Simu ya vivo y20 ni simu ya android ambayo imetoka mwaka 2020
Ni simu ambayo inaweza ikachuana na baadhi ya simu mpya za daraja la chini kama itel a58
Bei ya vivo y20 inazidi shilingi laki tatu kwa maduka mengi ya simu dar es salaam Tanzania
Lakini bei inatofautiana na ukubwa wa memori
Ukiitazama bei na sifa za simu utagundua y20 ni simu ya bei rahisi yenye bei kubwa kuliko ubora
Fuatilia posti yote kujifunza
Bei ya Vivo Y20 Tanzania
Bei ya vivo y20 yenye ukubwa wa 64GB na RAM ya 3GB ni shilingi 390,000/=
Kama unafahamu vigezo vinavyoifanya simu kuwa nzuri inaweza ikawa ngumu kukubaliana na bei yake
Kwa sababu sifa zake zinaendana na simu ya redmi 9a na infinix hot 12i
Lakini hizo simu zinaweza patikana chini ya laki tatu
Ila ina sifa za kuzifuatilia ambazo zinaweza kukuvutia kuimiliki simu bila kujali gharama zake
Sifa za simu ya Vivo Y20
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD |
Softawre |
|
Memori | eMMC 5.1,64GB, na RAM 3GB,6GB,4GB |
Kamera | Kamera tatu (vivo macho matatu)
|
Muundo | Urefu-6.51inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 390,000/= |
Upi ubora wa vivo y20
Ubora wa simu aina ya vivo y20 ni uwezo wake wa kukaa na chaji muda mrefu
Ina chaji inayopeleka umeme wa wastani
Ni simu ambayo inakubali mtandao wa 4G
Hivyo mtumiaji atapata kasi nzuri ya intaneti
Lakini kiuumla ubora kwenye nyanja zingine ni wa viwango vya chini usioendana na bei yake
Fuatilia uwezo wa y20 kwenye utendaji, processor, kioo na kasi ya kuchaji ufahamu ubora wake kiujumla
Uwezo wa Network
Vivo y20 ni simu ya 4G aina LTE Cat 13
LTE Cat 4 ni 4g ambayo spidi yake ya juu kabisa ya kudownload ni 390Mbps
Ni spidi ambayo ni ndogo ukilinganisha na simu kama samsung galaxy s21 ultra 5G
Simu inakubali intaneti ya 4g ya mitandao yote ya simu inayopatikana Tanzania
Kwa sababu ina masafa ya 4g yapatayo 14
Pitia ukura huu wenye kuelezea, masafa ya mtandao wa 4G ya mitandao ya simu Tanzania
Ubora wa kioo cha vivo y20
Kioo cha vivo y20 ni cha IPS LCD chenye resolution ya 720 x 1600 pixels
Ubora wa kioo katika uonyeshaji wa vitu kwa usahihi si mkubwa hasa kama simu haina HDR10
Na resolution ndogo ya 720p inapunguza muonekano mzuri wa vitu
Hivyo vivo y20 ina kioo chenye ubora mdogo na uangavu ambao sio mkubwa
Hivyo ukiwa unaitumia simu juani inaweza kukupa shida kuona vitu vizuri kwenye screen
Nguvu ya processor Snapdragon 460
Vivo y20 inatumia processor ya snapdragon 460 katika kufanya kazi zote ambazo mtumiaji wa simu anazifanya
Snapdragon 460 ina jumla ya core zipatazo nane (octa core) lakini ina nguvu ndogo
Utendaji wake hauwezi kucheza gemu kubwa kwa urahisi
Simu inaweza ikawa inapata joto sana hivyo simu italazimika kucheza gemu kwa ubora wa chini
Hii inasababishwa na processor kutumia muundo wa Kryo 260 silver
Kryo 260 silver inafanana na Cortex A53 ambayo huwa na mizunguko michache ya kuchakata data
Processor ina core 4 zeneye spidi ya 1.8 na core nne zingine zina spidi
Uwezo wa betri na chaji
Vivo y23 ni moja ya simu ambayo inaweza kukaa na chaji masaa yanayozidi 14 simu ikiwa kwenye intaneti muda
Kwa sababu simu ina betri lenye ujazo mkuwa wa 5000mAh
Simu nyingi ambazo betri zake ni kubwa kuliko 4000mAh hukaa na chaji kwa masaa yanayozidi 10
Pia ukaaji wa chaji wa muda mrefu unachangiwa na nguvu ndogo ya processor yake
Chaji yake inapeleka umeme wa wastani wa wati 18
Hivyo simu inaweza kuzidi masaa matatu kujaa kwa 100%
Ukubwa na aina ya memori
Memori ya vivo y20 ni aina ya eMMC yenye ukubwa wa 64GB
Utakutana na vivo zinazotofautiana na ukubwa wa RAM pekee
Kuna vivo yenye ram ya 3GB, 4GB na 6GB
Lakini usafirishaji wa data ni mdogo ukilinganisha na simu ambazo zinatumia memori aina ya UFS
Uimara wa bodi ya vivo y20
Kama ilivyo kawaida ya simu nyingi za daraja la chini ni kuwa na bodi ya plastiki
Y20 ni simu ambayo ina viwango vya chini hivyo usitegemee simu kuwa na vioo vigumu
Upande wa nyuma na upande wa mbele kote kuna plastiki
Mtumiaji atalazimia kununua kava ya simu kulinda ubora na kuimarisha uimara wa simu pindi inapoanguka kwa kimo kirefu
Ubora wa kamera
Simu ya vivo y20 ina jumla ya kamera tatu
Katika hizi kamera, ni kamera moja ambayo imewekewa teknolojia ya ulengaji ya PDAF
PDAF haina spidi kubwa ya kutambua kitu kinachopigwa picha ukilinganisha na dual pixel pdaf
Kamera nyingine ni aina ya marco maalumu kwa kupiga vitu kwa ukaribu
Kamera ya y20 inaweza kuchukua video ya aina moja
Ambayo ni video ya ubora wa full hd kwa spidi ndogo ya 30 fps
Ubora wa Software
Vivo y20 ni simu ya android 10 yenye inayotumoia software ya functouch 10.5
Kwa mwaka 2022, kuna toleo la android 12 hivyo baadhi ya simu zinapokea toleo jipya la androdi
Lakini vivo hii hawezai kupokea hata toleo la android 11
Hata hivyo android 10 bado ni mfumo endeshi wa simu unaokuja na vitu vizuri vingi
Na pia inaweza kutumia app mpya kwa kipindi cha miaka mingi
Yapi Madhaifu ya vivo y20
Kiujumla vivo y20 ni simu ya viwango vya chini ambayo ina madhaifu mengi
Madhaifu yake yanatokana na simu kuwa na bei ambayo inaweza kukupa simu nzuri zaidi
Y20 ina kioo chenye resolution ndogo
Simu haina ulinzi wa kuzuia maji kupenya
Simu pia ina ubora hafifu wa kamera
Kwani kamera haziwezi kurekodi video za 4k
Utendaji wa simu ni mdogo sanan kwa sababu ina chip ambayo nguvu yake haiwezi kufanya kazi kubwa kwa ufanisi
Neno la Mwisho
Kama utapata vivo y20 kwa bei ya chini 300,000/= utakuwa umeinunua kwa bei sahihi
Kinyume na hapo ni vizuri ukatafuta simu ya Redmi Note 10 5G
Redmi note 10 5g ina nguvu kubwa inayoifanya simu kuweza kufungua app ya aina yoyote kwa urahisi