SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

Sifa za Simu ya Xiaomi 12x

Sifa za simu

Sihaba Mikole

March 1, 2022

Simu ya xiaomi ni simu ambayo imezinduliwa mwishoni mwa mwaka 2021.

Ni moja ya simu zenye nguvu na hardware bora zinazochangia ufanisi kwenye utendaji.

Kwa kuzingatia sifa za simu ya xiaomi 12x unaweza ukadhani simu bei yake inalingana na samsung galaxy s22 ultra au iphone 13 pro max.

Lakini haipo hivyo kwa sababu simu nyingi za xiaomi redmi huuzwa kwa bei nafuu.

Lakini hii ina gharama kidogo zinazosababishwa na kutumia processor yenye nguvu, kioo chenye uwezo wa kuonyesha rangi nyingi, chaji inayopeleka umeme mwingi na mfumo wa memori wenye gharama unaopeleka data kwa kasi

Sifa za xiaomi 12x kwa ufupi

Sehemu Za Simu Sifa za Simu
Network 2g, 3g, 4g and 5g
Processor(SoC)
  • CPU – Snapdragon 870 5G
  • Core Zenye nguvu(2) – 1×3.2GHz kryo 585, 3×2.42GHz kryo 585
  • Core Za kawaida(6) – 4×1.8GHz kryo 585
  • GPU-Adreno 650
Display(Kioo) OLED, Refresh rate:120Hz
Softawre
  • Android 12
  • MIUI 13
Memori UFS 3.1, 128GB, 256GB na RAM 8GB,12GB
Kamera Kamera tatu

  1. 50MP,PDAF,OIS
  2. 13MP(Ultrawide)
  3. 5MP(macro)
  4. 32MP(Selfie Camera)
Muundo Urefu-6.28inchi
Chaji na Betri
  • 4500mAh-Li-Po
  • Chaji-67W
Bei ya simu(TSH) 1,640,625/=

Zichimbe kiundani sifa ambazo zimeorodheshwa kwenye jedwari na ufahamu maana hasa ya kila sifa kiufasaha.

Processor

Processor ya simu iliyomo kwenye xiaomi 12x ni Snapdragon 870.

Snapdragon 870 ni chipset ambayo ina modem ya 5G inasapoti bends nyingi za mitandao karibu yote duniani.

Hivyo ukienda sehemu yoyote duniani xiaomi 12x itashika mtandao vizuri.

Chip ya snapdragon ina nguvu kubwa na imetumika kwenye baadhi simu za tabaka la juu(high end).

Baadhi ya smartphone ambazo zimetumia chip ya snapdragon 870 ni Motorola edge S pro, Oppo Reno 6 Pro na nyinginezo unazoweza kuzikuta kwenye kurasa hii simu za snapdragone 870.

Kinachosababisha chip ya simu ya xiaomi 12x kuwa na nguvu sana ni kutumia muundo wa Kryo 585.

Muundo wa Kryo 585 ni muundo uliobuniwa qualcomm ambao unatumia miundo ya Cortex 77 kwa core zenye nguvu na Cortex 55 kwa core zenye nguvu ndogo.

Ila kampuni ya Qualcomm huboresha miundo ya cortex na kuipa majina ya Kryo.

Uchakataji wa data kwenye Kryo 585 ni mkubwa na kwa matumizi madogo ya umeme.

Hivyo maisha ya betri yanakuwa marefu wakati huo simu inakuwa na uwezo wa kufungua aina zote za app ikiwemo magemu yenye nguvu.

Chipset inatumia GPU ya Adreno 650.

Kwenye app ya GFXBench inayopima nguvu ya graphic card kwa kutumia video zenye resolution kubwa kama mapango ya atzech ambapo app huita Aztec Ruins High Tier, GPU ya Adreno 650 inafungua video kwa spidi kubwa ya 67fps.

Ambapo GPU iliyopo kwenye Infinix note 11 inaplay video kwa spidi ya 9.3fps hivyo kwenye simu ya infinix baadhi ya video zinaweza kuplay kwa kuganda ganda au taratibu sana.

Upande wa magemu Adreno 650 inasukuma gemu nyingi kwenye resolution kubwa bila kukwama na kwa spidi.

Kwa mfano gemu la League of Legends: Wild Rift simu ya xiomi 12x inalicheza kwenye Ultra HD(resolution kubwa sana) kwa spidi ya 117fps

Magemu mengine ambayo unaweza kuyaona hapa.

Unaweza ukawa usijue maana fps na umuhimu wale pitia ukurasa huu: fps ya apple gpu kwenye display

Memori

Simu ya xiaomi 12x inatumia memori aina ya UFS.

