Simu ya infinix note 12 vip ni simu ya android ambayo imetoka mwezi juni mwaka 2022
Ni ifinix ambayo inakuja na sifa nzuri hasa upande wa chaji, kioo na betri
Kitu kinachochangia bei ya infinix note 12 kuzidi laki nane kwenye maduka ya infinix
Fuatilia, vitu vinavyofanya simu kuwa bora na bei ya gharama
Simu hii ina ufanano wa kisifa na note 12
Fuatalia mgawanyiko wa bei upande wa memori na sifa zake zote ili ujue kama simu inastahili bei hiyo
Bei ya Infinix Note 12 VIP ya GB 256
Kwenye maduka ya infinix yaliyopo Dar Es Salaam simu inauzwa kwa shilingi 820,000/=
Bei inaweza kuwa kubwa lakini simu ina sifa zinazoweza wavutia wengi
Kikawaida simu nyingi za infinix huuzwa kwa bei rahisi
Lakini note 12 vip ni tofauti na bei yake itapata wakati mgumu kushindana na simu za redmi na oppo zinazopatikana kwa bei ya laki nane
Kwa sababu kuna baadhi ya sifa za VIP haziendani na bei
Sifa za Infinix Note 12 VIP
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | AMOLED, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.2, 256GB,128GB, na RAM 8GB, 4GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.7inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 830,000/= |
Upi ubora wa simu ya Infinix Note 12 VIP
Ubora mkubwa wa infinix note 12 vip ni uwezo wake wa kujaza betri kwa dakika CHACHE
Kwani simu inachukua chini ya dakika 20 betri kujaa kwa 100%
Lakini pia ni moja ya simu yenye display yenye uwezo wa kuonyesha rangi nyingi
Note 12 VIP inakaa na chaji masaa mengi kwa sababu ya kuwa na betri kubwa
Utendaji wa simu pia ni wa kuridhisha japo si sana
Na pia ina kamera inayotoa picha vizuri
Uwezo wa Network
Infinix Note 12 VIP inasapoti mtandao wa 4G aina ya LTE Cat 13
Simu yenye LTE Cat 13 inaweza kudownload kwa spidi inayofika 390 Mbps
Ila hakuna laini ya simu yenye kasi kubwa ya namna hii hapa Tanzania
Mtandao wenye 4G yenye kasi zaidi ni Halotel
Kwa maeneo ambayo nimewahi jaribu spidi yake inaenda mpaka 75Mbps
Uzuri Note 12 VIP ina masafa ya 4G yapatayo 13 yakiwemo yanayotumika hapa Tanzania
Ubora wa kioo cha infinix note 12 vip
Kioo cha infinix note 12 vip ni aina ya AMOLED
Kioo chake kina utajiri wa rangi zinazofikia bilioni moja
Hivyo simu inaweza kuonyesha vitu vingi kwa rangi zake halisi
Ubora wa kioo chake kuonyeza vitu vizuri unachangiwa pia na kuwa na resolution ya 1080 x 2400 pixels
Kioo chake ni chepesi wakati wa kutachi na kuscroll
Kwani kina refresh rate kubwa inayofikia 120 Hz
Hivyo ukiwa unaperuzi majina au sms simu itaonyesha orodha majina kwa haraka kila unapotachi
Nguvu ya processor MediaTek Helio G96
Infinix note 12 VIP inapewa nguvu ya kiutendaji na MediaTek Helio G96
Helio G96 ni processor ya simu yenye uwezo wa wastani.
