Simu nyingine mpya ya Samsung kwa mwaka 2023 ni Samsung Galaxy S23+
Inafanana kwa kiasi kikubwa na simu ya Samsung Galaxy S23 Ultra ila kuna Galaxy S23+ inavikosa
Kwa maana hiyo bei ya Samsung Galaxy S23+ itakuwa chili ila inazidi milioni mbili
Kwenye hii posti, utafahamu ubora na vitu vipya vya hii simu ambavyo vinatofautiana na simu zingine
Bei ya Samsung Galaxy S23+ ya GB 256
Kwenye masoko ya dunia bei yake kwa sasa inasamama shilingi za Tanzania 2,400,000/=
Kwa Tanzania bei inaweza kuwa kubwa na hata ikazidi 2,700,000/=
Lakini itategemea na wapi unanunua hiyo simu
Bei kubwa ya simu inasababishwa na ukweli kwamba hii ni simu ya daraja la juu
Ni simu ambayo utakuta kamera kali, spika zinatoa sauti nzuri, kioo kinachoonyesha vizuri na mengineyo mengi ambayo yaeoonyeshwa kwenye hii post
Sifa za Samsung Galaxy S23+
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Dynamic Amoled 2X, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 4.0, 256GB, 512GB, na RAM 8GB |
Kamera | Kamera TATU
|
Muundo | Urefu-6.6inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 2,400,000/= |
Upi Ubora wa Samsung Galaxy S23+
Kama ilivyoelezwa sifa nyingi za Galaxy s23 ultra zipo pia kwenye hii simu
Ina mfumo unaopleka chaji kwa kasi hivyo simu inawahi kujaa
Inatumia toleo jipya la android
Ni simu itakayokuwa inapata sapoti ya muda mrefu kwa karibu miaka minne
Ina mfumo wa memori unaosafirisha data kwa kasi kubwa
Ina kioo chenye uangavu mkubwa
Na pia ni simu yenye utendaji mkubwa wa kuweza kufungua app ya aina yoyote
Uwezo wa Network
Hii ni simu inayokuja na uwezo wa kukamata mtadao wa 5G na pia 4G
Inakubali aina zote za 5G yaani masafa mafupi, ya kati na marefu
Pia inatumia 4G aina ya LTE Cat 24 kama ilivyo kwa Galaxy S23 Ultra
Pitia, aina za network za simu zinazopatikana Tanzania
LTE Cat 24 ina spidi ya kudownload inayofika 2400Mbps
Kwa Tanzania hakuna mtandao wa simu ya 4G unaotoa kasi hii
Na hata ikiwepo ghrama yake itakuwa kubwa na sio ndogo
Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy S23+
Simu inatumia kioo cha dynamic amoled 2x chenye resolution kubwa ya 1080 x 2340 pixels
Resolution inayovifanya vitu vionekane vizuri kwenye screen.
Ubora wa hiki kioo unachangiwa na uwepo wa HDR10+ na Refresh rate
HDR10+ hutengeneza mlinganyo sahihi wa rangi hasa tofauti kati ya nyeusi na nyeupe
Huwa inafanya vitu vionekane kwa usahihi kuendana na jinsi vinavyoonekana kwenye mazingira halisi
Uangavu wa kioo cha Samsung Galaxy S23+ unafika nits 1700
Huu uangavu unampa uwezo mtumiaji kuona vitu vizuri kama simu ikiwa inatumika kwenye mazingira yenye mwanga mwingi wa jua
Nguvu ya processor Snapdragon 8 Gen 2
Galaxy S23+ inatumia chip mpya ya Snapdragon 8 Gen 2 inayokuja na GPU ya Adreno 740
Snapdragon 8 gen 2 imegawanyika sehemu nne zenye core jumla ya nane
Na core yenye kasi kubwa zaidi ipo moja na inafika GHz 3.36 aina ya Cortex X3
Kwenye hii kurasa kuna maelezo zaidi: aina ya processor za simu na core zake
Aina ya core hutumika pale simu inapofanya kazi kubwa kwa mfano kucheza gemu kama la Call of Duty
Na core ndogo zaidi zipo tatu hufanya kazi pale unapokuwa kwenye matumizi ya kawaida kama kupiga simu, kutumia whatsapp nk
Mgawanyo huu uhakikisha simu inakuwa na ufanisi mzuri wa matumizi ya betri
Kwa sababu processor ikiwa na nguvu sana chaji inawahi kuisha
Na unapocheza gemu iwe kwenye simu au laptop, GPU ndio huwa inahusika na hiyo kazi
GPU ikiwa na nguvu ndogo simu husumbuka kucheza gemu vizuri ama muonekano wa gemu unakuwa sio wa kuvutia na pia simu inachemka sana.
GPU ya Adreno 740 ni imara kwenye kucheza gemu, kwani gemu nyingi hucheza kwa fps 60
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya S23+ ina ukubwa wa 4700mAh aina ya Li-Ion
Inaizidi kidogo kiikubwa betri ya Apple iPhone Pro ila kwenye matumizi ya simu utendaji wa betri huwa upo tofauti
Matarijio ni kuwa betri inaweza kukaa na chaji kwa masaa zaidi 10 simu ikiwa inatumia intaneti ya 5G
Ina uwezo wa kupokea chaji yenye kasi ya wati 45
Hivyo simu inajaa kwa 65% kwa muda wa dakika 30
Ukubwa na aina ya memori
Galaxy S23+ inakuja na memori yenye kasi sana aina ya UFS 4.0
Kasi hii inaigeuza simu kuwa fasta wakati wa kuwasha na kufungua app mbalimbali
Na pia simu inakuwa fasta zaidi ukiwa unakopi mafaili kutoka kwenye kompyuta kwenda kwenye simu
Kuna matoleo ya aina mbili ya hii simu upande wa memori na zote zikiwa na ukubwa wa RAM wa GB 8
Kuna yenye ukubwa GB 256 na ya GB 512na hazina sehemu ya kuweka memori ya zaidi
Kama GB 256 ni ndogo kuweka mafaili mengi basi GB 512 inafaa lakini bei yake itakuwa kubwa zaidi
Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy S23+
Bodi yake imeundwa na glasi ya Gorilla Victus 2 upande wa nyuma na mbele
Na upande wa pembeni simu imewekwa aluminium
Vioo vya Gorilla Victus 2 vimeundwa kuhimili kupasuka inapoangushwa kwenye sehemu mbaya
Kampuni ya gorilla wanasema kuwa toleo hili linachagizwa na kuongezeka kwa uzito wa simu
Kwenye majaribio yao kioo hakikuvunjika pale simu ilipoangushwa kwenye kimo cha mita 1
Huu ni kama urefu wa rula tatu za sentimita 30
Unaweza pitia hapa kuona majaribio ya kuangusha simu zenye victus 2
Kiujumla hii ni simu yenye bodi imara, hata ukipanga kuiuza baada ya miaka miwili bodi yake itabaki kama ilivyo kwa kiwango kikubwa
Ubora wa kamera
Simu ina kamera tatu yaani samsung macho matatu
Ambapo ina kamera aina ya ultrawide, telephoto na ultrawide
Ukibwa wa lenzi unatofautiana na kamera iliyopo kwenye S23 Ultra
Ultra kamera yake ni kubwa yenye ukubwa wa 200MP wakati hii ina ukubwa ina ukubwa 50MP
Ila ubora wa picha pia ni mkubwa kwani megapixel pekee si kigezo cha kutoa picha bora
Aina ya ulengaji inayotumia ni dual pixel pdaf ambayo imetumika pia kwenye simu iPhone 14 Pro Max
Dual pixel pdaf na yenyewe inaweza kukitambua kitu kinachostahili kupigwa picha kwa haraka
Simu ina utulivu kwenye kurekodi video kutokana na uwepo wa OIS(Optical Image Stabilization)
Kamera zake zinaweza kurekodi video zenye resolution kubwa za 8K na 4K kwa ubora mkubwa
Ubora wa Software
Samsung Galaxy S23+ inakuja na toleo la Android 13 na mfumo wa One UI 5.1
Moja ya kitu cha kuvutia kwenye One UI 5.1 ni uwezo wake wa kujibu simu ukiwa unaendesha gari ama ukiwa umelala
Simu ikipigwa huku ukiwa unaendesha au umelala, one ui 5.1 itajibu kwa njia ya maandishi yaani meseji
Kuna uboreshaji wa salama wa data zako kwenye Android 13
Matoleo ya nyuma ya android yalikuwa yanaruhusu app kuweza kufanya kazi hata simu ikiwa imelokiwa
Hivyo app za kutrack simu zilitumia huu mwanya, ila android 13 mfumo umebadilika.
Kwani simu ikilock basi kila kitu kinajifunga
Pitia Hapa: Vitu Vipya Kwneye Android 13
Yapi Madhaifu ya Samsung Galaxy S23+
Galaxy S23+ haina sehemu ya kuweka memori za ziada
Pia hakuna sehemu ya kuweka earphone hivyo bluetooth itahusika
Na ikumbukwe bluetooth earphone nzuri hugharimu kiasi kikubwa ch pesa
Simu haiji na chaji hivyo kama hukuwahi miliki chaji yenye kasi itakulazimu ununue
Neno la Mwisho
Iwapo bajeti yako ni ndogo kuwa na Galaxy S23 Ultra, basi Samsung Galaxy S23+ ni mbadala mzuri
Kwani ufanano ni mkubwa na kuna vitu vichache ambavyo S23+ haina
Lakini kama bado pesa haitoshi utalazimika kuangalia brand zingine kama Xiaomi ama Tecno
Kuna Xiaomi 12 Pro na Tecno Phantom X2 Pro, kama hizo hazikuridhishi basi Sony lakini pia bei ni kubwa
Wazo moja kuhusu “Bei ya Simu Samsung Galaxy S23+ na Sifa Muhimu”
Me nipo kibaha barabara(roliondo) nikiitaji simu naipataje?