SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Ubora wa Simu ya Xiomi 12 Pro [Chaji yake inashangaza]

Simu Mpya

Sihaba Mikole

March 24, 2022

Ulishawahi kutumia simu inayowahi kujaa ndani ya dakika kumi nane?

Sio tu kujaa kwa haraka pia betri inakaa na chaji muda mrefu.

simu-ya-xiaomi-12

Simu ya Xiomi 12 Pro ni simu yenye uwezo wa kuchaji betri kwa haraka.

Sifa za xiaomi 12 pro zinaifanya simu kuwa na utendaji mkubwa na wa kasi.

Hii simu ina kioo kigumu kigumu.

Ina ulinzi imara wa kuilinda simu pale inapoanguka kutokana na aina ya kioo inachotumia.

Kwenye sehemu za simu za msingi imejitosheleza pakubwa japo mapungufu yapo.

Na mapungufu ya Xiaomi 12 Pro unaweza kuyagundua kwa kuangalia sifa zote za Xiaomi 12 Pro.

Sifa za simu ya Xiaomi 12 Pro.

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
  • CPU – Snapdragon 8 Gen 1
  • Core Zenye nguvu(4) – 1×3.00 GHz Cortex-X2 & 3×2.50 GHz, Cortex-A710 & 4×1.80 GHz
  • Core Za kawaida(4) – 4x 1.8 GHz – Cortex-A510
  • GPU-Adreno 730
Display(Kioo) LTPO AMOLED, Refresh rate:120Hz
Softawre
  • Android 12
  • MIUI 13
Memori UFS 3.1, 128GB, 256GB na RAM 8GB,12GB
Kamera Kamera nne

  1. 50MP,PDAF(main)
  2. 50MP(ultrawide)
  3. 50MP(Telephoto)
  4. 32MP(selfie camera)
Muundo Urefu-6.5inchi
Chaji na Betri
  • 4600mAh-Li-Po
  • Chaji-120W
Bei ya simu(TSH) 1,506,400/=

Taarifa za Xiaomi zingine utazikuta kwenye kurasa ya gsmarena ya xiaomi 12 pro

Upi ubora wa simu ya xiaomi 12 pro?

Kuna sehemu nane za simu zinazoonyesha ubora wa simu ya xiaomi 12 pro.

Xiaomi 12 ina ubora katika nyanja zifuatazo.

  1. Processor yenye nguvu
  2. Kioo kizuri
  3. Fast chaji.
  4. Network
  5. Glassi ngumu kwenye display
  6. Memori kubwa na yenye kasi
  7. Kamera kali

Muunganiko wa hizo sehemu saba zinaifanya simu kuwa ngumu na yenye uwezo wa kusukuma applikesheni bila kukwama.

Xiaomi 12 Pro inafungua gemu zote za simu.

Kiuhalisia simu nyingi zinaweza kufungua app yoyote.

Ila kwa simu zenye ubora mdogo hupata shida kufungua baadhi ya apps.

Na wakati mwingine simu inachemka sana.

Kwa sababu ya utendaji wa processor.

Utendaji wa processor upoje?

Xiaomi 12 Pro inatumia chipset ya Snapdragon 8 gen 1.

Snapdragon 8 gen 1 ina utendaji mkubwa inazidiwa kidogo sana na chip ya Apple A15 Bionic.

Uwezo wa snapdragon 8 gen 1 umethibitishwa na applikesheni za GeekBench na Antutu

Antuntu ni nini?

Antuntu ni applikesheni inayopima uwezo wa simu kwenye cpu(processor), ram na memori.

Antutu inaonyesha ubora wa chip kwa kutumia points.

Point nyingi zinaonyesha nguvu ya processor.

Snapdragon 8 gen 1 ina point 249768.

Ni processor chache(kama hakuna kabisa) za simu zinazofikia hizo point.

Vipi kuhusu Geekbench?

Geekbench inapima uwezo wa processor upande wa cores.

App ya geekbench inaonyesha ubora kwa kutumia alama(scores).

Alama zikiwa kubwa inamaanisha processor ya simu inautendaji mkubwa.

Iwapo hufahamu maana ya core pitia kurasa huu wa processor za simu.

Snapdragon 8 gen 1 ina alama 1216 kwenye core moja.

Na alama 3793 kwenye core nyingi.

Ni ngumu kukuta processor za simu za android zikifikia utendaji huo.

Kwa nini processor ya xiaomi 12 pro ina nguvu kubwa?

Processor ilyomo ndani ya simu ya xiaomi 12 pro ina sehemu(core) nane.

Processor hiyo ya Snapdragon 8 gen 1 imegawanyika sehemu tatu.

  • Sehemu(cores) yenye nguvu sana ipo moja
  • Core yenye nguvu ya wastani zipo tatu
  • Core yenye nguvu ndogo zipo  nne

snapdragon structure

Core yenye nguvu zaidi inatumia muundo wa Cortex X2.

Cortex X2 ni muundo ulioboreshwa huku ukifanya kazi kubwa kwa matumizi madogo ya umeme.

Core zenye nguvu ya wastani zinatumia Cortex-A710.

Cortex-A710 ni muundo wenye nguvu sana ukilinganisha na muundo wa Cortex 78 kushuka chini.

Wakati core zenye nguvu ndogo zimeundwa na Cortex A510 ambao umeongezewa uwezo wa utendaji.

Network

Processor ya snapdragon 8 gen 1 ina modem inayokubali mtandao wa 5G.

Na 4g pia inafanya kazi karibu kila nchi.

Simu ina network bands za 4G 24.

Kwa Tanzania inakubali 4G ya mitandao yote(Vodacom, Tigo, Halotel, TTCL, Smile, Zantel, Airtel).

Aina ya 4G iliyomo kwenye Xiaomi 12 Pro ni LTE Cat. 24

4G ya LTE Cat 24 inaweza kudownload file kwa spidi zaidi ya 1400Mbps

Spidi ya 1400Mbps inadowload faili la ukubwa wa 1020MB kwa sekunde sita.

Hakuna mtandao wa simu Tanzania wenye kasi hiyo.

Pia simu inasapoti aina zote za mtandao wa 5G.

Inasapoti  bands kumi na tano za mtandao wa 5G

Ila Tanzania hakuna mtandao wa 5G kwa mitandao yote ya simu.

Display(kioo) cha Xiaomi 12 Pro?

Kioo cha Xiaomi 12 Pro ni cha amoled.

Vioo vya Amoled vina utajiri wa rangi.

Wingi wa rangi unasababisha vitu kuonekana kwa rangi zake halisi ukilinganisha vioo vya IPS LCD.

Moja ya kitu kizuri kilichopo kwenye kioo ni HDR10+ na refresh rate kubwa ya 120Hz.

Uangavu wa kioo unafikia kiwango cha 1500 nits.

Nits 1500 zinafanya kioo kuonesha kiufanisi simu ikitumika juani

Kioo chake kina resolution kubwa ya 1440 x 3200 pixels

Ubora na ufanisi wa kioo katika kuonyesha vitu unakuwa mkubwa endapo resolution ni kubwa.

Resolution ndogo hazionyeshi vitu vizuri na kwa usahihi

HDR10+ na Refresh rate ni nini?

HDR10+ ni teknolojia inayotumika kwenye display kuboresha muonekano wa vitu kwa kuzingatia utofauti wa rangi.

muonekano wa picha ya hdr10+

Kwa mfano picha inaigwa kwenye mwanga mdogo giza hutawala na vitu kutoonekana vizuri.

Lakini HDR10+ inabalansi mwanga na kuonyesha kwa usahihi vitu vilivyopigwa picha.

Refresh rate inaboresha spidi ya screen katika uonyeshaji wa vitu.

Refresh rate kubwa inafanya simu kuwa nyepesi unapotachi.

Ubora wa kamera

Simu ya xioami 12 Pro ina kamera tatu zenye resolution ya 50MP.

Kamera zake ni nzuri kwa kuzingatia ubora wa picha zilizopigwa mchana na usiku na gsmarena.

Uzuri mwingine wa kamera ni kutumia teknolojia ya Dual Pixel PDAF kwa ajili ya ulengaji

Lakini pia kamera moja imewekewa OIS ambayo hutuliza mitikisiko pale anayerekodi video akiwa anatembea.

Aina za kamera za xiomi 12 pro

Xiaomi 12 pro ina aina tatu za kamera.

Kuna aina moja ya kamera inakosekana amabayo ni macro.

Kamera zilizopo ni.

  1. Telephoto
  2. Wide
  3. Ultrawide

Kamera ya Telephoto imebobea kwenye upigaji wa picha kwa vitu ambavyo vipo mbali sana na kamera.

Kamera ya Wide imebobea kwenye upigaji eneo pana

Kamera ya Ultrawide imebobea kupiga picha eneo pana kwa nyuzi kubwa.

Kamera ya ultrawide ya Xiaomi 12 Pro inaweza kupiga picha kwa upana wa nyuzi 120

Uwanja mkubwa kama wa Taifa unaweza onekana wote.

Ubora wa video

Kamera ya Xiaomi 12 Pro inarekodi aina nyingi za video.

Kamera zote zinarekodi video za 4K na 8k

Video za 4K na 8K zina resolution kubwa zinazofanya video kuonekana kwa uzuri

Na kingine hurekodi video ya 8K kwa spidi ya 24fps na kwa ubora wa HDR.

Spidi kubwa ya kurekodi inapatikana pale kamera ikiwa inarekodi video za 4k na Full HD.

4K zinarekodiwa kwa spidi ya 30fps na 60fps.

Na video za Full HD zinarekodiwa kwa spidi ya 30fps mpaka 960fps.

Pitia hii link inayolezea maana ya fps kiundani.

Tazama video chini kuona umuhimu wa fps kubwa.

Upande wa Software upoje?

Simu ya Xiaomi 12 Pro inatumia toleo jipya la Android yaani Android 12.

Na pia simu inatumia mfumo mpya wa Xiaomi unaoitwa MIUI 13.

Simu ya android 12 ina vitu vipya ambayo havipo kwenye Android 11 na android nyingine za nyuma.

Moja ya kitu kipya ni uwezo wa simu kufungua app kabla ya kumalizika kudownload.

Android 12 inaweza kukuonyesha applikesheni zinazotumia mic na kamera.

Hili linasaidia kuzigundua app ambazo zinakutrak.

Google wanasema Android 12 ina vitu vipya ambavyo vinawasaidia wenye muono hafifu kutumia simu kwa urahisi.

Uimara wa bodi ya simu?

Bodi ya Xiaomi 12 Pro imeundwa kwa glasi upande wa mbele na nyuma.

Upande wa mbele ni kioo cha Gorilla Glass Victus

Gorilla Glass Victus ni kioo kigumu kupasuka.

Majaribio ya Kampuni ya corning yameonyesha ugumu wa kioo kupasuka inapoanguka kwa kimo cha mita mbili.

Changamoto ni simu kutokuwa na viwango vya IP68.

Hivyo simu haina ulinzi wa kuzuia maji kupenya.

Simu ina urefu wa inchi 6.73 na inafiti kwenye kiganja kwa sehemu kubwa

Uwezo wa Betri na Chaji?

Xiaomi 12 Pro iantumia betri aina ya Li-Po la ukubwa wa 4600mAh.

Hii betri ni kubwa inayokaa na cheji muda mrefu.

Chaji yake inashangaza na inapeleka umeme mwingi wa wati 120.

picha inayofafanunua sifa za chaji yasimu ya xiaomi 12 pro

Umeme wa wati 120 unajaza betri ya xiaomi 12 pro kwa dakika 18 tu.

Simu teknolojia ya reverse charging.

Kwa maana inaweza kuchaji simu nyingine.

Bei ya Xiaomi 12 Pro?

Bei ya xiaomi 12 Pro inaanzia 1,500,000/=

Ila kwa Tanzania bei inaweza zidi 1,600,000/= hata ukiagiza aliexpress.

Usitegemee bei nafuu kwa maduka ya kariakoo.

Hii ni simu ya bei nafuu kwa kutazama sifa.

Kwa nini xiaomi 12 pro ni bei nafuu

Simu nyingi zinazotumia chipset ya Snapdragon 8 gen 1 zinauzwa zaidi ya 1,600,000/=

Kwa mfano Samsung galaxy S22 ultra inauzwa zaidi ya 2,000,000/=

Simu ya Oppo Find X5 Pro bei yake inafikia 3,000,000/=

Simu ya OnePlus 10 Pro inauzwa kwa zaidi ya 1,900,000/=

Kwa nini?

Ni processor yenye nguvu kwa sasa.

Processor ikiwa bora basi simu inakuwa nzuri tu.

Hivyo simu ya xioami 12 pro inayotumia Snapdragon 8 gen 1 kuuzwa bei ya milion 1.6 kunaifanya kuwa simu ya bei nafuu upande simu za tabaka la juu.

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

xiaomi 14 ultra

Simu 13 mpya na kali za Redmi na Xiaomi 2024

Kampuni ya Xiaomi sio ngeni kwa wengi Ni kampuni ya china inayotengeneza simu za madaraja yote kwa brandi za Xiaomi, Redmi na Poco Hapa kuna orodha ya simu mpya za […]

No Featured Image

Bei ya Redmi Note 13 na Sifa Zake Muhimu

Redmi Note 13 5G ni simu kutoka Xiaomi ya China ambayo bei yake kwa sasa ni shilingi laki nane Hii ni bei ya toleo lenye ukubwa wa GB 256 na […]

redmi 10a thumbnail

Bei ya Sasa ya Redmi 10A na Sifa Muhimu

Simu ya Redmi 10A iliiingia sokoni mwaka 2022 Ni aina ya simu inayolenga watu wenye matumizi ya kawaida kama sio machache Hivyo bei ya Redmi 10A ni chini ya laki […]

Jinsi ya Kutumia GPS kwenye Simu (Hatua kwa Hatua)

GPS kirefu chake ni Global Positioning System, ni mfumo wa utambuzi wa maeneo ambao unasimamiwa na Marekani Simujanja karibu zote zina huu mfumo Una faida kubwa sana hasa kama unajua […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram