SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Bei ya Simu ya Samsung Galaxy S9 na Sifa Zake (2022)

Brand

Sihaba Mikole

June 20, 2022

Simu ya Samsung Galaxy S9 ni simu ya daraja la kwanza ya mwaka 2018

Imepita miaka minne tangu imetoka ila ni simu inayoweza kuchuana na matoleo mapya ya simu za android

Ila bei ya Samsung Galaxy S9 haizidi laki nne kwenye maduka mengi ya kariakoo

muonekano wa samsung galaxy s9

Japokuwa haiwezi kuchuana na smartphone kama Xiaomi 12 Pro ila kuna ufanano wa baadhi ya vitu

Ifahamu xiaomi 12 pro kupitia ubora na sifa za xiaomi 12 pro

Ni vizuri ukalewa kama bei ya simu inaendana na sifa zake.

Bei ya Samsung Galaxy S9 Tanzania

Bei ya Samsung Galaxy S9 ya GB 64 na RAM ya GB ni shilingi 385,000/= kwa maduka mengi ya ilala na kariakoo

Ni bei ya galaxy s9 ambazo zimetumika

Hakuna toleo jipya kutoka kiwandani kwa sasa

Kiasi cha bei ni shindani na kinaendana na ubora wa simu kwa nyakati za sasa

Zitazame sifa zake kwenye jedwari chini uone jinsi hii simu inavyozizidi simu mpya nyingi za 2022

Sifa za Simu ya Samsung Galaxy S9

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
  • CPU – Snapdragon 845
  • Core Zenye nguvu(4) – 4×2.8 GHz Kryo 385 Gold
  • Core Za kawaida(4) – 4×1.7 GHz Kryo 385 Silver
  • GPU-Adreno 630
Display(Kioo) Super AMOLED,
Softawre
  • Android 8.0
  • One UI 2.5
Memori UFS 2.1,256GB,128GB,64GB na RAM 4GB
Kamera Kamera moja

  1. 12MP, dual pixel PDAF(wide)
Muundo Urefu-5.8inchi
Chaji na Betri
  • 3000mAh-Li-Po
  • Chaji-15W
Bei ya simu(TSH) 385,000/=

Upi ubora wa Samsung Galaxy S9?

Galaxy S9 imetengenezwa na kioo kigumu kuvunjika

Inatumia kioo chenye uangavu wa kuonyesha vitu kwa ubora

Ni simu inayoweza kuzuia maji kupenya

Inakuja na nafasi kubwa inayoweza kujaza mafaili mengi

samsung galaxy s9 summary

Ina kamera nzuri inayofanya simu kutoa picha na video nzuri

Huu ni ubora katika nyanja chache

Ukiingalia kila sifa kiundani utagundua kuwa kuna baadhi ya vitu simu ipo nyuma na wakati

Zifuatilie kuanzia uwezo wa network mpaka betri

Uwezo wa Network

Samsung S9 ina network ya 4G ikizingatiwa ni simu ya 2018

Aina ya 4G simu inayotumia ni LTE Cat 18

Network ya LTE Cat 18 ina spidi ya juu ya kudownload inayofikia 1200Mbps

Kwa maana kitu cha ukubwa wa GB 1.5 kinaweza kumalizika kudownload kwa sekunde kumi

samsung galaxy s9 network

Kwa bahati mbaya hakuna mtandao wa simu Tanzania unaotoa kasi hii

Uzuri ni kuwa simu ina masafa ya 4G yapatayo 22 yakiwemo ya mitandao ya simu nchini Tanzania

Hapa kuna ufafanuzi unaofafanua ubora wa simu kwenye network ya 4G na spidi yake

Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy S9

Kioo cha samsung galaxy s9 ni cha aina ya Super Amoled chenye resolution ya 1440 x 2960 pixels

Super Amoled huwa kina ubora mkubwa katika kuonyesha vitu kwa rangi zake halisi

Hasa rangi nyeusi

Ubora wa kioo unachagizwa na resolution yake kubwa na kuwa na HDR10

Kama hufahamu kuhusu hdr pitia, maana na umuhimu wa HDR kwenye simu

Nguvu ya processor Snapdragon 845

Processor ya simu ya Galaxy S9 ni Snapdragon 845

Kila utakachokifanya kwenye simu (kuanzia kupiga simu mpaka kucheza gemu) kinachakatwa na processor

Kama processor ina nguvu ndogo, simu inakuwa mbaya na nzito kufanya kazi kwa haraka

Lakini Snapdragon 845 ina nguvu kubwa inayoizidi hata Helio G96 iliyotumika kwenye Infinix Note 12 VIP

samsung galaxy s9 processor

Nguvu inatokana chip kuwa na core nane

Core nne zina nguvu inayokana na kutumia muundo wa Kryo 385 Gold

Kryo 385 Gold inaweza kufanya kazi tatu kwa mzunguko katika mizunguko bilioni mbili processor inayofanya kwa sekunde moja

Hii inafanya simu kuwa nyepesi wakati wa kufungua app kubwa

GPU ya Adreno 630

Kirefu cha GPU ni Graphic Processing Unit

Ni aina ya procesor inayoshughulikia na uonyeshaji wa picha (graphics) kwenye screen

GPU inawezesha simu kuonyesha picha, video, kucheza magemu nk

GPU nzuri huonyesha vitu kwa ustadi mkubwa

Adreno 630 inaweza kuonyesha na kucheza magemu kwa resolution kubwa

Kwa mfano gemu ya Call of Duty: Mobile inacheza kwa resolution kubwa na kwa kasi ya 55fps

Uwezo wa betri na chaji

Hii simu ina betri yenye ujazo mdogo

Kwani ukubwa wake ni 3000mAh

Ukubwa huu unakaa muda mdogo simu ikiwa inatumika sana

Uchambuzi wa GSMArena unaonyesha simu inatunza chaji masaa kumi kama ikiwa inatumika kwenye intaneti

Kama utaangalia video za youtube au instagram basi muda wa kukaa chaji unaweza ukawa chini

Simu nyingi mpya zinaweza kukaa na chaji masaa yanayozidi 14

Na kibaya pia chaji yake inapeleka umeme kidogo wa wati 15

Ukubwa na aina ya memori

Samsung Galaxy S9 inatumia memori aina ya UFS 2.2

UFS 2.2 inaweza kusafirisha data kwa kasi kubwa ya 1200MBps

Kitu kinachoongezea uwezo simu kufungua app kwa haraka na simu kuwaka kwa sekunde chache

Kuna matoleo matatu ya Samsung S9 upande wa memori

Unaweza ukaikuta yenye GB 64, 128 au GB 256

Ni memori zinazoweza kuhifadhi mafaili mengi

Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy S9

Upande wa mbele kwenye screen kuna kioo cha Gorilla 5

Kioo cha Gorilla 5 kinaweza kuhimili kupasuka kama simu ikianguka kwa kimo cha mita 1.2

Na upande wa nyuma simu ina kioo cha gorilla 5 pia

Na pembeni kumewekewa alumiamu

samsung galaxy s9 body

Hivyo simu inaweza isipoteze ubora wake wa rangi kwa kipindi kirefu

Ni tofauti na simu ambazo zimeundwa kwa bodi ya plastiki kama Infinix Hot 12i huwai kuchoka

Kutokana na kuchunika kwa rangi

Ubora wa kamera

Simu ina kamera moja tu inayoweza kupiga eneo la kawaida

Kamera yake ni nzuri kutokana na kutumi ulengaji(autofocus) ya dual pixel pdaf

dual pixel pdaf inatambua eneo na kitu kinachopigwa kwa haraka sana kuliko PDAF

samsung galaxy s9 kamera

Kitu kinachofanya picha iwe clear(vizuri) sana

Hata ukitazama picha ambazo Samsung S9 imezipiga nyakati za mchana na usiku utaona vitu viaonekana vizuri bila kupoteza ubora wa rangi

Zitazame baadhi ya picha ambazo kamera ya s9 imezipiga hapa

Ubora wa Software

Simu inakuja na Android toleo la 8 lakini inakubali android 10

Na imewekea mfumo wa Samsung unaofahamika One UI 2.5

samsung galaxy s9 software

One UI 2.5 inawezesha simu kuungana na tv

Na kisha screen ya simu kuonekana kama ilivyo kwenye tv inayokubali mfumo huo

Hii inafahamika kama Wireless Dex

Yapi Madhaifu ya Samsung Galaxy S9

Simu ya Samsung Galaxy S9 haiwezi kupokea toleo jipya la Android 12

Hivyo inakosa mambo mapya

Betri yake haitunzi moto kwa sababu ni dogo

Pia chaji yake inapeleka umeme unaojaza betri taratibu

Simu ni fupi na inaweza isiwavutie watu wanaopenda simu ndefu na pana

Upande wa kamera hauwezi kupiga eneo pana sana kwa sababu haina kamera ya Ultrawide

Neno la Mwisho

Bei ya Samsung Galaxy S9 inaifanya simu kuwa na bei nafuu huku ikiwa na ubora mwingi

Japokuwa hauwezi ukapata hii simu ikiwa  mpya bali ni used

Kama utakuwa sio mpenzi wa simu zilizotumika zipo simu nzuri za motorola

Maoni 21 kuhusu “Bei ya Simu ya Samsung Galaxy S9 na Sifa Zake (2022)

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

samsung a06

[VIDEO]-ubora wa picha na kiutendaji wa Samsung Galaxy A06

Hii ni video inayokupa nafasi kushuhudia sifa za ziada za samsung galaxy a06 hasa upande wa kamera Kama hujui, Galaxy A06 NI simu mpya ya daraja la chini ambayo imetoka […]

No Featured Image

Simu Mpya za Samsung 2024 (za bei rahisi na ghari)

Kuna simu zaidi ya tisa zilizotengenezwa na kampuni ya Samsung kutoka Hapa kuna orodha ya simu kumi mpya za samsung ambazo zimetoka mwishoni mwa mwaka 2023 hadi mwaka 2024 Ni […]

Bei ya Samsung Galaxy A25 na Sifa zake

Simu ya Samsung Galaxy A25 ilitoka rasmi mnamo mwezi desemba 2023 Ni simu ya daraja ambayo bei yake kwa Tanzania ni shilingi laki saba (700,000/=), hii ikiwa ni bei ya […]

samsung galaxy a15 thumbnail

Bei ya Samsung Galaxy A15 na Sifa Muhimu

Mwezi wa desemba 2023 ni mwezi ambao Simu ya Samsung Galaxy A15 ilizinduliwa Ni simu ya daraja la kati ambayo ina vitu vichache vinavyopatikana kwenye samsung za bei kubwa Ndio […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company