SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Ubora na bei ya simu ya Infinix Hot 12i (2022)

Bei Nafuu

Sihaba Mikole

April 16, 2022

Simu ya infinix hot 12i ni simu ya daraja la mwisho iliyoingia sokoni mnamo aprili 2022

Ni infinix ya macho matatu kama ilivyo kwa simu ya infinix hot 12 bila kusahau simu mpya ya Infinix Note 12 VIP

Ifahamu note 12 vip upitia hapa, sifa na bei ya infinix note 12 vip

Kwa mzoefu wa smartphone anaweza asivutiwe na ubora wake wa kiujumla

infinix hot 12i upande wa nyuma

Lakini unajua nini?

Vipo vya kuvutia upande wa betri na baadhi ya sifa zingine, zipitie moja moja uzifahamu na zote zimefafanuliwa humu

Bei ya infinix hot 12i kwa baadhi ya maduka haizidi laki tatu na nusu .

Bei yake inaweza ikawa ni ndogo ila si rafiki ukizijua simu za kampuni zingine utakazozikuta kwenye hii post

Bei ya Infinix hot 12i

Infinix hot 12i yenye ukubwa wa GB 64 na RAM 3G inauzwa shilingi 350,000/=

Na yenye ukubwa wa 64 GB na ram ya 2GB inauzwa shilingi 300,000/=

Epuka kutazama ukubwa wa memori pekee bila kujua aina ya memori ya simu.

Simu ina bei nafuu, ila zifahamu sifa zake na washindani wake kabla kufanya maamuzi

Sifa za Infinix hot 12i

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – Mediatek  Helio A22
  • Core Zenye nguvu() –
  • Core Za kawaida(4) – 4×2.0GHz Cortex A53
  • GPU-PowerVR GE8320
Display(Kioo) IPS LCD,
Softawre
  • Android 11
  • XOS 7.6
Memori eMMC 5.1, 64GB na RAM 3GB, 4GB, 2GB
Kamera Kamera nne

  1. 13MP,AF(wide)
  2. QVGA
  3. QVGA
Muundo Urefu-6.6inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
Bei ya simu(TSH) /=

Upi ubora wa Simu ya Infinix hot 12i

Ubora wa hot 12i upo sehemu mbili nayo ni betri na network

Simu ina betri kubwa

Utendaji wake wa simu unatumia umeme mdogo

Jambo linaliifanya simu kutunza umeme kwa masaa mengi

Ina 4g yenye kasi ya kuridhisha

Ila kwenye nyanja zingine simu inakosa ubora unaotakiwa kwa nyakati za sasa

Uwezo wa Network

Infinix hii inakubali mtandao wa 4G na 3G pia

Aina ya 4G simu inayotumia ni LTE Cat 7

LTE Cat 7 inaweza kudownload faili kwa kasi inayofika 300Mbps

network za infinix hot 12i

Ni spidi inayoweza kupakua mafaili makubwa kwa sekunde.

Ila jua hakuna kampuni ya simu inayotoa kasi kubwa inayofikia 300Mbps hapa Tanzania

Simu ina network bands za 4G zipatazo 12

Na laini zote za 4G Tanzania zitakubali bila tatizo

Ubora wa kioo cha Infinix hot 12i

Infinix hot 12i inatumia kioo aina ya ips lcd.

IPS LCD ina ubora wa chini kwenye uoneshaji wa rangi hasa rangi nyeusi

Hii simu ina resolution ya kawaida ambayo haiwezi ikawa ni standard kwa sasa.

Kwani resolution yake ina pixels 720 x 1612

Kwa bahati mbya display inakosa hdr10 ambayo ingekuwa inaboresha muonekano wa vitu

Nguvu ya processor Helio A22

Chip ya MediaTek Helio A22 ndio yenye kazi ya kufanya shughuli zote za simu ya infinix hot 12i

Utendaji wa Helio A22 ni mdogo sana sana sana

Simu inapata alama ndogo kwenye apps zinazopima ubora wa processor.

processor ya infinix 12i helio

Hii ni chip yenye core nne tu ambazo hazivuki spidi ya 2.oGHz.

Kitu kinachosababisha utendaji hafifu ni muundo wa core uliotumika kwenye processor

Kwani core zake zinatumia muundo wa Cortex A53

Kwenye simu zingine Cortex A53 hutumika kufanyia kazi ndogo ndogo

Ukiwa unacheza gemu kama fortine simu itachemka sana

Uwezo wa betri na chaji

Betri yake ina uwezo wa kukaa na chaji muda mrefu

Kwa sababu simu yenyewe inafaa kutumika kwa vitu vidogo na sio vitu vinavyohitaji nguvu kubwa

chaji na betri ya infinix hot 12i

Simu haina fast chaji.

Kwa hiyo betri itachelewa kujaa, na itachukua zaidi ya masaa matatu kujaa kwa 100%

Ukubwa na aina ya memori

Kama nilivyotangulia kusema, unapoanunua simu kwanza fahamu aina ya memori ya simu.

