Tecno Spark 10 ni toleo lingine jipya inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi april ya mwaka 2023
Ni toleo linalotoka pamoja na toleo zuri kiasi la Tecno Spark 10 Pro
Bei ya Tecno Spark 10 inazidi laki nne kwa Tanzania
Ni simu ya kawaida yenye vipengele vichache vya kuvutia
Vipengele ambavyo vinaweza kukuvutia kununua hii simu
Bei ya Tecno Spark 10 ya GB 128
Tecno ya ukubwa huu inauzwa kwa kiasi cha shilingi 350,000/= kwa maduka mengi Tanzania
Ukubwa wa memori na bei yake inamaanisha ni simu ya bei nafuu
Maana simu nyingi zenye GB 128 huuzwa kwa zaidi ya laki nne
Japo bei kubwa husababishwa na sifa zingine nzuri za ziada zinazoweza kukosekana kwenye tekno hii
Fuatilia sifa zake uelewe kiundani kuhusu spark 10
Sifa za Tecno Spark 10
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | 128GB, na RAM 8GB |
Kamera | Kamera MBILI
|
Muundo | Urefu-6.6inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 350,000/= |
Upi ubora wa simu ya Tecno Spark 10
Simu ina betri kubwa hivyo kuna uhakika wa kuitumia muda mrefu
Kioo chake kina refresh rate kubwa
Inakuja na RAM kubwa na memori ya kutosheleza kiasi
Spark 10 inatumia toleo jipya la android 13 kama ilivyo kwa simu ya samsung galaxy 23 plus
Vitu vingine ni vya kawaida sana ukizingatia ni simu ya bei ndogo
Uwezo wa Network
Hii simu ina uwezo wa kutumia mtandao wa 4G na 3G bila kusahau 2G
Haina teknoljia mpya ya 5G
Kutokana na kutoainishwa na aina ya processor simu inayotumia, ni ngumu kuelezea kasi ya kiwango cha juu ya 4G YAKE
Kwa maana si rahisi kufahamu aina ya LTE kama hujui chip iliyomo ndani ya simu
Kikubwa ni kuwa utaweza kutumia intaneti ya 4G ya mtandao wowote kwa sababu simu ina masafa yanayotumika na mitandao ya simu hapa Tanzania
Ubora wa kioo cha Tecno Spark 10
Tecno Spark 10 ina kioo cha kawaida aina IPS LCD
Hivyo simu ikipasuka bei ya kioo haitokugharimu sana
Ila ubora wa vioo vya IPS LCD sio mkubwa katika uonyeshaji wa rangi ukilinganisha na vioo vya AMOLED kama kilichopo kwenye simu ya Samsung Galaxy A54
Ukizingatia resolution ya kioo cha tecno spark 10 ni ndogo ambayo ni 720 x 1612 pixels
Ila spark 10 ina refresh rate inayofika mpaka 90Hz
Video chini inaonyesha utofauti wa refresh rate ya 60Hz, 90Hz na 120Hz
https://www.youtube.com/watch?v=IW8VWZJOGEE
Hii inamaanisha simu inakuwa fasta wakati wa kutachi, na mnato(animation) za kuvutia
Na refresh rate kubwa huwa inasaidia sana magemu kuchezeka vizuri
Vitu vingine vinavyopendezesha kioo simu haina
Nguvu ya processor
Tecno hawajaainisha chip simu inayotumia hata ukitembelea kurasa rasmi.
Ila sifa zilizoorodheshwa kwenye jedwari zinaonyesha wazi kuwa simu ina processor yenye nguvu ndogo
Hasa ukiangalia kiasi cha resolution kilichopo kwenye kioo
Mara nyingi kampuni za simu huweka resolution kubwa iwapo chip ikiwa na nguvu ya kutosha
Kivyovyote vile, spark 10 ni simu inayomlenga mtumiaji mwenye matumizi ya kawaida, anayependa simu inayokaa na chaji muda mrefu
Uwezo wa betri na chaji
Hii simu inakuja na betri ya ukubwa wa 5000mAh
Ukubwa huu wa betri simu inaweza kukaa na chaji kwa zaidi ya masaa 12 ikiwa kwenye intaneti
Ikizingatiwa inatumia kioo cha kawaida ambacho kinatumia umeme kidogo
Chaji yake ina kasi ya wastani ambayo ni wati 18
Ni spidi inayoweza kufanya betri kujaa kwa muda mrefu
Ukubwa na aina ya memori
Tecno spark 10 ipo ya aina moja tu upande wa memori
Memori yake ina ukubwa wa 128GB na RAM GB 8
Ni kiasi kinachoweza kutosheleza kuhifadhi mafaili mengi
Hata kama simu imejaa utaweza kuongeza memori kwa kuweka memori kadi
Ni tofauti na simu za siku hizi nyingi kama iPhone 14 Pro Max ambazo huondoa sehemu ya memori kadi
Uimara wa bodi ya Tecno Spark 10
Upande wa nyuma simu imewekewa kioo lakini sio cha gorilla
Kioo kinasaidia gamba ;a nyuma kutochunika kwa urahisi tofauti na simu zenye plastiki
Kwa mbele haina screen protekta ya kioo
Kiusalama zaidi itakulazimu kununua kava ya na pia protekta
Urefu wa simu ni inchi 6.6, kwa wapenda simu ndefu hili pia ni chagua sahihi
Ubora wa kamera
Mfumo wa kamera wa Tecno Spark 10 sio wa kuvutia sana
Fuatilia: simu zenye kamera nzuri za bei ndogo, uone utofauti
Ukianza upande wa kamera za nyuma kuna kamera mbili pekee
Kamera moja kubwa ina megapixel 50 na inatumia ulengaji wa PDAF
PDAF huwa inaifanya simu itambue na kukilenga kitu kinachopigwa picha kutokana na muelekeo wa kamera
Kasi yake si kubwa kama zile zenye dual pixel pdaf hasa kwa vitu vinavyotembea
Kamera ya pili haijulikani ina lenzi ya aina gani, ni ngumu kuielezea
Upande wa selfie(kamera ya mbele) ipo moja tu yenye megapixel 8
megapixel 8 sio mbaya lakini hii kamera haina PDAF
Kamera zake zinarekodi video za full hd pekee yake na hakuna OIS
Hivyo kama unarekodi huku ukiwa unatembea utahitajika kutuliza mkono
Ubora wa Software
Simu inakuja na Android 13 ikiwa inatumia mfumo wa HiOS 12 kutoka tecno
HiOS 12 inatoa uwezo wa kuongeza kiwango cha RAM ya simu
Mfumo wa android huwa unahitaji kiwango kikubwa cha RAM
Na pia kuna apps zinakula memori kubwa ya ram unapozifungua
RAM ya GB 8 ni kubwa ila unapokuwa na apps nyingi zinazohitaji memori kubwa zinasababisha memori kujaa
Kujaa kwa memori kunaweza kupunguza utendaji wa simu na mwishowe ukajikuta simu inakuwa nzito
Hivyo kuongeza ram kunasaidia kiasi
Yapi Madhaifu ya Tecno Spark 10
Tecno Spark 10 simu ya daraja la chini hivyo changamoto ni nyingi ikitegemeana na aina ya matumizi
Mfumo wa kamera sio mzuri kiujumla
Chaji yake haipeleke kwa kasi kubwa na kwa viwango vya kisasa
Kasi ya chaji ya simu za siku hizi ni wati 25
Kioo inatumia teknolojia ya IPS LCD huku ikiwa na resolution ndogo
Simu haina teknolojia mpya ya mawasiliano ya 5G ikizingatiwa baadhi ya mitandao wameanza kuweka 5G nchini
Neno la Mwisho
Tecno Spark 10 ni tecno ya bei ndogo yenye baadhi ya sifa nzuri
Kwa mtumiaji anaepedna simu inayokaaa na chaji tu na kioo chenye uitikaji wa haraka, hili ni chaguo sahihi
Iwapo sifa zilizopo kwenye hii simu hazijakuvutia utalazimika kutafuta mbadala
Na mbadala maana yake itakulazimu kuongeza bajeti ya simu kwa sababu kitu bora huwa kinahitaji bajeti ya uhakika
Maoni 26 kuhusu “Bei ya Tecno Spark 10 na Sifa Zake”
Inauzwa bei gani
Hii bei yake rasmi haijawekwa wazi kwa hapa TZ kwa sasa
Mahitaji cm tekno spak 10
Sikilizia kama wiki maana bado bei bado haijaainishwa
Naitaji cm tekno spak 10
Tekno spak 10
Nahitaji Tecno spark10 inauzwa shiingp? Nipo kigoma mjini
Inauzwa bei Gani mtuambie mapema tujue tuweke bajeti mapema ili tununue hiyo simu
Maoni yangu simu ninzuri sana inakiwango kizuri Cha kukizi mahitaji yetu ya chaji na uwepesi was mtandaoni Iko vizuri
Nahitaji kujuw bei ya cm
Nahitaji kujuw bei gan
Nahitaji kujua bei rasmi maana naihitaji
Noshngap
Hii imeelezwa ni 350k
Naitajaji simu ya spark 10 lakin nipo mkoani vip inaweza nifikia???
Inawezekana
MIMI NINAITAJI SPARK 10 NA HAPA NINA SPSRK 10C SASA INAWEZEKANA KUBADILISHA
Ulizia sehemu uliyonunua kama yupo tayari
Naitaji simu Tecno spark 10 nipo sengerema inabei gani
Ni shiling laki tatu na nusu
Nahitaji
Nahitaji Tecno spark 10 128
0752324754
Kwaiyo kiujumla bei lasimi ni 350000
Ndio
Ni nzuri naipataje
Bei ya tekno spark 10 k7 pro inauzwa xhingapi naitaji kufahamu