Kirefu cha UFS ni Universal Flash Storage, ni mfumo wenye kasi kubwa wa kuhifadhi na kusafirisha data.

UFS ina matoleo ya aina nyingi yanayotofautiana spidi.

Kwenye xiomi 12x kuna UFS 3.1 ambayo spidi inafika 2400Mbps.

Mfumo wa memori wa aina ya UFS unafanya simu ya xiomi 12x kuwaka na kuzimika kwa haraka.

Na pia unasaidia application kufunguka kwa haraka.

Na unachangia file ambalo simu inalodownload kuwahi kumalizika

Xiaomi 12x ina memori za ukubwa wa aina mbili.

Ipo ya 128GB na 256GB.

Na upande wa RAM zipo za 8GB na 12GB.

Aina ya RAM ya hii simu ni LPDDR5(Low Power Double Data Rate).

LPDDR5 ina bandwidth kubwa ya kusafirisha data nyingi kwa kasi.

Hivyo xiaomi  12x inaweza kufungua application nyingi kwa wakati mmoja bila kukwama na kwa matumizi madogo ya umeme

Display(Kioo)

Kioo cha xiaomi 12x ni aina ya OLED.

OLED yake ina rangi zaidi bilioni moja.

Vitu vingi ambavyo display inavionesha vitaonekana kwa uharisia wa rangi halisi kwa kiasi kikubwa.

Dispaly ya simu ya xiaomi 12x ina refresh rate ya 120Hz.

Refresh rate ni kitendo cha screen kuonyesha(kubadilisha) vitu vingine unavyovitaka pale unapokuwa unatachi simu.

Kwa mfano kama una simu yenye picha nyingi na ukafungua folda la picha.

Wakati unaanza ku-scroll kwenda chini kutafuta picha unayoitaka kadri unavo-scroll picha zingine zinatokea.

Au kwa mfano ukiwa unafungua app ya whatsapp kusoma meseji za group ambazo zinakuwa ni nyingi.

Kama simu ina refresh rate ndogo basi screen itakuwa inascroll taratibu

Na kinyume chake ni sahihi.

Refresh rate kubwa inafanya simu kuwa nyepesi na nzuri kucheza gemu.

Kioo ni angavu, uangavu unaofanya display kuonyesha vitu hata simu ikiwa inatumika kwenye jua kali.

Moja ya sifa za simu ya xiaomi 12x inayochangia ubora wa kioo kuonyesha vizuri ni kuwa na HDR10+

HDR10+ huonyesha video na picha vizuri na picha zinakuwa safi hasa kama video ilirekodiwa kwenye mwanga mdogo

Betri na mfumo wa chaji

Simu ina betri kubwa aina ya Li-Po lenye ujazo wa 4700mAh.

Betri ya 4700mAh inawahi kujaa kutokana na xiaomi 12x kuwa na chaji inayopeleka umeme mwingi wa 67W.

Inachukua dakika 39 tu simu kujaa.

Fast chaji inapunguza muda kusuburia simu kujaa.

Lakini umeme wa 67W ni mwingi na maisha ya betri yanaweza isha kwenye miaka michache.

Lakini kutokana na kuwa na processor ya snapdragon 870 ukiongeza na betri kubwa simu hii inaweza kaaa na chaji muda mrefu.

Bodi ya simu

Xiaomi 12x ni simu nyembamba na yenye uzito mdogo wa gramu 176.

Upande wa display unalindwa na kioo cha Gorilla Victus.

Kioo cha Gorilla Victus ni kigumu kiasi cha kwamba hauhitaji screen protector ya simu.

Kwenye maabara za Corning watengenezaji wa vioo vya Gorilla simu zenye victus zinastahamili kupasuka hata ikiwa imeangushwa kwa kimo cha mita mbili kutoka juu.

Kitu kimoja kikubwa ambacho simu inakosa ni kutokuwa na viwango IP68.

Simu nyingi za gharama huwa na uwezo wa kuzuia maji iwapo simu imedumbukia kwenye maji au ukiwa unatumia kwenye mvua yaani maji tiririka.

Maji yanaweza penya kirahisi kwenye Xiomi 12x.

Hili ni moja ya tatizo ambazo simu nyingi za infinix kama infinix zero 5g inalo.

Kupuuzia ulinzi dhidi ya maji.

Kamera

Simu ya xioami ina kamera tatu.

Xiaomi 12x ni simu yenye kamera nzuri kwa sababu moja ifuatayo.

Simu ina teknolojia ya OIS.

Ukiwa unarekodi video huku unatembelea OIS hutuliza kamera na video kutulia.

