SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Ubora wa Simu Mpya ya Samsung Galaxy A73 5G[na bei yake]

Sifa za simu

Sihaba Mikole

April 11, 2022

Simu mpya ya samsung galaxy a73 5g ni simu iliyoingia sokoni mnamo aprili 2022.

Ubora mkubwa wa galaxy A73 ni utendaji wa juu wa kusukuma kila aina ya gemu kwa resolution kubwa na kwa urahisi.

simu ya samsung galaxy a73

Hii ni simu ambayo iko kamili kwenye nyanja karibu zote.

Na mapungufu machache yanaifanya kuwa simu bora ya daraja la kati ya 2022

Kuelewa ubora wa samsung galaxy a73 itakupasa kujua sifa zote za simu na bei yake.

Bei ya Samsung Galaxy A73 5G

Bei ya samsung galaxy a73 5g haipo moja kulingana na memori na ukubwa wa Ram

Galaxy A73 5g ya GB 128 na Ram GB 8 inauzwa shilingi  1,286,295.79/=

Na samsung galaxy a73 5g ya gb 256 na ram gb 8 inauzwa shilingi 1,378,174.06/=

Hizi ni bei za India, kwa Tanzania bei ya simu inaweza ikazidi zaidi ya hapo ikizingatiwa ni simu mpya kabisa

Hakuna swali la kujiuliza kwa kuwa bei inaweza ikawa isiwe rafiki kwa watanzania wengi

Ila ukipitia ubora wa kila nyanja ulioanishwa humu utaona kuwa samsung a73 ni simu bora

Kizuri ni gharama.

Sifa za simu mpya ya Samsung Galaxy A73 5G

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
  • CPU -Snapdragon 778G 5G
  • Core zenye nguvu(4)- 4×2.4GHz Kryo 670 Gold
  • Core Za kawaida(4) – 4×1.8GHz Kryo 670 Silver
  • GPU-Adreno 642L
Display(Kioo) Super AMOLED Plus, Refresh rate:120Hz
Softawre
  • Android 12
  • One UI 4.1
Memori 128GB,256GB na RAM 8GB,6GB
Kamera Kamera nne

  1. 108MP,PDAF(wide)
  2. 12MP(ultrawide)
  3. 5MP(macro)
  4. 5MP(depth)
Muundo Urefu-6.7inchi
Chaji na Betri
  • 5000mAh-Li-Po
  • Chaji-25W
Bei ya simu(TSH) 1,286,295.79/=

Upi ubora wa Samsung Galaxy A73 5G

Samsung galaxy a73 5g ina kioo chenye refresh inayoifanya simu kuwa nyepesi wakati wa kuperuzi na kucheza magenu ya simu

Kamera yake ina sensa kubwa inayofaa zaidi wakati wa kuzoom

Simu inatunza chaji muda mrefu sababu ya kuwa na betri lenye ujazo mkubwa

Mfumo wake wa chaji unapeleka umeme wa kasi unaojaza betri ndani ya dakika chache

Simu imewezeshwa na matoleo mapya ya android.

Na itaweza kupokea kila toleo jipya la android kwa miaka minne mfululizo

Uwezo wa Network

Uwezo wake wa network kwa kuzingitia spidi ni wa kasi

Intaneti yake inawezeshwa na modem ya Snapdragon X53 5G Modem-RF yenye uwezo wa kupakua faili kwa spidi inayofikia 1200Mbps(LTE Cat 24)

SAMSUNG GALAXY A73 Network

Japokuwa kwa Tanzania ni ngumu kupata mtandao wa simu unaokupa spidi kubwa kama hiyo

Simu ina uwezo wa kukubali bands karibu zote za 4G, ila kuna network bands 18 za 4G

Kila laini ya simu itakubali kutumika kwenye simu ya samsung galaxy a73 5g kwa ajili ya intaneti ya 4G

5G yake inakubali network bands chache

Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy A73 5G

Simu inatumia vioo vya amoled aina super amoled plus.

Mara ya mwisho kwa vioo hivi kutumika ni mwaka 2012

Tangia hapo, amoled ya kawaida ndio kimekuwa kioo cha simu mpya ya samsung kwa miaka mingi.