Uwezo wake wa wastani unaifanya simu kuweza kucheza magemu mengi ya simu
Japokuwa gemu zinazohitaji nguvu kubwa kama Call of duty Mobile zinacheza kwa resolution za chini
Nguvu yake ya wastani inasababishwa na Core kubwa kutumia muundo wa Cortex A76
Cortex A76 inazidiwa kiutendaji na Cortex A78 kwa asilimia kubwa
Ndio maana app ya GeekBench inaipa alama 542 wakati chip ya Dimensity 900 yenye muundo wa Cortex A78 ina alama 710
Kiuhalisia infinix wangeifanya simu kuwa nzuri zaidi kama wangetumia chip ya dimensity 900
Core sita zina nguvu ndogo na zimetumia muundo wa Cortex A55
Huu ni muundo ambao huwa unatumia umeme kidogo
Mara nyingi hutmika pale ambapo simu ikiwa inafanya kazi nyepesi kama kupiga simu
Uwezo wa betri na chaji
Katika simu ambazo zinazowahi kujaa cha kwa haraka sana Infinix Note 12 VIP ipo
Ukiwa unachaji hii infinix basi simu inajaa ndani ya dakika 17 tu tena kwa 100%
Hii inatokana na chaji yake kupeleka umeme wa wati 120
Umeme huu unafanya betri ya simu yenye ukubwa wa 5000 mAh kujaa ndani ya dakika chache
Kutokana na betri kuwa kubwa, ukaaji wa chaji unachukua masaa yanayozidi 14 simu ikiwa kwenye intaneti masaa yote mfululizo
Ukubwa na aina ya memori
Kuna matoleo ya aina mbili ya hii simu
Kuna infinix note 12 vip ya GB 128 na ya GB 256
Huu ni ukubwa unaoweza kuhifadhi applikesheni na mafaili mengi
Lakini pia simu inatumia memori aina ya UFS 2.2
Memori za UFS husafirisha data kwa kasi kubwa kitu kinachoongezea simu utendaji
Tofauti na memori za eMMC ambazo husafirisha data kwa kasi ndogo
Simu ikiwa na ufs hufungua applikesheni kwa haraka bila kuchelewa
Uimara wa bodi ya infinix note 12 vip
Bodi ya infinix note 12 vip imetengenezwa kwa glassi upande wa nyuma
Na kwenye screen kumewekewa glassi ila sio za gorilla
Glassi hasa upande wa nyuma huepusha simu kuchunika rangi pindi inapotumika miaka mingi
Ila sio kila aina ya glassi ni imara hasa kama sio gorill 5 kwenda mbele
Hivyo kuna haja ya kuongeza protector na kava ili kuipa simu ulinzi zaidi
Ubora wa kamera
Simu ina jumla ya kamera tatu
Hivyo ni infinix nyingine ya macho mamatu ya mwaka huu 2022 ikiwemo pia Infinix Hot 12
Simu ina kamera aina ya ultrawide ambayo hupiga eneo pana tu.
Na pia kamera kubwa ina megapixel 108 na ina ulengaji aina ya PDAF na Laser AF
PDAF inasaidia kamera kulenga kitu kwa usahihi na kwa haraka hivyo picha inatokea ikiwa vizuri
Japokuwa hailngi kwa ustadi mkubwa kama teknolojia ya dual pixel pdaf
Na Laser AF hutumika kulenga vitu nyakati za usiku au kwenye mwanga hafifu
Upande wa video kamera zinarekodi za full hd na full hd plus pekee
Na kwa spidi ya 30fps na 60fps
Kwa bahati mbaya simu haina teknolojia ya OIS ambayo hutuliza kamera wakati wa kurekodi huku ukiwa unatembea
Ubora wa Software
Infinix note 12 Vip inakuja na toleo la android 12
Android 12 ina vitu vipya vingi ikiwemo kuonyesha app zinazotumia kamera kila ikufunguka
Hivyo inakuongezea usalama wa kuzitambua app zinazotumia kamera bila ruksa yako
Pia VIP inaambatana na software ya XOS 10.5
Baadhi ya mazuri ya XOS 10.5 ni kukupa uwezo wa kuongeza ukubwa wa RAM
RAM kubwa inaifanya simu kuweza kufungua apps nyingi kwa wakati mmoja bila kukwama kwama
Kitu kingine kilichopo kwenye mfumo XOS 10.5 ni uwezo wa kurudisha picha ambazo umezifuta
Kama ukifuta picha kwa kipindi cha siku 30 basi mfumo wa AI Gallery utaweza kuzirudisha hizo picha
Kwa mengi kuhusu XOS 10.5 tembele, vitu vinavyopatikana kwenye xos
Yapi Madhaifu ya infinix note 12 vip
Simu haina mtandao wa 5G
Japokuwa Tanzania haina 5G lakini waziri wa habari na mawasiliano alisema wameshaanza kupokea maombi ya kuweka 5G
Kwa hiyo kuna uwezekano 5G ikaanza kutumika miaka ya karibuni nchini
Pitia hapa kufahamu Uwanzishwaji wa mtandao wa 5G Tanzania
Si sawa kwa simu mpya ya laki nane kutokuwa na teknlojia mpya ya mawasiliano kwa mwaka 2022
Pia kamera zake hazina ois
Na simu inakosa ulinzi wa kuzuia maji kupenya
Aina hii ya ulinzi hujulikana kama IP
Neno la Mwisho
Bei ya infinix note 12 VIP inaipeleka simu kuingia kwenye ushindani mkali na simu za oppo a96 na Redmi Note 11 Pro 5G
Wakati ubora wa hizo simu mbili kwenye kila idara unaiacha kwa kiasi kikubwa ubora wa note 12 vip
Ila kwa mtu anayehitaji simu inayojaa haraka na inayokaa na chaji muda mrefu, note 12 vip inafaa sana
Wazo moja kuhusu “Bei ya Simu ya Infinix Note 12 VIP na Sifa Zake Muhimu”
Changamoto yangu kwenye Haina hii ya simu haisomi 4G hata H* inaisha 3G tuu nomba msahada