SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Simu 15 za OnePlus na Bei zake (Aina zote)

Brand

Sihaba Mikole

March 9, 2024

OnePlus inaweza ikawa ni jina geni kwa watumiaji wengi smartphone Tanzania

Ila OnePlus ni moja ya kampuni kutoka china inayotengeneza simujanja za madaraja ya kati na ya juu

Simu nyingi za OnePlus ni nzuri ni matoleo ya daraja la juu hushindana na simu za samsung na iphone

Hapa kuna orodha ya simu 20 za OnePlus na bei zake kwa mwaka 2024

1. OnePlus Nord N30 SE

Bei ya OnePlus Nord N30 SE: 450,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM:  4GB

Simu ya OnePlus Nord N30 SE iliingia sokoni mwezi januari 2024

Inatumia chip yenye nguvu ya wastan, processor hiyo ni Mediatek Dimensity 6020

Ni simu ya kamera mbili ambapo kamera kubwa ina megapixel 50 na picha zake ni nzuri kwa kiasi fulani

Hii simu inasapoti chaji inayopeleka umeme wa wati 33

Hivyo betri yake ya 5000mAh inawahi kujaa kwa dakika chache

2. OnePlus 12R

Bei ya OnePlus 12R: 1,500,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM:  8GB

OnePlus 12R ina kioo cha Amoled ambavyo huwa vina utajiri wa rangi

Betri yake ina ukubwa wa 5000mAh na chaji yake inapeleka umeme mwingi wa wati 100

OnePlus 12R

Kiwastani ndani ya nusu saa simu inaweza kujaa kwa 100%

Moja ya kamera yake inatumia teknolojia ya Laser AF kwenye ulengaji

Hii inasaidia kamera kutambua vizuri kitu kinachopigwa picha kikiwa hata kwenye mwanga mdogo

3. OnePlus 12

Bei ya OnePlus 12: 2,500,000/= ,Ukubwa wa Memori: 512GB, RAM:  16GB

Simu ya OnePlus 12 ni toleo ambalo lilitoka mwezi desemba 2023

Ina ubora mkubwa kwenye kila idara kiasi cha kuwa na sifa nyingi zinazoendana na Samsung Galaxy S24 Ultra

OnePlus 12

Utendaji wa OnePlus ni mkubwa kwa sababu inatumia processor yenye nguvu ya Snapdragon 8 Gen 3

Kioo chake cha LPTO AMOLED kinaongezewa ubora na teknolojia ya HDR10+

Pia betri yake kubwa ina mAh 5400 na chaji yake ina kasi pia kwa maana ina wati 100

4. OnePlus Ace 3

Bei ya OnePlus Ace 3: 900,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM:  12GB

Simu ya OnePlus Ace 3 ilianza kuuzwa rasmi mwezi wa kwanza 2024

Utendaji wake ni mkubwa kwa ina chip ya Snapdragon 8 Gen 2

Na yenyewe inakuja na betri kubwa ya kukaa na chaji masaa mengi

OnePlus Ace 3

Betri yake ina ujazo wa 5500mAh na haitoshi kuwa chaji inasapoti wati 100

Ina kamera tatu na kamera kuu ina OIS

OIS inasaidia kutuliza kamera ukiwa unarekodi video huku ukiwa unatembea

5. OnePlus Open

Bei ya OnePlus Open: 3,800,000/= ,Ukubwa wa Memori: 512GB, RAM:  16GB

OnePlus Open ni simu ya kufunika na kufunua

Pia upande wa nje una kioo na ukifunua pia kuna vioo kushoto mpaka kulia

Utengeneza wa simu wa aina unachangia simu kuwa na gharama kubwa

OnePlus Open

Ukizingatia OnePlus Open inatumia kioo cha amoled chenye teknoljia ya Dolby Vision

Betri yake inatosheleza kukaa na chaji muda japo ni 4800mAh

Na chaji yake inapeleka umeme wa wati 67

6. OnePlus Pad Go

Bei ya OnePlus Pad Go: 700,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM:  8GB

OnePlus Pad Go ni kishikwambi ambacho kina upana wa inchi 11.35

Hiki ni kipana zaidi ya vishikwambi walivyopatiwa walimu hapa Tanzania

Kioo chake ni cha aina IPS LCD chenye refresh rate ya 90Hz

OnePlus Pad Go

Ina bonge la betri ambayo ni 8000mAh

Hivyo kukaa na moto muda mrefu ni swala la kawaida

Ila kamera yake sio nzuri na ina kamera moja pekee

7. OnePlus Ace 2 Pro

Bei ya OnePlus Ace 2 Pro: 1,100,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM:  12GB

OnePlus Ace 2 Pro ni simu ya mwaka 2023 na yenye utendaji wa kuridhisha

Kama ilivyo ada kioo chake ni cha AmOLED chenye rangi 1 Bilioni

Betri yake ina ukubwa wa 5000mAh

OnePlus Ace 2 Pro

Moja ya kitu cha kustaajabisha ni kasi yake kubwa ya kuchaji

Hii simu chaji yake inapeleka umeme wa wati 150

Simu inaweza kujaa ndani ya dakika 15

8. OnePlus Nord CE3

Bei ya OnePlus Nord CE3: 800,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM:  8GB

Simu ya OnePlus Nord CE3  ni simu ya daraja la kati yenye sifa nyingi nzuri

Ina macho matatu na kamera kuu ina megapixel 50

OnePlus Nord CE3

Na inaweza kurekodi video za 4K

Utendaji wake ni wa wastani kutokana na kutumia chip yenye nguvu za wastani

Chip hiyo ni Snapdragon 782G

9. OnePlus Nord 3

Bei ya OnePlus Nord 3: 1,10,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM:  8GB

