Mnamo mwezi machi 2022 Samsung waliingiza sokoni simu ya Samsung Galaxy A13
Ni Samsung ya daraja la kati hivyo gharama yake imechangamka kidogo
Kwani bei ya Samsung Galaxy A13 kwa Tanzania inazidi laki tatu na nusu
Lakini kiubora Galaxy A13 inaigeuza simu kuwa ya gharama hasa kama utafananisha na simu za android nyingine.
Bei ya Samsung Galaxy A13 ya GB 64 Tanzania
Galaxy A13 yenye ujazo wa GB 64 na RAM GB 4 inafika shilingi 450,000/=
Hii ni bei kwa baadhi ya maduka Dar Es Salaam kariakoo simu ikiwa mpya
Ila sasa ukitazama uwezo wa simu kiutendaji utagundua bei yake haistahili kuzidi laki tatu
Kwa sababu sifa zake zinaendana sana na Redmi 9a inayopatikana kwa bei ya chini ya laki tatu.
Ziangazie sifa zake ikupe picha kwa nini simu ina gharama kubwa.
Sifa za Samsung Galaxy A13
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | PLS LCD |
Softawre |
|
Memori | eMMC 5.1, 128GB,64GB,32GB na RAM 3GB,6GB,4GB |
Kamera | Kamera nne
|
Muundo | Urefu-6.6inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 450,000/= |
Ni upi ubora wa simu ya Samsung Galaxy A13?
Galaxy 13 inakuja na matoleo mengi upande wa memori
Matoleo mengine yanaleta memori inayoweza kuhifadhi mafaili mengi
Ina betri kubwa inayodumu na chaji muda mrefu
Ni simu ambayo imewekewa kioo kigumu kwenye screen
Hivyo kuchunika na kupasuka si rahisi
Ni simu iliyo na sehemu ya memori kadi tofauti na simu nyingi za google pixel
Lakini kama sifa za simu zinavyoonyesha bei yake ina mkanganyiko ukitazama uwezo wa simu kwenye nyanja zote
Uwezo wa Network
Simu ya Samsung A13 ni simu ya 4G aina ya LTE Cat 7
Spidi yake ya juu kabisa ya kudownload inafika 300Mbps
Kama ukiwa marekani au china spidi hii unaifikia kiurahisi tu
Ila Tanzania kasi ya intaneti bado ni ndogo japokuwa kuna 4G
Na ina masafa yote yanayopatikana nchini
Ubora wa kioo cha Samsung Galaxy A13
Kioo cha samsung galaxy a13 ni cha PLS LCD
Ni aina nyingine ya LCD ambayo haina tofauti kubwa na IPS LCD
Koo chake kinatumia resolution ya 1080 x 2408 pixels
Walau ufanisi wa kuonyesha vitu unakuwa mzuri
Japo si sawa na simu zenye vioo vya OLED au AMOLED
Kibaya Galaxy A13 haina hdr10 na refresh rate yake ni ya kawaida
Nguvu ya processor Exynos 850
Samsung A13 inatumia chip ya Exynos 850 katika kufanya kazi zake
Ukichaguwa simu yenye processor dhaifu jua kuwa umechagua simu mbaya
Nguvu ya processor huwa inajulisha ubora wa simu na bei yake
Exynos 850 ina utendaji mdogo
Hiyo inatokana na chip kuwa na core nane zote zikiwa zinatumia muundo wa Cortex A55
Cortex A55 inafanya kazi(decode) chache kwa mzunguko mmoja ukilinganisha na muundo wa Cortex A76
Hii inafanya processor kutumia umeme mdogo kutokana na kufanya kazi chache
Ndio maana Exynos 850 kwenye app ya Geekbench ina alama 160
Sio simu nzuri kucheza magemu
Uwezo wa betri na chaji
Hii simu ina betri kubwa yenye uwezo wa kukaa na chaji muda mrefu
Ukaaji wa chaji unachangiwa sana na processor yake kutumia umeme mdogo
Hivyo haitoshangaza betri yake ya 5000mAh kukaa na chaji masaa zaidi ya 15 simu ikiwa kwenye intaneti muda wote
Ila simu inaweza chukua masaa mengi kujaa
Chaji ni ya wati 15
Kiasi hiki cha umeme kinaweza kikajaza betri ya 5000mAh kwa masaa yanayozidi matatu
Aina ya chaji ni ile yenye pini nene inayofahamika kama USB Type-C 2.0
Ukubwa na aina ya memori
Simu ina matoleo matano yanayoanzia na ukubwa wa GB 32 na RAM GB 3 mpaka GB 128 kwa RAM a GB 6
Japokuwa simu inatoa storage kubwa lakini aina ya memori inazotumia zinasafirisha data taratibu
Galaxy A13 inatumia memori ya eMMC 5.1 ambayo spidi yake ya juu ni 250MBps
Wakati memori za UFS 2.1 spidi yake inatembea mpaka 1200MBps
Hii ina maana gani?
