Vivo Y22 ni simu iliyotoka mwaka 2022 mwezi septemba
Hii ni simu ya daraja la kati hivyo ina baadhi ya vitu vyenye ubora wa kuridhisha nyingine ni za kawaida
Hivyo basi bei ya vivo y22 ni chini ya laki tano kwa hapa Tanzania
Ni moja ya simu ya bei nafuu zinazozalishwa na kampuni ya Vivo japo inakosa vitu vingi vilivyopo kwenye Samsung Galaxy A34 5G
Bei ya Vivo Y22 ya GB 64
Kwa Tanzania, vivo y22 inauzwa kwa gharama ya shilingi 400,000/=
Hii bei inaendana na simu ya Tecno Spark 10 Pro ya mwaka 2023, na simu zenye tabia zinazofanana nyingi
Inavyoonekana bei za simu zimeongezeka kwa kutazama sifa za vivo y22 hasa upande wa utendaji
Kwani utendaji wake ni wa kati kutokana na aina ya chip utakayotumia
Ila hii ni moja ya simu za bei rahisi yenye kamera yenye unafuu
Kufanya maamuzi ya kuimiliki, inabidi uelewe sifa zote za hii simujanja kwenye kila kipengele
Sifa za Vivo Y22
Sehemu Za Simu | Sifa za Simu |
---|---|
Network | 2g, 3g, 4g |
Processor(SoC) |
|
Display(Kioo) | IPS LCD |
Softawre |
|
Memori | 128GB,64G na RAM 6GB,4GB |
Kamera | Kamera mbili
|
Muundo | Urefu-6.55inchi |
Chaji na Betri |
|
Bei ya simu(TSH) | 400,000/= |
Upi Ubora wa Vivo Y22
Kamera yake inajitahidi kutoa picha nzuri kwa kiasi fulani ukizingatia na bei yake
Ukaaji wa chaji ni mkubwa na wa masaa mengi
Inaruhusu kuongeza ukubwa wa ram, hivyo utaweza fungua mafaili mengi bila shida
Ni simu inayokuja na sehemu ya kuweka earpgone na pia ina redio
Maana simu za madaraja ya juu yamesitisha kuweka redio na sehemu ya earphone
Na inapatikana kwe bei inayovumilika
Kiujumla ni simu iliyopo kati kwa kati ikitegemeana na aina ya matumizi yako
Fuatalia mada ya yote uwelewe nini kinachomaanishwa
Uwezo wa Network
Uwezo wake wa network unaishia kwenye mtandao wa 4G tu
4G yake ni aina ya LTE Cat 7 yenye kasi ya 300Mbps ambayo ni sawa na 37MB/s
Kwa maana kama unapakua gemu ya Call of duty kule play store yenye GB 2 karibu sekunde 60 kumaliza kudownload
Ila hii inategemea na nguvu ya mtandao wa simu unaotumia
Kama kuna sehemu ina mtandao wa faiba usio na kikomo basi kasi hii unaifikia kwa urahisi
Ni kasi ya kawaida ukilinganisha na simu ya Oppo A78 5G
Ubora wa kioo cha Vivo Y22
Vivo Y22 inakuja na kioo cha IPS LCD chenye resoulution ya 720 x 1612 pixels
Hiki ni kiwango kidogo cha resolution ikizangitiwa vioo vya IPS LCD havifikii vioo vya AMOLED
Uonyeshaji wa vitu upande wa rangi si wa kuvutia hasa rangi nyeusi
Kwenye eneo ambalo hii simu ipo nyuma ni kioo
Kwani kioo chake hakina refresh rate kubwa ya 90Hz kama ilivyo kwa Tecno Spark 10 Pro
Kwa bei ya hii simu ilipaswa ije na kioo zaidi ya hiki ambacho wamekiweka
Ila wapo watu wanaozingatia vitu vingine kama ukaaji wa chaji zaidi kuliko muonekano wa vitu kwenye screen
Nguvu ya processor MediaTek Helio G85
Vivo Y22 inatumia processor ya MediaTek Helio G85
Ni chip nzuri ila sio nzuri kwa kufanya vitu vizito hasa kucheza gemu kwenye resolution kubwa
Ukicheza gemu kama Fortnite utalazimika kupunguza settings za graphics ziwe chini ili kuepuka kugandaganda na kucheza gemu kwa angalau fremu 21
Kama ukiwa unaangalia video za 4K za youtube simu inakumbana na changamoto ya kuwa “slow”
Ila inafanya kazi kwa uzuri ukiwa unafanya kazi zingine na magemu mengine yanacheza vizuri
Hivyo uwezo wa chip ni wa kawaida na hii inachangiwa na simu kutumia Cortex A75 kwenye core kubwa mbili
Inashangaza kwani core kubwa zenye utendaji unaoridhisha kiasi ni Cortex A78
Uwezo wa betri na chaji
Chaji ya Vivo Y22 ina uwezo wa kupeleka umeme mpaka wati 18
Kasi ya wati 18 inajaza hii simu kwa masaa yanayokaribia matatu
Kasi hii sio kubwa kiivyo kwa sababu betri ya simu ni kubwa ina 5000mAh
Ukubwa wa beti wa 5000mAh unaifanya simu kukaa na chaji masaa mengi
Kama ukiwa unaperuzi intaneti muda wote simu inachukua wastani wa masaa 12 mpaka chaji kuisha
Ukaaji wa chaji unachangiwa na processor kuwa na nguvu ya kawaida na kioo chake chengwe mwangaza wa wastani wa nits 500
Nits 500 inaweza kuonyesha vitu ukiwa unaitumia simu kwenye jua kali japo si kwa mwanga mkubwa
Ukubwa na aina ya memori
Hii simu zipo za matoleo mawili tu upande wa memori
Kuna ya GB 128 na RAM ya GB 6, na ya GB 64 na RAM ya GB 4
Ukubwa huu unaweza ukaifadhi mafaili mengi ila kama unadownload mafaili makubwa inaweza kujaza simu
Vivo hii ina sehemu ya kuweka memori kadi
Kwa maana simu ikijaa utaweza kuongeza memori kupitia memori kadi]
Chip iliyomo kwenye simu inakubali memori za aina yaani eMMC au UFS 2.1
Lakini haijaainishwa na aina ipi ya memori ambayo vivo y22 inatumia
Uimara wa bodi ya Vivo Y22
Kupata simu yenye viwango vya IP kwa bei ya chini ya laki tano sio kitu unachoweza kukiona mara kwa mara
Bodi ya vivo y22 inaweza kuzuia maji tiririka kwani ina IP5X na IPX4
Kwa maana pia simu inaweza kuzuia vumbi kupenya ndani ya simu
Upadne wa nyuma, simu imewekwa plastiki kimuonekana ni kama plastiki ngumu kuchunika
Lakini kiuhakika zaidi ni mpaka itumike muda mrefu ndio utajua kuwa uimara wa plastiki yake hukoje
Haina kioo kigumu cha gorilla upande wa screen, sio mbaya hasa ukizingatia na bei yake kiujumla
Ubora wa kamera
Kwenye wa kamera hakuna vitu vingi muhimu na kuna kamera mbili tu
Kamera kubwa ina megapixel 50 na kamera ya pili aina ya macro ina megapixel 2
Kamera ya macro ni maalumu pale unapotaka kukipiga kitu ambacho kipo karibu sana na kamera ya simu
Ubora wa picha kwenye kamera kubwa ni kuridhisha kwenye mwanga mwingi
Ila kwenye mwanga haififu utendaji ni wa kiwango cha chini
Kwenye mwanga wa kutosha vitu vinaonekana vizuri japo kuna changamoto wa usahihi wa rangi
Kwa maana kamera inakuwa inang’arisha kitu tofauti na muoekano wake wa asili
Kwa mpenzi wa mitandao ya kijamii anaweza kuvutiwa nayo ila kamera bora huwa zinajitahidi kukitoa kitu kama kinavyoonekana
Upande wa video simu inaweza kurekodi video za full hd pekee yake kwani processor ya Helio G85 haina uwezo wa kuchakata video za 4K
Ubora wa Software
Simu ni ya mwaka 2022 hivyo ni ina Android 12, hakuna taarifa kama inaweza kupokea toleo la Android 13
Tutakutaarifu kama itawezekanika
Na pia ina mfumo wa vivo unaitwa Funtouch 12
Funtouch 12 haiji na applikesheni nyingi ambazo wewe huzihitaji kama ilivyo kwa mifumo mingine kama MIUI na HIOS
Pia ni mfumo unaoruhusu kuongeza kiwango cha RAM mpaka GB 1
Yapi Madhaifu ya Vivo Y22
Kama ilivyotangulia kuelezwa ni kuwa vivo y22 ni simu ambayo ipo kati kwa kati
Madhaifu yapo mengi na mazuri yapo pia, tutaeleza machache
Mfumo wa kamera unakosa kamera aina ya Ultrawide kwa ajili ya kupoga eneo pana
Utendaji wa chip ni wa kiwango cha wastani
Pia inatumia vioo vya lcd wakati kuna simu za bei ya laki nne zina vioo vya AMOLED mfano mzuri ni Redmi Note 10
Chaji yake haina kasi kubwa sana wakati simu nyingi za daraja kati unakutana na chaji ya wati 33
Neno la Mwisho
Vivo Y22 ni simu inayofaa kumzawadia mtu tena ambaye anapenda kupiga simu, intaneti, mitandao ya kijamii yaani matumizi ya kawaida
Kwa sababu ukaaji wa chaji ni mzuri
Ila kama unataka uwe unacheza magemu mengi, kufanyia kazi za kupiga picha, ni vizuri ukaangalia mbadala
Na izingatiwe bei ya hii simu inaipeleka kwenye ushidnani na matoleo mapya ya tecno moja kwa moja
Maoni 3 kuhusu “Bei ya Vivo Y22 na Sifa Muhimu (2023)”
Mi naomba ushauli naitaji kununua simu ya 400000 je mnanishauli ninunue simu gani maana mimi nilichagua vivoy22
Kwa bajeti ya 400,0000 machaguo ni mengi sana Redmi note 13, Samsung 14, infinix hot 40, redmi wana machaguo yenye hardware nzuri zaidi
Hizi cm za vivo hazijawahi kuwa na changamoto za mara kwa mara, ni imara na bora sana…..