OnePlus Nord 3 inatumia chip yenye nguvu katika utendaji wake ambayo ni Mediatek Dimensity 9000

Inatumia kioo cha Amoled chenye HDR10+ na refresh rate ya 120Hz

OnePlus Nord 3

Hii simu itakupa faida ya kuchaji simu kwa haraka kwani chaji yake inapeleka umeme wa wati 80

Kamera yake kuu viwango vyake ni vikubwa kwa kutazama teknolojia ilizoambatana nazo

Kwa kifupi kamera yake inaweza kurekodi video za 4K

10. OnePlus Nord CE 3 Lite

Bei ya OnePlus Nord CE 3 Lite: 680,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM:  8GB

Simu ya OnePlus Nord CE 3 Lite ni simu ya daraja la kati iliyotoka mwanzoni mwa mwaka 2023

Inatumia processor yenye nguvu ya wastani kiutendaji, chip hiyo ni Snapdragon 695 5G

OnePlus Nord CE 3 Lite

Tukija kwenye swala la betri na yenyewe ina 5000mAh

Kamera zake zipo tatu ila kamera kuu ndio nzuri kwa kiasi fulani japo sio kama OnePlus Nord 3

Kama ilivyo kwa OnePlus zingine na hii chaji yake ina kasi ya wati 67

11. OnePlus Ace 2V

Bei ya OnePlus Ace 2V: 900,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM:  12GB

Simu ya OnePlus Ace 2V inatumia processor ya Mediatek Dimensity 9000

Pamoja na kwamba hii simu imetoka mwaka 2023 mwanzoni kabisa ila ni simu inayofaa hata kwa mwaka 2024

OnePlus Ace 2V

Na yenyewe ni simu ya macho matatu kwa maana ina kamera ya wide, ultrawide na macro

Kamera kubwa zaidi ina megapixel 108

Betri na chaji ina viwango vya kuridhisha maana betri ni 5000mAh na chaji ni 80W

12. OnePlus Pad

Bei ya OnePlus Pad: 1,500,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM:  12GB

OnePlus Pad imetoka mwaka 2023 mnamo mwezi April

Hii ni kishikwambi chenye sifa nyingi nzuri kwenye kila idara

OnePlus Pad

Mfano kioo chake ni IPS LCD ambacho kina HDR10+, Dolby Vision na refesh rate kubwa ya 144Hz

Yaani kwa mpenzi wa magemu ataburudika sana na muonekano mzuri wa picha za gemu

Ikizingatiwa utendaji wake ni wenye nguvu kwani inatumia chip ya Mediatek Dimensity 9000

13. OnePlus 11R

Bei ya OnePlus 11R: 1,200,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM:  8GB

OnePlus 11R ina mwaka mmoja sasa tangu ilipotoka rasmi mwenzi februari 2024

Hata hivyo sifa zake upande wa kamera, chaji, kioo na betri inaipa simu kuendelea kuwa ni simu bora pia kwa mwaka huu

OnePlus 11R

Chaji yake inapeleka umeme wa wati 100

Na kioo cha OnePlus 11R ni cha amoled chenye HDR10+ na refresh rate ya 120Hz, ni kubwa sana

Kamera yake moja wapo ina ulengaji wa multi-direction pdaf

14. OnePlus Ace 2

Bei ya OnePlus Ace 2: 1,100,000/= ,Ukubwa wa Memori: 256GB, RAM:  12GB

OnePlus Ace 2 ilitoka mwezi februari mwakwa 2023

Inatumia processor yenye nguvu ya Snapdragon 8+ Gen 1

OnePlus Ace 2

Kioo chake ni cha Amoled chenye HDR10+

Kasi ya chaji yake ni 100W na betri ina ukubwa 5000mAh

15. OnePlus 11

Bei ya OnePlus 11: 1,800,000/= ,Ukubwa wa Memori: 128GB, RAM:  8GB

OnePlus 11 ni simu nyingine ya mwaka 2023 iliyo na ubora kwenye idara nyingi

Kioo chake ni cha amoled

Na ina kamera tatu ambazo zote ni nzuri

Chaji ya oneplus 11 ina kasi wati 80

Hivyo betri yake ya 5000mAh inawahi kujaa kwa haraka

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

simu mpya

Simu mpya kali 20 na bei zake kwa mwaka 2024

Hii ni orodha ya simu mpya ambazo zimetoka mwaka 2024 ama mwishoni mwa mwaka 2023 kutoka kwa kampuni zipatazo 11 Ni orodha inayohusisha simu za daraja la kati na la […]

No Featured Image

Bei ya Simu mpya ya Sony Xperia 1 V na Sifa Zake

Sony, kampuni ya japan imeachia toleo lingine jipya la xperia mwezi julai 2023 Toleo hilo ni Sony Xperia 1 IV ambalo ni la daraja la juu kwenye makundi ya simu […]

Jinsi ya Kutumia GPS kwenye Simu (Hatua kwa Hatua)

GPS kirefu chake ni Global Positioning System, ni mfumo wa utambuzi wa maeneo ambao unasimamiwa na Marekani Simujanja karibu zote zina huu mfumo Una faida kubwa sana hasa kama unajua […]

tecno spark 10c thumbnail2

Bei ya Tecno Spark 10C na Sifa Muhimu

Tecno Spark 10C ni toleo jipya la tecno kwa mwaka 2023 Spark 10C ina tofauti ndogo sana na simu ya Tecno Spark 10 Na tofauti yao ipo kwenye camera na […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram