SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Ubora wa Simu mpya za tecno 2022 [Na bei zake]

Simu Mpya

Sihaba Mikole

April 9, 2022

Kuna simu mpya za tecno zipatazo tisa.

Simu hizo zimetoka mwishoni mwa mwaka 2021 na mwanzoni mwa 2022

Kuna tecno mpya za daraja la kati na za daraja la chini

Kiubora, tecno za daraja la kati zitakupa utendaji mkubwa wa kamera na network tofauti na za daraja la chini.

Hizi ni baadhi.

Kuelewa ubora wa tecno mpya unapaswa kujua sifa za kila simu ya tecno

Tecno Pova 5G

Simu ya Tecno Pova 5g ni simu ya 5g ya tecno iliyotoka desemba 2021

Simu ina ubora wa network yenye nguvu na processor yenye utendaji mkubwa.

Kioo cha Tecno kina refresh kubwa inayofanya simu kucheza gemu kwa ubora

simu ya tecno pova 5g

Inatumia mfumo wa memori wenye spidi kubwa aina ya UFS

Na betri yake ni kubwa na simu ni ndefu

Sifa zingine za Tecno pova 5g zina ubora wa kawaida na wa chini hasa kamera mbili

Sifa na bei ya Tecno Pova 5G

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
 • CPU – Dimensity 900 5G
 • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.4 GHz Cortex-A78
 • Core Za kawaida(6) – 6×2.0 GHz Cortex-A55
 • GPU-Mali-G68 MC4
Display(Kioo) IPS LCD, Refresh rate:90Hz
Softawre
 • Android 11
 • HIOS 8.0
Memori UFS 3.1, 128GB na RAM 8GB
Kamera Kamera tatu

 1. 50MP,PDAF(wide)
 2. 2MP(ultrawide)
 3. QVGA
Muundo Urefu-6.9inchi
Chaji na Betri
 • 6000mAh-Li-Po
 • Chaji-18W
Bei ya Tecno Pova 5G(TSH) 672,858.59/=

Tecno Pop 5S

Simu ya Tecno Pop 5S ni simu ya bei nafuu iliyozinduliwa Februari 2022

Tecno Pop 5s ina ubora mmoja tu.

Na ubora huo ni simu inayopatikana kwa bei ya chini ya laki mbili

simu ya tecno pop 5s

Tecno Pop 5s haina ubora wa kuridhisha kwenye kamera, memori na processor

Ila ni simu inayokubali mtandao wa 4G

Sifa na bei ya Tecno Pop 5S

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
 • CPU – Spreadtrum UNISOC SC9832E
 • Core Za kawaida(4) – 4×1.4 GHz Cortex-A53
 • GPU-
Display(Kioo) IPS LCD
Softawre
 • Android 10
 • Go Edition
Memori eMMC 5.1, 32GB na RAM 2GB
Kamera Kamera mbili

 1. 5MP,PDAF(wide)
 2. QVGA
Muundo Urefu-5.7inchi
Chaji na Betri
 • 3020mAh-Li-Ion
Bei ya Tecno Pop 5S(TSH) 162,540.00/=

Tecno Spark 8C

Ubora wa simu ya Tecno spark 8c ni kuwa na betri kubwa na memori ya kutosha

Kimuonekano ni simu ndefu inayomuwezesha mtumiaji kuona vitu kwa usahihi

Lakini Tecno spark 8c ina ubora mdogo sana wa kamera na chip

simu ya tecno spark 8c

Tecno spark 8c imetoka februari 2022

Na ni simu ya bei nafuu yenye ubora wa chini ila ina ubora mzuri upande wa kioo

Kioo cha tecno spark 8C kina refresh rate kubwa japo ni kioo cha bei rahisi

Sifa na bei ya Tecno Spark 8C

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
 • CPU – 
 • Core Zenye nguvu() –
 • Core Za kawaida() –
 • GPU-
Display(Kioo) IPS LCD, Refresh rate:90Hz
Softawre
 • Android 11
 • Go Edition
Memori eMMC 5.1, 64GB na RAM 4GB, 3GB, 2GB
Kamera Kamera mbili

 1. 13MP,PDAF(wide)
 2. QVGA
Muundo Urefu-6.6inchi
Chaji na Betri
 • 5000mAh-Li-Po
Bei ya Tecno Spark 8C(TSH) 244,686.97/=

Tecno Pop 5X

Ubora mkubwa wa simu ya tecno pop 5x ni kukubali mtandao wa 4g

Kwenye nyanja ya utendaji simu ina processor yenye uwezo mdogo

Ubora wa kamera ni wa kiwango cha chini sana

simu ya tecno pop 5x

Kitu kikubwa kinachovutia kwenye hii simu ni bei

Kwani ni simu ya mwaka 2022 inayopatikana kwa bei ya chini ya laki mbili

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
 • CPU – Unisoc SC9832E
 • Core Ndogo(4) – 4×1.4GHz
 • GPU-Mali-T820 MP1
Display(Kioo) IPS LCD
Softawre
 • Android 10
 • Go Edition
Memori eMMC, 32GB na RAM 2GB
Kamera Kamera TATU

 1. 8MP,PDAF(wide)
 2. QVGA
 3. QVGA
Muundo Urefu-6.52inchi
Chaji na Betri
 • 4000mAh-Li-Po
Bei ya Tecno Pop 5x(TSH) 176,786.63/=

Tecno Pop 5 Pro

Simu ya Tecno Pop 5 Pro imeingia sokoni mnamo januari 2022

Ubora wa tecno pop 5 pro upo kwenye uangavu wa kioo

Si uangavu mkubwa sana ukilinganisha na simu za makampuni mengine

tecno pop 5 pro

Tecno Pop 5 Pro ina betri kubwa ya kutunza chaji muda mwingi

Lakini ubora wa kamera na processor ni wa kiwango cha chini

Japokuwa simu inauzwa chini ya laki tatu ila bei ni kubwa kwa kulinganisha ubora

Sifa na bei ya Pop 5 Pro

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
 • CPU – Mediatek Helio A22
 • Core Ndogo(4) – 4×2.0GHz Cortex A53
 • GPU-PowerVR GE8320
Display(Kioo) IPS LCD,
Softawre
 • Android 11
 • Go Edition
Memori eMMC, 32GB na RAM 3GB
Kamera Kamera mbili

 1. 8MP
 2. QVGA
Muundo Urefu-6.52inchi
Chaji na Betri
 • 6000mAh-Li-Po
Bei ya Tecno Pop 5 Pro(TSH) 275,272.84/=

Tecno Spark 8 Pro

Simu ya Tecno Spark 8 Pro ni simu mpya ya januari 2022

Ubora wake ni kuwa na utendaji mkubwa.

Hii inachangiwa na simu kuwa na processor yenye nguvu

simu ya tecno spark 8 pro

Kamera kubwa ya tecno spark 8 pro ni nzuri kiasi fulani

Lakini kamera mbili zilizobaki hazina ubora unaotakiwa kutoa picha safi

Betri yake ni kubwa na chaji ya Tecno Spark 8 Pro inapeleka umeme mwingi

Sifa na bei ya Tecno Spark 8 Pro

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
 • CPU – MediaTek Helio G85
 • Core Zenye nguvu(2) – 2×2.0 GHz Cortex-A75
 • Core Za kawaida(6) – 6×1.8 GHz Cortex-A55
 • GPU-Mali-G52 MC2
Display(Kioo) IPS LCD,
Softawre
 • Android 11
 • HIOS 7.6
Memori eMMC 5.1, 64GB,128GB na RAM 4GB,6GB
Kamera Kamera tatu

 1. 48MP,PDAF(wide)
 2. 2MP(depth)
 3. QVGA
Muundo Urefu-6.5inchi
Chaji na Betri
 • 5000mAh-Li-Po
 • Chaji-33W
Bei ya simu(TSH) 305,858.72/=

Tecno Spark Go 2022

Simu ya Tecno Spark Go 2022 imetoka mwezi desemba mwaka 2021

Ubora wa betri yake ni ujazo mkubwa unaoweza kutunza moto masaa mengi.

simu ya tecno spark go 2022

Ni simu ya tecno ya 4G inayouzwa kwa bei rahisi

Utendaji wa simu ni mdogo, na ubora wa kamera ni wa kiwango cha chini

Sifa na bei ya Tecno Spark Go 2022

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
 • CPU – 
 • Core ndogo(4) –
 • GPU-
Display(Kioo) IPS LCD,
Softawre
 • Android 11
 • Go Edition + HiOS 7.6
Memori eMMC 5.1, 32GB na RAM 2GB
Kamera Kamera mbili

 1. 13MP,PDAF(wide)
 2. QVGA
Muundo Urefu-6.52inchi
Chaji na Betri
 • 5000mAh-Li-Po
Bei ya simu(TSH) 244,686.97/=

Tecno Spark 8T

Simu ya Tecno Spark 8T ni simu iliyozinduliwa mnamo mwezi desemba mwaka 2021

Ubora wa Tecno spark 8t ni kuwa na processor yenye core nane,

Betri kubwa na kamera moja yenye resolution kubwa

simu ya tecno spark 8t

Sifa zingine ni za kawaida

Spark 8T ni simu ya bei rahisi inayouzwa chini ya laki tatu

Sifa na bei ya Tecno Spark 8T

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
 • CPU – MediaTek Helio G35
 • Core Zenye nguvu(2) – 4×2.3 GHz Cortex-A53
 • Core Za kawaida(6) – 4×1.8 GHz Cortex-A53
 • GPU-PowerVR GE8320
Display(Kioo) IPS LCD,
Softawre
 • Android 11
 • HIOS 7.6
Memori eMMC 5.1, 64GB na RAM 4GB
Kamera Kamera mbili

 1. 50MP,PDAF(wide)
 2. QVGA
Muundo Urefu-6.6inchi
Chaji na Betri
 • 5000mAh-Li-Po
Bei ya simu(TSH) 284,448.61/=

Tecno Pova Neo

Simu ya Tecno Pova Neo iliingia sokoni mnamo mwezi desemba mwaka 2021

Ubora wa tecno pova neo ni kuwa na betri kubwa inayoweza kukaa na chaji muda mrefu

Ubora wa kiutendaji si mkubwa

simu ya tecno pova neo

Chaji ya TECNO POVA NEO inapeleka umeme wa wastani

Kwa kuzingatia sifa, tecno mpya hii inauzwa bei ya juu ukilinganisha na simu ya Redmi 9T

Sifa na bei ya Tecno Pova Neo

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g
Processor(SoC)
 • CPU – MediaTek Helio G25
 • Core Kubwa(4) – 4×2.0 GHz Cortex-A53
 • Core ndogo(4) – 4×1.5 GHz Cortex-A53
 • GPU-PowerVR GE8320
Display(Kioo) IPS LCD,
Softawre
 • Android 11
 • HIOS 7.6
Memori eMMC 5.1, 64GB,128GB na RAM 8GB,4GB
Kamera Kamera mbili

 1. 13MP,AF(wide)
Muundo Urefu-6.8inchi
Chaji na Betri
 • 6000mAh-Li-Po
 • Chaji-18W
Bei ya simu(TSH) 389,786.35/=

Neno la Mwisho

Kiuhalisia simu mpya tisa za tecno zilizoorodheshwa ni moja tu yenye utendaji mkubwa

Simu hiyo ni Tecno Pova 5G.

Ila bei yake si rafiki kwa sababu simu ya Redmi note 11 5g ya GB 128 bei yake ni 647,424.45/=

Wakati Redmi Note 11 5G inaizidi Tecno Pova 5G vitu vingi.

Simu nane zilizobaki zina ubora wa chini.

Nunua ukiwa una matumizi madogo ya smartphone na ukiwa sio mpenzi wa kamera

Wazo moja kuhusu “Ubora wa Simu mpya za tecno 2022 [Na bei zake]

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

tecno camon premier 30

Ubora wa simu za Tecno Camon 30 na bei zake(Pro, Premier)

Tangu mwezi wa nne kampuni ya walitoa matoleo ya Tecno Camon 30 Matoleo ya Camon 30 yapo matatu ambayo ni ya daraja la kati yaani mid range Ubora wa kiujumla […]

tecno camon 30 thumb

Bei ya Tecno Camon 30 Pro na Sifa Muhimu

Simu ya Tecno Camon 30 Pro ilitangazwa mwezi februari ila imetoka rasmi mwezi wa nne 2024 Ni simu ya daraja la kati(midrange) hivyo bei yake sio sawa na Tecno matoleo […]

tecno camon 30 premier thumbnail

Bei ya Tecno Camon 30 Premier 5G na Sifa zake muhimu

Kwenye matoleo bora ya simu kutoka Tecno, matoleo ya Tecno Camon huja na ubora katika vipengele vingi Hata bei za matoleo ya Camon huzizidi bei za Tecno Spark na Tecno […]

Bei ya Tecno Spark 20 Pro+ na Sifa zake

Simu ya Tecno Spark 20 Pro+ ilitoka rasmi desemba ya mwaka 2023 ila kwa Tanzania imeanza kupatikana miezi ya karibuni Kwa Tanzania bei ya juu kabisa ya Tecno Spark 20 […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani
TUFUATE
Youtube Facebook Instagram twitter

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company