Simu ya Nokia C30 ni simu nzuri ya bei nafuu iliyotoka mwaka 2021.
Kiubora, simu haina ubora wa viwango vya iPhone 13 Pro Max au Galaxy C30
Lakini kwa kuangalia bei yake na sifa zake zinaifanya kuwa simu yenye ubora wa kati.
Baadhi ya vitu vina ubora mdogo na mengine yanavutia unaposoma sifa za nokia c30
Sifa za Simu ya Nokia C30
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD |
Softawre |
|
Memori | eMMC 5.1, 32GB, 64GB na RAM 3GB,2GB |
Kamera | Kamera mbili
|
Muundo | Urefu-6.82inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 253,691.32/= |
Upi ubora wa Nokia C30
Simu hii ya Nokia ina betri kubwa.
Betri yake inaisadia simu kukaaa na chaji muda mrefu
Aina ya hardware za simu zinatumia umeme mdogo.
Simu ni ndefu.
Urefu unaokuonyesha vitu kwa ukubwa kwenye screen
Network
Nokia c30 inakubali mtandao wa 4G
Aina ya 4G iliyopo kwenye simu ni LTE Cat 7
LTE Cat 4 spidi yake ya kudownload inaweza kufikia 301Mbps
Ni spidi inayoweza kudownload file la ukubwa wa 1300MB kwa sekunde 40 inategemea na spidi ya mtandao husika
Simu ina network bands 10 tu za 4G.
Mitandao ya simu Tanzania yote itakubali kwenye simu hii
Ubora wa kioo cha Nokia C30
Kioo cha nokia c30 ni aina ya IPS LCD
Kiubora IPS LCD inazidiwa na vioo vya amoled unapozungumzia utajiri wa rangi
Resolution ya simu ni ya kawaida isiyoendana na viwango vya sasa
Kwani ina ukubwa wa 720×1600 pixels
Kioo kina nits chache na refresh rate ndogo
Refresh na resolution ndogo zinatumia umeme mdogo
Nguvu ya processor Unisoc SC9863A
Kila kazi inayofanyika kwenye simu ya Nokia C30 inachakatwa na processor ya Unisoc SC983A
Processor ya Unisoc SC983A ina core nane(octacore)
Hizo sehemu nane zimegawanyika mara mbili.
Kuna core kwa ajili ya kazi kubwa
Na core kwa ajili ya kazi ndogo
Uwezo wa Core kubwa
Core kubwa zipo nne
Kila core ina spidi ya 1.6GHz
Core zote zimeundwa kwa muundo wa Cortex 55
Processoe zenye nguvu hutumia cortex 55 kwenye core ndogo.
Hii inamaanisha Unisoc SC983A ni procesor yenye nguvu ndogo
Hata kwenye geekbench ina alama ndogo.
Kiuhalisia si chip nzuri kucheza gemu
Uwezo wa Core ndogo
Core ndogo zipo nne na zina muundo wa cortex a55
Huu ni muundo sawa na ule wa core kubwa.
Kinachotautiana ni spidi.
Core ndogo zina spidi ya 1.2GHz
Spidi ni ndogo zaidi
Uwezo wa betri na chaji
Nokia C30 ina betri aina ya Li-Po yenye ukubwa wa 6000mAh
Betri hili litakaa na chaji kwa masaa mengi.
Kitu kimoja wapo kinachokula chaji kwenye simu huwa ni processor
Processor ikiwa na nguvu ndogo basi matumizi ya umeme hupungua pakubwa
Lakini ubora wa simu pia huwa mdogo.
Nokia C30 haina fast chaji.
Kwa hiyo betri lake litajaa kwa muda mrefu
Ukubwa na aina ya memori
Nokia c30 inatumia memori aina ya eMMCÂ 5.1.
eMMCÂ 5.1 ina spidi ya taratibu katika usafirishaji wa data ukilinganisha na memori UFS
Hivyo basi baadhi ya app zitafunguka taratibu.
Na simu kuchelewa kuwaka
Kuna aina tatu za nokia c30 upande wa memori
- 32GB 2GB RAM
- 32GB 3GB RAM
- 64GB 3GB RAM
Ni ukubwa kwa kiasi unaohifadhi mafaili mengi
Uimara wa bodi ya Nokia C30
Bodi ya hii simu ya nokia imeudwa kwa plastiki upande wa nyuma na kwenye fremu
Na ina ulinzi wa kioo kwenye screen.
Lakini sio kioo cha gorilla
Bodi za plastiki si imara pale simu inapoanguka.
Mtumiaji analazimika kununua kava kuilinda simu bila kusahau screen protector.
Umakini unahitajika wakati wa kununua screen protector.
Wafanya biashara wengi Tanzania wanauza screen protector nyepesi kupasuka
Ubora wa kamera
Kuna kamera mbili tu upande wa nyuma.
Kamera aina ya depth na wide.
Kamera zote hazitumii teknolojia nzuri za kamera aina ya dual pixel pdaf
Kumbuka kamera ya depth haipingi picha
Bali hupima umbali kati ya kamera na kitu kinachpigwa picha ili kamera ilenge kwa usahihi
Ubora wa video
Simu inaweza kurekodi aina moja tu ya video zenye ubora wa full hd.
Video za full hd zinarekodiwa kwa spidi ya 30fps
Ni spidi ndogo ukilinganisha na uwezo wa kamera ya simu ya iPhone SE 2022
Ubora wa Software
Nokia c30 ni simu ya android 11 inayotumia android aina ya Go Edition
Anadroid Go Edition ni mfumo endeshi wa android uliotengenezwa kwa ajili ya simu zenye nguvu ndogo kiutendaji.
Ni mfumo unaolenga simu zenye RAM ndogo chini ya 2GB.
Ni mfumo unaotumia data kidogo ya data.
Simu hii isingeweza kuhimili aina zingine za android kutokana na uwezo mdogo iliyo nayo.
Bei ya Nokia C30 Tanzania
Bei ya nokia c30 kwenye masoko ya dunia inauzwa shilingi 254,000/= za Tanzania.
Baadhi ya maduka ya kariakoo wanauzaa hii simu kwa bei 300,000/= mpaka 350,000/=
Sio simu mbaya ila kwa bei yake unapata simu nzuri inayoizidi hii.
Tazama hapa: Simu za bei rahisi
Yapi Madhaifu ya Nokia C30
Simu ina nguvu ndogo ya kiutendaji kwa sababu ya processor ndogo
Nokia hii haina kamera ya telephoto na ultrawide.
Nokia c30 haiwezi kurekodi video za 4K
Simu inakosa fast chaji hivyo betri inachukua muda kujaa
Bodi yake imeundwa kwa plastiki ambazo zina kawaida ya kuwahi kuchunika.
Mtumiaji wa hii simu atalazimika kununua screen protector kutokana na simu kutokutumia vioo vya gorilla
Neno la Mwisho
Kwa mtu mwenye bajeti ndogo ya simu basi nokia c30 inaweza msaidia kusukuma siku.
Lakini kama unazingatia utendaji hii ni simu ya kuachana nayo.
Kwa wapenzi wa screen kubwa nokia c30 itakidhi hitaji lako
Kiujumla simu ya c30 inamfaa mtu anayeanza kutumia smartphone