Lakini si simu nzuri sana kwa kupiga picha mkiwa out ama kumpiga mtu anaekimbia au kitu kinachotembea.

Sababu kubwa ni simu kutotumia autofocus aina ya dual pixel PDAF.

Dual pixel PDAF hulenga vitu kwa usahihi sana.

Sensa ya kamera ya xioami 12x imeundwa na sony, ni sensa nzuri.

Kuhusu app ya kamera ya xiomi 12x hakuna tathmini nyingi kuhusu hilo.

Ila unaweza kufuatilia baadhi ya channel za youtube zinazoelezea kamera ya hii simu.

Software

Xiomi 12x inatumia Android 12 na MIUI 13

Android 12 ina vitu vingi vipya.

Kwa kiasi kubwa android 12 imejikita sana kwenye usalama.

Simu ya android yenye mfumo huu mpya inaweza ikakuambia applications ambazo zinatumia vitu kama mic.

Kama kuna app inakutrack ambayo huijui utaweza kuitambua kwa sababu simu itakujukisha hiyo app inayorekodi sauti yako.

Kitu kingine kipya kwenye android 12 ni app kuweza kufunguka hata kabla kudownload kumalizika.

Fahamu mengi zaidi yaliyopo kwenye hii android mpya hapa

Upande wa MIUI 13, Xiaomi wanasema wameongeza ufanisi wa matumizi ya betri.

Kwa maana xiaomi 12x itakuwa na inatumia umeme kidogo na kufanya simu kukaa muda mrefu na chaji.

Kikawaida kampuni husifia sana mifumo yao

Lakini kiujumla MIUI si nzuri wala si mbaya.

Ipo kati kwa kati.

Mengineyo

Xiaomi ina gps za aina aina sita ambazo ni GLONASS (1), BDS (3), GALILEO (2), QZSS (2), NavIC na GPS.

Simu ina mfumo wa NFC(Near Field Communication)

NFC inaweza ikatumika kama mbadala wa kadi za benki.

Badala ya kutoa pesa kwa kadi simu inachukua nafasi master card au visa card.

Huu mfumo kwa hapa Tanzania bado.

Simu ina Fingerprint sensor ambayo ipo kwenye display.

Na inatumia bluetooth aina ya 5.2 ambayo inaweza kutuma file kwenye vifaa vingi kwa wakati mmoja.

Na pia bluetooth 5.2 inaweza kupokea mafaili kutoka kwenye vingi kwa wakati mmoja

Kama umezielewa sifa za simu ya xiaomi 12x basi utakuwa uemelewa sababu ya simu kuuzwa shilingi 1.6M.

Lakini kwa bei hiyo uaweza pata samsung s21 fe 5g inayoizidi xiaomi 12x kwenye nyanja nyingi.

Samsung s21 fe 5g inapatikana kwa bei chini ya hiyo na ina vitu vyote ambavyo vingine havipo kwenye xiomi 12x

Chaguo ni lako.

Maoni na Maswali

Email yako haitochapishwa, kwenye alama * lazima pajazwe ili ukomenti

Fuatilia Zaidi

xiaomi 14 ultra

Simu 13 mpya na kali za Redmi na Xiaomi 2024

Kampuni ya Xiaomi sio ngeni kwa wengi Ni kampuni ya china inayotengeneza simu za madaraja yote kwa brandi za Xiaomi, Redmi na Poco Hapa kuna orodha ya simu mpya za […]

No Featured Image

Bei ya Redmi Note 13 na Sifa Zake Muhimu

Redmi Note 13 5G ni simu kutoka Xiaomi ya China ambayo bei yake kwa sasa ni shilingi laki nane Hii ni bei ya toleo lenye ukubwa wa GB 256 na […]

redmi 10a thumbnail

Bei ya Sasa ya Redmi 10A na Sifa Muhimu

Simu ya Redmi 10A iliiingia sokoni mwaka 2022 Ni aina ya simu inayolenga watu wenye matumizi ya kawaida kama sio machache Hivyo bei ya Redmi 10A ni chini ya laki […]

Jinsi ya Kutumia GPS kwenye Simu (Hatua kwa Hatua)

GPS kirefu chake ni Global Positioning System, ni mfumo wa utambuzi wa maeneo ambao unasimamiwa na Marekani Simujanja karibu zote zina huu mfumo Una faida kubwa sana hasa kama unajua […]

SimuNzuri

Zigundue Sifa Za Simu Bora Kiundani

E-mail : simunzuriblog@gmail.com

Simu: +255 683 420 543

Whatsapp: +255 756 077 262

Kabila, Magu

Mwanza, Tanzania

Company

Find Us On

FB Twitter Instagram