Simu ya vivo v23 pro ni simu ya android ya mwaka 2022 yenye ufanisi mkubwa kwenye utendaji.
Ukizipitia sifa zake zilizoainishwa utaona nguvu kubwa ya processor na kamera yenye uwezo wa kurekodi video za resolution mbalimbali.
Na bei ya vivo v23 inaendana na vitu bora vingi vilivyopo kwenye simu
Sifa za hii simu zinaifanya kuwa moja ya simu bora ya daraja la kati kwa mwaka 2022
Bei ya Vivo V23 Pro Tanzania
Bei ya vivo v23 pro inafika shilingi 1,188,956.95/= za Tanzania
Hii ni bei ya vivo v23 ya GB 128 na Ram ya GB 8
Kwa hiyo bei yake inaongezeka kutokana na ukubwa wa memori.
Japokuwa bei inaweza onekana kubwa ila sifa zake kwenye display, memori, kamera na nguvu ya utendaji zimefanya bei ya simu kuwa juu.
Zifuatelie sifa zake zote kiundani
Sifa za Vivo V23 Pro
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | AMOLED, Refresh rate:90Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 3.1, 128GB, 256GB na RAM 8GB,12GB |
Kamera | Kamera (vivo ya macho matatu)
|
Muundo | Urefu-6.56inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 1,188,956.95/= |
Upi ubora wa Simu ya Vivo V23 Pro
Ukianza kuitumia vivo v23 pro utauona ubora wake kwenye display
Display yake inaonyesha vitu kwa ustadi kutokana na aina ya teknoloji iliyotumika kwenye kioo
Simu inawahi kujaa chaji kwa haraka
Kamera ya vivo ina rsolution kubwa inayofaa zaidi wakati wa kuzoom
Utendaji wa simu ya vivo v23 pro una nguvu ya kufungua gemu na aplikesheni ya aina yoyote
Simu inakuja na memori kubwa inayoweza kuhifadhi mafaili mengi na ya kutosha
Haya ni machache lakini ina uimara katika nyanja karibu zote.
Tuzame kiundani
Uwezo wa Network
Vivo v23 pro ina uwezo wa kutumia mtandao wa 4G na 5G.
Aina ya 4G simu inayotumia ni LTE Cat 17.
LTE cat 17 ni mtandao wa 4g unaoweza kudownload kwa kasi inayofikia 1600Mbps
Kama intaneti ya mtandao wa simu inakupa kasi hii basi unaweza kudownload faili la ukubwa 1300MB(1.3GB) kwa sekunde saba tu
Japokuwa kasi ya intaneti ya ya LTE Cat 17 Tanzania inapatikana kwa makampuni ya fiber kama zuku na sio laini za simu.
Kiujumla simu inakubali network bands za 4G saba tu
Bands hizo ni B1, B3, B5, B8, B38, B40 na B41.
Kuna baadhi ya laini za simu zinaweza zisikubali network ya 4G hapa Tanzania kutokana na kukosekana kwa baadhi ya bands wanazozitumia kwa ajili ya 4G.
Ubora wa kioo cha Vivo V23 Pro
Kioo cha Vivo v23 Pro ni kizuri kuliko kioo cha simu ya samsung a03s
V23 Pro ina kioo cha aina ya amoled.
Moja ya kitu kizuri kwenye kioo cha amoled ni kuwa na contrast kubwa.
Contrast kubwa inatengeza rangi nyingi
Hivyo inafanya kioo kuonyesha rangi za vitu kwa uhalisi wa asilimia za juu.
Na kizuri zaidi kioo cha simu kinaundwa na teknolojia ya HDR10+
HDR10+ kinaongeza utajiri wa rangi zaidi na kufanya kioo kionyeshe vitu kama vinaonekana na jicho la binadamu kwenye mazingira halisi
Ubora wake wa kioo pia unachagizwa na refresh rate kubwa inayofikia 90Hz
Hiki kiasi kinafanya simu kuwa nyepesi unapotachi.
Nguvu ya processor MediaTek Dimensity 1200
Processor iliyotumika kuipa nguvu vivo v23 pro ni MediaTek Dimensity 1200
MediaTek Dimensity 1200 ni processor ya simu yenye core nane
Core zake zimegawanyika sehemu tatu.
Dimensity 1200 inafanya vizuri sana kwenye applikesheni zinazopima nguvu ya chip ya simu
Kwenye app ya antutu mediatek dimensity ina alama 678,193
Geekbench inaipa alama 975 kwenye core moja
3DMark inaipa chipset alama 4180
Kifupi ni chip inayosukuma gemu yoyote.
Nguvu kubwa ya chipset inachagizwa na muundo na uwezo wa core zake kubwa na ndogo
Uwezo core kubwa
Core zenye nguvu ndogo zipo nne ila moja ina spidi inoyfikia 3.0GHz
Wakti core tatu zina spidi inayofikia 2.6GHz
Hizi core zina nguvu sana inayochangiwa na kutumia muundo wa Cortex A78
Cortex A78 inaifanya processor ya simu kuwa na utendaji imara pindi simu inapofungua applikesheni inayohitaji nguvu.