Hot 12i inatumia memori aina ya eMMC 5.1

Memori za eMMC huwa zina kasi ndogo katika kusafirisha data ukilinganisha na memori za UFS

Kitu kinachofanya simu kuchelewa kuwaka, na app kutokufunguka kwa haraka

Zipo infinix hot 12i za aina tatu upande wa memori

Ambazo ni 64GB na ram 2GB, 64GB na RAM 3GB, mwisho ni 64GB na RAM 4GB

Kiukubwa, memori itahifadhi vitu vya kutosha

Uimara wa bodi ya Infinix hot 12i

Bodi ya hii infinix imeundwa kwa plastiki upande wa nyuma na kwenye fremu.

Uimara wa plastiki huwa ni wa chini.

Ni rahisi simu kupasuka ama kuchunika rangi ikizingatiwa hot 12i hajawekewa kioo cha gorilla.

Ili kudhibiti uharibifu, utalazimika kuweka screen protecot imara

Bila hivyo uzito wake wa gramu 190 unaweza kuigharimu simu ikiwa haina kava na ikianguka kimo kirefu

Simu ni ndefu na inavutia kwa macho

Kwani urefu wake unafika inchi 6.6

Ubora wa kamera

Infinix hot 12i ni infinix ya macho matatu yenye kamera zenye resolution ndogo

Kwani kamera kubwa ina 13MP na inatumia teknolojia ya ulengaji AF.

Kwenye ulengaji AF inazidiwa na PDAF

kamera macho matatu za infinix hot 12i

Kamera zingine mbili ni za aina ya QVGA.

Usitatizwe na jina, QVGA ni kamera zenye resolution ndogo sana na teknolojia ambayo imepitwa na wakati

Resolution ya QVGA ni 320×240

Utapata picha mbaya ukitumia kamera hizi

Kiujumla ubora wa kamera wa simu ni wa chini

Ubora wa Software

Simu inakuja na android 11 na mfumo wa XOS 7.6

XOS 7.6 ina app ya XHIDE kwa ajili ya kuficha mafaili

Pia XOS ina mfumo kukualert pale simu inapotelewa kwenye chaji

Software ya infinix inamuwezesha mtumiaji kuseti vitu ambavyo mtoto atapaswa kuviona

Ina xclone inayosadia kuwa na akaunti nyingi za whatsapp kwenye simu moja.

XOS ni nzuri kama haitakuwa na matangazo mengi yanayokela

Yapi Madhaifu ya Infinix hot 12i

Simu ina mapungufu mengi tena kwa asilimia kubwa

Hatutayaelezea yote.

Kiujumla hii ni simu ina kiwango cha chini ukilinganisha bei

Moja ya sehemu ambayo imeshushwa sana ubora ni kamera

Kamera zina resolution ndogo, lakini display sio nzuri

Na utendaji wa simu ni mdogo kabisa.

Nadhani Infinix walipaswa kutumia Android toleo la Go Edition ili kuongeza ufanisi

Bei yake ni kubwa kuliko ubora

Neno la Mwisho

Simu ya infinix hot 12i inamfaa zaidi mtumiaji wa smartphone anayeanza kutumia simu

Ila simu inazidiwa pakubwa na simu ya Redmi 9a ya mwaka 2020

Wakati bei ya Redmi 9a haizidi laki mbili na nusu

Infinix hii ilipaswa iuzwe chini ya laki mbili

 

Maoni 8 kuhusu “Ubora na bei ya simu ya Infinix Hot 12i (2022)

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

infinix note 30 vip thumbnail

Bei ya Infinix Note 30 VIP na Sifa Zake

Infinix kwa mwaka 2023 wameachia matoleo mengi yakiwemo ya note series Moja ya toleo hilo ni Infinix Note 30 VIP ambayo imetoka mwezi Juni Haina tofauti sana na infinix note […]

infinix zero 30 5g thumbnail

Ubora na Bei ya Infinix Zero 30 5G (Infinix Kali)

Ni infinix kwa mara nyingine inajaribu kutengeneza hisia chanya juu ya ubora wa simu zao Unaweza kuliona hili kwa toleo jipya la Infinix Zero 30 5G Hii ni simu kali […]

iphone 15 pro thumbnail

Bei ya iPhone 15 Pro na Sifa Zake Muhimu

Kama ilivyotarajiwa hapo awali kuhusu ujio wa simu mpya za iphone kwa mwaka huu 2023 Moja ya simu hiyo ni iPhone 15 Pro ambayo imeongezewa utendaji Kiumuonekano hauwezi kutofautisha sana […]

iphone feki 2

Simu Origino ni Zipi na Unazitambuaje? (Hatua za kufuata)

Matoleo ya simu yamekuwa yakitoka mara kwa mara yakiwemo yenye bei kubwa na zinazotamaniwa na watu wengi Aina hizi ya simu huvutia watu wasio waaminifu kutengeneza simu feki zenye ufanano […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company