Kampuni ya Apple imeachia simu za aina nne kwa mwaka 2022
Moja ya simu iliyoingia sokoni ni iPhone 14 Pro Max
Ina muonekano unaofanana na iPhone 13 Pro Max kwa sehemu kubwa
Utofauti kati ya simu iphone toleo jipya na la zamani upo sana kwenye kioo (display), kamera na processor
Vitu vipya vinafanya bei ya iPhone 14 Pro Max kuwa kubwa kuliko 13 pro max pindi ilipotoka
Utafahamu sifa zake za muhimu miundani
Bei ya iPhone 14 Pro Max ya GB 128
Bei ya iPhone 14 Pro Max yenye ukubwa wa GB 128 ni shilingi 2,581,387.60/=
Uwezekano wa bei kuwa kubwa zaidi ya hiyo kwa hapa Tanzania ni mkubwa
Na iwapo GB 128 ni ndogo basi huna budi kuwa na zaidi ya shilingi milioni tatu
Kwani ya GB 1020 inaenda 3,754,745.60/=
Kwa hapa Tanzania bei yake ni lazima ifike milioni nne
Ila, bei inaendana na sifa za simu husika?
Jibu la hili swali utalipata kwa kupitia ufafanuzi wote uliopo hapa
Sifa za iPhone 14 Pro Max
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g na 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | LTPO Super Retina XDR OLED, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | NVMe, 256GB,128GB,512GB,1020GB na RAM 6GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.7inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 3,754,745.60/= |
Ni Upi Ubora wa iPhone 14 Pro Max
iPhone 14 Pro Max ni moja ya simu za apple zinazokaa na chaji masaa mengi hata ukiwa unaitumia muda mrefu kwenye intaneti
Ni simu ngumu kupasuka kutokana na ugumu wa bodi
Inatumia aina zote za mitandao ukiwemo ule wenye kasi
Ina mfumo endeshi mpya kabisa wenye vitu ambavyo havikuwepo kwenye mifumo endeshi iliyopita ya apple
Chaji yake inapeleka umeme unaojaza betri kwa haraka
Kamera zake tatu zinatoa picha nzuri hata nyakati za usiku
Ina nguvu kubwa ya utendaji kwani ina processor inayoizidi nguvu processor za simu karibu zote duniani
Tuitazame kiundani zaidi katika nyanja tofauti
Uwezo wa Network
Simu ya iPhone 14 Pro Max ni simu ya 5G kama ilivyo Samsung Galaxy S22+ 5G
5G yake inasapoti masafa yote kwa maana ya kati, chini na yale makubwa
Kwa sasa nchini inaingia akilini kumiliki simu ya 5G
Vodacom Tanzania wamefanya uzinduzi wa mtandao huu wenye kasi zaidi duniani kwa sasa
Kuelewa mtandao wa 5th Generation (kizazi cha tano) pitia, maana ya 5G na aina zake
Hata mtandao wa 4G simu inakubali karibu masafa yote ya nchi mbalimbali
Zingatia kwamba iPhone za mwaka 2022 kwa Marekani hazina sehemu ya kuweka laini ya simu
Bali zinakuja na eSIM(embeded SIM) ila kwa nchi zingine simu inakuwa na sehemu kwa ajili ya laini
eSIM inatumia software(dijitali) ambayo ipo kwenye chip inayofahamika kama eUICC kuweka laini kwenye simu bila kadi
Kitu kingine kipya kabisa ni uwezo wa simu kuwasiliana na satilaiti kwa ajili ya dharura
Hii inafaa kama simu ikiwa ipo kwenye maeneo yanayokosa mtandao wa simu za mkononi
Kuhusu eSIM, hapa Tanzania hakuna mtandao wenye huduma hii kwa sasa
Kenya mtandao wa Safaricom inayo hiyo huduma
Ubora wa kioo cha iPhone 14 Pro Max
Hii simu janja inatumia kioo cha OLED ambacho apple wanaita Super Retina XDR OLED
Moja kwa moja ubora wa kuonyesha vitu lazima uwe mkubwa
Kwa sababu vioo vya OLED (na AMOLED) huonyesha rangi nyingi na vina kiwango kikubwa cha utofautishaji wa rangi za vitu
Kioo chake ni angavu sana kwani kina kiwango cha unagavu (nits) zinazofika 2000
Kioo kikiwa na nits nyingi kinakuwa kinaweza kuonyesha vitu vizuri ukiwa unatumia simu nje kwenye jua
Mbali na wingi wa nits, ni kioo chenye HDR10, Dolby Vision, refresh rate ya 120Hz na resolution ya 1290 x 2796 pixels
Mpaka sasa unapata picha kwa nini bei ya iPhone 14 Pro Max inaanzia milioni mbili na nusu
HDR10 na Dolby Vision hizi ni teknolojia kwa ajili ya kurekebisha muonekano wa vitu uendane na jinsi kitu kinavyoonekana kwenye mazingira halisi.
Pitia, Jinsi HDR inavyofanya kazi na ufafanuzi wake kiundani
Refresh rate ya 120Hz huwa inafanya screen kuwa laini na nyepesi wakati unaperuzi
Nguvu ya processor Apple A16 Bionic
Linapokuja swala la processor za simu, apple huwa wako mbele kuliko washindani wake
Apple wanadai chip ya Apple A16 Bionic iliyopo kwenye iPhone 14 Pro Max ina nguvu kwa 40% kuliko washindani wake
Hali ndio ipo hivyo hasa kama utatumia app ya Geekbench na Antutu kupima nguvu ya processor
Kwenye Geekbench Apple A16 Bionic ina alama 1800 kwenye core moja
Antutu inaipa alama 978147
Wakati mshindani mkubwa wa chip za bionic ni Qualcomm kwa kutumia SoC ya Snapdragon 8+ Gen 1 ambayo imetumika kwenye baadhi ya simu mpya za Xiaomi
Geekbench inaipa Snapdragon 8+ Gen 1 alama 1321 kwenye core moja
Na majaribio ya Antutu inapata alama 1032660
Ukiitazama alama za Geekbench, snapdragon inazidiwa kwa 26%
Hii inamaanisha simu ina utendaji mkubwa na wa haraka unapotumia kwenye kazi zozote hasa kucheza magemu
Uwezo wa betri na chaji
Toleo jipya la iphone 2022 linakuja na betri lenye ukubwa wa 4323mAh aina ya Li-Ion
Hii betri ni kubwa inayoweza kukaa na chaji masaa mengi
Kwenye majaribio ya Tomhardware kwenye kutumia intaneti masaa mengi mfululizo simu inatunza chaji masaa 13 na dakika 39
Ni karibu masaa 14
Kwa kiwango hiki inamaanisha iPhone 14 Pro Max inaweza kukaa na chaji masaa mengi zaidi kwenye kazi za kawaida
Muda huo unaendana na simu ya Redmi Note 10 yenye betri la 5000mAh aina ya Li-Po
Kwa bahati mbaya simu haiji na chaji hivyo utalazimika kununua chaji
Chaji za iPhone za wati 25 zinaweza kujaza simu kwa 50% ndani ya nusu saa
Sio kitu cha ajabu hiki kwani simu ya Tecno Camon 19 5G VIP inajaa 100% kwa dakika 17 tu
Ukubwa na aina ya memori
Kwenye upande wa memori kuna matoleo manne ya iPhone 14 Pro Max
Kuna ya GB 128, 256, 512 na TB 1 zote zinatumia RAM ya 6
Memori zake ni za aina ya NVMe ambazo husafirisha data kwa kasi kubwa kuliko hata UFS
Uimara wa bodi ya iPhone 14 Pro Max
Simu imeundwa kwa bodi yenye glasi za Gorilla upande wa nyuma na mbele
Upande wa pembeni simi imewekewa chuma (stainless steel)
Kama iliyo ada, ni simu ngumu kupasuka
Lakini pia haipitishi maji iwapo simu ikidumbukia maji ya kina cha mita sita kwa muda wa nusu saa
Uimara wake unaendana na iPhone 13 Pro Max na hata iPhone 12 Pro Max
Ubora wa kamera
iPhone 14 Pro Max ni iphone macho matatu yenye kamera aina za wide, ultrawide na telephoto
Kwa mara ya kwanza Apple wametumia kamera yenye megapixel kubwa ya 48MP
Kwa picha chache zilizopigwa na hii simu, kamera yake inatoa picha nzuri
Lakini uchakataji wa picha umekuwa ni wa kupitiliza hata kwa kamera yenye 48
Uchakataji unalenga kupunguza Noise(vitu visivyohitajika) lakini unasababisha picha kupungua kwa uhalisia
Ukipiga picha kwa kamera ya 48MP itapiga picha ya 12MP kama haujaseti kutumia kamera ya 48MP
Kwenye video ukirekodi na kamera kubwa kwa kutumia ProRaw faili linakuwa kubwa mno
Kamera za Apple zinaishia kurekodi video za 4k tu pamoja na lenzi yake kuwa na uwezo wa kurekodi 8K
Ubora wa Software (iOS 16)
Simu ya iPhone 14 Pro Max inakuja na mfumo endeshi wa iOS 16
Huu ni mfumo unakuja na kitu kinaitwa Always On Display
Kwa maana ukilocki simu, saa na vitu vingine vinaonekana kwa sekunde kadhaa
Ni kitu ambacho kiliwepo kwa miaka mingi kwenye simu za Android hivyo Apple wamechelewa
Kitu kingine cha kuvutia ni Dynamic Island ambayo imeambatanishwa kwenye kamera ya mbele
Ukipiga simu au ukisikiliza mziki icon zake zinahamia kwenye hiyo sehemu
Pia ni sehemu unayoweza kuitumia kufungua baadhi ya app
Ifahamu zaid: Vitu vipya vilivyopo kwemye matoleo iphone 14
Yapi Madhaifu ya iPhone 14 Pro Max
Simu za iPhone 14 Pro Max zinalazimisha kununua chaji kwani haziji na chaji yake
Hazina sehemu ya kuwekea memori hii inaweza kuwa changamoto kwa simu yenye GB 128 na ikiwa inarekodi video za ProRaw nyingi
Huduma ya kutumia setilaiti inapatikana marekani pekee
iPhone 14 Pro Max iliyonunuliwa USA haitakuwa na uwezo wa kutumika kwenye nchi ambazo hazina huduma ya eSIM
Bei ya iPhone 14 Pro Max ni kubwa na si ndogo ukilinganisha na uwezo wa watanzania japo simu ina uwezo mkubwa
Neno la Mwisho
iPhone 14 Pro Max ni simu ya kuwa nayo kwa mwaka 2022
Lakini inafaa kama una hela ya kutosha
Kwa kiasi kikubwa bei yake inaendana na ubora wa simu
Na ni muhimu kujua kwa nini unahitaji simu ya zaidi ya milioni tatu
Wazo moja kuhusu “Bei ya iPhone 14 Pro Max na Sifa Zake Muhimu”
Orijino utaijuaje