Kikubwa ni kwamba vioo vya super amoled vinazarisha rangi nyingi sana kwa sababu ya contrast kubwa.

kioo cha samsung galaxy a73 5g

Na uzrui kioo kina refresh rate inayofikia 120Hz.

Refresh rate 120Hz inasaidia kuperuzi kwa kasi  kitabu, majina, sms, na kucheza magemu kwa urahisi

Resolution ya simu ni nzuri kuonesha vitu kwa ubora.

Kwani ina 1080 x 2400 pixels, hii hufahamika kama Full HD Plus

Nguvu ya processor Snapdragon 778 5G

Snapdragon 778 5g ni processor ya simu ya daraja la kati ambayo utendaji ni wa hali ya juu.

Kwenye app ya antutu snapdragon 778 ina alama 526,758

App ya geekbench processor ina alama 770 kwenye core moja

Hii inamaanisha simu mpya ya samsung galaxy a73 5g ina utendaji mkubwa kuliko galaxy a53 5g na a33 5g.

phone summary

Processor inakuja na core nane ambazo zipo core kubwa na core ndogo.

Uwezo wa core kubwa na ndogo unatambulisha utendaji wa processor na ulaji wa umeme wa betri ya simu

Uwezo wa core kubwa

Core zenye nguvu kubwa zipo nne zenye spidi ya 2.4GHz kila moja

Na zimeundwa kwa muundo wa Kryo 670 Gold

Kryo 670 Gold ni muundo wa Cortex A78 ulioboreshwa

Cortex A78 inatumia umeme kidogo kufanya kazi kubwa.

Na ni muundo unaosaidia simu kusukuma gemu ya aina yoyote.

Kwa mfano, simu zenye processor ya cortex A78 zinacheza gemu ya Call of Duty: Mobile kwa resolution kubwa ya UHD na kwa wastani wa 42fps

Gemu ikiwa na resolution kubwa sana baadhi ya simu huchemka na kushindwa kulicheza kwa urahisi

Uwezo wa core ndogo

Kuna core nne zenye nguvu ndogo.

Hizi huwa ni maalumu kwa ajili ya kazi ndogo ndogo simu inazozifanya.

Kwa mfano ukipiga simu, chip hutumia hizi core pekee yake.

Core ndogo zina spidi ya 1.8GHz kila core na zina muundo wa Cortex A55

Cortex A55 huwa inatumia chaji kidogo sana ukilinganisha na A53

Uwezo wa betri na chaji

Samsung A73 inatumia betri aina ya Li-Po lenye ukubwa wa 5000mAh

Samsung wanadai kuwa betri inakaa na chaji kwa masaa 17 simu ikiwa inatumia intaneti masaa mengi mfululizo

Hii simu haiji na chaji

Hivyo utalazimika kununua fast chaji ya samsung ya wati 25

Inaweza chukua chini ya masaa mawili kwa chaji ya wati 25 kujaza betri la 5000mAh

Ukubwa na aina ya memori

Chipset ya snapdragon 778 inasapoti memori za aina mbili.

Yaani UFS 3.0 na UFS 3.1

Yoyote ambayo ipo kwenye galaxy a73, hizo ni memori zenye kasi kubwa ya kusoma(read) na kuandika(write) faili(data)

Memori za UFS husaidia simu kufungua app kwa haraka

Ukiwasha simu ndani ya sekunde chache simu inawaka

Zipo aina tatu za samsung galaxy a73 kwenye memori

  1. 128GB, RAM 6GB
  2. 128GB, RAM 8GB
  3. 256GB, RAM 8GB

Simu inakupa machaguo makubwa ya memori kulingana na matumizi yako

Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy A73 5G

Bodi ya samsung galaxy a73 haipitishi maji hata punje kama simu ikizama kwenye kina cha mita moja kwa muda wa nusu saa.

Gorilla glass 5 inaipa ulinzi screen.

samsung galaxy a73 upande wa nyuma

Vioo vya gorilla glass 5 vinaweza kuzuia simu kupasuka pindi inapoanguka kwa kimo cha mita 1.2

Uzito wa simu ni gramu 181, ni simu nyepesi kubeba.

Urefu na upana wake unafikia inchi 6.7

Ubora wa kamera

Simu ina kamera nne.

Ni kamera moja tu yenye teknolojia ya OIS inayotuliza video pindi anayerokodi akiwa anatembea.

