Simu ya Infinix Hot 40 Pro ni simu janja ya daraja la kati ambayo imetoka pamoja na simu ya infinix hot 40
Hot 40 Pro ina ubora wa ziada kwenye utendaji na pia kamera yake inatoa picha vizuri kwa kiasi fulani
Kimuonekano simu inafanana na iphone 15 pro max hasa kwenye mpangilio wa kamera
Ila isikutishe maana bei ya infinix hot 40 pro haizidi laki nne na nusu na kiubora haifikii toleo lolote la iphone la hivi karibuni
Kumbuka bei yake inatofautiana na ukubwa wa memori ipo ya GB 128 na GB 256
Bei ya Infinix Hot 40 Pro ya GB 128
Bei rasmi ya hot 40 pro ya gb 128 ni shilingi laki na nusu japo inaweza kuzidi kwa maeneo mengine
Kiasi cha pesa kinaendana sana na sifa za simu
Kwa vitu ambavyo simu inakuja navyo ndivyo vitu vinavyochangia simu kuwa katika bei hii
Na hata simu kutoka kwa kampuni zingine zenye sifa sawa na hii infinix huuzwa kwa bei ya chini ya laki nne
Ni muhimu kuangalia kila sifa ili ujiridhishe iwapo ubora wa infinix hot 40 pro unaweza kukidhi mahitaji yako
Sifa za Infinix Hot 40 Pro
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.2, 256GB,128GB na RAM 8GB |
Kamera | Kamera TATU
|
Muundo | Urefu-6.78inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 350,000/= |
Upi ubora wa Infinix Hot 40 Pro
Eneo kubwa lenye maboresho kwenye hii simu ni utendaji
Utendaji wake ni mkubwa kuizidi simu kama Oppo A17K
Betri yake ina ukaaji mzuri wa chaji kutokana na kuwa na betri kubwa
Chaji yake inakufanya kuisubiria simu kwa muda mfupi kwani ina kasi kubwa ya kuchaji
Kioo chake kina refresh rate inayoizidi infinix hot 40 na uangavu mkubwa
Kama ilivyolezwa awali kuwa utendaji wa hii simu umeongezeka kidogo na unaizidi hata simu ya Redmi Note 10
Hivyo pia kuna maboresho pia kwenye uwezo wa network wa hot 40 pro
Uwezo wa Network
Simu inasapoti mpaka mtandao wa 4G haiji na uwezo wa 5G
Hata hivyo aina ya 4G inayasapoti ni ile yenye kasi kubwa ambayo ni nadra kuipata kwa hapa nchini
Aina ya 4G yake LTE Cat 13 yenye kasi ya kupakua vitu inafika 600Mbps
Yaani kwa mfano kama unapakua faili LA MUVI lenye ukubwa wa MB 750, simu itaweza kudownload kwa sekunde kumi
Ila mitandao karibu yote hapa nchini haitoi kasi hata ile yenye 5G
Mara nyingi ukijitahidi sana kwenye 4G unaweza fika 75Mbps
Ukiondoa uwezo wake wa network, ubora wa hot 40 pro kwenye kioo pia unavutia kiasi fulani
Ubora wa kioo cha Infinix Hot 40 Pro
Infinix Hot 40 Pro inatumia kioo cha IPS LCD
Japo kiubora vioo vya amoled huwa vipo, ila kioo cha hii simu kina resolution kubwa ya 1080×2460 pixels
Resolution kubwa ya kiasi hiki huboresha muonekano wa vitu kwenye skrini
Uangavu wa kwenye skrini ni mkubwa kwa wastani
Mtumiaji ataweza kuona vitu vizuri akiwa hata anaitumia simu juani
Kubwa zuri kuhusu kioo cha infinix hot 40 pro ni uwepo wa refresh rate kubwa
Hii inafanya kioo kuwa fasta na kiraini wakati wa kuperuzi
Simu inaruhusu kuzima refresh rate kubwa kwa sababu ukiiacha muda wote huwa inakula chaji
Uwepo wa refresh rate kubwa unafanya kazi vizuri kutegemeana na nguvu ya processor iliyotumika
Nguvu ya processor Mediatek Helio G99
Simu ya Infinix Hot 40 Pro inatumia chip ya Mediatek Helio G99
Helio G99 ni processor nzuri ya daraja la kati inayoweza kufanya kazi kubwa bila tatizo
Kwa wapenda magemu ya simu, mediatek helio g99 inacheza magemu mengi kwa fps nyingi hizi ukiwa umseti muonekano wenye ubora wa kati kwenye gemu
kwa baadhi ya magemu ukicheza kwa muonekano wa Ultra HD idadi ya fps hupungua hivyo gemu inakuwa sio ya kuvutia sana
Kiujumla nguvu yake ni kubwa kuliko hata Mediatek Helio G88 ambayo imetumika kwenye simu ya Tecno Spark 10 Pro
Helio G99 ina ufanisi wa kuridhisha katika matumizi ya betri.
Kwa simu yenye betri kubwa itaweza kukaa na chaji muda mrefu hata nyakati ambazo processor inafanya kazi kubwa
Hivyo ni vizuri ukaelewa uwezo wa betri ya infinix hot 40 pro
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya Hot 40 Pro ina ukubwa wa 5000mAh
Simu inakuja na chaji inayopeleka umeme wa wati 33
Kwa mujibu wa Infinix, chaji hii inajaza betri yake kwa 70% ndani ya dakika thelathini
Kwa mantiki hiyo chaji yake inaweza kujaza betri kwa 100% ndani ya dakika 70
Ukaaji wa chaji unaweza kudumu kwa zaidi ya masaa kumi
Kwani hiyo ni kawaida ya betri zenye ukubwa
Ukubwa na aina ya memori
Infinix Hot 40 Pro zinapatikana zenye GB 128 na GB 256 na zote zina ukubwa wa RAM 8
Na pia simu inaweza kutemia GB nane zingine za memori ya simu kama RAM
RAM kubwa inasaidia kufungua vitu vingi kwa wakati mmoja bila kuwa na mkwamo
Maana RAM inapojaa yote husababisha simu kuwa nzito
Mara nyingi unapocheza gemu hujaza RAM
Aina ya memori inayotumiwa na hii simu ni UFS 2.2
Kasi yake ya usafirishaji wa data ni mara ya simu zinazotumia mifumo eMMC kama Infinix Hot 40
Uimara wa bodi ya Infinix Hot 40 Pro
Infinix Hot 40 Pro haina viwango rasmi vinavyoainisha uwezo wa kuzuia maji ya waterprooof
Kwa maana hiyo kama ikizama kwenye maji ya kina kirefu unapaswa uitoe haraka
Vinginevyo maji yataingia
Ni tofauti sana na mfano wa simu ya Samsung Galaxy 23 Ultra yenye uwezo wa kuzuia maji kwa muda wa nusu saa kama ikizama kwenye kina cha mita 1.5
Ubora wa kamera
Simu inakuja na jumla ya kamera zipatazo tatu
Kati ya kamera tatu kamera moja yenye megapixel 108 inayopiga picha vizuri
Kamera nyingine aina ya macro haitoi picha vizuri kwa vitu vya karibu
Nyakati za mchana kamera kubwa inajitahidi katika uwasilishaji wa rangi
Kamera ya hii simu inakosa teknolojia muhimu ya ulengaji ya PDAF
Inaweza isiwe kamera nzuri kupiga vitu ambavyo viko kwenye mwendo kutokana na aina ya autofocus iliyopo
Ubora wa Software
Hii simu inakuja na Android 13 na XOS 13.5
xos 13.5 imejaribu kuiga muundo wa iphone wa dynamic island
Infinix huu mfumo wanaita dynamic ring
Unaweza fuatilia kiundani kwenye hii video
Washindani wa Infinix Hot 40 Pro
Kuna simu nyingi zinazoendana kisifa na Infinix Hot 40 Pro
Kwa maana hiyo hao ni washindani wa moja kwa moja
Kwa mfano simu ya Samsung Galaxy A15 4G ina utendaji sawa na hii infinix
Ila Galaxy A15 4g inakuja na kioo cha amoled, android 14 na kamera ya ultrawide
Vitu ambavyo havipo kwenye hii infinix wakati huo tofauti ya bei baina ya hizi simu mbili ni kama shilingi elfu hamsini tu
Mshindani mwingine ni kutoka kampuni ya Xiaomi kwa kupitia simu ya mwaka 2022 ya Xiaomi Poco M5 ambayo ina ultawide na kamera kubwa yenye ulengaji PDAF,
Xiaomi Poco M5 bei yake inaendana kabisa na infinix Hot 40 Pro
Neno la Mwisho
Infinix Hot 40 Pro ni simu ya bei nafuu ya daraja la inayoweza kukidhi mahitaji ya watumiaji wa kila lika
Kuna maboresho kwenye baadhi ya maeneo ila kwenye kamera hakuna tofauti na toleo la Infinix Hot 40
Kizuri ni kuwa simu inakuja na RAM na memori ya simu inayotosheleza kuhifadhi na kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja
Maoni 13 kuhusu “Bei ya Infinix Hot 40 Pro na Ubora wake”
Kwanini munasemA kamera sio nzuri kwenye upigaji picha?
Mfumo mzima WA kamera unakosa pdaf, kamera inarekodi 1080 yaani hairekodi 4k kama redmi note 10, usahihi WA rangi sio mkubwa ukilinganisha na Samsung au iPhone au hata infinix note 40 vip, Ila haiwezi kushangaza kutokana na bei ya simu hivyo si simu mbaya
hongeren san infinx
Nawapata wapi
Wewe unapatikana wapi
Kiukwel mumeupiga mwingi ktk swala zima lakutuleta kwenye ulimwengu wa kidigtor
Naweza kuipata kwa laki tatu kamili
Mimi nahitaji Infinix hot40i mkopo. Bei shs ngapi na nawapataje?
Hizo simu bei kamili ni ipi make Kuna wengne wanatangaza kwa laki mbili na nusu (250000)
Inategemeana kiongozi
Nashida na simu ya infinix hot 40i naipataje na bei yake ni shingap
nahitaji infinix hot 40pro yenye 128G bei yake ni shingapi ? napatikana munispaa ya kahama
Zinazopatikana kiurahisi ni za gb 256