Kizuri ni kuwa Cortex A78 ina matumizi madogo ya umeme wakati ikifanya kazi kubwa
Uwezo wa core ndogo
Ubora wa core ndogo kwenye processor za simu hupimwa kwa matumizi madogo ya umeme.
Core nne zenye nguvu ndogo zina spidi inayofikia 1.8GHz
Hizi zimeundwa kwa Cortex A55
Cortex A55 hutumika pale simu inapofanya kazi zinazohitaji nguvu ndogo
Huu ni muundo unaokula umeme wa betri kidogo lakini utendaji upo juu kiasi
Uwezo wa betri na chaji
Chaji ya vivo v23 pro inaweza kupeleka umeme kwa kasi inayofikia wati 44.
Ni kasi inayoweza kujaza betri lake aina ya Li-Po la ukubwa wa 5000mAh chini ya dakika 70
Kwa mujibu wa gsmarena, simu inaweza tunza moto kwa masaa 110 ikiwa haitumiki mara kwa mara
Kwa uzeufu wangu, simu zenye betri ya 5000mAh zinaweza kukaa na chaji kwa zaidi ya masaa 14 ikiwa kwenye intaneti masaa yote bila kuzima data
Hivyo kwa ukubwa huu betri simu ya vivo v23 pro ni moja ya simu inayotunza chaji japokuwa ina processor yaenye nguvu sana.
Ukubwa na aina ya memori
Memori iliyopo kwenye V23 Pro ina kasi kubwa ya kuandika na kusoma data.
Hivyo kasi hiyo inaifanya simu kufungua app kwa haraka sana.
Hii spidi kubwa inasababishwa na kutumika kwa memori aina ya UFS 3.1
Hizi ni memori tofauti na zile zilizopo kwenye simu mpya nyingi za tecno ambazo ni aina eMMC
Kuna vivo ya 128GB na 256GB
Uchaguzi ni wako kulingana na matumizi yako ya simu
Uimara wa bodi ya Vivo V23 Pro
Bodi ya Vivo V23 Pro ni imara kwa sababu imetengenezwa kwa glasi upande wa nyuma na mbele.
Japokuwa haijaainishwa kampuni ambayo imeunda vioo vya simu hii.
Simu pia ni nyepesi kubeba kwani ina uzito wa gramu 171
Huu ni uzito unaoweza kukufanya usihisi kama umebeba simu
Na simu ni ndefu kiasi kwani ina inchi zinazofikia 6.56
Ubora wa kamera
Kamera ya vivo v23 pro ina kamera yenye sensa kubwa ya 108MP
Kwenye upande wa autofocus, imetumika teknolojia ya pdaf.
Pdaf ina ulengaji mzuri lakini haiwezi kuifikia dual pixel pdaf au Laser AF ambazo zimetumika pia kwenye iphone ya bei nafuu ya iPhone SE 2022
Uzuri wa kamera zake zinaweza kurekodi mpaka video za 4K kwa spidi ya 30fps
Japokuwa simu hii haiwezi kuwekwa kwenye simu za vivo zenye kamera, lakini kamera yake imewezeshwa mfumo wa gyro-Eis
gyro-Eis ni aina nyingine ya teknolojia ya kamera kwa ajili ya kuituliza kamera pale anayerekodi video akiwa anatembea
Tofauti na OIS, gyro-EIS inatumia motion sensor.
Ubora wa Software
Vivo v23 pro ni simu ya android 12 inayotumia mfumo wa Funtouch 12
Simu ya android 12 inaweza kukuonyesha app inayotumia kamera na mic bila ruhusa yako
Hii itakusaidia kuzitambua app zinazokutrack.
Wakati Funtouch 12 inakupa uwezo wa kuongeza ram kwenye simu.
Kwa hiyo utaweza kutumia memori ya simu kama ram.
RAM inapokuwa kubwa inaongeza ufanisi wa simu kiutendaji kiasi fulani
Yapi Madhaifu ya Vivo V23 Pro
Udhaifu mkubwa wa simu hii ni kutokuwa na uwezo wa kuzuia maji kupenya.
Haina viwango vya aina yoyote vya IP-Ratings.
Kamera zake zinarekodi video kwaa spidi ndogo ya 30fps
Simu ina network bands za 4G chache sana.
Simu inakosa kamera ya telephoto na haina optical zoom
Neno la Mwisho
Simu ni nzuri na inaendana na bei yake
Washindani wakubwa wa hii simu ni, simu ya Oppo Realme GT Neo 2T, OnePlus Nord 2 5G na Xiaomi 11T
Xiaomi 11T ndio mshindani mkubwa zaidi kuliko mwingine.
Bei ya xiaomi 11T ni chini ya shilingi 800,000 na ina bends za 4G nyingi
Kiuhalisia Xiaomi 11T inaizidi vivo v23 kwenye kila kitu