Simu ya Samsung Galaxy S10+ iliingia sokoni mwaka 2019 ikiwa kama simu ya daraja la kwanza
Kwa mwaka 2023 kuna matoleo ya daraja la kati yanaoizidi Galaxy S10 Plus kutoka makampuni mengine na hata samsung yenyewe
Kitu kinachofanya bei ya samsung galaxy S10 Plus kuwa ndogo kwa sasa
Ila kwa sasa nyingi ni zile simu used kwa sababu ni miaka minne tayari imepita hivyo ni ngumu kupata ikiwa mpya kabisa
Bei ya Samsung Galaxy S10+ ya GB 128
Samsung yenye ukubwa ukubwa wa GB 128 na RAM ya GB 8 inauzwa shilingi 577,000 kwa hapa Tanzania
Bei ni ya simu iliyotumika na inaweza kukushangaza
Ukifuatilia sifa zake ambazo zimeorodheshwa na kisha ukaifananisha na simu ya Redmi Note 12 utaona galaxy ina vitu vingi vya ziada
Vitu ambavyo vinapatikana kwenye simu za bei ghari na kubwa
Kwa hiyo hata Samsung s10 plus used bei yake haiwezi kushuka sana
Kwa mfano uimara wa bodi na ubora wa kioo sio rahisi kukuta kwenye simu za daraja la kati zilizotoka kipindi cha 2022 na 2023
Sifa za Samsung Galaxy S10 Plus
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Dynamic AMOLED, |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.1, 512GB,128GB,1TB na RAM 8GB,6GB,12GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.4inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 577,000/= |
Upi ubora wa Samsung Galaxy S10 Plus
Simu ina kamera nzuri inazoziacha mbali simu zilizotoka miaka ya karibuni
Ina bodi ngumu na imara ambayo haipitishi maji kirahisi
Inakuja na memori kubwa ya kutosheleza kuhifadhi mafaili
Utendaji wake ni wa kuridhisha unaoweza kufungua vitu kwa wakati mmoja pasipo kuwa na shida
Ina kioo chenye rangi nyingi na chenye kuonyesha vitu kwa uzuri
Inatumia mifumo mitatu ya GPS kitu kinachokupa uhakika wa kupata data sahihi za eneo fulani
Uwezo wa Network
Kikawaida simu za daraja la juu kwa hivi sasa husapoti mtandao wa 5G
Lakini Samsung Galaxy S10 Plus inasapoti mwisho mtandao 4G
Inatokana na uhalisia kuwa 5G mwaka 2019 ndio ilikuwa inaanza kwa nchi chache sana
Kwenye upande wa 4G inatumia LTE Cat 20 ambayo kasi yake inafika 5000Mbps kwa kudownload
Hii ni kasi kubwa hata Oppo A78 5G ya 2023 haifikii
Hata hivyo usisahau 4g ya Tanzania haina kasi inayofika huko
Kingine ni kuwa simu ina masafa yanayotumika maeneo mengi duniani
Utaweza kusafiri nayo popote na ikawa inafanya kazi
Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy S10+
Kioo cha Samsung Galaxy S10+ ni aina AMOLED chenye HDR10+
Kikiwa kikiwa na HDR10+ inamaanisha kiasi cha rangi kinachozalishwa ni kikubwa
Kitu kinachoboresha muonekano wa vitu kwa uzuri
Ukizingatia vioo vya amoled huwa na muonekano sahihi wa rangi kama rangi nyeusi
Ukilinganisha rangi nyeusi kwenye kioo cha IPS LCD na AMOLED utaona utofauti mkubwa
Uzuri pia resolution yake ni 1440 x 3040 pixels ambayo ni kubwa sana
Maana hata simu za siku hizi nyingi huishia 2400pixel
Ndio maana bei ya kioo cha samsung galaxy s10+ ni kubwa kama unataka kupata ubora uleule
Nguvu ya processor Snapdragon 855
Kwenye upande wa processor kuna galaxy s10 plus za aina mbili
Kwa marekani na china zinatumia snapdragon 855 wakati maeneo mengine zinakuja na Exynos 9820
Kwa hapa tunazungumzia Snapdragon kwani ndio nzuri zaidi kuliko exynoss
Chip imegawanyika sehemu tatu, ambapo core yenye nguvu kubwa zaidi ipo moja na inatumia muundo wa Kryo 485 Gold (Cortex A76)
Utendaji wake ni mkubwa kwa kiasi fulani
Maana magemu mengi makubwa makubwa yanacheza kwa resolution kubwa kwa kiwango cha 60fps
Pamoja na processor kutumia nguvu ina ulaji mdogo wa chaji
Hivyo unapata utendaji mkubwa na kwa matumizi madogo ya umeme
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya Samsung Galaxy S10 Plus sio kubwa ukilinganisha na viwango vya sasa vya simu za android
Betri yake ina ukubwa wa 4100mAh
Inaweza kukaa na chaji mpaka masaa 11 ikiwa kwenye intaneti muda wote ukiwa unaperuzi
Chaji yake inapeleka umeme kiodogo kwani ni wa wati 15
Umeme huu unasababisha simu kuchukua masaa zaidi ya manne mpaka kujaa
Inahitaji kuwa mvumulivu
Ukubwa na aina ya memori
Kuna galaxy s10+ za aina nne upande wa memori zikianzia GB 128 hadi 1TB
Unaweza ukapata yenye ram ya GB 6, 8 au GB 12
Zenye memori kubwa na bei yake inakuwa kubwa zaidi inayoweza karibia milioni
Aina ya memori inayotumia ni UFS 2.1 ambazo huwa na kasi kubwa inayofika 1200MBps
Ni mara mbili ya memori za eMMC 5.1 zinazotumiwa sana na simu za bei nafuu
Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy S10 Plus
Samsung Galaxy S10 Plus bodi yake haipitishi maji kama ikizama kwenye kina cha mita 1.5 kwa muda wa nusu saa
Kwani ina viwango vya IP68
Kwenye kioo imewekewa glassi utoka kampuni ya Gorilla, na nyuma pia hivyo hivyo
Aina ya gorilla ni Gorilla Glass 6 hivi huwa ni vigumu kupasuka labda iwe imeanguka kwenye eneo baya sana
Kiujumla simu ina bodi ngumu na imara inayoweza kukaa muda mrefu
Ubora wa kamera
Simu ina jumla ya kamera tatu unaweza ita samsung macho matatu
Ina kamera ya telephoto maalumu kwa kupiga vitu vilivyopo mbali na ina megapixel 12
Ina kamera ya ultrawide kwa ajili ya kuchukua eneo kwa upana mkubwa na ina megapixel 16
Wakati kamera kuu ina megapixel 12 na kamera mbili zina OIS(Optical Image Stabilization)
Ubora wa picha ni wa kiwango kikubwa kwenye mwanga hafifu na kwenye mwanga mwingi
Vitu vinaonekana kwa ustadi bila kuathiriwa na mwanga mwingi
Na kiwango cha noise nyakati za usiku si rahisi kukitambua kwani vitu vinaonekana vizuri
Kamera inajitahidi kuonyesha rangi halisi za kitu kinachopigwa picha
Upande wa video inaweza kurekodi mpaka video za 4K tena kwa kiwango cha 60fps
Ubora wa Software
Wakati simu inatoka ilikuwa inakuja na Android 9
Lakini inakubali kupokea toleo jipya mpaka la Android 12
Kwa sasa hivi simu mpya zinatumia Android 13 na hivi karibuni Google watatangaza la kumi na nne
Hata hivyo android 12 bado ni mfumo mzuri unaoweza kusapoti app nyingi kwa muda mrefu
Kwa sababu ni android za zamani sana ndio zinazokutana na utata wa kupokea maboresho ya baadhi ya app.
Washindani wa Samsung Galaxy S10 Plus
Mshindani wa nyakati za sasa ni Samsung Galaxy A14 5G ambayo ina kila kitu kilichopo kwenye s10 plus na pia unapata 5G
Na mshindani mwingine ni Oppo Reno8 5G bila kusahau Redmi Note 12 ambazo zina utendaji unaondana na galaxy s10 plus
Pia, kwa simu za zamani kuna Apple iPhone XS, Huawei Mate 20 Pro na hata Xiaomi Mi 9 bila kusahau
Hizo zote zina sifa zinazoendana kwa kiasi kiukubwa
Neno la mwisho
Samsung Galaxy S10 Plus ni simu yenye umri mkubwa ila ina ubora unaoendana na simu mpya nyingi
Ukiwa nayo utajikuta huoni tofauti na mmiliki wa simu za toleo la daraja la kati
Ila kuna tofauti mkubwa sana kati ya Samsung Galaxy S23 Plus na hii
Kwa miaka ya sasa s10 haiwezi kuwekwa kwenye kundi la simu za daraja la kwanza
Maoni 19 kuhusu “Bei ya Samsung Galaxy S10 Plus na Ubora Wake 2023”
KIOO cha Samsung S10+ kinapatikana kwa bei gan kwa saiz na je ni original kama vile kile cha kutoka na cm?
Bei ya kioo cha samsung kwa sasa inaenda 250,000 kwa amoled, ila vya lcd ni chini ya hapo. Kupata display ya super amoled ni vizuri ukawatembelea samsung wenyewe kwenye maduka yao
Simu hutokana na utengenezagi ulio bora pia na ubora wa watengenezagi
I like the best phone than fake
Naomba kufahamu nitatambuaje kuwa hii S10+ kutoka Korean au kutambuwa kuwa hii ni original Asante
Vip kuhusu note10+
Mi simu nzuri pia
N Bei gan??
Nzuri sana
Kwanini simu inajaa had asilimia 85 aiongezeki tena
Sim ni nzuri san lakin natamani kujua unawezaje kubadilisha kamera na kutumia yapili au yatatu?
Ntajuaje simu original na simu fake pia naomba kujua s10plus na note 10 ipi Ina uwezo mkubwa
Utajuaje kama Samsung note 10+ Kams sio copy
Kuna njia nyingi rahisi
Ndg.habar vipi kuhusu a15 nayo
Ni nzuri
nawezaje kuwasiliana nanyi nahitaji sm
Upo mkoa gani
Kama simu inajaa asilimia 85 nenda settings katoe protect battery iwe off