Teknolojia ya autofocus iliyotumika ni pdaf.

Pdaf haina ulengaji mzuri wa kamera ukilinganisha dual pixel pdaf.

Kwa baadhi ya picha nilizoziona youtube, picha za samsung galaxy a73 zinapiga vizuri wakati wa mchana na usiku.

kamera nne za samsung galaxy a73 5g

Inabalansi rangi vizuri na wala huwezi ukaona noises kwenye mwanga mwingi

Kitu kizuri ni kwamba simu inaweza ikatumia kamera tatu kwa wakati mmoja

Hiyo inawezeshwa na ISP ya snapdragon

Ubora wa video

Simu inaweza kurekodi video za aina mbili

  1. 4k(uhd) kwa 30fps
  2. 1080(fhd) kwa 30fps au 60fps

Pia kamera zake zinatumia gyro-EIS kutuliza video wakati wa kurekodi.

gyro-EIS inatofautiana na OIS(itafafanunuliwa kwenye makala zingine)

Ubora wa Software

Hii simu ni samsung yenye android 12 na software ya One UI 4.1

One UI 4.1 inasaidia kuongeza ram ya simu

Unaweza ukaongeza ukubwa wa ram mpaka GB 8

Wakati android 12 imeboresha  namna ya ku-screen shot

Kwa maana unaweza ukascreen shot kurasa kwa urefu unaoutaka

One UI ni software inayosifiwa kuwa nyepesi na haina matangazo kama MIUI ya xiaomi au HIOS ya tecno

Yapi Madhaifu ya Samsung Galaxy A73 5G

Samsung Galaxy A73 5G haina sehemu ya kuweka earphone.

Hivyo utalazimika kununua adapta kama utahitaji kutumia earphone au earphone za bluetooth

Na haina sehemu ya kuweka memori kadi

Samsung hawajatumia autofocus ya dual pixel pdaf

Display yake haina HDR10 inayorekebisha muonekano wa vitu hasa vilivyopigwa kwenye mwanga mdogo

Kibaya zaidi, utalazimika kununua chaji kwa sababu simu haiji na chaji

5G ya galaxy a73 5g ina bands chache sana, japo nchini mwetu bado hatujaanza kutumia 5g

Neno la Mwisho

Ukiachana na kutekuwepo earphone na chaji, simu ya samsung a73 ni simu bora ya daraja la kati

Mshindani mkubwa wa hii simu ni simu ya xiaomi 12x

Bei ya xiaomi 12x inaizidi kidogo sana a73 5g

Ila ubora wa kioo, network, utendaji, kamera, spidi ya chaji,

Xiaomi 12x inaizidi pakubwa Galaxy A73

Xiaomi inapatikana kwa bei ya 1,393,200/=

Wazo moja kuhusu “Ubora wa Simu Mpya ya Samsung Galaxy A73 5G[na bei yake]

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

samsung galaxy a15 thumbnail

Bei ya Samsung Galaxy A15 na Sifa Muhimu

Mwezi wa desemba 2023 ni mwezi ambao Simu ya Samsung Galaxy A15 ilizinduliwa Ni simu ya daraja la kati ambayo ina vitu vichache vinavyopatikana kwenye samsung za bei kubwa Ndio […]

samsung a55 showcase

Bei ya Samsung Galaxy A55 na Ubora wake

Samsung Galaxy A55 imetoka mwezi machi mwaka 2024 na ni simu ya daraja la kati Bei ya Samsung Galaxy A55 kwa Tanzania ni shilingi milioni moja na laki moja na […]

thumbnail

Bei ya Samsung Galaxy A35 na Sifa zake

Samsung Galaxy A35 ni toleo jipya la samsung lilotoka mwezi machi 2024 Ni simu ya daraja la kati iliyochota baadhi ya sifa muhimu kutoka kwenye galaxy yenye bei kubwa Ndio […]

simu mpya

Simu mpya kali 20 na bei zake kwa mwaka 2024

Hii ni orodha ya simu mpya ambazo zimetoka mwaka 2024 ama mwishoni mwa mwaka 2023 kutoka kwa kampuni zipatazo 11 Ni orodha inayohusisha simu za daraja la kati na la […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram