SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Sifa za simu mpya ya Samsung Galaxy A23 [Kioo Kigumu]

Simu Mpya

Sihaba Mikole

April 1, 2022

Unatafuta simu mpya nzuri ya samsung inayouzwa bei nafuu?

Samsung ya bei rahisi huku ikiwa na kamera nzuri na ukaaji wa chaji muda mrefu?

Simu mpya ya Samsung galaxy a23 ina bonge la betri inayokaa na chaji muda mrefu

Kamera yake inakuja na teknolojia zinazorahisisha upigaji picha na uchukuaji wa video.

Samsung Galaxy A23 imezinduliwa mwaka 2022 mnamo mwezi wa tatu

Ni jambo la msingi kuzijua sifa za Galaxy A23 kiundani.

Maana baadhi ya nyanja, simu haivutii kabisa.

Sifa za Samsung Galaxy A23

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – Snapdragon 680 4G
  • Core Zenye nguvu(4) – 4×2.4 GHz Kryo 265 Gold
  • Core Za kawaida(4) – 4×1.9 GHz Kryo 265 Silver
  • GPU-Adreno 610
Display(Kioo) PLSLCD, Refresh rate:90Hz
Softawre
  • Android 12
  •  One UI 4.1
Memori eMMC 5.1, 64GB, 128GB na RAM 8GB, 4GB, 6GB
Kamera Kamera nne

  1. 50MP,PDAF(main)
  2. 5MP(ultrawide)
  3. 2MP(macro)
  4. 2MP(depth)
Muundo Urefu-6.6inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-25W
Bei ya simu(TSH) 594,862.37/=

Upi ni ubora wa simu mpya ya Samsung Galaxy A23

Sasung galaxy a23 inakuja na kioo kigumu kupasuka.

Kioo cha hii simu kinaweza kuchangia simu kudumu muda mrefu

Ubora mwingine wa simu ya galaxy a23 ni chaji yake na betri.

Betri ya Samsung galaxy ina ujazo mkubwa.

Na chaji yake inawahi kujaza simu kwa haraka.

Vipi kuhusu ubora wa network, memori, kioo, gpu na processor?

Kuna mkanganyiko kwenye nyanja hizo.

Ukifuatalia kila nyanja ya simu hii inaweza kukushangaza.

Ubora wa Network

Simu ya samsung galaxy a23 inakubali aina zote za network ikiwemo 4G

4G yake ina network bands 10 japokuwa kuna bands zaidi ya 24 za 4G

4G ya Galaxy A23 ni aina ya Cat 13 ambayo spidi ya juu kabisa kudownload ni 380Mbps

Bands ambazo zinakuja na galaxy A23 ni 1, 3, 5, 7, 8, 20, 28, 38, 40 na 41

Kwa Tanzania simu itakubali intaneti ya 4G ya mtandao wowote

Hizi ni network bands za mitandao mitano yenye wateja wengi Tanzania

Vodacom : 3

Tigo : 3 na 20

Airtel : 28

Halotel : 7

TTCL : 3 na 40

Simu itakusumbua ukisafiri nayo kwenda USA

Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy A23

Kioo cha samsung galaxy a23 ni aina ya PLS LCD

Samsung wanaunda vioo vya PLS wenyewe.

Wanadai uangavu wa vioo vya PLS ni mkubwa kwa asilimia 10.

Kiuhalisia havina tofauti sana na vioo vya IPS LCD

Samsung galaxy a23 ina display yenye refresh rate inayofikia 90Hz.

Kiasi hiki hufanya screen kuwa nyepesi pale unapatachi

Nguvu ya processor Snapdragon 680 4G

Processor ya Snapdragon 680 4G inaipa nguvu galaxy A23.

Snapdragon 680 ina core nane.

Core nne zina nguvu sana na zilizobaki zina nguvu ndogo

Kiujumla ni processor yenye nguvu ya wastani kwa kuzingaitia vipimo vya antutu, geekbench na 3DMark

Uwezo wa wastani unatokana na aina ya miundo iliyotumika kwenye core ndogo na kubwa.

Uwezo wa core zenye nguvu kubwa

Core 4 zenye nguvu sana zina spidi ya 2.4Ghz

Kila core imeundwa kwa muundo wa Kryo 265 Gold.

Gold ni neno kutoka qualcomm linalowakilisha core yenye nguvu.

Kryo 265 Gold ni muundo wa Cortex A73.

Muundo wa Cortex A73 unaifanya processor kuwa na nguvu za wastani.

Na kuweza kufungua app na gemu nyingi zinahitaji nguvu kubwa.

Kiutendaji ipo chini ukilinganisha Cortex A77 na Cortex A78

Cortex A77 na Cortex A78 zinaweza kupiga kazi kubwa kwa matumizi madogo ya betri

Uwezo wa core zenye nguvu ndogo

Uwezo wa core ndogo upimwa kwa matumizi madogo ya umeme.

Kikawaida simu inapaswa itumie nguvu ndogo pale inapotuma sms au kupiga simu.

Na kazi zingine ndogo ndogo.

Kama simu inawahi kuisha chaji haraka kwa kazi hizo ndogo basi utendaji wa core zenye nguvu ndogo si wa kurizisha.

Snapdragon 680 4g inatumia Cortex-A53(Kryo 265 silva) kwenye core ndogo nne

Ni moja ya core zenye ulaji mdogo sana wa umeme.

Japokuwa utendaji wake si mkubwa ukifananisha Cortex A55

Uwezo wa betri na chaji

Betri ya Samsung galaxy a23 ina ukubwa wa 5000mAh aina ya Li-Po

5000mAh ni ujazo mkubwa unaosaidia simu kukaa na chaji muda mrefu

Simu inakuja na fast chaji.

Chaji ya samsung galaxy a23 inapeleka umeme wa wati 25

Kimakadilio chaji inaweza jaza betri chini ya masaa mawili.

Simu zenye betri kubwa zinachelewa kuisha kwa takribani masaa 13 na zaidi zinapotumia intaneti

Ukubwa na aina ya memori

Samsung Galaxy A23 inatumia memori aina ya eMMc 5.1

eMMc 5.1 ni aina ya memori ambayo inasafirisha data kwa kasi ya 250MBps.

Ni kasi ndogo inayoweza kuchelesha simu kuwaka na app kufunguka kwa haraka.

eMMc 5.1 ni teknolojia ambayo wakati wake unaisha kwani simu mpya nyingi zinatumia memori za UFS

Zipo samsung galaxy a23 za aina nne.

  • 64GB ROM na 4GB RAM
  • 64GB ROM na 6GB RAM
  • 128GB ROM na 6GB RAM
  • 128GB ROM na 8GB RAM

Memori inatoa uwanja mpana wa kuhifadhi vitu vingi.

Ram kubwa inasaidia kufungua app nyingi kwa wakati moja kiurahisi

Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy A23

Bodi ya Samsung galaxy A23 imeundwa kwa glasi ya gorilla toleo la 6 upande wa mbele.

Majaribio ya kudondosha simu za gorilla 6 yameonesha simu kustahimili kupasuka kwa kimo cha mita mbili.

Frame zinaundwa kwa plastiki.

Na upande wa nyuma ni plastiki pia

Plastiki zina kawaida ya kuwahai kuchakaa.

Simu sio nzito kwani ina gramu 195

Urefu wake na upana unajaa kwenye kiganja kwa asilimia kubwa

Ubora wa kamera

Simu ina kamera za aina nne.

  1. Ultrawide
  2. Macro
  3. Wide
  4. Depth

Kamera moja tu ina teknolojia ya OIS(Optical Image Stabilization)

OIS husaidia kutuliza video pale anayerekodi akiwa anatembea

Kwa bahati teknolojia ya autofocus iliyotumika PDAF badala ya Dual Pixel PDAF

Jifunze: Maana ya autofus

Dual Pixel PDAF inafanya kamera ya simu kulenga kwa usahihi mkubwa kitu kinachpigwa picha.

Ubora wa video

Kamera ya galaxy a23 inaweza kurekodi video za ubora wa aina mbili.

Kamera za nyuma zinarekodi video za 4k na full hd.

Wakati selfie kamera inaweza kurekodi video zenye ubora wa aina moja tu yaani full hd.

Hizi aina mbili za video huonyesha picha kwa ubora.

Japokuwa video zinarekodiwa kwa spidi ndogo ya 30FPS.

Jifunze: Maaana ya FPS

Ubora wa Software

Samsung galaxy a23 ni simu ya Android 12.

Android 12 inawezeshwa na software ya samsung ya One UI 4.1

Baadhi ya vitu vipya vya ambavyo havipo kweye android 11 ni uwezo wa simu kuonyesha kwenye screen app ambazo zinatumia mic na kamera bila wewe kujua.

Kitu kinachokupa uwezo wa kutambua app zinazokutrak

Kitu kingine ni aina mpya ya screenshot

Screenshot ya android 12 inaweza kupiga picha ukurasa mzima bila kukata vipande pande.

Wakati One UI 4.1 inakuwezesha kutumia memori ya simu kuwa ram

Baadhi ya vitu vipya vya android 12 vimetolewa kutoka one ui

Bei ya Samsung Galaxy A23 Tanzania

Bei ya Samsung galaxy a23 kwa Tanzania inaweza kuzidi 600,000/= kutegemea na memori na ram

Simu za samsung zilizopo kundi la kati huuzwa kwa bei ghari kwa maduka ya karikoo.

Umakini unahitajika.

Kiujumla bei ya hii simu inaweza ikawa kubwa .

Kwa bei hiyo unawza pata redmi ambazo zina chipset yenye nguvu na 5G pia

Yapi Madhaifu ya Samsung Galaxy A23

Kuna kasoro chache za hii simu

Moja wapo ni Samsung galaxy a23 kutokuwa na viwango IP ratings

IP ratings huonyesha uwezo simu kuzuia maji.

Na kamera kutokutumia dual pixel pdaf.

Memori ya galaxy a23 haina spidi kubwa ya kusafirisha data kwa kasi

Vioo vya LCD vinazidiwa ubora na vioo vya amoled

Neno la Mwisho

Samsung galaxy a23 inafanana na oppo a96 kutokana na kutumia processor ya aina moja.

Kwa mtumiaji wa kawaida simu inafaa kuwa nayo.

Kama unapenda sana kamera basi Samsung galaxy s22 ulta na iPhone 13 Pro Max ni machaguo sahihi

Maoni 8 kuhusu “Sifa za simu mpya ya Samsung Galaxy A23 [Kioo Kigumu]

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

samsung galaxy a15 thumbnail

Bei ya Samsung Galaxy A15 na Sifa Muhimu

Mwezi wa desemba 2023 ni mwezi ambao Simu ya Samsung Galaxy A15 ilizinduliwa Ni simu ya daraja la kati ambayo ina vitu vichache vinavyopatikana kwenye samsung za bei kubwa Ndio […]

samsung a55 showcase

Bei ya Samsung Galaxy A55 na Ubora wake

Samsung Galaxy A55 imetoka mwezi machi mwaka 2024 na ni simu ya daraja la kati Bei ya Samsung Galaxy A55 kwa Tanzania ni shilingi milioni moja na laki moja na […]

thumbnail

Bei ya Samsung Galaxy A35 na Sifa zake

Samsung Galaxy A35 ni toleo jipya la samsung lilotoka mwezi machi 2024 Ni simu ya daraja la kati iliyochota baadhi ya sifa muhimu kutoka kwenye galaxy yenye bei kubwa Ndio […]

simu mpya

Simu mpya kali 20 na bei zake kwa mwaka 2024

Hii ni orodha ya simu mpya ambazo zimetoka mwaka 2024 ama mwishoni mwa mwaka 2023 kutoka kwa kampuni zipatazo 11 Ni orodha inayohusisha simu za daraja la kati na la […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram