SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Ipi Simu Bora: Infinix Zero 5G vs Redmi Note 10 5G

Ulinganishi

Sihaba Mikole

February 22, 2022

Unafahamu kwamba mwaka 2022 Infinix imezindua simu ya 5g inayotumia processor yenye nguvu.

Kiuwezo na kisifa infinix zero 5g inaendana kwa kiasi kikubwa na simu ya xiaomi redmi note 10 5g.

Simu zote zinachagizwa na sifa kuu moja ya kuwa na mtandao wa 5g.

Kwa kutazama sifa za infinix zero 5g na redmi note 10 5g utagundua kuwa hizi simu hazipo sawa.

Kuna moja ambayo ina uwezo zaidi kuliko nyingine.

Sifa za infinix zero 5g

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
  • CPU – Dimensity 900 5G
  • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.4 GHz Cortex-A78
  • Core Za kawaida(6) – 6×2.0 GHz Cortex-A55
  • Mali-G68 MC4
Display(Kioo) IPS LCD, Refresh rate:120Hz
Softawre
  • Android 11
  • XOS 10
Memori UFS 3.1, 128GB na RAM 8GB
Kamera Kamera tatu

  1. 48MP,PDAF(main)
  2. 13MP(telephoto)
  3. 2MP
  4. 16MP(depth)
Muundo Urefu-6.78inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-33W
Bei ya simu(TSH) 654,140/=

Sifa za xiaomi redmi note 5g

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
  • CPU – Dimensity 700 5G
  • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.2 GHz Cortex-A76
  • Core Za kawaida(6) – 6×2.0 GHz Cortex-A55
  • GPU-Mali-G57 MC2
Display(Kioo) IPS LCD, Refresh rate:90Hz
Softawre
  • Android 11
  • MIUI 12
Memori UFS 2.2, 128GB,64GB,256GB na RAM 8GB,4GB
Kamera Kamera tatu

  1. 48MP,PDAF(main)
  2. 8MP(macro)
  3. 2MP(depth)
  4. 8MP(selfie camera)
Muundo Urefu-6.5inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-18W
Bei ya simu(TSH) 515,500/=

Sasa basi, ipi simu bora kati ya infinix zero 5g na redmi note 10 5g?

Infinix zero 5g ni simu bora kwa kutazama sifa zifuatazo.

Processor

Simu ya xiaomi redmi note 10 5g inatumia chip ya MediaTek Dimensity 700 5G.

Ni tofauti na simu ya Infinix zero 5g inayotumia processor ya MediaTek 900 5g

MediaTek 900 5g inatumia muundo wa Cortex A78 kwenye core zenye nguvu.

Cortex A78 ina nguvu ya kufungua apps kubwa kwa matumizi madogo ya betri ukilinganisha na Cortex A76 iliyotumika kwenye Dimensity 700 5G.

Ukiwa unacheza gemu kama la PUGB, infinix zero 5g itacheza kwa haraka na kwa matumizi madogo ukilinganisha na simu ya Xiaomi Redmi Note 10 5G.

Hata upande wa gpu, infinix zero 5g ina nguvu kubwa ya kusukuma kila aina ya gemu.

Upande wa software zinatest uwezo wa processor, MediaTek Dimensity 900 inafanya vizuri kiutendaji.

Kwenye app ya GeekBench 5.1 Dimensity 900 ina point 706 wakati Dimensity 700 ina point 562.

Processor ikiwa nzuri uwezo wa kupata simu nzuri ni mkubwa.

Kwenye upande wa SoC infinix zero 5g ni mshindi.

Network

Simu zote zinasapoti mtandao wa 5g.

Simu zote zinakubali 5g ya mmWave ambayo ina kasi kubwa kuliko za Mid Band na Lower Band.

Upande wa network upo sawa ila kama simu inadownload file simu ya infinix zero 5g inaweza kumaliza kudownload kuliko redmi note 10 5g.

Hii inasababishwa na mfumo wa kasi wa memori uliopo kwenye zero 5g.

Utafahamu utofauti wa storage iliyopo kwenye zero 5g na redmi note 10 5g.

Modem za Dimensity 900 na dimensity 700 kiwango chake cha juu cha kudonload ni 2.77Gbps

Kiwango hiki kiweze kufikiwa kwenye eneo lenye mtandao mzuri wa 5G ni lazima memori ya simu iwe na kasi kubwa ya kuhifadhi mafaili.

Hivyo upande wa network upendeleo utaenda kwa Infinix zero 5g.

Display

Simu zote zinatumia vioo vya IPS LCD.

IPS LCD ni vioo vizuri lakini kutokana na kuja kwa aina ya vioo vya AMOLED umefanya vioo vya IPS LCD kuwa vibaya.

Vioo vya AMOLED vimeboresha screen kuonyesha rangi nyingi na vizuri iliyokolea.

Hivyo picha na video zinazoonekana kwenye vioo vya amoled huonokana kwa rangi zake halisi kwa kiasi kikubwa.

Kioo cha infinix zero ni chapesi(smooth) na kizuri kuchezea gemu ukilinganisha na kioo kilichopo kwenye redmi note 10 5g.

Kwa mfano,

Ukiwa folder la picha za whatsapp picha zinakuwa ni nyingi na inakuwa ngumu kutafuta picha ambayo ipo chini.

Hivyo ukiwa una-scroll kwenda juu kioo cha cha infinix zero 5g kitakuwa kinascroll kwa haraka sana kuliko cha redmi note 5g.

Uwepesi wa kioo utasaidia kuifikia picha unayotaka kwa muda mfupi.

Hilo linachangiwa na kitu kinaitwa refresh rate.

Refresh rate ya zero 5g ni kubwa inayofikia 120Hz wakati redmi note 10 5g inafikia 90Hz.

Kitu ambacho redmi note 10 5g inaizidi infinix ni kuwa na glassi ya gorilla 3.

Gorilla 3 ni kioo kigumu kuchunika

Memori

Moja ya kitu cha muhimu kwenye upande wa memori ya smartphone ni aina ya mfumo wa memori.

Simu za infinix zero 5g na redmi note 10 5g zinatumia mfumo wa UFS.

Memori aina ya UFS husafirisha data kwa kasi sana.

Memori zenye kasi hufanya simu na application kufunguka kwa haraka.

UFS zimeganyika kwenye matoleo mengin.

Memori ya Redmi note 10 5g ni UFS 2.2 wakati infinix zero 5g ni UFS 3.1

UFS 3.1 ina kasi kubwa inayofikia 2400Mbps.

Ukiwa unakopi faili la 5GB, infinix zero 5g itakopi file kwa sekunde 17.

Na Redmi note 10 5g itakopi kwa sekunde 34.

Infinix ipo ya aina moja tu upande wa memori ambayo ina ukubwa wa 128GB.

Wakati redmi zipo za aina tatu ambazo ni 64GB, 128GB na 256GB.

Kwa mtumiaji anayehifadhi mafaili mengi kwenye simu anaweza chagua redmi.

Kwenye RAM simu zote mbili zina RAM yenye ukubwa wa 8GB.

RAM iliyopo kwenye chipset ya Dimensity 900 inasapoti ram inayosafirisha data nyingi.

Aina hiyo ya RAM ni LPDDR5.

LPDDR5 inaweza kusafirisha data kwa spidi ya 5500Mbps.

Ila haifahamiki infinix zero 5g imetumia ram ipi kati ya LPDDR4 na LPDDR5.

Lakini infinix zero 5g ina mfumo mzui wa memori unaochagiza utendaji mkubwa wa simu kiujumla.

Chaji na Betri

Betri ya Infinix zero 5g ina ukubwa wa 5000mAh.

Pia betri ya xiaomi redmi note 10 5g ina ukubwa wa 5000mAh.

Chaji ya infinix zero 5g inapeleka umeme mwingi wa wati 33.

Uememe wa wati 33 unawahi kujaza simu ndani ya dakika chache ukilinganisha na chaji ya redmi note 10 5g yenye wati 18.

Betri ya redmi note 10 5g itachelewa kujaa kwa sababu betri ni kubwa na chaji inapeleka umeme kidogo wa 18W.

Ukirejea upande wa processor.

Zero 5g inatumia processor yenye uwezo mkubwa na matumizi madogo ya umeme.

Processor hiyo inachangia simu kukaa na chaji muda mrefu.

Ndio maana infinix zero 5g inatunza moto kuliko redmi note 10 5g.

Kama zero 5g ikiwa haitumikii inakaa na chaji masaa 140 tofauti redmi note 10 5g inayokaa na chaji masaa 121.

Kiufupi Infinix zero 5g ina matumizi mazuri ya betri na kasi kubwa ya kuchaji.

Kamera

Mfumo wa kamera wa infinix zero 5g ni mzuri kuliko wa redmi note 10 5g.

Kamera ya redmi note 10 5g inakosa vitu vingi na ina uwezo wa kawaida kuchukua video.

Simu ya redmi note 10 5g inakosa teknolojia ya optical zoom.

Optical zoom inazoom kitu cha mbali bila kupoteza resolution ya kamera kwa maana ubora wa picha unabaki kama ulivyo.

Kamera ya xiomi hii haiwezi kuchukua video zenye ubora wa 4K.

Ambapo inifnix zero 5g inarekodi video za 4k vizuri.

Ukilinganisha hizi simu mbili na simu mpya za samsung s22 au iphone za zamani utaona kuwa kamera simu za note 10 5g na zero 5g zina ubora mdogo sana.

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

xiaomi 14 ultra

Simu 13 mpya na kali za Redmi na Xiaomi 2024

Kampuni ya Xiaomi sio ngeni kwa wengi Ni kampuni ya china inayotengeneza simu za madaraja yote kwa brandi za Xiaomi, Redmi na Poco Hapa kuna orodha ya simu mpya za […]

No Featured Image

Bei ya Redmi Note 13 na Sifa Zake Muhimu

Redmi Note 13 5G ni simu kutoka Xiaomi ya China ambayo bei yake kwa sasa ni shilingi laki nane Hii ni bei ya toleo lenye ukubwa wa GB 256 na […]

infinix note 30 vip thumbnail

Bei ya Infinix Note 30 VIP na Sifa Zake

Infinix kwa mwaka 2023 wameachia matoleo mengi yakiwemo ya note series Moja ya toleo hilo ni Infinix Note 30 VIP ambayo imetoka mwezi Juni Haina tofauti sana na infinix note […]

infinix zero 30 5g thumbnail

Ubora na Bei ya Infinix Zero 30 5G (Infinix Kali)

Ni infinix kwa mara nyingine inajaribu kutengeneza hisia chanya juu ya ubora wa simu zao Unaweza kuliona hili kwa toleo jipya la Infinix Zero 30 5G Hii ni simu kali […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram