Simu ya Redmi Note 11 Pro 5G ni simu mpya ya xiaomi ya mwaka 2022.
Ukiwa na redmi note 11 pro 5g hautakuwa na wasi wasi simu kupasuka.
Simu ina kioo kigumo na display bora na angavu
Mtumiaji wa note 11 pro anaweza kutumia laini ya simu yoyote duniani.
Simu ina networks bands za 4g na 5g nyingi.
Sifa za redmi note 11 pro na bei yake zinaweza kukuvuta kuimiliki simu
Sifa za Redmi Note 11 Pro 5G
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g and 5g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | Super AMOLED, Refresh rate:120Hz |
Softawre |
|
Memori | UFS 2.2, 64GB, 128GB na RAM 8GB, 6GB, 4GB |
Kamera | Kamera tatu
|
Muundo | Urefu-6.67inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 700,942/= |
Upi ni ubora wa simu ya Redmi note 11 pro 5g?
Ubora wa redmi note 11 pro 5g umegawanyika katika sehemu tano.
Kwanza, network ya 4g inakubali mitandao mingi duniani
Kioo chake kina kiwango kikubwa cha uangavu
Simu ina bodi ngumu kuchunika na kupasuka
Chaji yake inajaza betri kwa dakika chini ya 50
Processor ya note 11 pro 5g ina nguvu ya utendaji wa kufungua aina yoyote ya app.
Network
Redmi note 11 pro 5g inakubali aina zote za mitandao ikiwemo 4g na 5g
4G ya redmi note 11 ni aina ya Cat 18.
Na simu ina network bands za 4g zipatazo 20
Spidi ya intaneti ya lte cat 18 inafikia 1174Mbps ambayo ni sawa 146.75MBps
Iwapo mtandao wa simu unakupa spidi hii basi simu itadownload file la 1300MB kwa sekunde 8 tu
Intaneti za 4g kwa mitandao yote ya Tanzania inakubali kwenye simu hii ya xiaomi
Network bands za 5g zipo kumi
Bands hizo ni 1, 3, 5, 7, 8, 20, 28, 38, 40, 41, 66, 77, na 78
Bands za 5g unazoziano hapo ni Lower Band na Mid Band 5g
Simu haina 5g bands zenye spidi kubwa sana
Ubora wa kioo cha Redmi note 11 pro 5g
Redmi note 11 pro 5g inatumia kioo aina ya super amoled
Vioo vya super amoled hutengenezwa na samsung.
Huwa vina contrast ratio kubwa sana na kufanya kioo cha super amoled kuwa rangi nyingi (zaidi ya bilioni)
Kioo cha redmi note 11 pro 5g ni kizuri kucheza gemu.
Kwani kina refresh ya 120Hz.
Referesh kubwa hufanya simu kuwa nyepesi pale unapoperuzi namba za simu nyingi au sms
Uangavu wake unafikia 1700nits na kuifanya simu kuonyesha vitu vizuri sana ikiwa juani
Simu ina resolution kubwa ya 1080 x 2400 pixels hivyo picha huonekana kwa ubora mkubwa
Nguvu ya processor Snapdragon 695 5G
Simu ya Redmi note 11 pro 5g inatumia processor aina ya Snapdragon 695 5g.
Kwa mujibu wa data za antutu na 3dmark Snapdragon 695 5g inaizidi processor ya Helio g96
Helio g96 imetumika kwenye simu ya Infinix note 11 pro
Snapdragon 695 5g ina core nane(octacore).
Core zenye nguvu sana zipo mbili
Na core zenye nguvu ndogo zipo sita
Uwezo wa core kubwa
Kila core yenye nguvu ina spidi ya 2.2GHz
Core zote zinatumia muundo wa Kryo 660 Gold.
Kryo 600 ni muundo ulioboreshwa wa Cortex A78
Kwenye simu, Cortex A78 inafanya kazi pale simu inapofanya kazi nzito
Kama kucheza gemu na kutumia applikesheni nyingi wakati mmoja
Cortex A76 ina utendaji mkubwa na inatumia umeme mdogo ukifananisha Cortex A73 na Cortex A76
Ndio maana Redmi note 11 pro 5g inaweza cheza gemu la Mobile Legends: Bang Bang kwa resolution kubwa sana(Ultra HD) kwa spidi ya 42fps.
Wakati Samsung Galaxy A22 yenye helio g80 inacheza mobile legends kwa full hd na sio ultra hd.
Ikijaribu ultra hd betri ya galaxy inaweza isha chaji mapema
Kwa sababu processor ya simu ya Galaxy A22 inatumia Cortex-A75
Uwezo wa core Ndogo
Core zenye nguvu ndogo zipo sita.
Na kila moja ina spidi ya 1.7GHz
Zote zinatumia muundo wa Kryo 660 silva.
Huu ni muundo wa Cortex A55.
Cortex A55 ina ufanisi mkubwa wa matumizi madogo ya betri.
Utendaji wake ni mkubwa ukilinganisha Cortex A53
Uwezo wa betri na chaji
Betri ya redmi note 11 pro 5g ina ukubwa wa 5000mAh aina ya Li-Po
Na chaji ya redmi note 11 pro 5g inapeleka umeme mwingi wa 67 wati.
Umeme wa wati 67 unaweza jaza simu kwa 100% chini ya dakika 50.
Xiaomi wanasema chaji ya redmi inajaza simu kwa dakika 42 tu
Betri yake ina uwezo wa kukaa na chaji masaa 115 simu ikiwa imetulia.
Ukiwa unatumia intaneti bila kuzima data masaa yote chaji itadumu kwa masaa 13 (maabala ya gsmarena)
Sio masaa mengi ukifananisha na samsung galaxy a23 au vivo t1 5g
Ukubwa na aina ya memori
Memori iliyopo kwenye Redmi note 11 pro 5g ni aina ya UFS 2.2
UFS 2.2 zinaifanya simu kuwaka kwa haraka sana.
Na app kufunguka kwa kasi
Yapo matoleo manne ya Redmi note 11 pro 5g kwa upande wa memori
- 64GB ROM, 6GB RAM
- 128GB ROM, 4GB RAM
- 128GB ROM, 6GB RAM
- 128GB ROM, 8GB RAM
Ram ikiwa kubwa simu inakuwa na uwezo kufungua app nyingi kwa wepesi kwa wakati mmoja
Uimara wa bodi ya Redmi note 11 pro 5g
Redmi note 11 pro 5g pro imeundwa kwa glasi upande wa nyuma.
Na kioo chake kimepewa ulinzi na glasi ya gorilla toleo la la 5(Gorilla glass 5)
Gorilla glass 5 ni kioo kigumu kupasuka simu ikianguka kwa kimo cha mita 1.2(data za majaribio ya gorilla)
Hivi ni vioo ambavyo vinazuia sana michubuko ya kioo
Ukiwa na kioo cha gorilla haina ulazima wa kununua screen protector wala kava ya simu
Simu inauwezo wa kuzuia manyunyu ya mvua na vumbi kwa sababu ina IP53
Simu ina ina uzito wa gramu 202.
Ubora wa kamera
Kamera za redmi note 11 pro 5g zipo tatu.’
Kamera kubwa ina resolution ya 108MP
Ila ukipiga picha inatokea ya resolution ya 12MP
Kwenye kamera zake tatu hakuna kamera ya telephoto
Hivyo simu inatumia app ya kamera kuzoom vitu vilivyo mbali na kamera
Ubora wa picha
Redmi note 11 pro 5g inatoa picha safi nyakati za mchana
Picha za gsmarena walizopiga kwa hii simu zinaonekana bila kuwa na ukungu(noises)
Vitu vivlivyopo kwenye picha vinaonekana kwa usahihi ukiikuza picha
Noise(ukungu) unaonekana kwenye nyakati za usiku kwa kiwango kidogo
Lakini exposure ya kamera inajitahidi kubalansi mwanga.
Kwa bahati mbaya kamera zake hazitumii teknolojia ya dual pixel pdaf kulenga vitu
Lakini pia hakuna OIS kwenye kamera zote tatu
Hivyo kama unarekodi video ukiwa unatembea video itakuwa haitulii
Ubora wa video
Xiaomi redmi note 11 pro 5g inarekodi aina moja ya video kwa spidi ya 30fps
Video zinaweza kurekodia ni aina ya full hd(1080p)
Simu haizwezi kurekodi video za 4k na 8k kama iPhone 13 pro max
Ubora wa Software
Redmi note 11 pro 5g ni simu ya android 11 yenye software ya MIUI 13
Ukiwa na MIUI 13 ulaji wa betri unapungua kwa asilimia 10 kwa mujibu wa Xiaomi
Kwenye MIUI kuna ongezeko la wallpaper za kuvutia
Upande wa Multitasking miui inawezesha kufungua app nyingine kwenye sidebar.
Kwa mfano unaweza kuangalia video ya youtube wakati unaperuzi mtandao kutumia chrome
Mfumo endeshi wa xiaomi unakuwezesha kuweka alama(watermak) document zako.
Hivyo inazuia wizi wa haki miliki
Bei ya Redmi note 11 pro 5g Tanzania
Bei ya simu ya redmi note 11 pro 5g inafika shilingi 710,000 za Tanzania.
Bei yake inatofautiana na ukubwa wa memori
- redmi note 11 pro 5g ya 6GB na 64GB inauzwa shilingi 601,035.63/=
- redmi note 11 pro 5g ya 6GB na 128GB inauzwa shilingi 647,424.45/=
- redmi note 11 pro 5g ya 8GB na 128GB inauzwa inauzwa shilingi 677,592.26/=
Mshindani wa simu hii ya redmi ni vivo t1 5g na Oppo a96 5g.
Hizi simu mbili zinaachwa mbali kiubora na redmi iliyopo hapa
Oppo a96 5g ina gharama kubwa ukilinganisha redmi note 11 pro 5g
Yapi Madhaifu ya Redmi note 11 pro 5g
Udhaifu wa kwanza wa redmi note 11 pro 5g ni kukaa na chaji muda mchache wakati ukitumia intaneti
Simu haina bands za 5g zenye frequency kubwa
Bands zenye frequency kubwa huwa na kasi kubwa ya intaneti
Kamera hazijatumia teknolojia nzuri ya autofocus kama dual pixel pdaf.
Na pia hakuna kamera ya telephoto wala optical zoom
Pamoja na kuzinduliwa mwaka 2022 simu inakuja na android 11 badala ya android 12
Neno la Mwisho
Mapungufu ya note 11 pro 5g ni machache
Simu imekamilika idara nyingi
Ukihitaji utendaji, simu inafaa
Na ukihitaji kamera nzuri pia simu inafiti
Maoni 3 kuhusu “Sifa za simu ya Redmi Note 11 Pro 5G(Ubora mwingi)”
maoni yangu mimi nilikuwa naitaji ya bei ya promotion
Mimi nilikuwa naitaji ya 12C yenye uwezo eMMC 5.1 128GB 64GB ,3GB and RAM 3GB ,6GB, 4GB yenye thamani laki 350000 . Lalini mimi ni likuwa naomba bei ya punguzo tafadhali
PI hapa dar es salaam ofisi zenu zipo wapi