ratings vinavyoainisha uwezo wa simu kuzuia maji na vumbi
Kamera zake hazitoi picha nzuri nyakati za usiku kwenye mwanga mdogo
Bei yake ni kubwa ukilinganisha na ubora wa simu
Kioo chake kina resolution ndogo
Spidi ya juu ya 4g sio kubwa sana
Neno la Mwisho
Samsung galaxy a22 ni simu inayokaa na chaji muda mrefu sana
Kwa mtumiaji anayetumia intaneti sana hii simu itamsaidia pakubwa.
Hautakuwa na haja ya kuchaji mara kwa mara.
Kwa hilo na kioo cha amoled basi galaxy a22 ni ya kuimiliki
Lakini kama unazingatia utendaji na ubora wa kamera galaxy a22 haitokufaa
Maoni 2 kuhusu “Sifa za kipekee za simu ya Samsung Galaxy A22”
Naweza kufahamu bei ya kioo kwa Tanzania sababu kioo cha simu yangu kimepasuka
Bei ya kioo chake kwa sasa sina taarifa nayo, nitakuangalizia