SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Sifa za simu ya Vivo T1 5G [Ubora na Mapungufu]

Sifa za simu

Sihaba Mikole

April 1, 2022

Vivo T1 5G ni simu mpya ya android ambayo imezinduliwa mwaka 2022

Sifa za simu ya vivo T1 5g zinaonyesha simu kuwa na utendaji wa kutumia applikesheni yeyote inayohitaji nguvu kiurahisi.

Kwani Vivo T1 5G inatumia chipset yenye nguvu kubwa kiutendaji.

Kwa mtafutaji wa simu nzuri za vivo atavutiwa na sifa nyingi za Vivo T1 5G.

Japo yapo mapungufu na unaweza kuyagundua kwenye jedwari la sifa.

Hii ni moja ya simu ya 5G ya bei nafuu

Sifa za Vivo T1 5G

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
  • CPU –  Snapdragon 695 5G
  • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.2 GHz Kryo 660 Gold
  • Core Za kawaida(6) – x1.7 GHz Kryo 660 Silver
  • GPU-Adreno 619
Display(Kioo) IPS LCD, Refresh rate:120Hz
Softawre
  • Android 11
  •  Funtouch 12
Memori 128GB na RAM 8GB,6GB, 4GB
Kamera Kamera tatu

  1. 50MP,PDAF(wide)
  2. 2MP(macro)
  3. 2MP(depth)
  4. 16MP(selfie camera)
Muundo Urefu-6.58inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-18W
Bei ya simu(TSH) 461,324.37/=

Upi ni ubora wa simu ya vivo T1 5G

Ubora wa vivo t1 5g ni uwezo wake wa kukaa na chaji.

Hilo linachangiwa na kutumia processor yenye nguvu lakini inatumia umeme kidgo.

Na ubora mwingine ni software ya Vivo inayojilakana  kama Funtouch 12

Funtouch os 12 inamuwezesha mtumiaji wa vivo kuongeza ukubwa wa memori na urahisi wa kutumia simu

Lakini pia simu ina radio na sehemu ya kuweka memori kadi ya ziada

Inatumia aina tano za GPS kitu kinachosaidia simu kukadiria eneo kwa usahihi mkubwa

Network

Simu inakubali aina zote za mitandao ikiwemo 4G na 5G

4G ya vivo t1 5g ni aina ya cat 18

4G ya LTE Cat 18 inaweza kufikia spidi ya juu ya kudownload ya 1174Mbps

Hii simu ina bands chache za 4G.

Kwa kutazama bands za mitandao ya simu Tanzania, Hii vivo itagoma kwa baadhi laini za simu.

Vodacom – 3

Tigo – 20 na 3

Airtel-28

Halotel-7

TTCL-3 na 40

Wakati network bands za vivo t1 5g ni 1, 3, 5, 8, 38, 40 na 41

Hivyo basi intaneti ya 4g ya Airtel na Halotel itagoma

Ubora wa kioo cha vivo T1 5G

Kioo cha vivo T1 5g ni aina ya IPS LCD chenye refresh rate ya 12oHz

Refresh rate ya 120 inafanya kioo cha simu kuwa chepesi kucheza gemu

Na kioo kinakuwa kilaini unaposcroll majina ama meseji

Kioo kina resolution 1080 x 2408 pixels

Hii ni kiwango ambacho kinaonyesha picha na video kwa uangavu

Kwa bahati hatuna taarifa za kiwango cha muangaza(nits) ili kujua uwezo wa screen kuonyesha vitu juani

Nguvu ya processor Snapdragon 695 5G

Ukiona simu imetumia processor ya Snapdragon 695 5g basi jua kuwa hivyo simu ina utendaji wa kasi.

Vivo T1 5g imeundwa kwa processor ya snapdragon 695 5g.

Ni processor yenye core nane (octacore)

Jifunze: Maana ya Core kwenye processor za simu.

Core zenye nguvu zipo mbili

Na core zenye nguvu ndogo zipo sita

Kwenye platform za geekbench, antutu na 3Dmark snapdragon 695 5g inaizidi mbali processor ya Snapdragon 680 iliyotumika kwenye Oppo A96

Uwezo wa core zenye nguvu kubwa

Kuna core mbili ambazo ni kwa ajili ya kufanya kazi zinazohitaji nguvu tu.

Kila core ina kasi ya 2.2GHz

Core hizo zimeundwa kwa muundo wa Kryo 660 Silver.

Kryo 660 Gold ni core aina ya Cortex A78

Cortex A78 ina kufungua app nzito kama magemu kwa haraka wakati huo ikitumia umeme mdogo

Na ndio simu zenye processor hii hukaa na chaji muda mwingi

Hivyo muundo wa Kryo 660 unapunguza betri ya simu kupata joto sana wakati ukicheza gemu

Uwezo wa core zenye nguvu ndogo

Core ndogo zinatumia muundo wa Kryo 660 Silva

Kryo 660 Silva ni core aina ya Cortex A55

Cortex A55 hutumia umeme mdogo sana lakini pia kuna kaongezeko kautendaji

Hii inamaanisha kama unatumia simu ya vivo t1 5g kutuma sms ama kupiga simu, vivo itakaa na chaji muda mwingi

Kila core ndogo ambazo zipo sita zina spidi ya 1.7GHz

Uwezo wa betri na chaji

Betri ya vivo t1 5g ina ujazo wa 5000mAh aina ya Li-Po.

Chaji yake inapeleka umeme wa wastani wa wati 18.

Umeme wa wati unaweza kuchukua zaidi ya masaa mawili kujaza betri la 5000mAh

Lakini ukaaji wa chaji lazima utakuwa ni mkubwa.

Kwa sababu vivo t1 5g haijatumia vioo vya amoled.

Na processor yake ina ufanisi mzuri wa matumizi ya betri

Vivo wanadai simu inaweza kutumika kwa masaa 19 kwa kuangalia video za youtube

Ukubwa na aina ya memori

Vivo T1 5g zipo za aina tatu linapokuja swala la memori na ram

  1. 128GB ROM na 4GB RAM
  2. 128GB ROM na 6GB RAM
  3. 128GB ROM na 8RAM

Aina ya ram ya vivo hii ni LPDDR4X.

Hizi ni ram zinazosafirisha data kwa kasi kubwa

Pia ukubwa wa ram unaruhusu simu kuhifadhi mafaili ya kutosha

Uimara wa bodi ya vivo T1 5G

Upande wa nyuma na fremu zina plastiki.

Kioo kimewekea ulinzi wa kioo lakini sio kioo cha gorilla

Bodi za plastiki zina kawaida ya kuwahi kuchoka hivyo kava inahitajika

Urefu na upana wa simu unajaa kwenye kiganja

Simu ni nyepesi kubeba kwa sababu ina uzito wa gramu 187

Ubora wa kamera

Simu ya vivo t1 5g ina kamera tatu.

Katika kamera tatu hakuna kamera za telephoto na ultrawide

Hii inamaanisha simu inategemea app ya kamera kuzoom kitu ambacho kipo mbali

Aina hii ya zoom huitwa digital zoom.

Ubora wa picha za digital zoom hupungua ukilinganisha optical zoom ya Telephoto

Pia hutoweza kupiga picha eneo pana sana kwa sababu ya kutokuwa na ultrawide

Ubora wa video

T1 5G inaweza kurekodi aina moja tu ya video.

Simu hii inarekodi video za ubora wa full hd kwa spidi ya 30fps

Kamera zake hazirekodi video za 4k wala 8k

Ubora wa Software

Mfumo endeshi wa vivo t1 5g ni android 11 na Funtouch os 12

Android 11 ni nzuri ila simu itakosa vitu vipya vitamu sana vya android 12

Upande wa FuntouchOs 12, mtumiaji wa simu anaweza kuongeza ukubwa wa ram kwa kutumia memori ya ram.

Huu mfumo unawezesha kutumia app nyingi(Multitasking) kwa wakati mmoja kwa urahisi

Inazipanga app katika gridi inayotengeneza urahisi wa kuchagua app ya kutumia

Albamu ya picha ya funtouchos 12 inakuwezesha kutengeneza slideshow(picha mnato) ya picha nyingi

Bei ya vivo T1 5G Tanzania

Bei ya vivo T1 5g inafikia shilingi 462,000/=za kitanzania

Ukilinganisha na simu zingine zenye sifa sawa na hii vivo, hii simu inauzwa kwa bei nafuu.

Lakini unafuu wa bei umekuja na gharama

Kwenye hii simu, vivo wamepunguza ubora wa kamera na kioo

Hii ni tofauti na Oppo A96 5g ambayo ina kioo cha OLED

Yapi Madhaifu ya vivo T1 5G

Sehemu inakosa viwango vya IP vinavyofafanua uwezo wa simu kuzuia maji

Vivo T1 5g haina vioo vya gorilla na bodi yake ni plastiki

Ina network bands chache ambazo zinakataa baadhi ya laini

Chaji yake inapeleka umeme mdogo

Simu inakuja na android 11 wakati simu mpya zinakuja na android 12

Inakosa bands ya 5g yenye kasi kubwa

Neno la Mwisho

Kwa mtu anayependa simu yenye uwezo mkubwa Vivo T1 5G

Kwa mpenzi wa kamera na display nzuri yapo machagua tofauti na hii simu

Kwa kuzingatia bei na uwezo wa simu, hii si simu ya kukosa kuwa nayo.

Ni simu ya bei nafuu

Wazo moja kuhusu “Sifa za simu ya Vivo T1 5G [Ubora na Mapungufu]

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

No Featured Image

Simu 14 mpya za Vivo za ubora mkubwa na bei zake (2024)

Tangu mwishoni mwa mwaka 2023 mpaka mwaka huu 2024 Vivo imeachia matoleo mengi ya simu Katika matoleo hayo yapo ya bei ndogo, bei ya kati na bei kubwa Kwa maana […]

simu mpya

Simu mpya kali 20 na bei zake kwa mwaka 2024

Hii ni orodha ya simu mpya ambazo zimetoka mwaka 2024 ama mwishoni mwa mwaka 2023 kutoka kwa kampuni zipatazo 11 Ni orodha inayohusisha simu za daraja la kati na la […]

vivo y02t

Bei ya Vivo Y02t na Sifa Zake

Vivo Y02t ni simu ya bei nafuu ambayo imetoka katikati ya mwaka 2023 Bei ya vivo y02t haizidi laki tatu kwa hapa Tanzania kutokana na aina ya sifa ambazo simu […]

Jinsi ya Kutumia GPS kwenye Simu (Hatua kwa Hatua)

GPS kirefu chake ni Global Positioning System, ni mfumo wa utambuzi wa maeneo ambao unasimamiwa na Marekani Simujanja karibu zote zina huu mfumo Una faida kubwa sana hasa kama unajua […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram