Unafahamu kuwa simu ya infinix note 11 Pro ni simu inayoweza shindana na simu nyingi za tabaka la kati?
Hilo linatokana na aina ya processor(chipset) simu inayotumia.
Infinix note 11 Pro inaweza ikawa moja ya simu ya infinix yenye kamera nzuri.
Ukizitazama sifa za infinix note 11 pro utaona kuwa simu ina kioo kizuri na mfumo wa betri ulio imara kwa spidi ya kuchaji.
Note 11 Pro imekamilika kwenye idara nyingi na mapufungu yapo machache.
Sifa za infinix note 11 pro kiufupi
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.2, 128GB na RAM 8GB, 4G |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.95inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 650,000/= |
Upi ubora wa simu ya Infinix note 11 Pro?
Ubora wa simu ya infinix unapatikana hasa kwenye processor, kioo, upana na urefu wa simu pamoja na mfumo wa chaji.
Infinix note 11 Pro inakuja na chaji inayojaza simu kwa muda mfupi.
Kimakadirio betri inaweza kujaa ndani ya dakika 70.
Kioo cha infinix note 11 pro kina refresh rate kubwa.
Simu inaweza kufungua app yoyote kwa urahisi kwa sababu ya processor yenye nguvu.
Kiubora hii simu inaikaribia simu ya infinix zero 5g
Kufahamu ubora wa simu hii kwenye kila nyanja iangazie simu katika nyanja nane zifuatazo.
Network
Infinix note 11 pro inakubali mtandao wa 4G.
4g yake ni ya kundi la 13 (cat 13).
Ambayo spidi yake ya juu kudownload ni 390Mbps
Simu haina modem inayosapoti 5g
Kwa Tanzania hakuna mtandao wa simu wowote wenye minara ya 5G.
4G ya infinix note 11 pro inasapoti network bands 12 kati ya 24.
Kwa maana simu inaweza kutokubali 4g za baadhi ya mitandao.
Ila kwa Tanzania inakubali intaneti ya 4G za mitandao yote.
4g Network bands zinazopatikana Tanzania
Bands za 4G zilizomo ndani ya Infinix note 11 pro ni 1, 2, 3, 4, 5, 7, 8, 20, 28, 38, 41 na 40
Ili laini ya simu ikubali mtandao wa 4g kwenye note 11 pro inapaswa iwe na moja ya hizo band.
Hizi hapa ni aina za 4g bands za mitandao mitano inayotumiwa sana Tanzania.
Halotel – 7
Vodacom- 3
AirTel- 28
Tigo- 20 na 3
TTCL- 3 na 40
Kiufupi laini za mitandao yote nchini zitafanya kazi vizuri tu.
Ubora Kioo cha infinix 11 pro?
Ininix 11 Pro inatumia kioo cha IPS LCD.
Display yake ni kubwa inayoweza onyesha vitu kwa ubora.
Hilo linachangiwa na resolution kubwa ya 1080 x 2460 pixels
Hiki kioo ni kizuri kwa wapenzi wa magemu.
Kwa sababu kina refresh rate inayofikia 120Hz.
Refresh rate ikiwa kubwa simu inakuwa nyepesi hasa ukiwa una-scroll kwenda juu au chini.
Uangavu wa kioo si mkubwa.
GSMArena walipima uangavu wake unaofikia 470nits.
Kwenye jua kali screen inaweza isionyeshe vitu vizuri.
Nguvu ya processor ipoje?
Simu ya infinix note 11 pro inatumia processor yenye utendaji mkubwa.
Processor yake ni MediaTek Helio G96.
Mifumo inayopima nguvu za processor kama 3DMark na geekbench inaonyesha MediaTek Helio G96 inazipita baadhi ya processor za Snapdragon.
Helio G96 ina core nane.
Kuna core zenye nguvu na zenye uwezo wa kawaida.
Uwezo wa Core zenye nguvu
Core zenye nguvu sana zipo mbili.
Kila core ina spidi ya 2.05 GHz
Core zote zinatumia muundo wenye nguvu aina ya Cortex A76.
Pitia maelezo ya kina yanayofafanua aina ya processor za simu zenye nguvu.
Cortex A76 inafanya utendaji wa simu kuwa sawa na baadhi ya laptop kama ARM Holding wanavyodai.
Muudo wa Cortex A76 una utendaji mkubwa na matumizi madogo ya betri ukilinganisha Cortex A73.
Uwezo wa core zenye nguvu ndogo
Ubora wa core ndogo unaangaliwa kwenye matumizi madogo ya betri.
Helio G96 ina core ndogo sita.
Kila core ina spidi ya 2.0 GHz
Na core zote zinatumia muundo wa Cortex A55.
ARM Holding wanasema Cortex A55 imeongeza utendaji kwa asilimi 18.
Na imeongeza utunzaji wa chaji kwa 15% ukilinganisha na Cortex A53.
Cortex A53 imetumika kwenye processor ya Helio G35 inayopatikana kwenye simu ya Xiaomi Redmi 9C.
Mpangalio wa processor ya Helio G96 unafanya simu ya Infinix note 11 pro kukaa na chaji muda mrefu.
Na utendaji mkubwa unaotumia umeme kidogo
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya infinix note 11 pro ni aina ya Li-Po yenye ujazo wa 5000mAh.
Chaji ya infinix note 11 pro inapeleka umeme wa wati 33.
Umeme wa wati 33 unaweza jazi betri ya ukubwa 5000mAh ndani ya dakika 75.
Lakini chaji ya infinix note 11 pro inajaza simu kwa dakika 125 (pitia hapa)
Infinix note 11 pro ni moja ya simu inayotunza chaji muda mrefu.
Ikiwa haitumiki simu inakaa na chaji masaa 128.
Simu ikiwa inatumia intaneti betri inaisha baada ya masaa 17 na dakika 34
Ukubwa na aina ya memori
Infinix note 11 pro inatumia memori aina ya UFS 2.2
Ni mfumo unaosafirisha data kwa kasi kubwa.
Kasi inayofanya simu kuwaka na kungua app kwa sekunde chache.
Memori za simu zina ukubwa wa 128GB.
Ukubwa unaweza kuhifadhi mafaili na app za kutosha.
Kuna infinix note 11 pro ya 4GB RAM na 8GB RAM.
RAM kubwa inasaidia simu kufungua vitu vingi kwa wakati mmoja bila kukwama.
Na RAM ya simu ni aina ya LPDDR4X
LPDDR4X ni aina ya RAM inayotumia umeme mdogo kwa kusafirisha data kwa kasi kubwa.
Uimara wa bodi
Bodi ya infinix note 11 pro ni plastiki upande wa nyuma na fremu.
Na display imewekewa glassi lakini sio vioo vya gorilla.
Mara nyingi plastiki haziwezi kuhimili kupasuka endapo simu imeanguka kwa kimo kirefu.
Hii simu ni ndefu inakaribia inchi 7
Na ina uzito wa gramu 209
Ubora wa kamera
Kamera za infinix note 11 zipo tatu.
Kamera mbili zinatumia teknolojia ya autofocus(ulengaji) aina ya PDAF.
Aina ya kamera tatu ni
- Wide
- Telephoto
- Macro
Kwa kulinganisha na simu zingine zenye kamera nzuri hii simu ina ubora wa kawaida.
Telephoto inaweza kuzoom kwa kutumia lens(optical zoom) mara mbili
Ubora wa video
Simu inaweza kurekodi video zenye ubora full hd(1440) pekee kwa spidi ya 30fps
Ni tofauti na simu ya xiaomi 12 pro
Selfie camera pia inarekodi picha ubora wa full hd pekee
Ubora wa picha
Ukizitazama picha zilizopigwa na gsmarena infinix note 11 pro inatoa picha nzuri nyakati za mchana.
Noise ziko kwa kiasi kidogo japokuwa simu ina shida ya contrast kwa vitu ambavyo vipo mbali
Infinix note 11 pro inatoa picha nzuri nyakati za usiku pia.
Japokuwa kuna changamoto kidogo ya dynamic range.
Kwa sababu baadhi ya vitu rangi zinatawala pakubwa(exposure kubwa)
Kwa mfano uangavu wa taa ni mkubwa kiasi cha kutengeneza ukungu mweupe kwa mbali kwenye giza
Lakini kamera inatoa pivha safi kwa kiasi kikubwa
Ubora wa Software
Simu ya infinix note 11 pro inakuja na android 11
Android 11 inawezeshwa na software ya Infinix ya XOS 10
Hakuna taarifa za infinix note 11 pro kupokea toleo jipya la Android 12
Kuna mapya mengi yameongezeka ambayo hayapo kwenye android 11
Infinix wanasema XOS 10 inafungua app kwa haraka.
Kwa maana ukitachi icon ya app basi ndani ya sekunde chache app inafunguka
XOS 10 ina theme nyingi za kuboresha muonekano wa simu
Bei ya infinix note 11 pro
Bei ya infinix note 11 pro inafika shilingi 650,000/= kwa Tanzania hasa maduka ya kariakoo
Wengine wanauza 620,000/= moja ya comment ya akaunti rasmi ya instagram infinix Tanzania ilionyesha
Simu ni nzuri lakini bei ni kubwa kidogo
Kwa nini?
Bei hii inakupa simu bora kuliko hii ya Redmi note 11 pro 5g
Baadhi ya simu zinazotumia processor mpya za dimensity zinapatikana kwa bei ya chini ya 450,000/=
Mfano mzuri ni Redmi note 10 5G.
Bei ya infinix note 11 inaweza nunua simu kali kila idara ya Samsung Galaxy A52
Yapi madhaifu ya Infinix note 11 Pro?
Simu zinazouzwa kuanzia laki sita na kuendelea hutumia chip zenye nguvu zaidi ya processor Helio G96.
Infinix hawajaweka ulinzi wa kuzuia maji kupenya ndani ya simu.
Kwa maana infinix note 11 pro inakosa viwango vya IP67
Kamera hazikuwekewa teknolojia bora zaidi za kulenga(autofocus) kama dual pixel PDAF.
Simu nyingi za tabaka la kati hutumia GPS zaidi ya moja.
Ila infinix note 11 pro inatumia GPS moja pekee.
Network yake ina bands chache za 4G hivyo baadhi ya mitandao duniani ikagoma kutumika kwenye simu.
Maoni 8 kuhusu “Sifa za simu ya Infinix note 11 Pro [Madhaifu na Ubora]”
Yeah kiukweli hii simu ni nzuri maana naitumia na iko bomba kabisa
Hakika hili simu naitumia na nimeipenda iko vizuri sana
Hakika hili simu ni nzuri sana nimeipenda
Natamani kuipata hiyo simu asa tatizo kwa kipindi hiki Cha novemba 2023 sizani kama zipo
Mim nauza nitafute 0627593618
Ni simu nzuri mno
Kweli simu ni Kali sana naitumia kwanza muonekano Hadi ubora wake simu ni Kali naitwa Meshack Sareyo nipo Minjingu Ofisi za Yehova Niss Limited studio
Naitaji mfuniko wa sim yangu