Kama unakopi faili la ukubwa 2500MB, Samsung hii itakopi kwa sekunde 10
Wakati simu yenye UFS 2.1 itakopi kwa sekunde mbili (2)
Memori ikiwa na kasi kubwa hufanya simu kuwaka ama kuzimika kwa haraka
Uimara wa bodi ya Samsung Galaxy A13
Bodi ya samsung galaxy a13 imetengenezwa kwa plastiki upande wa nyuma
Na imewekewa kioo cha Gorilla Glass 5 kwenye screen
Hiki huwa ni kioo kinachostahamili kuvunjiaka kama simu ikianguka kwa kimo cha mita 1.2
Hii simu ina sehemu ya kuweka memori kadi
Na ni simu ya laini mbili
Ubora wa kamera
Simu ina kamera nne hivyo unaweza kuita samsung macho manne
Ila ni kamera moja tu inayokidhi uwezo wa kutoa picha nzuri na kurekodi video za 4K
Kamera hiyo ni aina ya Wide yenye resolution ya 50MP
Na yenye kutumia ulengaji wa PDAF
Kamera zingine ni depth ambazo hutumika kuweka ukungu(bokeh effect) upande wa nyuma wa kitu kinachpigwa picha
Kamera ya ultrawide inaweza kupiga picha eneo pana kwa nyuzi 123
Pamoja na kuwa na kamera ya 50MP, Galaxy A13 haiwezi kurekodi video za 4K
Kwani processor yake ina nguvu ndogo kuweza kufanya kazi hiyo
Ubora wa Software
Galaxy A13 inakuja na Android 12 pamoja na mfumo wa One UI 4.1
One UI 4.1 ina kitu kinaitwa Ram plus
Ram plus inakupa uwezo wa kuongeza ukubwa wa RAM
Kitu kinachosaidia simu kuweza kufungua app nyingi kwa wakati mmoja na kwa urahisi
Ram plus inachukua sehemu ya memori ya simu
Ila inaweza isiwe na maana sana ukizingatia simu ina memori za eMMC 5.1
Yapi Madhaifu ya Samsung Galaxy A13
Bei ya Samsung Galaxy A13 ni kubwa kutokana na utendaji mdogo wa chip
Simu haijatumia kioo cha amoled
Kwa sababu simu ya redmi note 10 inayopatikana kwa bei ya chini ya laki nne na nusu ina kioo cha AMOLED
Simu haina kamera nzuri japokuwa ina jumla ya kamera nne
Inatumia memori zenye uwezo mdogo wa kusafirisha data
Chaji yake haipeleki umeme mwingi
Simu za laki nne nyingi huja na chaji ya umeme wa wati 33
Haina redio
Hitimisho
Kuna watumiaji wa simu huwa wanapenda brand maarufu bila kujari sifa za simu
Hivyo kwa mpenzi wa samsung hii ni simu itakayomfaa.
Lakini kama utendaji wa simu ni kipaumbele, basi haustahili kutoa laki nne kwenye hii simu
Yapo matoleo megi yaliyofafanuliwa kwenye tovuti hii.
Kiuhalisia Samsung Galaxy A13 inakaa kwa Redmi 10C
Wakati Redmi 10C inapatikana kwa bei ya chini ya laki tatu na nusu aliexpress
Pitia hapa ujifunze: Jinsi ya kununua simu mtandaoni kupitia aliexpress
Maoni 15 kuhusu “Bei ya Simu ya Samsung Galaxy A13 na Sifa Muhimu (2022)”
Sorry nina sm kama hii ya smsung a13 toka ni nunue nina mwezi mmoja tu lkn sas ilikuwa iki weka chaj inapeleka ndani ya mada mawili imejaa lkn saiv ina sumbua nikiweka chaj ina ingiza taratibu na inaleta maneno haya check your charger connection .. make sure the cable and charger are properly connected sasa naomba msaada
Hii simu ulinunua ikiwa mpya, ili kujua tatizo jaribu kuchaji na chaja nyingine ili ujue kama ni betri au chaji, Ila uwezekano ni kuwa chaji haijakaza vizuri kama ni orijino
Ningependa kujua Samsung a12 na Samsung a13 ipi nzuri zaidi
Samsung a13 ni nzuri zaidi
Je kati ya a13 na a51 ipi ni nzuri au bora zaidi?
Je kati ya Samsung a13 na Samsung a51 ipi ni nzuri au bora zaidi?
A51 ni Simu nzuri zaidi
Nami nilitaka kukununua a13 je kama wezangu mwanishaulije hapa maana kunayo nyengine nilipenda pia a14 ipi nzr kati ya a13 a14
Je kati ya a13 na a14 ipi nzr zaidi
A14 ni nzuri zaidi
Kwa maelezo yako inaonekana Samsung a13 haiwez kurekod video ya 4k sijakuelewa hapo na Nina was I was kua siyo nzuri
Kwakweli nimesoma maelezo yenu kwa uzur kabisa na nimeelewa mwenyewe ni tumia SAMSUNG A13 galaxy kumbe inasifa kemukemu namna hii.
Kuna tetesi kuwa simu za Samsung ikiwemo hii A13 hazifurashiwi ukisahau password imekula kwako je ni kweli?
Sijawahi kusikia
A15 5G Na A24 Ipi nzuri zaidi